WEBVTT 00:00:00.970 --> 00:00:04.000 Unafanya nini katika jukwaa hili 00:00:05.390 --> 00:00:08.508 mbele ya watu wote hawa? NOTE Paragraph 00:00:08.532 --> 00:00:09.906 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:00:09.930 --> 00:00:11.081 Kimbia! NOTE Paragraph 00:00:11.105 --> 00:00:12.108 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:00:12.132 --> 00:00:13.310 Kimbia sasa. NOTE Paragraph 00:00:14.734 --> 00:00:17.701 Hii ni sauti ya hofu yangu inaongea. 00:00:18.539 --> 00:00:21.475 Hata kama hakuna tatizo lolote, 00:00:21.499 --> 00:00:25.458 Kuna wakati huwa napata hisia za mahangaiko, 00:00:25.482 --> 00:00:28.444 kama hatari inaninyemelea kwenye kona. NOTE Paragraph 00:00:29.057 --> 00:00:31.173 Unaona, miaka michache iliyopita, 00:00:31.197 --> 00:00:33.694 Niligundulika na ugonjwa wa msongo wa hofu 00:00:33.718 --> 00:00:34.868 na mawazo -- 00:00:35.289 --> 00:00:37.709 hali mbili ambazo huenda pamoja. 00:00:38.073 --> 00:00:42.338 Sasa, kuna wakati nisingemuambia mtu yoyote, 00:00:42.362 --> 00:00:44.822 hususani mbele ya umati mkubwa. 00:00:44.846 --> 00:00:46.373 Kama mwanamke mwenye ngozi nyeusi, 00:00:46.397 --> 00:00:50.037 Nimetakiwa kujijengea ustahimilivu wa hali ya juu ili kufanikiwa. 00:00:50.061 --> 00:00:52.040 Na kama watu wengi katika jamii yangu, 00:00:52.064 --> 00:00:55.872 Nilikuwa na imani potofu kwamba msongo wa mawazo ni kiashiria cha udhaifu, 00:00:55.896 --> 00:00:57.432 udhaifu wa tabia. 00:00:57.456 --> 00:00:59.030 Lakini sikuwa dhaifu; 00:00:59.054 --> 00:01:00.524 Nilikuwa nimefanikiwa kwa hali ya juu. 00:01:00.925 --> 00:01:03.128 Nilipata Shahada ya Uzamili kwenye masomo ya vyombo vya habari 00:01:03.152 --> 00:01:07.261 na kuwa na kazi za hadhi ya juu katika tasnia ya filamu na televisheni. 00:01:07.734 --> 00:01:10.784 Nimeshinda hata tuzo mbili za Emmy kwa uchapakazi kazi wangu. 00:01:11.436 --> 00:01:14.452 Hakika, Nilitumika sana, 00:01:14.476 --> 00:01:17.146 Nilikosa hamu katika vitu nilivyozoea kuvifurahia, 00:01:17.170 --> 00:01:18.468 nilikula mara chache, 00:01:18.492 --> 00:01:20.395 nilisumbuka kupata usingizi 00:01:20.419 --> 00:01:23.043 na nilijihisi kutengwa na kushuka thamani. 00:01:23.562 --> 00:01:24.914 Lakini kuwa na masononeko? 00:01:24.938 --> 00:01:26.462 Hapana, sio mimi. NOTE Paragraph 00:01:27.921 --> 00:01:30.127 Ilinichukua wiki kadhaa kabla ya kukubaliana na hali yangu, 00:01:30.151 --> 00:01:31.580 lakini daktari alikuwa sahihi: 00:01:31.604 --> 00:01:32.882 Nilikumbwa na msongo wa mawazo. 00:01:33.411 --> 00:01:36.959 Bado, sikumwambia mtu yoyote kuhusu majibu ya uchunguzi. 00:01:37.522 --> 00:01:39.135 Nilihisi aibu. 00:01:39.159 --> 00:01:41.676 Sikudhani nilipaswa kusongwa na mawazo. 00:01:42.418 --> 00:01:44.048 Nilikuwa na maisha yenye kipaumbele 00:01:44.072 --> 00:01:47.172 yenye familia iliyo na upendo na kazi iliyo na mafanikio. 00:01:47.708 --> 00:01:50.300 Na nilipowaza kuhusu maafa yasiyofikirika 00:01:50.324 --> 00:01:52.812 ambayo mababu zangu walipitia katika nchi hii 00:01:52.836 --> 00:01:54.804 ili niwe na maisha bora, 00:01:54.828 --> 00:01:56.506 aibu yangu iliongezeka zaidi. 