Napenda kujifunza lugha za kigeni.
napenda sana kiasi kwamba hujifunza lugha mpya kila baada ya miaka miwili,
sasa hivi najifunza lugha ya nane.
Pale watu wanapogundua kuhusu mimi, mara huniuliza,
"Unafanyaje hivyo? Siri yako ni ipi?"
Na niwe muwazi, kwa miaka mingi, jibu langu litakuwa,
"Sifahamu. Napenda tu kujifunza lugha."
Lakini watu hawakufurahishwa na jibu hilo.
Walitaka kufahamu kwanini wanatumia miaka kujaribu kuijfunza hata lugha moja,
kamwe hawafanikiwa unenaji,
na mimi natokea, nikijifunza lugha moja baada ya nyingine.
Walitaka kujua siri ya wanaisimu,
watu wanaoongea lugha nyingi.
Na hii ilinifanya kushangaa, pia,
wanaisimu wengine wanafanyaje?
Kitu gani tulichonacho?
Na kipi ambacho kinatuwezesha sisi
kujifunza lugha kwa haraka kuliko watu wengine?
Niliamua kukutana na watu wengine kama mimi ili kutambua.
Sehemu nzuri ya kuonana na wanaisimu wengi
ni katika hafla ambapo mamia ya wapenzi wa lugha
hukutana pamoja.
Kuna baadhi ya hafla za wanaisimu ambazo huandaliwa duniani kote,
na kwa hiyo niliamua kwenda huko
na kuwauliza wanaisimu kuhusu njia wanazotumia.
Nilikutana na Benny kutoka Ireland,
ambaye aliniambia kwamba njia yake ni kuanza kuongea kuanzia siku ya kwanza.
Hujifunza misemo michache kutoka katika kitabu cha misemo cha wasafiri
na huenda kukutana na wenyeji wa lugha husika
na kuanza maongezi nao moja kwa moja.
Hajali kukosea kuongea hata mara 200 kwa siku,
kwa sababu hivyo ndivyo anajifunza, ukilinganisha na mrejesho.
Na kilicho bora ni kwamba, haitaji kusafiri sana leo,
Sababu kwa urahisi unaweza fanya maongezi na wenyeji wa lugha
ukiwa umepumzika katika chumba chako, ukitumia tovuti.
Nilikutana pia na Lucas kutoka Brazil
ambaye alikuwa na njia ya kuvutia ya kujifunza Kirussia.
Kiurahisi aliwaalika waongeaji wa lugha ya Kirussia wapatao 100 kama marafiki katika mtandao wake wa Skype,
na kisha alianza kupiga soga na mmoja wao
na akaandika "Habari" kwa Kirussia.
Yule mtu alijibu," Nzuri, hujambo?"
Lucas alinakili haya maongezi na kuweka katika chumba cha maandishi alipoanza soga na mtu mwingine,
na mtu alijibu. "Nipo salama, asante, na wewe hujambo?"
Lucas alinakili tena na kuweka katika soga na mtu wa kwanza,
na katika njia hii, aliwafanya watu wawili wasiojuana kuwa katika maongezi
bila kufahamu hilo.
(Kicheko)
Si punde alianza kuchapa maneno mwenyewe,
kwa sababu alikuwa na maongezi kama haya mengi
kwamba aligundua jinsi gani maongezi ya Kirussia ambavyo kwa kawaida huanza.
Njia yenye werevu sana, si ndiyo?
Na kisha nilikutana na mwanaisimu ambaye muda wote huanza kwa kuigiza sauti za lugha,
na wengine ambao amara zote hujifunza maneno 500 ya mara kwa mara katika lugha,
na wengine ambao huanza kwa kusoma kitabu cha sarufi.
Kama ningeuliza wanaisimu mbalimbali mia moja,
Nilisikia namna mia moja mbalimbali za kujifunza lugha.
Kila mtu alikuwa na njia tofauti ya kujifunza lugha,
na wote mwishoni huja na matokeo sawa ya kuongea lugha baadhi kwa ufasaha.
Na nilikuwa nawasikiliza wanaisimu hawa wakinieleza kuhusu njia zao,
ghafla ikaniamsha:
kitu kimoja ambacho wote tunacho
ni kwamba tumeweza kutafuta namna ya kufurahia mchakato ya kujifunza lugha.
Na hawa wanaisimu wote walikuwa wanaongelea kuhusu kujifunza lugha
na ilikuwa inafurahisha sana.
Ungewaona nyuso zao
walipokuwa wakinionyesha chati za rangi zikielezea sarufi
na kadi za maneno zilizotengenezwa kwa uangalifu,
na takwimu zao kuhusu kujifunza maneno ya lugha kwa kutumia programu ya simu janja,
au wanavyopenda kupika kutokana na maelezo ya upishi yaliyoandikwa katika lugha ya kigeni.
Wote wanatumia njia mbalimbali,
Lakini wanahakikisha ni kitu ambacho binafsi wanapendelea kufanya.
