[Script Info] Title: [Events] Format: Layer, Start, End, Style, Name, MarginL, MarginR, MarginV, Effect, Text Dialogue: 0,0:00:03.63,0:00:07.36,Default,,0000,0000,0000,,[Matayarisho:\NNani huamua ninachoona mtandaoni?] Dialogue: 0,0:00:08.38,0:00:09.53,Default,,0000,0000,0000,,Hujambo, jina langu ni Taylor. Dialogue: 0,0:00:09.53,0:00:11.78,Default,,0000,0000,0000,,Natafiti intaneti na uandishi wa habari, Dialogue: 0,0:00:11.78,0:00:16.08,Default,,0000,0000,0000,,na jinsi sisi kama raia tunapokea taarifa kuhusu dunia. Dialogue: 0,0:00:17.39,0:00:19.63,Default,,0000,0000,0000,,Katika siku za zamani wakati watu walipokea taarifa, Dialogue: 0,0:00:19.78,0:00:22.69,Default,,0000,0000,0000,,mara nyingi iliamuliwa na watu. Dialogue: 0,0:00:22.69,0:00:25.38,Default,,0000,0000,0000,,Kuna wanadamu ambao waliamua mambo ambayo tulihitaji kujua. Dialogue: 0,0:00:25.56,0:00:28.55,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hivyo tulipofungua gazeti au kutazama habari za jioni, Dialogue: 0,0:00:28.55,0:00:32.57,Default,,0000,0000,0000,,ni mtu aliyeamua tulichosikia na kutazama. Dialogue: 0,0:00:33.24,0:00:36.55,Default,,0000,0000,0000,,Matokeo ya hayo ni kwambo sote tulifahamu mambo yanayofanana. Dialogue: 0,0:00:38.06,0:00:40.74,Default,,0000,0000,0000,,Sasa mtandao umebadilisha kila kitu. Dialogue: 0,0:00:41.09,0:00:44.02,Default,,0000,0000,0000,,Unapoingia mtandaoni, unapofungua programu, Dialogue: 0,0:00:44.49,0:00:47.22,Default,,0000,0000,0000,,unachoona hakibainishwi na mtu Dialogue: 0,0:00:47.49,0:00:48.71,Default,,0000,0000,0000,,lakini na mashine. Dialogue: 0,0:00:49.59,0:00:51.82,Default,,0000,0000,0000,,Na hili ni nzuri kwa njia nyingi: Dialogue: 0,0:00:51.98,0:00:54.05,Default,,0000,0000,0000,,Inakuruhusu utumie Ramani za Google; Dialogue: 0,0:00:54.05,0:00:56.52,Default,,0000,0000,0000,,Inakuruhusu uagize chakula mtandaoni; Dialogue: 0,0:00:56.52,0:01:00.16,Default,,0000,0000,0000,,Inakuruhusu uwasiliane na marafiki kote duniani Dialogue: 0,0:01:00.16,0:01:01.87,Default,,0000,0000,0000,,na kushiriki maelezo... Dialogue: 0,0:01:02.29,0:01:04.91,Default,,0000,0000,0000,,Lakini kuna vipengele vya mashine hii Dialogue: 0,0:01:05.22,0:01:07.51,Default,,0000,0000,0000,,ambavyo tunahitaji kufikiri kwa makini kuvihusu Dialogue: 0,0:01:07.74,0:01:11.62,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu vinabainisha maelezo ambayo sote tunayapokea Dialogue: 0,0:01:11.79,0:01:15.05,Default,,0000,0000,0000,,kama raia katika jamii na katika demokrasia. Dialogue: 0,0:01:15.49,0:01:17.03,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hivyo unapofungua programu Dialogue: 0,0:01:17.18,0:01:20.53,Default,,0000,0000,0000,,na unaonyeshwa picha katika mipasho yako ya Snapchat, Dialogue: 0,0:01:20.76,0:01:24.42,Default,,0000,0000,0000,,maelezo hayo yote yamebainisha na mashine hii, Dialogue: 0,0:01:24.46,0:01:28.95,Default,,0000,0000,0000,,na mashine hiyo inaendeshwa na marupurupu ya kampuni Dialogue: 0,0:01:28.95,0:01:32.25,Default,,0000,0000,0000,,ambayo inamiliki tovuti au inamiliki programu. Dialogue: 0,0:01:32.68,0:01:36.54,Default,,0000,0000,0000,,Na marupurupu hayo ni kwa ajili yako kutumia mara nyingi uwezavyo Dialogue: 0,0:01:36.54,0:01:38.08,Default,,0000,0000,0000,,katika programu hiyo. Dialogue: 0,0:01:38.68,0:01:42.09,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hivyo wanafanya mambo yanayokufanya uhisi vizuri kuhusu kuwa hapo. Dialogue: 0,0:01:42.25,0:01:44.55,Default,,0000,0000,0000,,Wanaruhusu watu kupenda picha