00:01:56.980 --> 00:01:59.073 Nilikuwa nimesimama kwenye mabega yao. 00:01:59.097 --> 00:02:00.699 Ningewezaje kuwaangusha? 00:02:01.382 --> 00:02:03.435 Nilinyanyua kichwa changu na kuangalia juu, 00:02:03.459 --> 00:02:05.819 na kuweka tabasamu katika uso wangu 00:02:05.843 --> 00:02:07.551 na kutoiambia nafsi yoyote. NOTE Paragraph 00:02:10.466 --> 00:02:13.743 Mnamo tarehe 4, Julai mwaka 2013, 00:02:14.479 --> 00:02:16.667 dunia yangu ilipasuka ndani yangu. 00:02:17.399 --> 00:02:20.300 Hiyo ilikuwa siku nilipokea simu kutoka kwa mama yangu 00:02:20.324 --> 00:02:24.514 akiniambia kwamba mpwa wangu mwenye miaka 22, Paul, amejiua, 00:02:24.538 --> 00:02:27.179 baada ya miaka kadhaa ya kupambana na msongo wa mawazo na hofu. 00:02:28.668 --> 00:02:31.823 Hakuna maneno ambayo yanaweza kuelezea namna gani nilijisikia vibaya. 00:02:32.667 --> 00:02:33.961 Mimi na Paul tulikuwa karibu, 00:02:33.985 --> 00:02:36.039 lakini sikutambua alikuwa akipitia maumivu makubwa. 00:02:36.696 --> 00:02:40.254 Hakuna yeyote kati yetu ambaye aliwahi kumwambia mwenzie kuhusu mahangaiko aliyokuwa akipitia. 00:02:40.278 --> 00:02:42.442 Aibu na unyanyapaa ulitufanya wote kuwa kimya. NOTE Paragraph 00:02:44.161 --> 00:02:48.164 Sasa, namna yangu ya kupambana na mikosi ni kuitazama bila uoga, 00:02:48.188 --> 00:02:51.346 kwa hiyo nilitumia miaka miwili baadaye kufanyia utafiti msongo wa mawazo na hofu, 00:02:51.370 --> 00:02:54.137 na niligundua jambo la kushangaza. 00:02:54.764 --> 00:02:56.738 Taasisi ya Afya Duniani imetoa ripoti ikisema 00:02:56.762 --> 00:03:01.986 kwamba msongo wa mawazo ni sababu kuu ya magonjwa na ulemavu 00:03:02.010 --> 00:03:03.349 duniani. 00:03:04.039 --> 00:03:07.030 Wakati sababu hasa ya msongo wa mawazo haijatambulika, 00:03:07.054 --> 00:03:10.152 utafiti unaelezea kwamba magonjwa mengi ya akili hujitokeza, 00:03:10.176 --> 00:03:11.903 walau katika sehemu, 00:03:11.927 --> 00:03:14.582 kwa sababu ya kutolingana kwa kemikali katika ubongo, 00:03:14.606 --> 00:03:18.508 na/au katika utengenezaji wa mwanzo wa jenetikia. 00:03:19.041 --> 00:03:21.202 Kwa hiyo huwezi kuachana nayo tu. NOTE Paragraph 00:03:22.907 --> 00:03:24.638 Kwa Wamarekani weusi, 00:03:24.662 --> 00:03:28.718 vileta msongo wa mawazo kama ubaguzi wa rangi na utofauti wa hali ya kiuchumi katika jamii 00:03:28.742 --> 00:03:33.782 huwaweka katika asilimia 20 zaidi ya kupata ugonjwa wa akili, 00:03:33.806 --> 00:03:36.218 na bado hutafuta huduma za afya ya akili 00:03:36.242 --> 00:03:38.981 katika kiwango sawa na nusu ya Wamarekani weupe. 00:03:39.544 --> 00:03:42.394 Sababu moja ni unyanyapaa, 00:03:42.418 --> 00:03:48.635 ikiwa asilimia 63 ya Wamarekani weusi hukosea kwa kuwaza kwamba msongo wa mawazo ni udhaifu. 00:03:49.603 --> 00:03:53.861 Cha kusikitisha, kasi ya watoto weusi ambao hujiua 00:03:53.885 --> 00:03:56.572 imeongezeka mara mbili katika miaka 20 iliyopita. NOTE Paragraph 00:03:57.843 --> 00:04:00.048 Sasa, hii ni habari njema: 00:04:00.603 --> 00:04:04.885 asilimia 70 ya watu ambao wanasumbuka na msongo wa mawazo hali zao zitaboreka 00:04:04.909 --> 00:04:08.266 kwa kupata tiba na dawa. 00:04:09.458 --> 00:04:11.120 Wakipewa taarifa, 00:04:11.144 --> 00:04:12.851 Nimechukua uamuzi: 00:04:12.875 --> 00:04:15.843 Sitakuwa kimya tena. 00:04:16.740 --> 00:04:18.543 Na baraka za familia yangu, 00:04:18.567 --> 00:04:20.460 Nitasimulia hadithi yetu 00:04:20.484 --> 00:04:23.298 katika matumaini ya kuleta mjadala wa kitaifa. NOTE Paragraph 00:04:24.140 --> 00:04:26.911 Rafiki yangu, Kelly Pierre-Loius, alisema, 00:04:26.935 --> 00:04:29.426 "Kuwa ngangari hutuua." 