Tuone kama tunaweza kuandika 0.15 kama sehemu. Kitu cha muhimu hapa ni kuangalia nafasi ipi tarakimu izi zipo. Kwa hiyo hii 1 hapa, iko kwenye sehemu ya makumi, unaweza kuiona kama 1 mara 1/10. Hii 5 hapa ipo kwenye sehemu ya mamia, unaweza kuiona kama 5 mara 1/100. Kama nitaiandika hii , nitaandika kama jumla ya -- hii 1 inawakilisha 1 mara 1/10, kwa hiyo kimsingi itakuwa 1/10 jumlisha na hii 5 inawakilisha5 mara 100, hivyo itakuwa jumlisha 5/100. Na kama tunataka kuzijumlisha, tunataka kupata viasili vyenye kufanana. Asili zenye kufanana ni 100. 10 zote na --kigawe kidogo cha ushirika. 100 ni kigawe cha 10 na 100. Hivyo tunaweza kuandika hii kama kitu juu ya 100 jumlisha kitu juu ya 100. Hii haibadilika. Hii ilishakuwa 5/100. Kama tukizidisha asili hapa kwa 10-- hiki ndo tunachokifanya; tunazidisha kwa 10-- baadae tutatakiwa tuzidishe hii asili kwa 10. Na hii ni sawa na 10/100. Na hapa tushajumlisha. Hii ni sawa na 10 jumlisha 5 ni 15/100. Na unatakiwa kufanya hii haraka kidogo kwa kutambua hii. Unaweza sema, angalia, nafasi yangu ndogo hapa ni kwenye sehemu ya mamia. Badala ya kuiita hii 1/10, nitaiita hii 10/100. Au ninaweza kusema hii yote ni 15/100. Na kama nataka kupunguza hii kwenye kiwango cha chini, tutapata ngoja tuone, zote kiasi na asili zinagawanyika kwa 5. Hivyo ngoja tugawanye zote kwa 5. Kwa hiyo kiasi , 15 gawanya kwa 5, ni 3. Asili, 100 gawanya kwa 5, ni 20. Na hii inahusu kurahisisha kadri tutakavyopata.