0:00:00.970,0:00:04.000 Unafanya nini katika jukwaa hili 0:00:05.390,0:00:08.508 mbele ya watu wote hawa? 0:00:08.532,0:00:09.906 (Kicheko) 0:00:09.930,0:00:11.081 Kimbia! 0:00:11.105,0:00:12.108 (Kicheko) 0:00:12.132,0:00:13.310 Kimbia sasa. 0:00:14.734,0:00:17.701 Hii ni sauti ya hofu yangu inaongea. 0:00:18.539,0:00:21.475 Hata kama hakuna tatizo lolote, 0:00:21.499,0:00:25.458 Kuna wakati huwa napata hisia za mahangaiko, 0:00:25.482,0:00:28.444 kama hatari inaninyemelea kwenye kona. 0:00:29.057,0:00:31.173 Unaona, miaka michache iliyopita, 0:00:31.197,0:00:33.694 Niligundulika na ugonjwa wa msongo wa hofu 0:00:33.718,0:00:34.868 na mawazo -- 0:00:35.289,0:00:37.709 hali mbili ambazo huenda pamoja. 0:00:38.073,0:00:42.338 Sasa, kuna wakati nisingemuambia mtu yoyote, 0:00:42.362,0:00:44.822 hususani mbele ya umati mkubwa. 0:00:44.846,0:00:46.373 Kama mwanamke mwenye ngozi nyeusi, 0:00:46.397,0:00:50.037 Nimetakiwa kujijengea ustahimilivu wa hali ya juu ili kufanikiwa. 0:00:50.061,0:00:52.040 Na kama watu wengi katika jamii yangu, 0:00:52.064,0:00:55.872 Nilikuwa na imani potofu kwamba msongo wa mawazo ni kiashiria cha udhaifu, 0:00:55.896,0:00:57.432 udhaifu wa tabia. 0:00:57.456,0:00:59.030 Lakini sikuwa dhaifu; 0:00:59.054,0:01:00.524 Nilikuwa nimefanikiwa kwa hali ya juu. 0:01:00.925,0:01:03.128 Nilipata Shahada ya Uzamili kwenye masomo ya vyombo vya habari 0:01:03.152,0:01:07.261 na kuwa na kazi za hadhi ya juu katika tasnia ya filamu na televisheni. 0:01:07.734,0:01:10.784 Nimeshinda hata tuzo mbili za Emmy kwa uchapakazi kazi wangu. 0:01:11.436,0:01:14.452 Hakika, Nilitumika sana, 0:01:14.476,0:01:17.146 Nilikosa hamu katika vitu nilivyozoea kuvifurahia, 0:01:17.170,0:01:18.468 nilikula mara chache, 0:01:18.492,0:01:20.395 nilisumbuka kupata usingizi 0:01:20.419,0:01:23.043 na nilijihisi kutengwa na kushuka thamani. 0:01:23.562,0:01:24.914 Lakini kuwa na masononeko? 0:01:24.938,0:01:26.462 Hapana, sio mimi. 0:01:27.921,0:01:30.127 Ilinichukua wiki kadhaa kabla ya kukubaliana na hali yangu, 0:01:30.151,0:01:31.580 lakini daktari alikuwa sahihi: 0:01:31.604,0:01:32.882 Nilikumbwa na msongo wa mawazo. 0:01:33.411,0:01:36.959 Bado, sikumwambia mtu yoyote kuhusu majibu ya uchunguzi. 0:01:37.522,0:01:39.135 Nilihisi aibu. 0:01:39.159,0:01:41.676 Sikudhani nilipaswa kusongwa na mawazo. 0:01:42.418,0:01:44.048 Nilikuwa na maisha yenye kipaumbele 0:01:44.072,0:01:47.172 yenye familia iliyo na upendo na kazi iliyo na mafanikio. 0:01:47.708,0:01:50.300 Na nilipowaza kuhusu maafa yasiyofikirika 0:01:50.324,0:01:52.812 ambayo mababu zangu walipitia katika nchi hii 0:01:52.836,0:01:54.804 ili niwe na maisha bora, 0:01:54.828,0:01:56.506 aibu yangu iliongezeka zaidi. 0:01:56.980,0:01:59.073 Nilikuwa nimesimama kwenye mabega yao. 0:01:59.097,0:02:00.699 Ningewezaje kuwaangusha? 