00:04:30.743 --> 00:04:32.162 Alikuwa sahihi. 00:04:32.186 --> 00:04:36.208 Tunabidi kuondokana na hizo imani ziilizopitwa na wakati 00:04:36.232 --> 00:04:37.787 kuhusu mwanamke mweusi jasiri 00:04:37.811 --> 00:04:40.021 na mwanaume mweusi kuwa mwanaume hasa, 00:04:40.045 --> 00:04:42.965 ambaye, haijalishi mara ngapi wakidondoshwa, 00:04:42.989 --> 00:04:45.224 hujifuta na kisha husonga mbele. 00:04:45.770 --> 00:04:49.485 Kuwa na hisia sio dalili ya udhaifu. 00:04:50.521 --> 00:04:52.404 Hisia zinamaanisha kwamba sisi ni binadamu. 00:04:52.850 --> 00:04:54.869 Na pale tunapoukana ubinadamu wetu, 00:04:54.893 --> 00:04:57.009 hutuacha wapweke ndani, 00:04:57.033 --> 00:05:00.037 tukitafuta njia za kujiponya ili kuepukana na upweke. 00:05:00.585 --> 00:05:03.330 Dawa yangu ilikuwa mafanikio makubwa. NOTE Paragraph 00:05:04.371 --> 00:05:07.672 Siku hizi, naweza kusimulia hadithi yangu wazi, 00:05:07.696 --> 00:05:09.906 na kuwauliza wengine kusimulia zao, pia. 00:05:10.406 --> 00:05:11.854 Naamini hicho ndicho kinachoweza 00:05:13.820 --> 00:05:14.070 kusaidia watu wanaohangaika katika ukimya 00:05:14.497 --> 00:05:16.706 ili wajue kwamba hawapo peke yao 00:05:16.730 --> 00:05:18.415 na kujua kwamba kwa msaada, 00:05:18.439 --> 00:05:19.780 wanaweza kupona. 00:05:19.804 --> 00:05:21.969 Sasa, bado nina mahangaiko yangu, 00:05:21.993 --> 00:05:24.281 hasa kutokana na hofu, 00:05:24.305 --> 00:05:25.908 lakini ninaweza kukabiliana na hali hio 00:05:25.932 --> 00:05:30.806 kwa kutafakari kila siku, kufanya yoga na kula vizuri kiasi. NOTE Paragraph 00:05:30.830 --> 00:05:31.898 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:05:31.922 --> 00:05:34.144 Kama nikiona kwamba hali inaanza kuwa mbaya, 00:05:34.168 --> 00:05:36.212 Huwa nawasiliana na mtoa tiba wangu, 00:05:36.236 --> 00:05:39.299 mwanamke mweusi anayeitwa Dawn Armstrong, 00:05:39.323 --> 00:05:41.296 ambaye ni mcheshi 00:05:41.320 --> 00:05:43.557 na mwenye uzoea ambao hunipa faraja. 00:05:45.126 --> 00:05:46.764 Daima nitajuta 00:05:47.390 --> 00:05:49.456 sikuwepo kumsaidia mpwa wangu. 00:05:50.226 --> 00:05:52.013 Lakini tumaini langu la kweli 00:05:52.695 --> 00:05:55.766 ni kwamba niwahamasishe wengine kutokana na somo nililojifunza. NOTE Paragraph 00:05:59.182 --> 00:06:01.652 Maisha ni mazuri. 00:06:02.646 --> 00:06:04.208 Kuna wakati yanavurugika, 00:06:04.232 --> 00:06:06.166 na hayatabiriki siku zote. 00:06:07.034 --> 00:06:08.237 Lakini kila kitu kitakuwa sawa 00:06:08.261 --> 00:06:11.046 unapokuwa na mfumo ambao utakusaidia kuyashinda yote. 00:06:11.513 --> 00:06:13.934 Nina imani kama mzigo wako ukiwa mzito sana, 00:06:13.958 --> 00:06:15.664 utaomba msaada, pia. NOTE Paragraph 00:06:15.688 --> 00:06:16.855 Asante. NOTE Paragraph 00:06:16.879 --> 00:06:19.761 (Makofi)