Karibu tena.
Wakanada wengi hawatahitaji kushawishiwa kuwa chanjo ya UVIKO inastahili,
pindi ifikapo.
Lakini jinsi ulivyosikia, Wakanada wengi wapo na maswali.
Kwa hivyo kujibu baadhi,
Dkt. Cora Constantinescu, mtaalam wa magonjwa ya kuambukizwa
anayehudumu katika kliniki ya kuchunguza mienendo ya kusita kuchanjwa
katika hospitali ya watoto ya Alberta iliyoko Caligary.
Na daktari, sikujua sehemu kama yako ipo
Ni nani hasa huletwa kwako?
Tumeifanya kuwa mchakato nyoofu
na tumefikia jamii ya matabibu
na kuwaambia kuwa tuko hapa
kuwaunga mkono wanapotuletea wagonjwa.
Unaona kushawishi watu kuchanjwa kuwa kazi yako?
Naona kuwa ni kazi yangu kuwasaidia watu
wanapofanya uamuzi kuchanja.
Mdahalo huo huwa vipi? Unaanzia wapi?
Ninaanza kwa kujikumbusha kila wakati
kuwa katika kiini cha kila miadi ya kusita kuchanjwa
ni mzazi anayejaribu
uamuzi mwafaka kwao na familia yao.
Na inahitaji ukakamavu mwingi kuja
kwa sababu wanapambana na uoga mwingi na habari potofu,
na kwa ujumla ukosefu wa uaminifu.
Kwa hivyo tunatumia muda mwingi kujenga uhusiano na uaminifu na kila familia,
kuwaelewa ilituweze kubinafsisha
mawasiliano na ujumbe tunaowapa kuhusu chanjo.
Halafu tunahushisha afya ya umma kwa karibu
kisha wanafululiza na kupeana chanjo.
Na inashangaza kuwa unasema kuwa kuna huu ukosefu wa uaminifu.
Unawezaje kuanza kushauri
serikali ya mkoani, serikali ya mtaa, ama serikali ya jumuiya
kuiunda?
Nafikiri kuwa tunapofikiria kuhusu uaminifu,
lazima tufikirie kwa kiwango cha ubinafsi na kwa kiwango cha umma.
na kwa kiwango binafsi,
inarejelea hii wazo ya kuweka kwa taswira
na kuelewa ni nini manufaa ya chanjo
na hatari ya ugonjwa kwa kila mmoja wetu.
Kwa hivyo ikija kwa UVIKO kwa mfano,
Ningependa kuhimiza kila mkanada kufikiria kile hili janga,
limewamelifanyia,
na kile limewanyanganya.
Kwa hivyo, inaweza kuwa wengine wamepoteza wapendwa wao,
wengine wamepoteza kutangamana kwao, uwezekano wa watoto kwenda shule.
Kuna gharama kwa kila mmoja wetu
na kwa hivyo, kuna manufaa kwa kila mmoja wetu.
Halafu, itabidi sote twende kuchanjwa
ili tuonyeshe kuwa tuko kwa hili pamoja.
Halafu tunapozidi kwenda kiwango cha umma,
Ni muhimu sana kuanza kujenga uhusiano huu.
Na ni kazi ngumu kutekeleza,
kwa sababu inabidi umezingatia utata wa tabia za binadamu,
hususan kuhusu UVIKO-19.
Na taasisi zetu za afya haziwezi fanya hii pekee yao.
Sitaki hii kutokezea kama swali ya kijinga,
lakini ni vipi unajua unachofanya kimefaulu?
Kwa sababu sio wewe unayepeana chanjo, sawa?
Unafuatilia viwango vya mafanikio?
Kulingana na jinsi tunavyoitazama
ni uwezekano wa takriban asilimia 50 mpaka 60.
kuwa wagonjwa watafululiza kupokea chanjo.
baada ya kuhudhuria kliniki yetu.
na katika ulimwengu wa kusita kuchanjwa hayo ni mafanikio.
Huu umekuwa mdahalo wa kusisimua.
Dkt. Constantinescu, asante sana kwa muda wako.
nimefurahia kuwa hapa, asante kwa kunialika.