1 00:00:01,760 --> 00:00:04,656 Napenda kujifunza lugha za kigeni. 2 00:00:04,680 --> 00:00:08,736 napenda sana kiasi kwamba hujifunza lugha mpya kila baada ya miaka miwili, 3 00:00:08,760 --> 00:00:10,856 sasa hivi najifunza lugha ya nane. 4 00:00:10,880 --> 00:00:13,496 Pale watu wanapogundua kuhusu mimi, mara huniuliza, 5 00:00:13,520 --> 00:00:15,616 "Unafanyaje hivyo? Siri yako ni ipi?" 6 00:00:15,640 --> 00:00:18,656 Na niwe muwazi, kwa miaka mingi, jibu langu litakuwa, 7 00:00:18,680 --> 00:00:21,000 "Sifahamu. Napenda tu kujifunza lugha." 8 00:00:21,720 --> 00:00:23,976 Lakini watu hawakufurahishwa na jibu hilo. 9 00:00:24,000 --> 00:00:27,976 Walitaka kufahamu kwanini wanatumia miaka kujaribu kuijfunza hata lugha moja, 10 00:00:28,000 --> 00:00:29,536 kamwe hawafanikiwa unenaji, 11 00:00:29,560 --> 00:00:32,616 na mimi natokea, nikijifunza lugha moja baada ya nyingine. 12 00:00:32,640 --> 00:00:34,856 Walitaka kujua siri ya wanaisimu, 13 00:00:34,880 --> 00:00:36,600 watu wanaoongea lugha nyingi. 14 00:00:37,400 --> 00:00:38,816 Na hii ilinifanya kushangaa, pia, 15 00:00:38,840 --> 00:00:41,136 wanaisimu wengine wanafanyaje? 16 00:00:41,160 --> 00:00:42,656 Kitu gani tulichonacho? 17 00:00:42,680 --> 00:00:44,616 Na kipi ambacho kinatuwezesha sisi 18 00:00:44,640 --> 00:00:47,080 kujifunza lugha kwa haraka kuliko watu wengine? 19 00:00:47,880 --> 00:00:50,720 Niliamua kukutana na watu wengine kama mimi ili kutambua. 20 00:00:51,760 --> 00:00:53,816 Sehemu nzuri ya kuonana na wanaisimu wengi 21 00:00:53,840 --> 00:00:56,136 ni katika hafla ambapo mamia ya wapenzi wa lugha 22 00:00:56,160 --> 00:00:59,016 hukutana pamoja. 23 00:00:59,040 --> 00:01:02,336 Kuna baadhi ya hafla za wanaisimu ambazo huandaliwa duniani kote, 24 00:01:02,360 --> 00:01:03,736 na kwa hiyo niliamua kwenda huko 25 00:01:03,760 --> 00:01:06,200 na kuwauliza wanaisimu kuhusu njia wanazotumia. 26 00:01:07,200 --> 00:01:09,136 Nilikutana na Benny kutoka Ireland, 27 00:01:09,160 --> 00:01:13,320 ambaye aliniambia kwamba njia yake ni kuanza kuongea kuanzia siku ya kwanza. 28 00:01:14,240 --> 00:01:17,136 Hujifunza misemo michache kutoka katika kitabu cha misemo cha wasafiri 29 00:01:17,160 --> 00:01:18,736 na huenda kukutana na wenyeji wa lugha husika 30 00:01:18,760 --> 00:01:21,576 na kuanza maongezi nao moja kwa moja. 31 00:01:21,600 --> 00:01:24,376 Hajali kukosea kuongea hata mara 200 kwa siku, 32 00:01:24,400 --> 00:01:26,840 kwa sababu hivyo ndivyo anajifunza, ukilinganisha na mrejesho. 33 00:01:27,480 --> 00:01:30,616 Na kilicho bora ni kwamba, haitaji kusafiri sana leo, 34 00:01:30,640 --> 00:01:33,576 Sababu kwa urahisi unaweza fanya maongezi na wenyeji wa lugha 35 00:01:33,600 --> 00:01:36,296 ukiwa umepumzika katika chumba chako, ukitumia tovuti. 36 00:01:36,320 --> 00:01:38,096 Nilikutana pia na Lucas kutoka Brazil 37 00:01:38,120 --> 00:01:40,600 ambaye alikuwa na njia ya kuvutia ya kujifunza Kirussia. 