zako. Dialogue: 0,0:01:44.98,0:01:47.94,Default,,0000,0000,0000,,Wanakuonyesha maudhui ambayo wanafikiri ungependa kuyaona Dialogue: 0,0:01:48.07,0:01:50.85,Default,,0000,0000,0000,,ambayo huenda yatakufanya ufurahie zaidi au ukasirike zaidi Dialogue: 0,0:01:50.85,0:01:53.88,Default,,0000,0000,0000,,ambayo yatasababisha msukumo wa hisia kutoka kwako ili usiondoke hapo. Dialogue: 0,0:01:54.26,0:01:57.17,Default,,0000,0000,0000,,Hii ni kwa sababu wanataka kukuonyesha matangazo mengi zaidi iwezekanavyo Dialogue: 0,0:01:57.17,0:01:58.17,Default,,0000,0000,0000,,ukiwa mahali pale Dialogue: 0,0:01:58.17,0:02:00.16,Default,,0000,0000,0000,,kwa kuwa huo ndio muundo wao wa biashara. Dialogue: 0,0:02:00.90,0:02:04.41,Default,,0000,0000,0000,,Pia wanachukua fursa hio hio ya wewe kutumia programu yao Dialogue: 0,0:02:04.41,0:02:06.14,Default,,0000,0000,0000,,kukusanya data kukuhusu. Dialogue: 0,0:02:06.37,0:02:08.00,Default,,0000,0000,0000,,Na wanatumia data hii Dialogue: 0,0:02:08.00,0:02:11.55,Default,,0000,0000,0000,,kubuni wasifu wa kina wa maisha na tabia yako, Dialogue: 0,0:02:11.84,0:02:13.92,Default,,0000,0000,0000,,na kisha wasifu hizi zinaweza kutumiwa Dialogue: 0,0:02:13.92,0:02:16.93,Default,,0000,0000,0000,,kukuonyesha matangazo zaidi, Dialogue: 0,0:02:17.20,0:02:19.70,Default,,0000,0000,0000,,na kisha hilo hubainisha unachoona pia. Dialogue: 0,0:02:21.47,0:02:25.17,Default,,0000,0000,0000,,Lakini haya yote hayahusu tu muundo wa biashara wa kampuni hizi, Dialogue: 0,0:02:25.61,0:02:28.28,Default,,0000,0000,0000,,ina athari kwa demokrasia yetu Dialogue: 0,0:02:28.74,0:02:34.51,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu tunachoona mtandaoni imebadilishwa kutufaa sisi, Dialogue: 0,0:02:34.99,0:02:36.18,Default,,0000,0000,0000,,tunachopenda Dialogue: 0,0:02:36.45,0:02:37.84,Default,,0000,0000,0000,,tunachoamini, Dialogue: 0,0:02:38.25,0:02:41.20,Default,,0000,0000,0000,,kwa tunachotaka kuona au kuamini. Dialogue: 0,0:02:41.52,0:02:43.50,Default,,0000,0000,0000,,Ni hiyo inamaanisha kuwa kama jamii, Dialogue: 0,0:02:43.76,0:02:47.50,Default,,0000,0000,0000,,sote hatupati maarifa au maelezo sawa Dialogue: 0,0:02:47.50,0:02:50.20,Default,,0000,0000,0000,,ambayo ni ngumu kwa demokrasia inayotuhitaji Dialogue: 0,0:02:50.20,0:02:52.62,Default,,0000,0000,0000,,tufanye kazi kwa pamoja na kufahamu mambo yanayofanana Dialogue: 0,0:02:52.85,0:02:55.17,Default,,0000,0000,0000,,ili kufanya uamuzi unaohusu maisha yetu pamoja. Dialogue: 0,0:02:55.39,0:02:57.03,Default,,0000,0000,0000,,Sote tunapojua mambo tofauti Dialogue: 0,0:02:57.03,0:03:01.06,Default,,0000,0000,0000,,na sote tunatengwa katika vifungu vyetu vidogo vya maelezo, Dialogue: 0,0:03:01.57,0:03:04.86,Default,,0000,0000,0000,,ni vigumu kwetu kuelewana. Dialogue: 0,0:03:04.86,0:03:07.67,Default,,0000,0000,0000,,Hatuna hali au maarifa yanayofanana. Dialogue: 0,0:03:08.24,0:03:11.34,Default,,0000,0000,0000,,Nafikiri ni muhimu zaidi tufikiri kwa umakini Dialogue: 0,0:03:11.54,0:03:13.90,Default,,0000,0000,0000,,kuhusu maelezo tunayopokea mtandaoni, Dialogue: 0,0:03:14.25,0:03:17.17,Default,,0000,0000,0000,,na kuhusu kampuni na miundo inayobainisha Dialogue: 0,0:03:17.34,0:03:19.46,Default,,0000,0000,0000,,tunachoona mtandoani. Dialogue: 0,0:03:21.50,0:03:24.70,Default,,0000,0000,0000,,[NewsWise ni mradi wa CIVIX& Shirika la Uandishi wa Habari la Kanada] Dialogue: 0,0:03:25.17,0:03:27.60,Default,,0000,0000,0000,,Manukuu yametolewa na Claudia Contreras\NUkaguzi umefanywa na Carol Wang