Nimegundua kwamba hivi ndivyo mimi hujifunza lugha.
Nilipokuwa najifunza Kispanyola, nilichoshwa na maandishi katika kitabu.
Namaanisha, nani ambaye anataka kusoma kuhusu Jose
akiuliza kuhusu uelekeo wa kwenda kituo gari moshi. Sawa?
Nilitaka kusoma "Harry Porter" badala yake,
kwa sababu ndicho kilikuwa kitabu nikipendacho sana nikiwa mdogo,
na nimekisoma mara nyingi.
Kwa hiyo nilipata tafsiri "Harry Porter" katika lugha ya Kispanyola na nikaanza kusoma,
na kwa uhakika, sikuelewa chochote kile mwanzoni,
lakini niliendelea kusoma kwa sababu nilikipenda kitabu,
na mwishoni mwa kitabu, niliweza kukifatilia bila matatizo yoyote.
Na jambo sawa lilitokea wakati nikijifunza Kijerumani.
Niliamua kuangalia "Marafiki," ucheshi ninaopendelea, kwa Kijerumani,
na tena, mwanzoni ilikuwa upuuzi tu.
Sikuelewa ni wapi neno moja limeishia na lingine lilipoanzia,
lakini niliendelea kuangalia kila siku kwa sababu ilikuwa ni "Marafiki."
Naweza kuangalia katika lugha yoyote. Napenda sana.
Na baada sehemu ya pili au ya tatu,
kiukweli, maongezi yalianza kuleta maana.
Nilitambua hili baada ya kukutana na wanaisimu wengine.
Sisi si wenye talanta
na hatuna njia za kukatiza katika kujifunza lugha.
Tumeweza kutafuta njia ya kufurahia mchakato,
namna ya kubadili usomaji wa lugha kutoka kama somo la shule lisilofurahisha
hadi katika shughuli ya kuvutia ambayo hutaona shida kuifanya kila siku.
Kama hupendelei kuandika maneno kwenye karatasi,
unaweza mara zote kuyachapa kwenye programu ya simu.
Kama hupendelei kusikiliza vitabu vinavyochosha,
tafuta video zinazovutia katika Youtube au katika vipindi vya lugha.
Kama wewe ni mtu unayependelea upekee
na hauwezi kuwaza ni namna gani utaweza ongea na wenyeji wa lugha moja kwa moja,
unaweza kujifunza kujiongelesha mwenyewe.
Unaweza kuongea na nafsi yako ukiwa katika chumba chako,
ukieleza mipango yako ya mwisho wa wiki, siku yako ilikwendaje,
au hata kupiga picha zisizo na mpangilio katika simu yako
na kuelezea kuhusu picha hiyo kwa rafiki yako wa kufikirika.
Hivi ndivyo wanaisimu hujifunza lugha,
na habari njema ni kwamba, inapatikana kwa mtu yoyote
nani ambaye yuko tayari kujifunza katika mikono yake.
Hivyo kukutana na wanaisimu wengine kulinisaidia kutambua
kwamba ni muhimu sana kupata burudani
katika mchakato wa kujifunza lugha,
lakini pia furaha yenyewe pekee haitoshi.
Kama unataka kuweza kufikia ufasaha katika lugha ya kigeni,
utahitajika kutumia kanuni tatu zaidi.
Kwanza, unahitaji njia zilizo bora.
Ukijaribu kukumbuka listi ya maneno kwa ajili ya mtihani wa kesho,
maneno yatahifadhiwa katika kumbukumbu yako ya muda mfupi
na utayasahau baada ya siku chache.
Kama, hata hivyo, unataka kukaa na maneno kwa muda mrefu,
unahitaji kuyarudia katika kipindi cha siku chache
ukifanya kitu kinachofahamika kama kurudia kwa nafasi.
Unaweza kutumia programu za simu ambazo zinatumia mfumo huu kama vile Anki au Memrise,
au unaweza kuandika orodha ya neno katika kijitabu ukitumia njia ya Goldlist,
ambayo ni maarufu kwa wanaisimu wengi.
Kama huna uhakika ni njia ipi inayofaa na kipi kinachopatikana,
angalia chaneli za Youtube na tovuti za wanaisimu
kupata hamasa kutoka kwao.
Kama inawafaa wao, lazima itakufaa na wewe pia.
Kanuni ya tatu ya kufuata
ni kutengeneza mfumo katika kujifunza kwako.
Wote tupo bize na hakuna aliye na muda wa kujifunza lugha mpya leo.
Lakini tunaweza pata muda kama tukipanga mbele kidogo.
Unaweza kuamka dakika kumi na tano mapema kabla ya muda wa kawaida wa kuamka?
Huo utakuwa muda mzuri wa kuweza kupitia baadhi ya maneno.
Unaweza sikiliza kipindi ukiwa unarudi nyumbani wakati unaendesha?
