WEBVTT 00:00:01.760 --> 00:00:04.656 Napenda kujifunza lugha za kigeni. 00:00:04.680 --> 00:00:08.736 napenda sana kiasi kwamba hujifunza lugha mpya kila baada ya miaka miwili, 00:00:08.760 --> 00:00:10.856 sasa hivi najifunza lugha ya nane. 00:00:10.880 --> 00:00:13.496 Pale watu wanapogundua kuhusu mimi, mara huniuliza, 00:00:13.520 --> 00:00:15.616 "Unafanyaje hivyo? Siri yako ni ipi?" 00:00:15.640 --> 00:00:18.656 Na niwe muwazi, kwa miaka mingi, jibu langu litakuwa, 00:00:18.680 --> 00:00:21.000 "Sifahamu. Napenda tu kujifunza lugha." 00:00:21.720 --> 00:00:23.976 Lakini watu hawakufurahishwa na jibu hilo. 00:00:24.000 --> 00:00:27.976 Walitaka kufahamu kwanini wanatumia miaka kujaribu kuijfunza hata lugha moja, 00:00:28.000 --> 00:00:29.536 kamwe hawafanikiwa unenaji, 00:00:29.560 --> 00:00:32.616 na mimi natokea, nikijifunza lugha moja baada ya nyingine. 00:00:32.640 --> 00:00:34.856 Walitaka kujua siri ya wanaisimu, 00:00:34.880 --> 00:00:36.600 watu wanaoongea lugha nyingi. 00:00:37.400 --> 00:00:38.816 Na hii ilinifanya kushangaa, pia, 00:00:38.840 --> 00:00:41.136 wanaisimu wengine wanafanyaje? 00:00:41.160 --> 00:00:42.656 Kitu gani tulichonacho? 00:00:42.680 --> 00:00:44.616 Na kipi ambacho kinatuwezesha sisi 00:00:44.640 --> 00:00:47.080 kujifunza lugha kwa haraka kuliko watu wengine? 00:00:47.880 --> 00:00:50.720 Niliamua kukutana na watu wengine kama mimi ili kutambua. NOTE Paragraph 00:00:51.760 --> 00:00:53.816 Sehemu nzuri ya kuonana na wanaisimu wengi 00:00:53.840 --> 00:00:56.136 ni katika hafla ambapo mamia ya wapenzi wa lugha 00:00:56.160 --> 00:00:59.016 hukutana pamoja. 00:00:59.040 --> 00:01:02.336 Kuna baadhi ya hafla za wanaisimu ambazo huandaliwa duniani kote, 00:01:02.360 --> 00:01:03.736 na kwa hiyo niliamua kwenda huko 00:01:03.760 --> 00:01:06.200 na kuwauliza wanaisimu kuhusu njia wanazotumia. NOTE Paragraph 00:01:07.200 --> 00:01:09.136 Nilikutana na Benny kutoka Ireland, 00:01:09.160 --> 00:01:13.320 ambaye aliniambia kwamba njia yake ni kuanza kuongea kuanzia siku ya kwanza. 00:01:14.240 --> 00:01:17.136 Hujifunza misemo michache kutoka katika kitabu cha misemo cha wasafiri 00:01:17.160 --> 00:01:18.736 na huenda kukutana na wenyeji wa lugha husika 00:01:18.760 --> 00:01:21.576 na kuanza maongezi nao moja kwa moja. 00:01:21.600 --> 00:01:24.376 Hajali kukosea kuongea hata mara 200 kwa siku, 00:01:24.400 --> 00:01:26.840 kwa sababu hivyo ndivyo anajifunza, ukilinganisha na mrejesho. 00:01:27.480 --> 00:01:30.616 Na kilicho bora ni kwamba, haitaji kusafiri sana leo, 00:01:30.640 --> 00:01:33.576 Sababu kwa urahisi unaweza fanya maongezi na wenyeji wa lugha 00:01:33.600 --> 00:01:36.296 ukiwa umepumzika katika chumba chako, ukitumia tovuti. NOTE Paragraph 00:01:36.320 --> 00:01:38.096 Nilikutana pia na Lucas kutoka Brazil 00:01:38.120 --> 00:01:40.600 ambaye alikuwa na njia ya kuvutia ya kujifunza Kirussia. 