1 00:00:00,970 --> 00:00:04,000 Unafanya nini katika jukwaa hili 2 00:00:05,390 --> 00:00:08,508 mbele ya watu wote hawa? 3 00:00:08,532 --> 00:00:09,906 (Kicheko) 4 00:00:09,930 --> 00:00:11,081 Kimbia! 5 00:00:11,105 --> 00:00:12,108 (Kicheko) 6 00:00:12,132 --> 00:00:13,310 Kimbia sasa. 7 00:00:14,734 --> 00:00:17,701 Hii ni sauti ya hofu yangu inaongea. 8 00:00:18,539 --> 00:00:21,475 Hata kama hakuna tatizo lolote, 9 00:00:21,499 --> 00:00:25,458 Kuna wakati huwa napata hisia za mahangaiko, 10 00:00:25,482 --> 00:00:28,444 kama hatari inaninyemelea kwenye kona. 11 00:00:29,057 --> 00:00:31,173 Unaona, miaka michache iliyopita, 12 00:00:31,197 --> 00:00:33,694 Niligundulika na ugonjwa wa msongo wa hofu 13 00:00:33,718 --> 00:00:34,868 na mawazo -- 14 00:00:35,289 --> 00:00:37,709 hali mbili ambazo huenda pamoja. 15 00:00:38,073 --> 00:00:42,338 Sasa, kuna wakati nisingemuambia mtu yoyote, 16 00:00:42,362 --> 00:00:44,822 hususani mbele ya umati mkubwa. 17 00:00:44,846 --> 00:00:46,373 Kama mwanamke mwenye ngozi nyeusi, 18 00:00:46,397 --> 00:00:50,037 Nimetakiwa kujijengea ustahimilivu wa hali ya juu ili kufanikiwa. 19 00:00:50,061 --> 00:00:52,040 Na kama watu wengi katika jamii yangu, 20 00:00:52,064 --> 00:00:55,872 Nilikuwa na imani potofu kwamba msongo wa mawazo ni kiashiria cha udhaifu, 21 00:00:55,896 --> 00:00:57,432 udhaifu wa tabia. 22 00:00:57,456 --> 00:00:59,030 Lakini sikuwa dhaifu; 23 00:00:59,054 --> 00:01:00,524 Nilikuwa nimefanikiwa kwa hali ya juu. 24 00:01:00,925 --> 00:01:03,128 Nilipata Shahada ya Uzamili kwenye masomo ya vyombo vya habari 25 00:01:03,152 --> 00:01:07,261 na kuwa na kazi za hadhi ya juu katika tasnia ya filamu na televisheni. 26 00:01:07,734 --> 00:01:10,784 Nimeshinda hata tuzo mbili za Emmy kwa uchapakazi kazi wangu. 27 00:01:11,436 --> 00:01:14,452 Hakika, Nilitumika sana, 28 00:01:14,476 --> 00:01:17,146 Nilikosa hamu katika vitu nilivyozoea kuvifurahia, 29 00:01:17,170 --> 00:01:18,468 nilikula mara chache, 30 00:01:18,492 --> 00:01:20,395 nilisumbuka kupata usingizi 31 00:01:20,419 --> 00:01:23,043 na nilijihisi kutengwa na kushuka thamani. 32 00:01:23,562 --> 00:01:24,914 Lakini kuwa na masononeko? 33 00:01:24,938 --> 00:01:26,462 Hapana, sio mimi. 34 00:01:27,921 --> 00:01:30,127 Ilinichukua wiki kadhaa kabla ya kukubaliana na hali yangu, 35 00:01:30,151 --> 00:01:31,580 lakini daktari alikuwa sahihi: 36 00:01:31,604 --> 00:01:32,882 Nilikumbwa na msongo wa mawazo. 37 00:01:33,411 --> 00:01:36,959 Bado, sikumwambia mtu yoyote kuhusu majibu ya uchunguzi. 38 00:01:37,522 --> 00:01:39,135 Nilihisi aibu. 39 00:01:39,159 --> 00:01:41,676 Sikudhani nilipaswa kusongwa na mawazo. 40 00:01:42,418 --> 00:01:44,048 Nilikuwa na maisha yenye kipaumbele 41 00:01:44,072 --> 00:01:47,172 yenye familia iliyo na upendo na kazi iliyo na mafanikio. 42 00:01:47,708 --> 00:01:50,300 Na nilipowaza kuhusu maafa yasiyofikirika 43 00:01:50,324 --> 00:01:52,812 ambayo mababu zangu walipitia katika nchi hii 44 00:01:52,836 --> 00:01:54,804 ili niwe na maisha bora, 45 00:01:54,828 --> 00:01:56,506 aibu yangu iliongezeka zaidi. 46 00:01:56,980 --> 00:01:59,073 Nilikuwa nimesimama kwenye mabega yao. 47 00:01:59,097 --> 00:02:00,699 Ningewezaje kuwaangusha? 