Wakati manabii na walimu wa kanisa la mwanzo
wakifunga na kusali,
Roho Mtakatifu aliwaita Paulo na Barnaba
kwenda kwenye safari yao ya kwanza ya kimisionari.
Kanisa lilisali pamoja
kabla yakuwatuma.
Mikono iliwekwa juu yao,
na tulisali kwa unyenyekevu.
Kama kanisa lenye ushikamano,
tuliomba kwa ajili ya usalama wao
na kwamba Mungu angewapa
maneno sahihi
ya kuongea kwa umati.
Tuliomba wamisionari wetu
wangefanikiwa
kusambaza injili.
Paulo na Barnaba walisafiri
sehemu mbalimbali.
Ndani Cyprus, walitangaza neno
la Mungu katika masinagogu ya Wayahudi.
Ndani ya Posiaidoni Antioki
Karibia mji mzima ulikusanyika
kusikiliza neno la Bwana.
Pindi mataifa mengine waliposikia
ujumbe wao, waliamini.
Neno la Bwana lilitangazwa
sehemu zote,
na wafuasi walijazwa
na furaha na Roho Mtakatifu.
Paulo na Barnaba
walichagua viongozi katika kila kanisa
na walisali pamoja na kufunga
wakiwasifu kwa Mungu.
Walikusanya kanisa pamoja
na kuripoti
yote Mungu aliyofanya
kupitia wao
na jinsi gani alifungua mlango
wa imani kwa wasioamini.