00:01:41.200 --> 00:01:46.856 Kiurahisi aliwaalika waongeaji wa lugha ya Kirussia wapatao 100 kama marafiki katika mtandao wake wa Skype, 00:01:46.880 --> 00:01:50.776 na kisha alianza kupiga soga na mmoja wao 00:01:50.800 --> 00:01:52.240 na akaandika "Habari" kwa Kirussia. 00:01:53.000 --> 00:01:55.576 Yule mtu alijibu," Nzuri, hujambo?" 00:01:55.600 --> 00:02:00.056 Lucas alinakili haya maongezi na kuweka katika chumba cha maandishi alipoanza soga na mtu mwingine, 00:02:00.080 --> 00:02:03.656 na mtu alijibu. "Nipo salama, asante, na wewe hujambo?" 00:02:03.680 --> 00:02:06.656 Lucas alinakili tena na kuweka katika soga na mtu wa kwanza, 00:02:06.680 --> 00:02:10.136 na katika njia hii, aliwafanya watu wawili wasiojuana kuwa katika maongezi 00:02:10.160 --> 00:02:11.576 bila kufahamu hilo. NOTE Paragraph 00:02:11.600 --> 00:02:12.856 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:02:12.880 --> 00:02:14.776 Si punde alianza kuchapa maneno mwenyewe, 00:02:14.800 --> 00:02:16.936 kwa sababu alikuwa na maongezi kama haya mengi 00:02:16.960 --> 00:02:19.976 kwamba aligundua jinsi gani maongezi ya Kirussia ambavyo kwa kawaida huanza. 00:02:20.000 --> 00:02:22.336 Njia yenye werevu sana, si ndiyo? NOTE Paragraph 00:02:22.360 --> 00:02:26.856 Na kisha nilikutana na mwanaisimu ambaye muda wote huanza kwa kuigiza sauti za lugha, 00:02:26.880 --> 00:02:31.296 na wengine ambao amara zote hujifunza maneno 500 ya mara kwa mara katika lugha, 00:02:31.320 --> 00:02:34.720 na wengine ambao huanza kwa kusoma kitabu cha sarufi. 00:02:35.600 --> 00:02:37.896 Kama ningeuliza wanaisimu mbalimbali mia moja, 00:02:37.920 --> 00:02:41.536 Nilisikia namna mia moja mbalimbali za kujifunza lugha. 00:02:41.560 --> 00:02:45.176 Kila mtu alikuwa na njia tofauti ya kujifunza lugha, 00:02:45.200 --> 00:02:49.080 na wote mwishoni huja na matokeo sawa ya kuongea lugha baadhi kwa ufasaha. NOTE Paragraph 00:02:50.120 --> 00:02:54.416 Na nilikuwa nawasikiliza wanaisimu hawa wakinieleza kuhusu njia zao, 00:02:54.440 --> 00:02:56.736 ghafla ikaniamsha: 00:02:56.760 --> 00:02:59.896 kitu kimoja ambacho wote tunacho 00:02:59.920 --> 00:03:05.456 ni kwamba tumeweza kutafuta namna ya kufurahia mchakato ya kujifunza lugha. 00:03:05.480 --> 00:03:08.256 Na hawa wanaisimu wote walikuwa wanaongelea kuhusu kujifunza lugha 00:03:08.280 --> 00:03:09.536 na ilikuwa inafurahisha sana. 00:03:09.560 --> 00:03:11.136 Ungewaona nyuso zao 00:03:11.160 --> 00:03:13.776 walipokuwa wakinionyesha chati za rangi zikielezea sarufi 00:03:13.800 --> 00:03:16.296 na kadi za maneno zilizotengenezwa kwa uangalifu, 00:03:16.320 --> 00:03:19.336 na takwimu zao kuhusu kujifunza maneno ya lugha kwa kutumia programu ya simu janja, 00:03:19.360 --> 00:03:23.560 au wanavyopenda kupika kutokana na maelezo ya upishi yaliyoandikwa katika lugha ya kigeni. 