[Matayarisho: Nani huamua ninachoona mtandaoni?] Hujambo, jina langu ni Taylor. Natafiti intaneti na uandishi wa habari, na jinsi sisi kama raia tunapokea taarifa kuhusu dunia. Katika siku za zamani wakati watu walipokea taarifa, mara nyingi iliamuliwa na watu. Kuna wanadamu ambao waliamua mambo ambayo tulihitaji kujua. Kwa hivyo tulipofungua gazeti au kutazama habari za jioni, ni mtu aliyeamua tulichosikia na kutazama. Matokeo ya hayo ni kwambo sote tulifahamu mambo yanayofanana. Sasa mtandao umebadilisha kila kitu. Unapoingia mtandaoni, unapofungua programu, unachoona hakibainishwi na mtu lakini na mashine. Na hili ni nzuri kwa njia nyingi: Inakuruhusu utumie Ramani za Google; Inakuruhusu uagize chakula mtandaoni; Inakuruhusu uwasiliane na marafiki kote duniani na kushiriki maelezo... Lakini kuna vipengele vya mashine hii ambavyo tunahitaji kufikiri kwa makini kuvihusu kwa sababu vinabainisha maelezo ambayo sote tunayapokea kama raia katika jamii na katika demokrasia. Kwa hivyo unapofungua programu na unaonyeshwa picha katika mipasho yako ya Snapchat, maelezo hayo yote yamebainisha na mashine hii, na mashine hiyo inaendeshwa na marupurupu ya kampuni ambayo inamiliki tovuti au inamiliki programu. Na marupurupu hayo ni kwa ajili yako kutumia mara nyingi uwezavyo katika programu hiyo. Kwa hivyo wanafanya mambo yanayokufanya uhisi vizuri kuhusu kuwa hapo. Wanaruhusu watu kupenda picha zako. Wanakuonyesha maudhui ambayo wanafikiri ungependa kuyaona ambayo huenda yatakufanya ufurahie zaidi au ukasirike zaidi ambayo yatasababisha msukumo wa hisia kutoka kwako ili usiondoke hapo. Hii ni kwa sababu wanataka kukuonyesha matangazo mengi zaidi iwezekanavyo ukiwa mahali pale kwa kuwa huo ndio muundo wao wa biashara. Pia wanachukua fursa hio hio ya wewe kutumia programu yao kukusanya data kukuhusu. Na wanatumia data hii kubuni wasifu wa kina wa maisha na tabia yako, na kisha wasifu hizi zinaweza kutumiwa kukuonyesha matangazo zaidi, na kisha hilo hubainisha unachoona pia. Lakini haya yote hayahusu tu muundo wa biashara wa kampuni hizi, ina athari kwa demokrasia yetu kwa sababu tunachoona mtandaoni imebadilishwa kutufaa sisi, tunachopenda tunachoamini, kwa tunachotaka kuona au kuamini. Ni hiyo inamaanisha kuwa kama jamii, sote hatupati maarifa au maelezo sawa ambayo ni ngumu kwa demokrasia inayotuhitaji tufanye kazi kwa pamoja na kufahamu mambo yanayofanana ili kufanya uamuzi unaohusu maisha yetu pamoja. Sote tunapojua mambo tofauti na sote tunatengwa katika vifungu vyetu vidogo vya maelezo, ni vigumu kwetu kuelewana. Hatuna hali au maarifa yanayofanana. Nafikiri ni muhimu zaidi tufikiri kwa umakini kuhusu maelezo tunayopokea mtandaoni, na kuhusu kampuni na miundo inayobainisha tunachoona mtandoani. [NewsWise ni mradi wa CIVIX& Shirika la Uandishi wa Habari la Kanada] Manukuu yametolewa na Claudia Contreras Ukaguzi umefanywa na Carol Wang