0:02:01.382,0:02:03.435 Nilinyanyua kichwa changu na kuangalia juu, 0:02:03.459,0:02:05.819 na kuweka tabasamu katika uso wangu 0:02:05.843,0:02:07.551 na kutoiambia nafsi yoyote. 0:02:10.466,0:02:13.743 Mnamo tarehe 4, Julai mwaka 2013, 0:02:14.479,0:02:16.667 dunia yangu ilipasuka ndani yangu. 0:02:17.399,0:02:20.300 Hiyo ilikuwa siku nilipokea simu kutoka kwa mama yangu 0:02:20.324,0:02:24.514 akiniambia kwamba mpwa wangu mwenye miaka 22, Paul, amejiua, 0:02:24.538,0:02:27.179 baada ya miaka kadhaa ya kupambana na msongo wa mawazo na hofu. 0:02:28.668,0:02:31.823 Hakuna maneno ambayo yanaweza kuelezea namna gani nilijisikia vibaya. 0:02:32.667,0:02:33.961 Mimi na Paul tulikuwa karibu, 0:02:33.985,0:02:36.039 lakini sikutambua alikuwa akipitia maumivu makubwa. 0:02:36.696,0:02:40.254 Hakuna yeyote kati yetu ambaye aliwahi kumwambia mwenzie kuhusu mahangaiko aliyokuwa akipitia. 0:02:40.278,0:02:42.442 Aibu na unyanyapaa ulitufanya wote kuwa kimya. 0:02:44.161,0:02:48.164 Sasa, namna yangu ya kupambana na mikosi ni kuitazama bila uoga, 0:02:48.188,0:02:51.346 kwa hiyo nilitumia miaka miwili baadaye kufanyia utafiti msongo wa mawazo na hofu, 0:02:51.370,0:02:54.137 na niligundua jambo la kushangaza. 0:02:54.764,0:02:56.738 Taasisi ya Afya Duniani imetoa ripoti ikisema 0:02:56.762,0:03:01.986 kwamba msongo wa mawazo ni sababu kuu ya magonjwa na ulemavu 0:03:02.010,0:03:03.349 duniani. 0:03:04.039,0:03:07.030 Wakati sababu hasa ya msongo wa mawazo haijatambulika, 0:03:07.054,0:03:10.152 utafiti unaelezea kwamba magonjwa mengi ya akili hujitokeza, 0:03:10.176,0:03:11.903 walau katika sehemu, 0:03:11.927,0:03:14.582 kwa sababu ya kutolingana kwa kemikali katika ubongo, 0:03:14.606,0:03:18.508 na/au katika utengenezaji wa mwanzo wa jenetikia. 0:03:19.041,0:03:21.202 Kwa hiyo huwezi kuachana nayo tu. 0:03:22.907,0:03:24.638 Kwa Wamarekani weusi, 0:03:24.662,0:03:28.718 vileta msongo wa mawazo kama ubaguzi wa rangi na utofauti wa hali ya kiuchumi katika jamii 0:03:28.742,0:03:33.782 huwaweka katika asilimia 20 zaidi ya kupata ugonjwa wa akili, 0:03:33.806,0:03:36.218 na bado hutafuta huduma za afya ya akili 0:03:36.242,0:03:38.981 katika kiwango sawa na nusu ya Wamarekani weupe. 0:03:39.544,0:03:42.394 Sababu moja ni unyanyapaa, 0:03:42.418,0:03:48.635 ikiwa asilimia 63 ya Wamarekani weusi hukosea kwa kuwaza kwamba msongo wa mawazo ni udhaifu. 0:03:49.603,0:03:53.861 Cha kusikitisha, kasi ya watoto weusi ambao hujiua 0:03:53.885,0:03:56.572 imeongezeka mara mbili katika miaka 20 iliyopita. 