00:03:24.680 --> 00:03:26.416 Wote wanatumia njia mbalimbali, 00:03:26.440 --> 00:03:30.216 Lakini wanahakikisha ni kitu ambacho binafsi wanapendelea kufanya. NOTE Paragraph 00:03:30.240 --> 00:03:34.136 Nimegundua kwamba hivi ndivyo mimi hujifunza lugha. 00:03:34.160 --> 00:03:37.736 Nilipokuwa najifunza Kispanyola, nilichoshwa na maandishi katika kitabu. 00:03:37.760 --> 00:03:39.496 Namaanisha, nani ambaye anataka kusoma kuhusu Jose 00:03:39.520 --> 00:03:42.656 akiuliza kuhusu uelekeo wa kwenda kituo gari moshi. Sawa? 00:03:42.680 --> 00:03:45.016 Nilitaka kusoma "Harry Porter" badala yake, 00:03:45.040 --> 00:03:47.176 kwa sababu ndicho kilikuwa kitabu nikipendacho sana nikiwa mdogo, 00:03:47.200 --> 00:03:48.856 na nimekisoma mara nyingi. 00:03:48.880 --> 00:03:52.496 Kwa hiyo nilipata tafsiri "Harry Porter" katika lugha ya Kispanyola na nikaanza kusoma, 00:03:52.520 --> 00:03:55.856 na kwa uhakika, sikuelewa chochote kile mwanzoni, 00:03:55.880 --> 00:03:58.096 lakini niliendelea kusoma kwa sababu nilikipenda kitabu, 00:03:58.120 --> 00:04:02.256 na mwishoni mwa kitabu, niliweza kukifatilia bila matatizo yoyote. 00:04:02.280 --> 00:04:04.896 Na jambo sawa lilitokea wakati nikijifunza Kijerumani. 00:04:04.920 --> 00:04:08.216 Niliamua kuangalia "Marafiki," ucheshi ninaopendelea, kwa Kijerumani, 00:04:08.240 --> 00:04:11.336 na tena, mwanzoni ilikuwa upuuzi tu. 00:04:11.360 --> 00:04:14.536 Sikuelewa ni wapi neno moja limeishia na lingine lilipoanzia, 00:04:14.560 --> 00:04:17.216 lakini niliendelea kuangalia kila siku kwa sababu ilikuwa ni "Marafiki." 00:04:17.240 --> 00:04:19.616 Naweza kuangalia katika lugha yoyote. Napenda sana. 00:04:19.640 --> 00:04:21.656 Na baada sehemu ya pili au ya tatu, 00:04:21.680 --> 00:04:24.040 kiukweli, maongezi yalianza kuleta maana. NOTE Paragraph 00:04:25.080 --> 00:04:28.136 Nilitambua hili baada ya kukutana na wanaisimu wengine. 00:04:28.160 --> 00:04:29.736 Sisi si wenye talanta 00:04:29.760 --> 00:04:32.176 na hatuna njia za kukatiza katika kujifunza lugha. 00:04:32.200 --> 00:04:36.016 Tumeweza kutafuta njia ya kufurahia mchakato, 00:04:36.040 --> 00:04:39.416 namna ya kubadili usomaji wa lugha kutoka kama somo la shule lisilofurahisha 00:04:39.440 --> 00:04:42.640 hadi katika shughuli ya kuvutia ambayo hutaona shida kuifanya kila siku. 00:04:43.520 --> 00:04:45.696 Kama hupendelei kuandika maneno kwenye karatasi, 00:04:45.720 --> 00:04:47.416 unaweza mara zote kuyachapa kwenye programu ya simu. 00:04:47.440 --> 00:04:50.256 Kama hupendelei kusikiliza vitabu vinavyochosha, 00:04:50.280 --> 00:04:54.576 tafuta video zinazovutia katika Youtube au katika vipindi vya lugha. 00:04:54.600 --> 00:04:56.296 Kama wewe ni mtu unayependelea upekee 00:04:56.320 --> 00:04:59.336 na hauwezi kuwaza ni namna gani utaweza ongea na wenyeji wa lugha moja kwa moja, 00:04:59.360 --> 00:05:01.696 unaweza kujifunza kujiongelesha mwenyewe. 