1 00:00:03,634 --> 00:00:07,363 [Matayarisho: Nani huamua ninachoona mtandaoni?] 2 00:00:08,066 --> 00:00:09,526 Hujambo, jina langu ni Taylor. 3 00:00:09,526 --> 00:00:11,778 Natafiti intaneti na uandishi wa habari, 4 00:00:11,778 --> 00:00:16,077 na jinsi sisi kama raia tunapokea taarifa kuhusu dunia. 5 00:00:17,109 --> 00:00:19,628 Katika siku za zamani wakati watu walipokea taarifa, 6 00:00:19,728 --> 00:00:22,638 mara nyingi iliamuliwa na watu. 7 00:00:22,648 --> 00:00:25,551 Kulikuwa na wanadamu walioamua mambo ambayo tulihitaji kujua. 8 00:00:25,560 --> 00:00:28,550 Kwa hivyo tulipofungua gazeti au kutazama habari za jioni, 9 00:00:28,550 --> 00:00:32,570 ni mtu aliyeamua tulichosikia na kutazama. 10 00:00:33,240 --> 00:00:36,546 Matokeo ya hayo ni kwamba sote tulifahamu mambo yanayofanana. 11 00:00:38,059 --> 00:00:40,742 Sasa mtandao umebadilisha kila kitu. 12 00:00:41,090 --> 00:00:44,017 Unapoingia mtandaoni, unapofungua programu, 13 00:00:44,486 --> 00:00:47,224 unachoona hakibainishwi na mtu 14 00:00:47,489 --> 00:00:48,710 lakini na mashine. 15 00:00:49,589 --> 00:00:51,820 Na hili ni nzuri kwa njia nyingi: 16 00:00:51,984 --> 00:00:54,053 Inakuruhusu utumie Ramani za Google; 17 00:00:54,053 --> 00:00:56,523 Inakuruhusu uagize chakula mtandaoni; 18 00:00:56,523 --> 00:01:00,162 Inakuruhusu uwasiliane na marafiki kote duniani 19 00:01:00,162 --> 00:01:01,870 na kushiriki maelezo... 20 00:01:02,290 --> 00:01:04,911 Lakini kuna vipengele vya mashine hii 21 00:01:05,221 --> 00:01:07,511 ambavyo tunahitaji kufikiri kwa makini kuvihusu 22 00:01:07,741 --> 00:01:11,618 kwa sababu vinabainisha maelezo ambayo sote tunayapokea 23 00:01:11,793 --> 00:01:15,050 kama raia katika jamii na katika demokrasia. 24 00:01:15,489 --> 00:01:17,029 Kwa hivyo unapofungua programu 25 00:01:17,179 --> 00:01:20,531 na unaonyeshwa picha katika mipasho yako ya Snapchat, 26 00:01:20,764 --> 00:01:24,420 maelezo hayo yote hubainishwa na mashine hii, 27 00:01:24,465 --> 00:01:28,951 na mashine hiyo huendeshwa na marupurupu ya kampuni 28 00:01:28,951 --> 00:01:32,251 ambayo inamiliki tovuti au inamiliki programu. 29 00:01:32,684 --> 00:01:36,540 Na marupurupu hayo ni kwa ajili yako kutumia muda mwingi iwezekanavyo 30 00:01:36,540 --> 00:01:38,080 katika programu hiyo. 31 00:01:38,680 --> 00:01:42,087 Kwa hivyo wanafanya mambo yanayokufanya uhisi vizuri kuhusu kuwa hapo. 32 00:01:42,250 --> 00:01:44,553 Wanawaruhusu watu kupenda picha zako. 33 00:01:44,975 --> 00:01:47,943 Wanakuonyesha maudhui ambayo wanafikiri ungependa kuyaona 34 00:01:48,066 --> 00:01:50,850 yatakayokufanya ufurahie zaidi au ukasirike zaidi 35 00:01:50,850 --> 00:01:53,880 yatakayokufanya uwe na hisia zitakazosababisha usiondoke hapo. 36 00:01:53,970 --> 00:01:57,173 Hii ni kwa sababu wanataka kukuonyesha matangazo mengi iwezekanavyo 37 00:01:57,173 --> 00:01:58,173 ukiwa mahali pale 38 00:01:58,173 --> 00:02:00,160 kwa kuwa huo ndio muundo wao wa biashara. 39 00:02:00,897 --> 00:02:04,414 Pia wanachukua fursa hio hio ya wewe kutumia programu yao 40 00:02:04,414 --> 00:02:06,140 kukusanya data kukuhusu. 41 00:02:06,370 --> 00:02:08,005 Na wanatumia data hii 42 00:02:08,005 --> 00:02:11,553 kubuni wasifu wa kina wa maisha na tabia yako, 43 00:02:11,845 --> 00:02:13,924 na kisha wasifu hizi zinaweza kutumiwa 44 00:02:13,924 --> 00:02:16,930 kukuonyesha matangazo zaidi, 45 00:02:17,200 --> 00:02:19,700 na kisha hilo hubainisha unachoona pia. 46 00:02:21,470 --> 00:02:25,170 Lakini haya yote hayahusu tu muundo wa biashara wa kampuni hizi, 47 00:02:25,614 --> 00:02:28,277 yana athari kwa demokrasia yetu 48 00:02:28,735 --> 00:02:34,509 kwa sababu tunachoona mtandaoni imebadilishwa kutufaa sisi, 49 00:02:34,990 --> 00:02:36,183 tunachopenda 50 00:02:36,453 --> 00:02:37,843 tunachoamini, 51 00:02:38,253 --> 00:02:41,203 kwa tunachotaka kuona au kuamini. 52 00:02:41,523 --> 00:02:43,498 Ni hiyo inamaanisha kuwa kama jamii, 53 00:02:43,756 --> 00:02:47,500 sote hatupati maarifa au maelezo sawa 54 00:02:47,500 --> 00:02:50,197 ambayo ni ngumu kwa demokrasia inayotuhitaji 55 00:02:50,197 --> 00:02:52,621 tushirikiane na kujua mambo yanayofanana 56 00:02:52,851 --> 00:02:55,171 ili kufanya uamuzi unaohusu maisha yetu pamoja. 57 00:02:55,391 --> 00:02:57,030 Sote tunapojua mambo tofauti 58 00:02:57,030 --> 00:03:01,059 na sote tunatengwa katika vifungu vyetu vidogo vya maelezo, 59 00:03:01,567 --> 00:03:04,860 ni vigumu zaidi kwetu kuelewana. 60 00:03:04,860 --> 00:03:07,670 Hatuna hali au maarifa yanayofanana. 61 00:03:08,241 --> 00:03:11,335 Nafikiri ni muhimu zaidi tufikiri kwa umakini 62 00:03:11,545 --> 00:03:13,897 kuhusu maelezo tunayopokea mtandaoni, 63 00:03:14,247 --> 00:03:17,167 na kuhusu kampuni na miundo inayobainisha 64 00:03:17,337 --> 00:03:19,455 tunachoona mtandaoni. 65 00:03:21,504 --> 00:03:24,832 [NewsWise ni mradi wa CIVIX& Shirika la Uandishi wa Habari la Kanada] 66 00:03:24,912 --> 00:03:28,445 Manukuu yametolewa na Claudia Contreras Ukaguzi umefanywa na Carol Wang