[Matayarisho:
Nani huamua ninachoona mtandaoni?]
Hujambo, jina langu ni Taylor.
Natafiti intaneti na uandishi wa habari,
na jinsi sisi kama raia tunapokea
taarifa kuhusu dunia.
Katika siku za zamani
wakati watu walipokea taarifa,
mara nyingi iliamuliwa na watu.
Kulikuwa na wanadamu walioamua
mambo ambayo tulihitaji kujua.
Kwa hivyo tulipofungua gazeti
au kutazama habari za jioni,
ni mtu aliyeamua
tulichosikia na kutazama.
Matokeo ya hayo ni
kwamba sote tulifahamu mambo yanayofanana.
Sasa mtandao umebadilisha kila kitu.
Unapoingia mtandaoni,
unapofungua programu,
unachoona hakibainishwi na mtu
lakini na mashine.
Na hili ni nzuri kwa njia nyingi:
Inakuruhusu utumie Ramani za Google;
Inakuruhusu uagize chakula mtandaoni;
Inakuruhusu uwasiliane
na marafiki kote duniani
na kushiriki maelezo...
Lakini kuna vipengele vya mashine hii
ambavyo tunahitaji
kufikiri kwa makini kuvihusu
kwa sababu vinabainisha
maelezo ambayo sote tunayapokea
kama raia katika jamii
na katika demokrasia.
Kwa hivyo unapofungua programu
na unaonyeshwa picha
katika mipasho yako ya Snapchat,
maelezo hayo yote
hubainishwa na mashine hii,
na mashine hiyo huendeshwa
na marupurupu ya kampuni
ambayo inamiliki tovuti
au inamiliki programu.
Na marupurupu hayo ni kwa ajili yako
kutumia muda mwingi iwezekanavyo
katika programu hiyo.
Kwa hivyo wanafanya mambo yanayokufanya
uhisi vizuri kuhusu kuwa hapo.
Wanawaruhusu watu kupenda picha zako.
Wanakuonyesha maudhui
ambayo wanafikiri ungependa kuyaona
yatakayokufanya
ufurahie zaidi au ukasirike zaidi
yatakayokufanya uwe na hisia
zitakazosababisha usiondoke hapo.
Hii ni kwa sababu wanataka
kukuonyesha matangazo mengi iwezekanavyo
ukiwa mahali pale
kwa kuwa huo ndio muundo wao wa biashara.
Pia wanachukua fursa hio hio
ya wewe kutumia programu yao
kukusanya data kukuhusu.
Na wanatumia data hii
kubuni wasifu wa kina
wa maisha na tabia yako,
na kisha wasifu hizi zinaweza kutumiwa
kukuonyesha matangazo zaidi,
na kisha hilo hubainisha unachoona pia.
Lakini haya yote hayahusu tu
muundo wa biashara wa kampuni hizi,
yana athari kwa demokrasia yetu
kwa sababu tunachoona mtandaoni
imebadilishwa kutufaa sisi,
tunachopenda
tunachoamini,
kwa tunachotaka kuona au kuamini.
Ni hiyo inamaanisha kuwa kama jamii,
sote hatupati maarifa au maelezo sawa
ambayo ni ngumu kwa demokrasia
inayotuhitaji
tushirikiane na kujua mambo yanayofanana
ili kufanya uamuzi
unaohusu maisha yetu pamoja.
Sote tunapojua mambo tofauti
na sote tunatengwa katika
vifungu vyetu vidogo vya maelezo,
ni vigumu zaidi kwetu kuelewana.
Hatuna hali au maarifa yanayofanana.
Nafikiri ni muhimu zaidi
tufikiri kwa umakini
kuhusu maelezo tunayopokea mtandaoni,
na kuhusu kampuni
na miundo inayobainisha
tunachoona mtandaoni.
[NewsWise ni mradi wa CIVIX&
Shirika la Uandishi wa Habari la Kanada]
Manukuu yametolewa na Claudia Contreras
Ukaguzi umefanywa na Carol Wang