00:05:01.720 --> 00:05:04.296 Unaweza kuongea na nafsi yako ukiwa katika chumba chako, 00:05:04.320 --> 00:05:07.216 ukieleza mipango yako ya mwisho wa wiki, siku yako ilikwendaje, 00:05:07.240 --> 00:05:09.376 au hata kupiga picha zisizo na mpangilio katika simu yako 00:05:09.400 --> 00:05:13.136 na kuelezea kuhusu picha hiyo kwa rafiki yako wa kufikirika. 00:05:13.160 --> 00:05:15.656 Hivi ndivyo wanaisimu hujifunza lugha, 00:05:15.680 --> 00:05:18.536 na habari njema ni kwamba, inapatikana kwa mtu yoyote 00:05:18.560 --> 00:05:21.240 nani ambaye yuko tayari kujifunza katika mikono yake. NOTE Paragraph 00:05:22.520 --> 00:05:24.616 Hivyo kukutana na wanaisimu wengine kulinisaidia kutambua 00:05:24.640 --> 00:05:27.656 kwamba ni muhimu sana kupata burudani 00:05:27.680 --> 00:05:29.776 katika mchakato wa kujifunza lugha, 00:05:29.800 --> 00:05:32.840 lakini pia furaha yenyewe pekee haitoshi. 00:05:33.680 --> 00:05:36.416 Kama unataka kuweza kufikia ufasaha katika lugha ya kigeni, 00:05:36.440 --> 00:05:38.920 utahitajika kutumia kanuni tatu zaidi. NOTE Paragraph 00:05:39.760 --> 00:05:42.360 Kwanza, unahitaji njia zilizo bora. 00:05:43.160 --> 00:05:46.576 Ukijaribu kukumbuka listi ya maneno kwa ajili ya mtihani wa kesho, 00:05:46.600 --> 00:05:48.976 maneno yatahifadhiwa katika kumbukumbu yako ya muda mfupi 00:05:49.000 --> 00:05:50.905 na utayasahau baada ya siku chache. 00:05:51.400 --> 00:05:54.336 Kama, hata hivyo, unataka kukaa na maneno kwa muda mrefu, 00:05:54.360 --> 00:05:57.296 unahitaji kuyarudia katika kipindi cha siku chache 00:05:57.320 --> 00:05:59.536 ukifanya kitu kinachofahamika kama kurudia kwa nafasi. 00:05:59.560 --> 00:06:03.816 Unaweza kutumia programu za simu ambazo zinatumia mfumo huu kama vile Anki au Memrise, 00:06:03.840 --> 00:06:07.176 au unaweza kuandika orodha ya neno katika kijitabu ukitumia njia ya Goldlist, 00:06:07.200 --> 00:06:09.896 ambayo ni maarufu kwa wanaisimu wengi. 00:06:09.920 --> 00:06:13.656 Kama huna uhakika ni njia ipi inayofaa na kipi kinachopatikana, 00:06:13.680 --> 00:06:16.696 angalia chaneli za Youtube na tovuti za wanaisimu 00:06:16.720 --> 00:06:18.496 kupata hamasa kutoka kwao. 00:06:18.520 --> 00:06:21.440 Kama inawafaa wao, lazima itakufaa na wewe pia. NOTE Paragraph 00:06:22.840 --> 00:06:24.816 Kanuni ya tatu ya kufuata 00:06:24.840 --> 00:06:27.000 ni kutengeneza mfumo katika kujifunza kwako. 00:06:27.720 --> 00:06:31.936 Wote tupo bize na hakuna aliye na muda wa kujifunza lugha mpya leo. 00:06:31.960 --> 00:06:35.736 Lakini tunaweza pata muda kama tukipanga mbele kidogo. 00:06:35.760 --> 00:06:39.176 Unaweza kuamka dakika kumi na tano mapema kabla ya muda wa kawaida wa kuamka? 00:06:39.200 --> 00:06:42.496 Huo utakuwa muda mzuri wa kuweza kupitia baadhi ya maneno. 00:06:42.520 --> 00:06:46.256 Unaweza sikiliza kipindi ukiwa unarudi nyumbani wakati unaendesha? 00:06:46.280 --> 00:06:49.736 Sasa, hiyo itakuwa nzuri kupata uzoefu wa kusikiliza. 