WEBVTT 00:00:03.634 --> 00:00:07.363 [Matayarisho: Nani huamua ninachoona mtandaoni?] 00:00:08.066 --> 00:00:09.526 Hujambo, jina langu ni Taylor. 00:00:09.526 --> 00:00:11.778 Natafiti intaneti na uandishi wa habari, 00:00:11.778 --> 00:00:16.077 na jinsi sisi kama raia tunapokea taarifa kuhusu dunia. 00:00:17.109 --> 00:00:19.628 Katika siku za zamani wakati watu walipokea taarifa, 00:00:19.728 --> 00:00:22.638 mara nyingi iliamuliwa na watu. 00:00:22.648 --> 00:00:25.551 Kulikuwa na wanadamu walioamua mambo ambayo tulihitaji kujua. 00:00:25.560 --> 00:00:28.550 Kwa hivyo tulipofungua gazeti au kutazama habari za jioni, 00:00:28.550 --> 00:00:32.570 ni mtu aliyeamua tulichosikia na kutazama. 00:00:33.240 --> 00:00:36.546 Matokeo ya hayo ni kwamba sote tulifahamu mambo yanayofanana. 00:00:38.059 --> 00:00:40.742 Sasa mtandao umebadilisha kila kitu. 00:00:41.090 --> 00:00:44.017 Unapoingia mtandaoni, unapofungua programu, 00:00:44.486 --> 00:00:47.224 unachoona hakibainishwi na mtu 00:00:47.489 --> 00:00:48.710 lakini na mashine. 00:00:49.589 --> 00:00:51.820 Na hili ni nzuri kwa njia nyingi: 00:00:51.984 --> 00:00:54.053 Inakuruhusu utumie Ramani za Google; 00:00:54.053 --> 00:00:56.523 Inakuruhusu uagize chakula mtandaoni; 00:00:56.523 --> 00:01:00.162 Inakuruhusu uwasiliane na marafiki kote duniani 00:01:00.162 --> 00:01:01.870 na kushiriki maelezo... 00:01:02.290 --> 00:01:04.911 Lakini kuna vipengele vya mashine hii 00:01:05.221 --> 00:01:07.511 ambavyo tunahitaji kufikiri kwa makini kuvihusu 00:01:07.741 --> 00:01:11.618 kwa sababu vinabainisha maelezo ambayo sote tunayapokea 00:01:11.793 --> 00:01:15.050 kama raia katika jamii na katika demokrasia. 00:01:15.489 --> 00:01:17.029 Kwa hivyo unapofungua programu 00:01:17.179 --> 00:01:20.531 na unaonyeshwa picha katika mipasho yako ya Snapchat, 00:01:20.764 --> 00:01:24.420 maelezo hayo yote hubainishwa na mashine hii, 00:01:24.465 --> 00:01:28.951 na mashine hiyo huendeshwa na marupurupu ya kampuni 00:01:28.951 --> 00:01:32.251 ambayo inamiliki tovuti au inamiliki programu. 00:01:32.684 --> 00:01:36.540 Na marupurupu hayo ni kwa ajili yako kutumia muda mwingi iwezekanavyo 00:01:36.540 --> 00:01:38.080 katika programu hiyo. 00:01:38.680 --> 00:01:42.087 Kwa hivyo wanafanya mambo yanayokufanya uhisi vizuri kuhusu kuwa hapo. 00:01:42.250 --> 00:01:44.553 Wanawaruhusu watu kupenda picha zako. 00:01:44.975 --> 00:01:47.943 Wanakuonyesha maudhui ambayo wanafikiri ungependa kuyaona 00:01:48.066 --> 00:01:50.850 yatakayokufanya ufurahie zaidi au ukasirike zaidi 00:01:50.850 --> 00:01:53.880 yatakayokufanya uwe na hisia zitakazosababisha usiondoke hapo. 00:01:53.970 --> 00:01:57.173 Hii ni kwa sababu wanataka kukuonyesha matangazo mengi iwezekanavyo 00:01:57.173 --> 00:01:58.173 ukiwa mahali pale 00:01:58.173 --> 00:02:00.160 kwa kuwa huo ndio muundo wao wa biashara. 00:02:00.897 --> 00:02:04.414 Pia wanachukua fursa hio hio ya wewe kutumia programu yao 00:02:04.414 --> 00:02:06.140 kukusanya data kukuhusu. 00:02:06.370 --> 00:02:08.005 Na wanatumia data hii 00:02:08.005 --> 00:02:11.553 kubuni wasifu wa kina wa maisha na tabia yako, 00:02:11.845 --> 00:02:13.924 na kisha wasifu hizi zinaweza kutumiwa 00:02:13.924 --> 00:02:16.930 kukuonyesha matangazo zaidi, 00:02:17.200 --> 00:02:19.700 na kisha hilo hubainisha unachoona pia. 00:02:21.470 --> 00:02:25.170 Lakini haya yote hayahusu tu muundo wa biashara wa kampuni hizi, 00:02:25.614 --> 00:02:28.277 yana athari kwa demokrasia yetu 00:02:28.735 --> 00:02:34.509 kwa sababu tunachoona mtandaoni imebadilishwa kutufaa sisi, 00:02:34.990 --> 00:02:36.183 tunachopenda 00:02:36.453 --> 00:02:37.843 tunachoamini, 00:02:38.253 --> 00:02:41.203 kwa tunachotaka kuona au kuamini. 00:02:41.523 --> 00:02:43.498 Ni hiyo inamaanisha kuwa kama jamii, 00:02:43.756 --> 00:02:47.500 sote hatupati maarifa au maelezo sawa 00:02:47.500 --> 00:02:50.197 ambayo ni ngumu kwa demokrasia inayotuhitaji 00:02:50.197 --> 00:02:52.621 tushirikiane na kujua mambo yanayofanana 00:02:52.851 --> 00:02:55.171 ili kufanya uamuzi unaohusu maisha yetu pamoja. 00:02:55.391 --> 00:02:57.030 Sote tunapojua mambo tofauti 00:02:57.030 --> 00:03:01.059 na sote tunatengwa katika vifungu vyetu vidogo vya maelezo, 00:03:01.567 --> 00:03:04.860 ni vigumu zaidi kwetu kuelewana. 00:03:04.860 --> 00:03:07.670 Hatuna hali au maarifa yanayofanana. 00:03:08.241 --> 00:03:11.335 Nafikiri ni muhimu zaidi tufikiri kwa umakini 00:03:11.545 --> 00:03:13.897 kuhusu maelezo tunayopokea mtandaoni, 00:03:14.247 --> 00:03:17.167 na kuhusu kampuni na miundo inayobainisha 00:03:17.337 --> 00:03:19.455 tunachoona mtandaoni. 00:03:21.504 --> 00:03:24.832 [NewsWise ni mradi wa CIVIX& Shirika la Uandishi wa Habari la Kanada] 00:03:24.912 --> 00:03:28.445 Manukuu yametolewa na Claudia Contreras Ukaguzi umefanywa na Carol Wang