38 00:01:41,200 --> 00:01:46,856 Kiurahisi aliwaalika waongeaji wa lugha ya Kirussia wapatao 100 kama marafiki katika mtandao wake wa Skype, 39 00:01:46,880 --> 00:01:50,776 na kisha alianza kupiga soga na mmoja wao 40 00:01:50,800 --> 00:01:52,240 na akaandika "Habari" kwa Kirussia. 41 00:01:53,000 --> 00:01:55,576 Yule mtu alijibu," Nzuri, hujambo?" 42 00:01:55,600 --> 00:02:00,056 Lucas alinakili haya maongezi na kuweka katika chumba cha maandishi alipoanza soga na mtu mwingine, 43 00:02:00,080 --> 00:02:03,656 na mtu alijibu. "Nipo salama, asante, na wewe hujambo?" 44 00:02:03,680 --> 00:02:06,656 Lucas alinakili tena na kuweka katika soga na mtu wa kwanza, 45 00:02:06,680 --> 00:02:10,136 na katika njia hii, aliwafanya watu wawili wasiojuana kuwa katika maongezi 46 00:02:10,160 --> 00:02:11,576 bila kufahamu hilo. 47 00:02:11,600 --> 00:02:12,856 (Kicheko) 48 00:02:12,880 --> 00:02:14,776 Si punde alianza kuchapa maneno mwenyewe, 49 00:02:14,800 --> 00:02:16,936 kwa sababu alikuwa na maongezi kama haya mengi 50 00:02:16,960 --> 00:02:19,976 kwamba aligundua jinsi gani maongezi ya Kirussia ambavyo kwa kawaida huanza. 51 00:02:20,000 --> 00:02:22,336 Njia yenye werevu sana, si ndiyo? 52 00:02:22,360 --> 00:02:26,856 Na kisha nilikutana na mwanaisimu ambaye muda wote huanza kwa kuigiza sauti za lugha, 53 00:02:26,880 --> 00:02:31,296 na wengine ambao amara zote hujifunza maneno 500 ya mara kwa mara katika lugha, 54 00:02:31,320 --> 00:02:34,720 na wengine ambao huanza kwa kusoma kitabu cha sarufi. 55 00:02:35,600 --> 00:02:37,896 Kama ningeuliza wanaisimu mbalimbali mia moja, 56 00:02:37,920 --> 00:02:41,536 Nilisikia namna mia moja mbalimbali za kujifunza lugha. 57 00:02:41,560 --> 00:02:45,176 Kila mtu alikuwa na njia tofauti ya kujifunza lugha, 58 00:02:45,200 --> 00:02:49,080 na wote mwishoni huja na matokeo sawa ya kuongea lugha baadhi kwa ufasaha. 59 00:02:50,120 --> 00:02:54,416 Na nilikuwa nawasikiliza wanaisimu hawa wakinieleza kuhusu njia zao, 60 00:02:54,440 --> 00:02:56,736 ghafla ikaniamsha: 61 00:02:56,760 --> 00:02:59,896 kitu kimoja ambacho wote tunacho 62 00:02:59,920 --> 00:03:05,456 ni kwamba tumeweza kutafuta namna ya kufurahia mchakato ya kujifunza lugha. 63 00:03:05,480 --> 00:03:08,256 Na hawa wanaisimu wote walikuwa wanaongelea kuhusu kujifunza lugha 64 00:03:08,280 --> 00:03:09,536 na ilikuwa inafurahisha sana. 65 00:03:09,560 --> 00:03:11,136 Ungewaona nyuso zao 66 00:03:11,160 --> 00:03:13,776 walipokuwa wakinionyesha chati za rangi zikielezea sarufi 67 00:03:13,800 --> 00:03:16,296 na kadi za maneno zilizotengenezwa kwa uangalifu, 68 00:03:16,320 --> 00:03:19,336 na takwimu zao kuhusu kujifunza maneno ya lugha kwa kutumia programu ya simu janja, 69 00:03:19,360 --> 00:03:23,560 au wanavyopenda kupika kutokana na maelezo ya upishi yaliyoandikwa katika lugha ya kigeni. 70 00:03:24,680 --> 00:03:26,416 Wote wanatumia njia mbalimbali, 71 00:03:26,440 --> 00:03:30,216 Lakini wanahakikisha ni kitu ambacho binafsi wanapendelea kufanya. 