[Matayarisho:
Nani huamua ninachoona mtandaoni?]
Hujambo, jina langu ni Taylor.
Natafiti intaneti na uandishi wa habari,
na jinsi sisi kama raia tunapokea taarifa kuhusu dunia.
Katika siku za zamani wakati watu walipokea taarifa,
mara nyingi iliamuliwa na watu.
Kuna wanadamu ambao waliamua mambo ambayo tulihitaji kujua.
Kwa hivyo tulipofungua gazeti au kutazama habari za jioni,
ni mtu aliyeamua tulichosikia na kutazama.
Matokeo ya hayo ni kwambo sote tulifahamu mambo yanayofanana.
Sasa mtandao umebadilisha kila kitu.
Unapoingia mtandaoni, unapofungua programu,
unachoona hakibainishwi na mtu
lakini na mashine.
Na hili ni nzuri kwa njia nyingi:
Inakuruhusu utumie Ramani za Google;
Inakuruhusu uagize chakula mtandaoni;
Inakuruhusu uwasiliane na marafiki kote duniani
na kushiriki maelezo...
Lakini kuna vipengele vya mashine hii
ambavyo tunahitaji kufikiri kwa makini kuvihusu
kwa sababu vinabainisha maelezo ambayo sote tunayapokea
kama raia katika jamii na katika demokrasia.
Kwa hivyo unapofungua programu
na unaonyeshwa picha katika mipasho yako ya Snapchat,
maelezo hayo yote yamebainisha na mashine hii,
na mashine hiyo inaendeshwa na marupurupu ya kampuni
ambayo inamiliki tovuti au inamiliki programu.
Na marupurupu hayo ni kwa ajili yako kutumia mara nyingi uwezavyo
katika programu hiyo.
Kwa hivyo wanafanya mambo yanayokufanya uhisi vizuri kuhusu kuwa hapo.
Wanaruhusu watu kupenda picha zako.
Wanakuonyesha maudhui ambayo wanafikiri ungependa kuyaona
ambayo huenda yatakufanya ufurahie zaidi au ukasirike zaidi
ambayo yatasababisha msukumo wa hisia kutoka kwako ili usiondoke hapo.
Hii ni kwa sababu wanataka kukuonyesha matangazo mengi zaidi iwezekanavyo
ukiwa mahali pale
kwa kuwa huo ndio muundo wao wa biashara.
Pia wanachukua fursa hio hio ya wewe kutumia programu yao
kukusanya data kukuhusu.
Na wanatumia data hii
kubuni wasifu wa kina wa maisha na tabia yako,
na kisha wasifu hizi zinaweza kutumiwa
kukuonyesha matangazo zaidi,
na kisha hilo hubainisha unachoona pia.
Lakini haya yote hayahusu tu muundo wa biashara wa kampuni hizi,
ina athari kwa demokrasia yetu
kwa sababu tunachoona mtandaoni imebadilishwa kutufaa sisi,
tunachopenda
tunachoamini,
kwa tunachotaka kuona au kuamini.
Ni hiyo inamaanisha kuwa kama jamii,
sote hatupati maarifa au maelezo sawa
ambayo ni ngumu kwa demokrasia inayotuhitaji
tufanye kazi kwa pamoja na kufahamu mambo yanayofanana
ili kufanya uamuzi unaohusu maisha yetu pamoja.
Sote tunapojua mambo tofauti
na sote tunatengwa katika vifungu vyetu vidogo vya maelezo,
ni vigumu kwetu kuelewana.
Hatuna hali au maarifa yanayofanana.
Nafikiri ni muhimu zaidi tufikiri kwa umakini
kuhusu maelezo tunayopokea mtandaoni,
na kuhusu kampuni na miundo inayobainisha
tunachoona mtandoani.
[NewsWise ni mradi wa CIVIX& Shirika la Uandishi wa Habari la Kanada]
Manukuu yametolewa na Claudia Contreras
Ukaguzi umefanywa na Carol Wang