Ilikuwa kipindi cha pasaka, na tulikuwa katika chumba cha juu Yerusalemu. Tulikuwa tunasali kwa pamoja. Tulikuwa tunasali kwa majuto makubwa na unyenyekevu, na tulikuwa tunatubu dhambi zetu. Tulikuwa tunatafuta maono ya Bwana, nguvu, na Roho Mtakatifu. Kulikuwa na hisia za nguvu ya umoja wakati tukisali pamoja kwa bidii. Ghfla kulikuwa na sauti ya upepo mkali iliyojaa chumba kizima tulipokaa. Kisha ndimi za moto zilishuka chini na huu moto ukakaa kwa watu. Watu wote kwenye chumba walijazwa na Roho Mtakatifu. Sasa, kumbuka kwamba katika kipindi cha pasaka watu walitoka nchi tofauti kuabudu, na sasa, ghafla walisikia injili katika lugha zao. Matokeo ya hii, watu 3,000 waliongezwa kwenye waamini ndani ya siku moja. Watu walijitoa kwa mafundisho ya mtume na urafiki- kuvunja mkate na kwa sala. Kila siku walikutana pamoja katika mahakama ya hekalu. Majumbani kwao, walikata mkate na kula pamoja, na namba ya waliookolewa iliongezeka kila siku.