72 00:03:30,240 --> 00:03:34,136 Nimegundua kwamba hivi ndivyo mimi hujifunza lugha. 73 00:03:34,160 --> 00:03:37,736 Nilipokuwa najifunza Kispanyola, nilichoshwa na maandishi katika kitabu. 74 00:03:37,760 --> 00:03:39,496 Namaanisha, nani ambaye anataka kusoma kuhusu Jose 75 00:03:39,520 --> 00:03:42,656 akiuliza kuhusu uelekeo wa kwenda kituo gari moshi. Sawa? 76 00:03:42,680 --> 00:03:45,016 Nilitaka kusoma "Harry Porter" badala yake, 77 00:03:45,040 --> 00:03:47,176 kwa sababu ndicho kilikuwa kitabu nikipendacho sana nikiwa mdogo, 78 00:03:47,200 --> 00:03:48,856 na nimekisoma mara nyingi. 79 00:03:48,880 --> 00:03:52,496 Kwa hiyo nilipata tafsiri "Harry Porter" katika lugha ya Kispanyola na nikaanza kusoma, 80 00:03:52,520 --> 00:03:55,856 na kwa uhakika, sikuelewa chochote kile mwanzoni, 81 00:03:55,880 --> 00:03:58,096 lakini niliendelea kusoma kwa sababu nilikipenda kitabu, 82 00:03:58,120 --> 00:04:02,256 na mwishoni mwa kitabu, niliweza kukifatilia bila matatizo yoyote. 83 00:04:02,280 --> 00:04:04,896 Na jambo sawa lilitokea wakati nikijifunza Kijerumani. 84 00:04:04,920 --> 00:04:08,216 Niliamua kuangalia "Marafiki," ucheshi ninaopendelea, kwa Kijerumani, 85 00:04:08,240 --> 00:04:11,336 na tena, mwanzoni ilikuwa upuuzi tu. 86 00:04:11,360 --> 00:04:14,536 Sikuelewa ni wapi neno moja limeishia na lingine lilipoanzia, 87 00:04:14,560 --> 00:04:17,216 lakini niliendelea kuangalia kila siku kwa sababu ilikuwa ni "Marafiki." 88 00:04:17,240 --> 00:04:19,616 Naweza kuangalia katika lugha yoyote. Napenda sana. 89 00:04:19,640 --> 00:04:21,656 Na baada sehemu ya pili au ya tatu, 90 00:04:21,680 --> 00:04:24,040 kiukweli, maongezi yalianza kuleta maana. 91 00:04:25,080 --> 00:04:28,136 Nilitambua hili baada ya kukutana na wanaisimu wengine. 92 00:04:28,160 --> 00:04:29,736 Sisi si wenye talanta 93 00:04:29,760 --> 00:04:32,176 na hatuna njia za kukatiza katika kujifunza lugha. 94 00:04:32,200 --> 00:04:36,016 Tumeweza kutafuta njia ya kufurahia mchakato, 95 00:04:36,040 --> 00:04:39,416 namna ya kubadili usomaji wa lugha kutoka kama somo la shule lisilofurahisha 96 00:04:39,440 --> 00:04:42,640 hadi katika shughuli ya kuvutia ambayo hutaona shida kuifanya kila siku. 97 00:04:43,520 --> 00:04:45,696 Kama hupendelei kuandika maneno kwenye karatasi, 98 00:04:45,720 --> 00:04:47,416 unaweza mara zote kuyachapa kwenye programu ya simu. 99 00:04:47,440 --> 00:04:50,256 Kama hupendelei kusikiliza vitabu vinavyochosha, 100 00:04:50,280 --> 00:04:54,576 tafuta video zinazovutia katika Youtube au katika vipindi vya lugha. 101 00:04:54,600 --> 00:04:56,296 Kama wewe ni mtu unayependelea upekee 102 00:04:56,320 --> 00:04:59,336 na hauwezi kuwaza ni namna gani utaweza ongea na wenyeji wa lugha moja kwa moja, 103 00:04:59,360 --> 00:05:01,696 unaweza kujifunza kujiongelesha mwenyewe. 