00:06:49.760 --> 00:06:53.216 Kuna vitu vingi tunaweza fanya bila hata ya kupanga muda wa ziada, 00:06:53.240 --> 00:06:55.896 kama vile kusikiliza kipindi ukiwa unaelekea kazini, 00:06:55.920 --> 00:06:57.576 au wakati unafanya kazi za nyumbani. 00:06:57.600 --> 00:07:00.896 Kitu muhimu ni kutengeneza mpango katika kujifunza. 00:07:00.920 --> 00:07:03.416 "Nitajifunza kuongea kila Jumanne na Alhamisi 00:07:03.440 --> 00:07:05.496 na rafiki kwa dakika 20. 00:07:05.520 --> 00:07:09.936 Nitasikiliza video katika Youtube wakati nikipata kifungua kinywa." 00:07:09.960 --> 00:07:12.096 Kama utatengeneza mfumo katika kujifunza, 00:07:12.120 --> 00:07:14.016 huna haja ya kutafuta muda wa ziada, 00:07:14.040 --> 00:07:16.480 kwa sababu itakuwa namna ya maisha yako ya kila siku. NOTE Paragraph 00:07:17.880 --> 00:07:21.096 Na mwisho, kama unataka kujifunza lugha kwa ufasaha, 00:07:21.120 --> 00:07:23.840 unahitaji kuwa na subira kidogo. 00:07:24.600 --> 00:07:27.336 Haiwezekani kujifunza lugha ndani ya miezi miwili, 00:07:27.360 --> 00:07:31.256 lakini inawezekana kabisa kufanya mabadiliko yanayoonekana katika miezi miwili, 00:07:31.280 --> 00:07:35.016 kama utajifunza katika kiasi kidogo kidogo kila siku katika namna ambayo unafurahia. 00:07:35.040 --> 00:07:37.176 Na hakuna kitu ambacho kinatuhamasisha zaidi 00:07:37.200 --> 00:07:38.440 ya mafanikio yetu. NOTE Paragraph 00:07:39.120 --> 00:07:41.016 Nakumbuka vizuri wakati 00:07:41.040 --> 00:07:44.720 nilipoelewa utani wa kwanza kwa Kijerumani nilipokuwa naangalia "Marafiki." 00:07:45.280 --> 00:07:47.136 Nilifurahia sana na kuhamasika 00:07:47.160 --> 00:07:50.176 kwamba niliendelea kuangalia sehemu mbili zaidi siku hiyo, 00:07:50.200 --> 00:07:51.936 na nilivyoendelea kuangalia, 00:07:51.960 --> 00:07:56.176 Niliendelea kuelewa zaidi, ushindi huu mdogo, 00:07:56.200 --> 00:07:59.656 na hatua kwa hatua, nilifika katika hatua ambapo ningetumia lugha 00:07:59.680 --> 00:08:02.536 kwa uhuru na ufasaha kuweza kuelezea chochote. 00:08:02.560 --> 00:08:04.080 Hii ni hisia ya kusisimua. 00:08:04.800 --> 00:08:06.496 Siwezi tosheka na hisia hiyo, 00:08:06.520 --> 00:08:09.336 na ndiyo maana najifunza lugha mpya kila miaka miwili. NOTE Paragraph 00:08:09.360 --> 00:08:11.416 Kwa hiyo ndiyo siri nzima ya mwanaisimu. 00:08:11.440 --> 00:08:14.296 Tafuta njia madhubuti ambayo unaweza kuitumia kwa mfumo 00:08:14.320 --> 00:08:17.616 katika kipindi cha muda fulani katika njia ambayo unafurahia, 00:08:17.640 --> 00:08:21.520 na hivi ndivyo wanaisimu hujifunza lugha ndani ya miezi, na siyo miaka. NOTE Paragraph 00:08:23.160 --> 00:08:24.776 Sasa, baadhi yenu mnaweza kuwaza, 00:08:24.800 --> 00:08:27.136 "Ni vizuri sana kufurahia kujifunza lugha, 00:08:27.160 --> 00:08:29.696 lakini si kwamba nyinyi wanaisimu 00:08:29.720 --> 00:08:32.320 mna talanta sana na wengi wetu hatuna hiyo talanta?" NOTE Paragraph 00:08:33.320 --> 00:08:36.400 Hivyo, kuna kitu kimoja sijawaambia kuhusu Benny na Lucas. 