Mifumo ya kuishi imekuwa kwa mabilioni chache ya miaka. na itakuwa kwa miaka nyinginezo. Katika ulimwengu wa kuishi, hakuna mfumo wa kuzoa taka. Badala yake, vifaa vinayeyuka. Taka ya aina moja ni chakula ya aina nyingine; jua hupeana kawi; vitu vinamea, halafu hufa; na virutubisho hurudi salama mchangani. Na inatendeka. Ila kama binadamu, tumekubali mtazamo finyu; tunachukua, tunaunda, na hatimaye tunatupa. Simu mpya inatokea. Kwa hivyo tunatupilia mbali ile zee. Mashine yetu ya kufulia nguo inaharibika. Kwa hivyo tunanunua mpya. Kila wakati tunapofanya hivi tunapora raslimali isiyo na mwisho na mara si haba tunazalisha taka zenye sumu. Haiwezi kutendeka kwa muda mrefu. Kwa hivyo ni nini inaweza? Tukikubali mfumo mzunguko wa ulimwengu wa kuishi unafanya kazi, je tunaweza badili jinsi tunavyofikiri ndio tuweze kufanya kazi kwa uchumi mzunguko? Hebu tuanze na mzunguko wa kibayolojia. Taka zetu zinawezaje kujenga mtaji badala ya kuipunguza? Kwa kufikiria upya na kubuni upya bidhaa na vijenzi na vifurushi vyao, tunawezaunda vifaa salama na vinayoweza kuwa mbolea na kuwezesha kumea kwa mimea. Na jinsi wanavyoseama filamuni, "Hakuna raslimali iliyopotea katika kuunda kifaa hiki." Vipi kuhusu mashine za kufulia nguo, simu za rununu na majokofu? Tunajua ya kuwa hayayeyuki kuwa mbolea. Hapa tunazungumza kuhusu dhana nyingine: jinsi ya kuzungusha vyuma vyenye thamani, Mapolima na maaloi, ndio yawezeke kudumisha ubora na kuendelea kutumika baada ya muda wa ununuzi wa bidhaa binafsi. Yamkini bidhaa za leo ziwe raslimali za kesho? Ina mantiki ya kibiashara. Badala ya itikadi ya tupa na badilisha ambayo tumekuja kuzoea, tunaweza twaa ile ya rudisha na ufanye upya. pale ambapo bidhaa na vijenzi vimeundwa kutenganishwa na kufanywa upwa. Suluhisho moja inaweza kuwa kufikiria upya taswira yetu ya umiliki. Ingekuwaje kama hatungekuwa wamiki halisi wa teknolojia zetu? Tunazipa leseni kutoka kwa waundaji. Sasa, hebu tuunganishe mizunguko hii mbili pamoja. Tafakari kama tungeweza kubuni bidhaa kurudia watengenezaji wao, vifaa vyao vya kiteknolojia vikitumika tena, na vijenzi vyao vya kibiyolojia vikiongeza ubora wa kilimo Na tafakari kuwa hivi bidhaa vinatengenezwa na kusafirishwa kutumia nishati mbadala. Hapa tuna modeli inayojenga ustawi kwa muda mrefu. Na habari njema ni kuwa tiyari kuna makampuni ambazo zinaanza kukubali jinsi hii ya utendakazi Lakini uchumi mzunguko siyo ya muundaji mmoja kubadlisha bidhaa moja. Ni ya kuunganisha makampuni ambazo zipo katika muundomsingi na uchumi kuungana. Ni kuhusu kawi. Ni kuhusu kufikiria upya mfumo mwenyewe wa kufanya kazi. Tupo na nafasi mwafaka kufungua taswira na upeo upya. Badala ya kubakia kunaswa na kufadhaishwa kwa sasa, na ubunifu na uvumbuzi, tunaweza kihakika kufikiria upya na kubuni upya kesho yetu.