0:03:57.843,0:04:00.048 Sasa, hii ni habari njema: 0:04:00.603,0:04:04.885 asilimia 70 ya watu ambao wanasumbuka na msongo wa mawazo hali zao zitaboreka 0:04:04.909,0:04:08.266 kwa kupata tiba na dawa. 0:04:09.458,0:04:11.120 Wakipewa taarifa, 0:04:11.144,0:04:12.851 Nimechukua uamuzi: 0:04:12.875,0:04:15.843 Sitakuwa kimya tena. 0:04:16.740,0:04:18.543 Na baraka za familia yangu, 0:04:18.567,0:04:20.460 Nitasimulia hadithi yetu 0:04:20.484,0:04:23.298 katika matumaini ya kuleta mjadala wa kitaifa. 0:04:24.140,0:04:26.911 Rafiki yangu, Kelly Pierre-Loius, alisema, 0:04:26.935,0:04:29.426 "Kuwa ngangari hutuua." 0:04:30.743,0:04:32.162 Alikuwa sahihi. 0:04:32.186,0:04:36.208 Tunabidi kuondokana na hizo imani ziilizopitwa na wakati 0:04:36.232,0:04:37.787 kuhusu mwanamke mweusi jasiri 0:04:37.811,0:04:40.021 na mwanaume mweusi kuwa mwanaume hasa, 0:04:40.045,0:04:42.965 ambaye, haijalishi mara ngapi wakidondoshwa, 0:04:42.989,0:04:45.224 hujifuta na kisha husonga mbele. 0:04:45.770,0:04:49.485 Kuwa na hisia sio dalili ya udhaifu. 0:04:50.521,0:04:52.404 Hisia zinamaanisha kwamba sisi ni binadamu. 0:04:52.850,0:04:54.869 Na pale tunapoukana ubinadamu wetu, 0:04:54.893,0:04:57.009 hutuacha wapweke ndani, 0:04:57.033,0:05:00.037 tukitafuta njia za kujiponya ili kuepukana na upweke. 0:05:00.585,0:05:03.330 Dawa yangu ilikuwa mafanikio makubwa. 0:05:04.371,0:05:07.672 Siku hizi, naweza kusimulia hadithi yangu wazi, 0:05:07.696,0:05:09.906 na kuwauliza wengine kusimulia zao, pia. 0:05:10.406,0:05:11.854 Naamini hicho ndicho kinachoweza 0:05:13.820,0:05:14.070 kusaidia watu wanaohangaika katika ukimya 0:05:14.497,0:05:16.706 ili wajue kwamba hawapo peke yao 0:05:16.730,0:05:18.415 na kujua kwamba kwa msaada, 0:05:18.439,0:05:19.780 wanaweza kupona. 0:05:19.804,0:05:21.969 Sasa, bado nina mahangaiko yangu, 0:05:21.993,0:05:24.281 hasa kutokana na hofu, 0:05:24.305,0:05:25.908 lakini ninaweza kukabiliana na hali hio 0:05:25.932,0:05:30.806 kwa kutafakari kila siku, kufanya yoga na kula vizuri kiasi. 0:05:30.830,0:05:31.898 (Kicheko) 0:05:31.922,0:05:34.144 Kama nikiona kwamba hali inaanza kuwa mbaya, 0:05:34.168,0:05:36.212 Huwa nawasiliana na mtoa tiba wangu, 0:05:36.236,0:05:39.299 mwanamke mweusi anayeitwa Dawn Armstrong, 0:05:39.323,0:05:41.296 ambaye ni mcheshi 0:05:41.320,0:05:43.557 na mwenye uzoea ambao hunipa faraja. 0:05:45.126,0:05:46.764 Daima nitajuta 0:05:47.390,0:05:49.456 sikuwepo kumsaidia mpwa wangu. 0:05:50.226,0:05:52.013 Lakini tumaini langu la kweli 0:05:52.695,0:05:55.766 ni kwamba niwahamasishe wengine kutokana na somo nililojifunza. 0:05:59.182,0:06:01.652 Maisha ni mazuri. 0:06:02.646,0:06:04.208 Kuna wakati yanavurugika, 0:06:04.232,0:06:06.166 na hayatabiriki siku zote. 0:06:07.034,0:06:08.237 Lakini kila kitu kitakuwa sawa 0:06:08.261,0:06:11.046 unapokuwa na mfumo ambao utakusaidia kuyashinda yote. 0:06:11.513,0:06:13.934 Nina imani kama mzigo wako ukiwa mzito sana, 0:06:13.958,0:06:15.664 utaomba msaada, pia. 0:06:15.688,0:06:16.855 Asante. 0:06:16.879,0:06:19.761 (Makofi)