00:08:37.159 --> 00:08:42.976 Benny alikuwa na miaka 11 ya kiselti cha Kiyalandi na miaka mitano ya lugha ya Kijerumani shuleni. 00:08:43.000 --> 00:08:46.216 Hakuweza kuongea baada ya kuhitimu masomo. 00:08:46.240 --> 00:08:50.416 Mpaka miaka 21, aliwaza kwamba hakuwa na jeni ya lugha 00:08:50.440 --> 00:08:52.856 na hakuweza kuongea lugha nyingine. 00:08:52.880 --> 00:08:55.816 Kisha akaanza kutafuta njia yake ya kujifunza lugha, 00:08:55.840 --> 00:08:59.696 ambapo ilikuwa ni kuongea na wenyeji wa lugha na kupata mrejesho kutoka kwao, 00:08:59.720 --> 00:09:03.680 na leo Benny anaweza kwa urahisi kufanya maongezi katika lugha 10. 00:09:05.120 --> 00:09:08.416 Lucas amejaribu kujifunza Kiingereza shuleni kwa miaka 10. 00:09:08.440 --> 00:09:11.056 Alikuwa ni moja ya wanafunzi wanaofanya vibaya darasani. 00:09:11.080 --> 00:09:12.696 Rafiki zake walikuwa wakimtania 00:09:12.720 --> 00:09:15.336 na kumpa kitabu cha Kirussia kama utani 00:09:15.360 --> 00:09:19.096 kwa sababu waliamini hawezi kamwe kujifunza lugha hiyo, au lugha yoyote. 00:09:19.120 --> 00:09:21.496 Na kisha Lucas akaanza kufanya majaribio na njia yake, 00:09:21.520 --> 00:09:23.320 akitafuta njia yake ya kujifunza, 00:09:24.520 --> 00:09:28.696 kwa mfano, kwa kupiga soga na watu asiowajua katika Skype. 00:09:28.720 --> 00:09:30.536 Na katika miaka 10, 00:09:30.560 --> 00:09:33.880 Lucas anaweza kuongea lugha 11 kwa ufasaha. NOTE Paragraph 00:09:35.000 --> 00:09:36.560 Je hiyo inaonekana kama miujiza? 00:09:37.440 --> 00:09:40.040 Sasa, ninaona miujiza kama hii kila siku. 00:09:40.760 --> 00:09:42.096 Na kama mshauri wa lugha, 00:09:42.120 --> 00:09:44.536 Nasaidia watu kujifunza lugha wenyewe, 00:09:44.560 --> 00:09:45.856 na naona hili kila siku. 00:09:45.880 --> 00:09:50.056 Watu hupata shida kujifunza lugha kwa miaka mitano, kumi, hata ishirini, 00:09:50.080 --> 00:09:53.936 na ghafla huchukua hatua ya kujifunza mikononi mwao, 00:09:53.960 --> 00:09:57.256 kuanza kutumia makala wanazofurahia, njia madhubuti zaidi, 00:09:57.280 --> 00:09:59.096 au wanaanza kufatilia kujifunza kwao 00:09:59.120 --> 00:10:02.056 kwamba wanaweza kuridhika na maendeleo yao, 00:10:02.080 --> 00:10:04.016 na hapo ndipo ghafla 00:10:04.040 --> 00:10:08.240 kwa maajabu wanatambua kipaji cha lugha ambacho walikuwa wanakosa maisha yao yote. NOTE Paragraph 00:10:09.480 --> 00:10:11.656 Kwa hiyo kama umejaribu pia kujifunza lugha 00:10:11.680 --> 00:10:14.096 na ukakata tamaa, 00:10:14.120 --> 00:10:16.376 na kama huna kipaji cha lugha, 00:10:16.400 --> 00:10:17.936 jaribu tena. 00:10:17.960 --> 00:10:20.816 Labda upo karibu kidogo na njia moja ya kuburudika 00:10:20.840 --> 00:10:22.602 ili kujifunza lugha hiyo kwa ufasaha. 00:10:22.960 --> 00:10:26.896 Labda upo karibu kuja kuwa mwanaisimu. NOTE Paragraph 00:10:26.920 --> 00:10:28.136 Asante. NOTE Paragraph 00:10:28.160 --> 00:10:32.360 (Makofi)