(Swahili translation by Schuyler Cyprian Wood, SUNY Downstate Medical Center) Mpango huu utaonyesha jinsi utaratibu wa Gram stain una weza kutofautisha gram chanya bakteria na gram negativu bakteria kwa kuwakilisha matukio katika kimuundo kisichonekana na jicho tupu. Video hii ni ya kwanza kwenye video mbili katika mfululizo huu kuonyesha utaratibu wa stain ya gram chanya bakteria na miundo muhimu ya uso bakteria kuwakilishwa kwa picha. Mduara katika kona ya kulia na chini inaonyesha jinsi bakteria kuonekana katika hadubini kama zilikuwa kuchunguzika wakati wa kila hatua ya utaratibu wa staini. Kabla ya kuwa na staini, bakteria zitakuwa uwazi na hazionekani katika darubini. Baada ya utumizi wa joto kwenye slide, imwagie na crystal violet kwa dakika moja. Kisha safishwa na maji. rangi ya staini (crystal violet) inabaki ukutani wa seli bakteria, kwa hiyo bakteria zinaonekana rangi ya bluu katika hadubini zikiwachunguzika katika hatua hii ya utaratibu. Kisha, slide ni mwagilika na iodini kwa dakika moja halafu kuosheka tena. Wakati wa hatua hii crystal violet na iodini zinachanganya kuunda tata kubwa ndani ya tabaka ya ukuta seli. Kwenye hadubini, bakteria kuonekana giza bluu au nyeusi baada ya hatua hii. Sasa, slide kuoshwa kwa mchanganyiko wa pombe na asetoni. Hata hivyo, tata za crystal violet na iodini hazitoki mshiko wa tabaka nene za ukuta seli wa bakteria gram chanya na bado viumbe vina rangi ya bluu au nyeusi. Hatimaye slide ni mwagilika na nyekundu neutral au safranin kwa dakika moja na kisha kuosheka tena. stain nyekundu pia imo ukutani bakteria lakini rangi nyekundu haionekani kwa sababu ya rangi ya bluu kwamba inashinda kuonekana katika bakteria. Kwa hivyo, kwa mujibu wa muundo tata wa ukuta gram chanya hizi bakteria zitaonekana bluu au nyeusi katika darubini baada ya utaratibu huu wa gram stain.