Sasa, hiyo itakuwa nzuri kupata uzoefu wa kusikiliza.
Kuna vitu vingi tunaweza fanya bila hata ya kupanga muda wa ziada,
kama vile kusikiliza kipindi ukiwa unaelekea kazini,
au wakati unafanya kazi za nyumbani.
Kitu muhimu ni kutengeneza mpango katika kujifunza.
"Nitajifunza kuongea kila Jumanne na Alhamisi
na rafiki kwa dakika 20.
Nitasikiliza video katika Youtube wakati nikipata kifungua kinywa."
Kama utatengeneza mfumo katika kujifunza,
huna haja ya kutafuta muda wa ziada,
kwa sababu itakuwa namna ya maisha yako ya kila siku.
Na mwisho, kama unataka kujifunza lugha kwa ufasaha,
unahitaji kuwa na subira kidogo.
Haiwezekani kujifunza lugha ndani ya miezi miwili,
lakini inawezekana kabisa kufanya mabadiliko yanayoonekana katika miezi miwili,
kama utajifunza katika kiasi kidogo kidogo kila siku katika namna ambayo unafurahia.
Na hakuna kitu ambacho kinatuhamasisha zaidi
ya mafanikio yetu.
Nakumbuka vizuri wakati
nilipoelewa utani wa kwanza kwa Kijerumani nilipokuwa naangalia "Marafiki."
Nilifurahia sana na kuhamasika
kwamba niliendelea kuangalia sehemu mbili zaidi siku hiyo,
na nilivyoendelea kuangalia,
Niliendelea kuelewa zaidi, ushindi huu mdogo,
na hatua kwa hatua, nilifika katika hatua ambapo ningetumia lugha
kwa uhuru na ufasaha kuweza kuelezea chochote.
Hii ni hisia ya kusisimua.
Siwezi tosheka na hisia hiyo,
na ndiyo maana najifunza lugha mpya kila miaka miwili.
Kwa hiyo ndiyo siri nzima ya mwanaisimu.
Tafuta njia madhubuti ambayo unaweza kuitumia kwa mfumo
katika kipindi cha muda fulani katika njia ambayo unafurahia,
na hivi ndivyo wanaisimu hujifunza lugha ndani ya miezi, na siyo miaka.
Sasa, baadhi yenu mnaweza kuwaza,
"Ni vizuri sana kufurahia kujifunza lugha,
lakini si kwamba nyinyi wanaisimu
mna talanta sana na wengi wetu hatuna hiyo talanta?"
Hivyo, kuna kitu kimoja sijawaambia kuhusu Benny na Lucas.
Benny alikuwa na miaka 11 ya kiselti cha Kiyalandi na miaka mitano ya lugha ya Kijerumani shuleni.
Hakuweza kuongea baada ya kuhitimu masomo.
Mpaka miaka 21, aliwaza kwamba hakuwa na jeni ya lugha
na hakuweza kuongea lugha nyingine.
Kisha akaanza kutafuta njia yake ya kujifunza lugha,
ambapo ilikuwa ni kuongea na wenyeji wa lugha na kupata mrejesho kutoka kwao,
na leo Benny anaweza kwa urahisi kufanya maongezi katika lugha 10.
Lucas amejaribu kujifunza Kiingereza shuleni kwa miaka 10.
Alikuwa ni moja ya wanafunzi wanaofanya vibaya darasani.
Rafiki zake walikuwa wakimtania
na kumpa kitabu cha Kirussia kama utani
kwa sababu waliamini hawezi kamwe kujifunza lugha hiyo, au lugha yoyote.
Na kisha Lucas akaanza kufanya majaribio na njia yake,
akitafuta njia yake ya kujifunza,
kwa mfano, kwa kupiga soga na watu asiowajua katika Skype.
Na katika miaka 10,
Lucas anaweza kuongea lugha 11 kwa ufasaha.
Je hiyo inaonekana kama miujiza?
Sasa, ninaona miujiza kama hii kila siku.
Na kama mshauri wa lugha,
Nasaidia watu kujifunza lugha wenyewe,
na naona hili kila siku.
Watu hupata shida kujifunza lugha kwa miaka mitano, kumi, hata ishirini,
na ghafla huchukua hatua ya kujifunza mikononi mwao,
kuanza kutumia makala wanazofurahia, njia madhubuti zaidi,
au wanaanza kufatilia kujifunza kwao
kwamba wanaweza kuridhika na maendeleo yao,
na hapo ndipo ghafla
kwa maajabu wanatambua kipaji cha lugha ambacho walikuwa wanakosa maisha yao yote.
Kwa hiyo kama umejaribu pia kujifunza lugha
na ukakata tamaa,
na kama huna kipaji cha lugha,
jaribu tena.
Labda upo karibu kidogo na njia moja ya kuburudika
ili kujifunza lugha hiyo kwa ufasaha.
Labda upo karibu kuja kuwa mwanaisimu.
Asante.
(Makofi)