Umekua ukifunga lakini Hakuna matokeo?
Jaribu haya kuanzia leo
Wow! Mungu wangu utakua hapa na ushuhuda
NEEMA na Amani kwenu katika Jina la Yesu
Karibu katika kipindi kingine cha 'Urithi unaoishi'
Leo tunawaletea maonesho mawili kutoka kwa Nabii TB Joshua
Akiongelea Mada muhimu Sana na yenye maelekezo
Ambayo itakusaidia Maisha yako ya ukristo
Onyesho la Kwanza limechukuliwa katikati ya ibada
Na ya pili imeoneshwa katikati ya ushuhuda
Kutoka kwa binti wa Afrika ya kusini, aliepokea uponyaji
Kutoka kwenye nguvu za giza zilizo mpeleka kwenye uchawi
Na wakati Nabii TB Joshua anasikiliza ushuhuda wake
Alitumia uzoefu wa Maisha Yake kama fursa
Kufundisha watu kanuni hii muhimu
Sasa barikiwa wakati una jifunza Aina hii ya maombi
Aina ya mfungo unaovuta uelekeo wa Mungu
Hebu tuangalie
Kama hutaki shetani akutumikishe, Tafadhali fanyia kazi tabia yako
Hii ina maana kuanzia Leo, usianze kumuambia Mungu 'niponye'
Kemea udhaifu wako
Kuanzia Leo acha kusema 'Mungu nibariki'
Kemea udhaifu wako
Kuanzia Leo acha kusema 'Mungu nilinde'
Watu wananifatilia, Wanataka kuniua
Unapoteza muda wako
Nenda moja kwa moja - Kemea udhaifu wako
Hiyo ni njia anayo tumia shetani, kuingia
Kukutesa na umasikini
Kukutesa na kutojiamini
Kukutesa na magonjwa
Kukutesa na chochote unachokiongelea
Anatumia udhaifu wetu kutuingia
Ukifunga huo mlango, shetani hayupo tena
Kaka njoo, niyakusumbua Leo, sababu Hua unanisumbua
Simama hapa kaka, Tafadhali simama
Simama hapa
Huyu mtu atapita hapa Kuja kwanhi
Lakini sisi wawili tukiwa karibu Sana, Hakuna njia ya yeye kupita
Ina maana unaishi kwa ukamilfu-wingi wa maisha
Kilicho kizuri ni kufunga hiyo
Huo udhaifu
Hapa ni mlango wa udhaifu, kwa mtu huyu kupitia na kuja
Na mateso ya umasikini
Mateso ya magonjwa
Mateso ya kurudishwa nyuma - taja kila Aina ya mateso
Hapa ni Mahali pa kupita
Badala ya kusema 'Mungu niponye'
Inaleta maana yoyote kusema 'Mungu niponye?'
Kwanini usifunge njia na uwe na Maisha mazuri
Lakini tunaendelea kusema 'niponye'
Unapokua magonjwa unasema 'niponye'
Unapokua maskini unasema 'nibariki'
Unapokua tasa unasema 'nibariki na uzao'
Hapana, Mungu anajua Hali yako
Unapoanza kumuambia Mungu 'nataka kwenda kule'
Ina maanisha kusema Mungu ni kipofu
Mungu alie kuumba anakujua
Anajua pasipo Mahali Palo, anajua mawazo yako
Na wewe unamwambia 'mimi ni maskini, nibariki'
Inaleta maana?
Unasema nini Sasa? Kufanya na kutengeneza Maisha yako
Inabidi uimarishe Maisha yako
Maisha mengi yame chomolewa kutoka wa Muumbaji
Ili kuimarisha Maisha Tena, lazima tukemee udhaifu wetu
Hiki ndicho Mungu alimuambia Mtume Paul
Mara Tatu alimuambia 'niponye Nina mwiba kwenye mwili wangu'
Kila Muda Mungu alimuambia 'NEEMA yangu inakutosha'
Hii ina maana 'Ukamilifu wangu unakutosha'
Kila Muda mtume Paul alisema'niponye' Mungu alisema Neema yangu yakutosha
Ina maana tafuta Kwanza ufalme. Uponyaji, baraka, na kila kitu kitaongezwa
Mungu anatumia Paul kama mfano kwetu sote
Hatukusikia chochote baada ya Mungu kutamka Neno lile
'NEEMA yangu yakutosha
Hakuna rekodi kuhusu hiyo tena
Hatukuwahi kusikia ugonjwa huo ndio ulio muua Paul
Na Paulo aillishi umri alio ahidiwa na Mungu
Nini changamoto yako Sasa? Udhaifu
Mwambie jirani yako "changamoto yangu ni udhaifu" sio ugumu wa Maisha
Sio magonjwa. Sio masumbuko
Changamoto yangu ni udhaifu wangu
Hiyo ndio changamoto yako
Kama ungekua unaombea Hilo kwa muda
Hali yako isingebaki hivyo
Kwa ufupi, maombi yako kuanzia Leo yawe ni dhidi ya udhaifu wako
Mimi ni maskini - Mungu anajua
Naumwa--Mungu anajua
Mimi ni tasa - Mungu anajua
Changamoto yoyote uliyonayo Mungu anaijua
Sio lazima kuipa jina
Nipo hivi, nahitaji hivi
Ziba njia ambayo shetani anatumia kukutesa
Ziba njia ambayo shetani anatumia kukuumiza ambayo ni udhaifu
Anatumia udhaifu wetu kutudhuru
Anatumia madhaifu yetu kutushambulia
Anatumia madhaifu yetu kutupiga
Huo ni udhaifu, omba dhidi ya udhaifu wako
Na pale mlango huu utazimbwa, vitu vingine vitaongezeka kwako
Kitu kimoja kuhusu udhaifu
Unapofungua mdomo na kusema 'Mungu naongea sana'
Tafadhali naomba neema sitaki kuongea sana
Baada ya maombi kama mwanadamu utataka kujaribu kile ulichokiombea
Unapenda na kutaka kuanza kuongea sana
Utakumbuka kwamba uliomba dhidi yake
Kama mtu akisema TB Joshua unasemaje kuhusu hili?
Usijali - nitakuona baadae
Sababu hutaki kuongea sana
Sababu ni mjinga tu, ataomba dhidi ya udhaifu wa kuongea sana
Na baada ya maombi unaendelea kuongea sana
Unaombea Tena, Bwana sitaki kuongea sana
Kwa muda unavyo endelea kuombea dhidi yake
Unatakiwa kuanza kuishi kile unacho kiombea
Mwambie jirani yako, ishi Maisha ya maombi yako
Ambayo ni, unayoomba kwenye maombi, Anza kuyaishi
'sitaki kuongea sana'
Baada ya maombi ' Nita ishi Maisha ya kutoongea sana'
Ukitaka kufunga, mfungo inaleta jibu kutoka kwa Mungu