Tafuta thamani ya 3 kwenye namba 4, 356. Ninapofikiria thamani ya namba fanya mazoezi mengi ili iwe kawaida kwako Ila ninapoona swali kama hili ninapenda kuirefusha ili tujue ina maana gani, nitaiandika tena namba . Kama ningetakiwa kuliiandika tena--ningetumia rangi tofauti. kwa hiyo 4, 356 ni sawa na --fikiria nilichosema. ni sawa na 4,000 jumlisha 300 jumlisha 50 jumlisha 6. Na ungeisoma hivi kama nilivyosema elfu nne, mia tatu, na hamsini na sita. Njia nyingine ni sawa na kusema hii ni elfu 4 jumlisha mia 3 jumlisha 50, makumi matano jumlisha 6. Na badala ya 6, ungesema jumlisha mamoja 6. Tukirudi kwenye swali letu hii 4,356 ni sawa na 4--nitaiandika hapa chini. Nitaiandika kama hivi. Hii ni sawa na elfu 4, mia 3, makumi 5 na mamoja 6. Hivyo ukiulizwa thamani ya 3 kwenye 4, 356, tunashughulika na 3 hapa, na thamani yake. Iko kwenye sehemu ya mamia. Kama kuna 4 hapa, tungesema tutashughulika na mamia 4. kama ni 5, mamia 5. ni ya tatu kutoka kulia. Hii ni sehemu ya mamoja. Hii ni mamoja 6, makumi 5, mamia 3. Hivyo hapa jibu ni sehemu ya mamia.