104 00:05:01,720 --> 00:05:04,296 Unaweza kuongea na nafsi yako ukiwa katika chumba chako, 105 00:05:04,320 --> 00:05:07,216 ukieleza mipango yako ya mwisho wa wiki, siku yako ilikwendaje, 106 00:05:07,240 --> 00:05:09,376 au hata kupiga picha zisizo na mpangilio katika simu yako 107 00:05:09,400 --> 00:05:13,136 na kuelezea kuhusu picha hiyo kwa rafiki yako wa kufikirika. 108 00:05:13,160 --> 00:05:15,656 Hivi ndivyo wanaisimu hujifunza lugha, 109 00:05:15,680 --> 00:05:18,536 na habari njema ni kwamba, inapatikana kwa mtu yoyote 110 00:05:18,560 --> 00:05:21,240 nani ambaye yuko tayari kujifunza katika mikono yake. 111 00:05:22,520 --> 00:05:24,616 Hivyo kukutana na wanaisimu wengine kulinisaidia kutambua 112 00:05:24,640 --> 00:05:27,656 kwamba ni muhimu sana kupata burudani 113 00:05:27,680 --> 00:05:29,776 katika mchakato wa kujifunza lugha, 114 00:05:29,800 --> 00:05:32,840 lakini pia furaha yenyewe pekee haitoshi. 115 00:05:33,680 --> 00:05:36,416 Kama unataka kuweza kufikia ufasaha katika lugha ya kigeni, 116 00:05:36,440 --> 00:05:38,920 utahitajika kutumia kanuni tatu zaidi. 117 00:05:39,760 --> 00:05:42,360 Kwanza, unahitaji njia zilizo bora. 118 00:05:43,160 --> 00:05:46,576 Ukijaribu kukumbuka listi ya maneno kwa ajili ya mtihani wa kesho, 119 00:05:46,600 --> 00:05:48,976 maneno yatahifadhiwa katika kumbukumbu yako ya muda mfupi 120 00:05:49,000 --> 00:05:50,905 na utayasahau baada ya siku chache. 121 00:05:51,400 --> 00:05:54,336 Kama, hata hivyo, unataka kukaa na maneno kwa muda mrefu, 122 00:05:54,360 --> 00:05:57,296 unahitaji kuyarudia katika kipindi cha siku chache 123 00:05:57,320 --> 00:05:59,536 ukifanya kitu kinachofahamika kama kurudia kwa nafasi. 124 00:05:59,560 --> 00:06:03,816 Unaweza kutumia programu za simu ambazo zinatumia mfumo huu kama vile Anki au Memrise, 125 00:06:03,840 --> 00:06:07,176 au unaweza kuandika orodha ya neno katika kijitabu ukitumia njia ya Goldlist, 126 00:06:07,200 --> 00:06:09,896 ambayo ni maarufu kwa wanaisimu wengi. 127 00:06:09,920 --> 00:06:13,656 Kama huna uhakika ni njia ipi inayofaa na kipi kinachopatikana, 128 00:06:13,680 --> 00:06:16,696 angalia chaneli za Youtube na tovuti za wanaisimu 129 00:06:16,720 --> 00:06:18,496 kupata hamasa kutoka kwao. 130 00:06:18,520 --> 00:06:21,440 Kama inawafaa wao, lazima itakufaa na wewe pia. 131 00:06:22,840 --> 00:06:24,816 Kanuni ya tatu ya kufuata 132 00:06:24,840 --> 00:06:27,000 ni kutengeneza mfumo katika kujifunza kwako. 133 00:06:27,720 --> 00:06:31,936 Wote tupo bize na hakuna aliye na muda wa kujifunza lugha mpya leo. 134 00:06:31,960 --> 00:06:35,736 Lakini tunaweza pata muda kama tukipanga mbele kidogo. 135 00:06:35,760 --> 00:06:39,176 Unaweza kuamka dakika kumi na tano mapema kabla ya muda wa kawaida wa kuamka? 136 00:06:39,200 --> 00:06:42,496 Huo utakuwa muda mzuri wa kuweza kupitia baadhi ya maneno. 137 00:06:42,520 --> 00:06:46,256 Unaweza sikiliza kipindi ukiwa unarudi nyumbani wakati unaendesha? 138 00:06:46,280 --> 00:06:49,736 Sasa, hiyo itakuwa nzuri kupata uzoefu wa kusikiliza. 