48 00:02:01,382 --> 00:02:03,435 Nilinyanyua kichwa changu na kuangalia juu, 49 00:02:03,459 --> 00:02:05,819 na kuweka tabasamu katika uso wangu 50 00:02:05,843 --> 00:02:07,551 na kutoiambia nafsi yoyote. 51 00:02:10,466 --> 00:02:13,743 Mnamo tarehe 4, Julai mwaka 2013, 52 00:02:14,479 --> 00:02:16,667 dunia yangu ilipasuka ndani yangu. 53 00:02:17,399 --> 00:02:20,300 Hiyo ilikuwa siku nilipokea simu kutoka kwa mama yangu 54 00:02:20,324 --> 00:02:24,514 akiniambia kwamba mpwa wangu mwenye miaka 22, Paul, amejiua, 55 00:02:24,538 --> 00:02:27,179 baada ya miaka kadhaa ya kupambana na msongo wa mawazo na hofu. 56 00:02:28,668 --> 00:02:31,823 Hakuna maneno ambayo yanaweza kuelezea namna gani nilijisikia vibaya. 57 00:02:32,667 --> 00:02:33,961 Mimi na Paul tulikuwa karibu, 58 00:02:33,985 --> 00:02:36,039 lakini sikutambua alikuwa akipitia maumivu makubwa. 59 00:02:36,696 --> 00:02:40,254 Hakuna yeyote kati yetu ambaye aliwahi kumwambia mwenzie kuhusu mahangaiko aliyokuwa akipitia. 60 00:02:40,278 --> 00:02:42,442 Aibu na unyanyapaa ulitufanya wote kuwa kimya. 61 00:02:44,161 --> 00:02:48,164 Sasa, namna yangu ya kupambana na mikosi ni kuitazama bila uoga, 62 00:02:48,188 --> 00:02:51,346 kwa hiyo nilitumia miaka miwili baadaye kufanyia utafiti msongo wa mawazo na hofu, 63 00:02:51,370 --> 00:02:54,137 na niligundua jambo la kushangaza. 64 00:02:54,764 --> 00:02:56,738 Taasisi ya Afya Duniani imetoa ripoti ikisema 65 00:02:56,762 --> 00:03:01,986 kwamba msongo wa mawazo ni sababu kuu ya magonjwa na ulemavu 66 00:03:02,010 --> 00:03:03,349 duniani. 67 00:03:04,039 --> 00:03:07,030 Wakati sababu hasa ya msongo wa mawazo haijatambulika, 68 00:03:07,054 --> 00:03:10,152 utafiti unaelezea kwamba magonjwa mengi ya akili hujitokeza, 69 00:03:10,176 --> 00:03:11,903 walau katika sehemu, 70 00:03:11,927 --> 00:03:14,582 kwa sababu ya kutolingana kwa kemikali katika ubongo, 71 00:03:14,606 --> 00:03:18,508 na/au katika utengenezaji wa mwanzo wa jenetikia. 72 00:03:19,041 --> 00:03:21,202 Kwa hiyo huwezi kuachana nayo tu. 73 00:03:22,907 --> 00:03:24,638 Kwa Wamarekani weusi, 74 00:03:24,662 --> 00:03:28,718 vileta msongo wa mawazo kama ubaguzi wa rangi na utofauti wa hali ya kiuchumi katika jamii 75 00:03:28,742 --> 00:03:33,782 huwaweka katika asilimia 20 zaidi ya kupata ugonjwa wa akili, 76 00:03:33,806 --> 00:03:36,218 na bado hutafuta huduma za afya ya akili 77 00:03:36,242 --> 00:03:38,981 katika kiwango sawa na nusu ya Wamarekani weupe. 78 00:03:39,544 --> 00:03:42,394 Sababu moja ni unyanyapaa, 79 00:03:42,418 --> 00:03:48,635 ikiwa asilimia 63 ya Wamarekani weusi hukosea kwa kuwaza kwamba msongo wa mawazo ni udhaifu. 80 00:03:49,603 --> 00:03:53,861 Cha kusikitisha, kasi ya watoto weusi ambao hujiua 81 00:03:53,885 --> 00:03:56,572 imeongezeka mara mbili katika miaka 20 iliyopita. 82 00:03:57,843 --> 00:04:00,048 Sasa, hii ni habari njema: 83 00:04:00,603 --> 00:04:04,885 asilimia 70 ya watu ambao wanasumbuka na msongo wa mawazo hali zao zitaboreka 84 00:04:04,909 --> 00:04:08,266 kwa kupata tiba na dawa. 85 00:04:09,458 --> 00:04:11,120 Wakipewa taarifa, 86 00:04:11,144 --> 00:04:12,851 Nimechukua uamuzi: 87 00:04:12,875 --> 00:04:15,843 Sitakuwa kimya tena. 88 00:04:16,740 --> 00:04:18,543 Na baraka za familia yangu, 89 00:04:18,567 --> 00:04:20,460 Nitasimulia hadithi yetu 90 00:04:20,484 --> 00:04:23,298 katika matumaini ya kuleta mjadala wa kitaifa. 