0:00:03.634,0:00:07.363 [Matayarisho:[br]Nani huamua ninachoona mtandaoni?] 0:00:08.376,0:00:09.526 Hujambo, jina langu ni Taylor. 0:00:09.526,0:00:11.778 Natafiti intaneti na uandishi wa habari, 0:00:11.778,0:00:16.077 na jinsi sisi kama raia tunapokea taarifa kuhusu dunia. 0:00:17.389,0:00:19.628 Katika siku za zamani wakati watu walipokea taarifa, 0:00:19.778,0:00:22.688 mara nyingi iliamuliwa na watu. 0:00:22.688,0:00:25.381 Kuna wanadamu ambao waliamua mambo ambayo tulihitaji kujua. 0:00:25.560,0:00:28.550 Kwa hivyo tulipofungua gazeti au kutazama habari za jioni, 0:00:28.550,0:00:32.570 ni mtu aliyeamua tulichosikia na kutazama. 0:00:33.240,0:00:36.546 Matokeo ya hayo ni kwambo sote tulifahamu mambo yanayofanana. 0:00:38.059,0:00:40.742 Sasa mtandao umebadilisha kila kitu. 0:00:41.090,0:00:44.017 Unapoingia mtandaoni, unapofungua programu, 0:00:44.486,0:00:47.224 unachoona hakibainishwi na mtu 0:00:47.489,0:00:48.710 lakini na mashine. 0:00:49.589,0:00:51.820 Na hili ni nzuri kwa njia nyingi: 0:00:51.984,0:00:54.053 Inakuruhusu utumie Ramani za Google; 0:00:54.053,0:00:56.523 Inakuruhusu uagize chakula mtandaoni; 0:00:56.523,0:01:00.162 Inakuruhusu uwasiliane na marafiki kote duniani 0:01:00.162,0:01:01.870 na kushiriki maelezo... 0:01:02.290,0:01:04.911 Lakini kuna vipengele vya mashine hii 0:01:05.221,0:01:07.511 ambavyo tunahitaji kufikiri kwa makini kuvihusu 0:01:07.741,0:01:11.618 kwa sababu vinabainisha maelezo ambayo sote tunayapokea 0:01:11.793,0:01:15.050 kama raia katika jamii na katika demokrasia. 0:01:15.489,0:01:17.029 Kwa hivyo unapofungua programu 0:01:17.179,0:01:20.531 na unaonyeshwa picha katika mipasho yako ya Snapchat, 0:01:20.764,0:01:24.420 maelezo hayo yote yamebainisha na mashine hii, 0:01:24.465,0:01:28.951 na mashine hiyo inaendeshwa na marupurupu ya kampuni 0:01:28.951,0:01:32.251 ambayo inamiliki tovuti au inamiliki programu. 0:01:32.684,0:01:36.540 Na marupurupu hayo ni kwa ajili yako kutumia mara nyingi uwezavyo 0:01:36.540,0:01:38.080 katika programu hiyo. 0:01:38.680,0:01:42.087 Kwa hivyo wanafanya mambo yanayokufanya uhisi vizuri kuhusu kuwa hapo. 0:01:42.250,0:01:44.553 Wanaruhusu watu kupenda picha zako. 0:01:44.975,0:01:47.943 Wanakuonyesha maudhui ambayo wanafikiri ungependa kuyaona 0:01:48.066,0:01:50.850 ambayo huenda yatakufanya ufurahie zaidi au ukasirike zaidi 0:01:50.850,0:01:53.880 ambayo yatasababisha msukumo wa hisia kutoka kwako ili usiondoke hapo. 0:01:54.260,0:01:57.173 Hii ni kwa sababu wanataka kukuonyesha matangazo mengi zaidi iwezekanavyo 0:01:57.173,0:01:58.173 ukiwa mahali pale 0:01:58.173,0:02:00.160 kwa kuwa huo ndio muundo wao wa biashara. 0:02:00.897,0:02:04.414 Pia wanachukua fursa hio hio ya wewe kutumia programu yao 0:02:04.414,0:02:06.140 kukusanya data kukuhusu. 0:02:06.370,0:02:08.005 Na wanatumia data hii 0:02:08.005,0:02:11.553 kubuni wasifu wa kina wa maisha na tabia yako, 0:02:11.845,0:02:13.924 na kisha wasifu hizi zinaweza kutumiwa 0:02:13.924,0:02:16.930 kukuonyesha matangazo zaidi, 0:02:17.200,0:02:19.700 na kisha hilo hubainisha unachoona pia. 0:02:21.470,0:02:25.170 Lakini haya yote hayahusu tu muundo wa biashara wa kampuni hizi, 0:02:25.614,0:02:28.277 ina athari kwa demokrasia yetu 0:02:28.735,0:02:34.509 kwa sababu tunachoona mtandaoni imebadilishwa kutufaa sisi, 0:02:34.990,0:02:36.183 tunachopenda 0:02:36.453,0:02:37.843 tunachoamini, 0:02:38.253,0:02:41.203 kwa tunachotaka kuona au kuamini. 0:02:41.523,0:02:43.498 Ni hiyo inamaanisha kuwa kama jamii, 0:02:43.756,0:02:47.500 sote hatupati maarifa au maelezo sawa 0:02:47.500,0:02:50.197 ambayo ni ngumu kwa demokrasia inayotuhitaji 0:02:50.197,0:02:52.621 tufanye kazi kwa pamoja na kufahamu mambo yanayofanana 0:02:52.851,0:02:55.171 ili kufanya uamuzi unaohusu maisha yetu pamoja. 0:02:55.391,0:02:57.030 Sote tunapojua mambo tofauti 0:02:57.030,0:03:01.059 na sote tunatengwa katika vifungu vyetu vidogo vya maelezo, 0:03:01.567,0:03:04.860 ni vigumu kwetu kuelewana. 0:03:04.860,0:03:07.670 Hatuna hali au maarifa yanayofanana. 0:03:08.241,0:03:11.335 Nafikiri ni muhimu zaidi tufikiri kwa umakini 0:03:11.545,0:03:13.897 kuhusu maelezo tunayopokea mtandaoni, 0:03:14.247,0:03:17.167 na kuhusu kampuni na miundo inayobainisha 0:03:17.337,0:03:19.455 tunachoona mtandoani. 0:03:21.504,0:03:24.702 [NewsWise ni mradi wa CIVIX& Shirika la Uandishi wa Habari la Kanada] 0:03:25.172,0:03:27.595 Manukuu yametolewa na Claudia Contreras[br]Ukaguzi umefanywa na Carol Wang