139 00:06:49,760 --> 00:06:53,216 Kuna vitu vingi tunaweza fanya bila hata ya kupanga muda wa ziada, 140 00:06:53,240 --> 00:06:55,896 kama vile kusikiliza kipindi ukiwa unaelekea kazini, 141 00:06:55,920 --> 00:06:57,576 au wakati unafanya kazi za nyumbani. 142 00:06:57,600 --> 00:07:00,896 Kitu muhimu ni kutengeneza mpango katika kujifunza. 143 00:07:00,920 --> 00:07:03,416 "Nitajifunza kuongea kila Jumanne na Alhamisi 144 00:07:03,440 --> 00:07:05,496 na rafiki kwa dakika 20. 145 00:07:05,520 --> 00:07:09,936 Nitasikiliza video katika Youtube wakati nikipata kifungua kinywa." 146 00:07:09,960 --> 00:07:12,096 Kama utatengeneza mfumo katika kujifunza, 147 00:07:12,120 --> 00:07:14,016 huna haja ya kutafuta muda wa ziada, 148 00:07:14,040 --> 00:07:16,480 kwa sababu itakuwa namna ya maisha yako ya kila siku. 149 00:07:17,880 --> 00:07:21,096 Na mwisho, kama unataka kujifunza lugha kwa ufasaha, 150 00:07:21,120 --> 00:07:23,840 unahitaji kuwa na subira kidogo. 151 00:07:24,600 --> 00:07:27,336 Haiwezekani kujifunza lugha ndani ya miezi miwili, 152 00:07:27,360 --> 00:07:31,256 lakini inawezekana kabisa kufanya mabadiliko yanayoonekana katika miezi miwili, 153 00:07:31,280 --> 00:07:35,016 kama utajifunza katika kiasi kidogo kidogo kila siku katika namna ambayo unafurahia. 154 00:07:35,040 --> 00:07:37,176 Na hakuna kitu ambacho kinatuhamasisha zaidi 155 00:07:37,200 --> 00:07:38,440 ya mafanikio yetu. 156 00:07:39,120 --> 00:07:41,016 Nakumbuka vizuri wakati 157 00:07:41,040 --> 00:07:44,720 nilipoelewa utani wa kwanza kwa Kijerumani nilipokuwa naangalia "Marafiki." 158 00:07:45,280 --> 00:07:47,136 Nilifurahia sana na kuhamasika 159 00:07:47,160 --> 00:07:50,176 kwamba niliendelea kuangalia sehemu mbili zaidi siku hiyo, 160 00:07:50,200 --> 00:07:51,936 na nilivyoendelea kuangalia, 161 00:07:51,960 --> 00:07:56,176 Niliendelea kuelewa zaidi, ushindi huu mdogo, 162 00:07:56,200 --> 00:07:59,656 na hatua kwa hatua, nilifika katika hatua ambapo ningetumia lugha 163 00:07:59,680 --> 00:08:02,536 kwa uhuru na ufasaha kuweza kuelezea chochote. 164 00:08:02,560 --> 00:08:04,080 Hii ni hisia ya kusisimua. 165 00:08:04,800 --> 00:08:06,496 Siwezi tosheka na hisia hiyo, 166 00:08:06,520 --> 00:08:09,336 na ndiyo maana najifunza lugha mpya kila miaka miwili. 167 00:08:09,360 --> 00:08:11,416 Kwa hiyo ndiyo siri nzima ya mwanaisimu. 168 00:08:11,440 --> 00:08:14,296 Tafuta njia madhubuti ambayo unaweza kuitumia kwa mfumo 169 00:08:14,320 --> 00:08:17,616 katika kipindi cha muda fulani katika njia ambayo unafurahia, 170 00:08:17,640 --> 00:08:21,520 na hivi ndivyo wanaisimu hujifunza lugha ndani ya miezi, na siyo miaka. 171 00:08:23,160 --> 00:08:24,776 Sasa, baadhi yenu mnaweza kuwaza, 172 00:08:24,800 --> 00:08:27,136 "Ni vizuri sana kufurahia kujifunza lugha, 173 00:08:27,160 --> 00:08:29,696 lakini si kwamba nyinyi wanaisimu 174 00:08:29,720 --> 00:08:32,320 mna talanta sana na wengi wetu hatuna hiyo talanta?" 175 00:08:33,320 --> 00:08:36,400 Hivyo, kuna kitu kimoja sijawaambia kuhusu Benny na Lucas. 