91 00:04:24,140 --> 00:04:26,911 Rafiki yangu, Kelly Pierre-Loius, alisema, 92 00:04:26,935 --> 00:04:29,426 "Kuwa ngangari hutuua." 93 00:04:30,743 --> 00:04:32,162 Alikuwa sahihi. 94 00:04:32,186 --> 00:04:36,208 Tunabidi kuondokana na hizo imani ziilizopitwa na wakati 95 00:04:36,232 --> 00:04:37,787 kuhusu mwanamke mweusi jasiri 96 00:04:37,811 --> 00:04:40,021 na mwanaume mweusi kuwa mwanaume hasa, 97 00:04:40,045 --> 00:04:42,965 ambaye, haijalishi mara ngapi wakidondoshwa, 98 00:04:42,989 --> 00:04:45,224 hujifuta na kisha husonga mbele. 99 00:04:45,770 --> 00:04:49,485 Kuwa na hisia sio dalili ya udhaifu. 100 00:04:50,521 --> 00:04:52,404 Hisia zinamaanisha kwamba sisi ni binadamu. 101 00:04:52,850 --> 00:04:54,869 Na pale tunapoukana ubinadamu wetu, 102 00:04:54,893 --> 00:04:57,009 hutuacha wapweke ndani, 103 00:04:57,033 --> 00:05:00,037 tukitafuta njia za kujiponya ili kuepukana na upweke. 104 00:05:00,585 --> 00:05:03,330 Dawa yangu ilikuwa mafanikio makubwa. 105 00:05:04,371 --> 00:05:07,672 Siku hizi, naweza kusimulia hadithi yangu wazi, 106 00:05:07,696 --> 00:05:09,906 na kuwauliza wengine kusimulia zao, pia. 107 00:05:10,406 --> 00:05:11,854 Naamini hicho ndicho kinachoweza 108 00:05:13,820 --> 00:05:14,070 kusaidia watu wanaohangaika katika ukimya 109 00:05:14,497 --> 00:05:16,706 ili wajue kwamba hawapo peke yao 110 00:05:16,730 --> 00:05:18,415 na kujua kwamba kwa msaada, 111 00:05:18,439 --> 00:05:19,780 wanaweza kupona. 112 00:05:19,804 --> 00:05:21,969 Sasa, bado nina mahangaiko yangu, 113 00:05:21,993 --> 00:05:24,281 hasa kutokana na hofu, 114 00:05:24,305 --> 00:05:25,908 lakini ninaweza kukabiliana na hali hio 115 00:05:25,932 --> 00:05:30,806 kwa kutafakari kila siku, kufanya yoga na kula vizuri kiasi. 116 00:05:30,830 --> 00:05:31,898 (Kicheko) 117 00:05:31,922 --> 00:05:34,144 Kama nikiona kwamba hali inaanza kuwa mbaya, 118 00:05:34,168 --> 00:05:36,212 Huwa nawasiliana na mtoa tiba wangu, 119 00:05:36,236 --> 00:05:39,299 mwanamke mweusi anayeitwa Dawn Armstrong, 120 00:05:39,323 --> 00:05:41,296 ambaye ni mcheshi 121 00:05:41,320 --> 00:05:43,557 na mwenye uzoea ambao hunipa faraja. 122 00:05:45,126 --> 00:05:46,764 Daima nitajuta 123 00:05:47,390 --> 00:05:49,456 sikuwepo kumsaidia mpwa wangu. 124 00:05:50,226 --> 00:05:52,013 Lakini tumaini langu la kweli 125 00:05:52,695 --> 00:05:55,766 ni kwamba niwahamasishe wengine kutokana na somo nililojifunza. 126 00:05:59,182 --> 00:06:01,652 Maisha ni mazuri. 127 00:06:02,646 --> 00:06:04,208 Kuna wakati yanavurugika, 128 00:06:04,232 --> 00:06:06,166 na hayatabiriki siku zote. 129 00:06:07,034 --> 00:06:08,237 Lakini kila kitu kitakuwa sawa 130 00:06:08,261 --> 00:06:11,046 unapokuwa na mfumo ambao utakusaidia kuyashinda yote. 131 00:06:11,513 --> 00:06:13,934 Nina imani kama mzigo wako ukiwa mzito sana, 132 00:06:13,958 --> 00:06:15,664 utaomba msaada, pia. 133 00:06:15,688 --> 00:06:16,855 Asante. 134 00:06:16,879 --> 00:06:19,761 (Makofi)