176 00:08:37,159 --> 00:08:42,976 Benny alikuwa na miaka 11 ya kiselti cha Kiyalandi na miaka mitano ya lugha ya Kijerumani shuleni. 177 00:08:43,000 --> 00:08:46,216 Hakuweza kuongea baada ya kuhitimu masomo. 178 00:08:46,240 --> 00:08:50,416 Mpaka miaka 21, aliwaza kwamba hakuwa na jeni ya lugha 179 00:08:50,440 --> 00:08:52,856 na hakuweza kuongea lugha nyingine. 180 00:08:52,880 --> 00:08:55,816 Kisha akaanza kutafuta njia yake ya kujifunza lugha, 181 00:08:55,840 --> 00:08:59,696 ambapo ilikuwa ni kuongea na wenyeji wa lugha na kupata mrejesho kutoka kwao, 182 00:08:59,720 --> 00:09:03,680 na leo Benny anaweza kwa urahisi kufanya maongezi katika lugha 10. 183 00:09:05,120 --> 00:09:08,416 Lucas amejaribu kujifunza Kiingereza shuleni kwa miaka 10. 184 00:09:08,440 --> 00:09:11,056 Alikuwa ni moja ya wanafunzi wanaofanya vibaya darasani. 185 00:09:11,080 --> 00:09:12,696 Rafiki zake walikuwa wakimtania 186 00:09:12,720 --> 00:09:15,336 na kumpa kitabu cha Kirussia kama utani 187 00:09:15,360 --> 00:09:19,096 kwa sababu waliamini hawezi kamwe kujifunza lugha hiyo, au lugha yoyote. 188 00:09:19,120 --> 00:09:21,496 Na kisha Lucas akaanza kufanya majaribio na njia yake, 189 00:09:21,520 --> 00:09:23,320 akitafuta njia yake ya kujifunza, 190 00:09:24,520 --> 00:09:28,696 kwa mfano, kwa kupiga soga na watu asiowajua katika Skype. 191 00:09:28,720 --> 00:09:30,536 Na katika miaka 10, 192 00:09:30,560 --> 00:09:33,880 Lucas anaweza kuongea lugha 11 kwa ufasaha. 193 00:09:35,000 --> 00:09:36,560 Je hiyo inaonekana kama miujiza? 194 00:09:37,440 --> 00:09:40,040 Sasa, ninaona miujiza kama hii kila siku. 195 00:09:40,760 --> 00:09:42,096 Na kama mshauri wa lugha, 196 00:09:42,120 --> 00:09:44,536 Nasaidia watu kujifunza lugha wenyewe, 197 00:09:44,560 --> 00:09:45,856 na naona hili kila siku. 198 00:09:45,880 --> 00:09:50,056 Watu hupata shida kujifunza lugha kwa miaka mitano, kumi, hata ishirini, 199 00:09:50,080 --> 00:09:53,936 na ghafla huchukua hatua ya kujifunza mikononi mwao, 200 00:09:53,960 --> 00:09:57,256 kuanza kutumia makala wanazofurahia, njia madhubuti zaidi, 201 00:09:57,280 --> 00:09:59,096 au wanaanza kufatilia kujifunza kwao 202 00:09:59,120 --> 00:10:02,056 kwamba wanaweza kuridhika na maendeleo yao, 203 00:10:02,080 --> 00:10:04,016 na hapo ndipo ghafla 204 00:10:04,040 --> 00:10:08,240 kwa maajabu wanatambua kipaji cha lugha ambacho walikuwa wanakosa maisha yao yote. 205 00:10:09,480 --> 00:10:11,656 Kwa hiyo kama umejaribu pia kujifunza lugha 206 00:10:11,680 --> 00:10:14,096 na ukakata tamaa, 207 00:10:14,120 --> 00:10:16,376 na kama huna kipaji cha lugha, 208 00:10:16,400 --> 00:10:17,936 jaribu tena. 209 00:10:17,960 --> 00:10:20,816 Labda upo karibu kidogo na njia moja ya kuburudika 210 00:10:20,840 --> 00:10:22,602 ili kujifunza lugha hiyo kwa ufasaha. 211 00:10:22,960 --> 00:10:26,896 Labda upo karibu kuja kuwa mwanaisimu. 212 00:10:26,920 --> 00:10:28,136 Asante. 213 00:10:28,160 --> 00:10:32,360 (Makofi)