WEBVTT 00:00:00.390 --> 00:00:03.460 Wanawake wana haki sawa kama wanaume. 00:00:03.870 --> 00:00:07.247 Iwapo mwanaume, mvulana wanaweza kwenda shule, mbona msichana asiende? 00:00:07.381 --> 00:00:09.141 [Malala Yousafzai] 00:00:09.738 --> 00:00:11.998 [Mwanamke shujaa wa Wasichana wa mwaka wa 2013] 00:00:12.410 --> 00:00:13.780 Nisipoenda shuleni 00:00:13.780 --> 00:00:17.530 basi nitakuwa ninatii baba na ndugu yangu, 00:00:17.530 --> 00:00:19.340 nitakuwa nikiosha nguo kila siku, 00:00:19.340 --> 00:00:20.558 na kisha nitaolewa, 00:00:20.558 --> 00:00:22.518 kisha nitakuwa nikiwashughulikia watoto, 00:00:22.518 --> 00:00:24.030 na maisha yangu yataisha. 00:00:24.640 --> 00:00:27.499 Hao watu ambao wanatuzuia kupata elimu, 00:00:28.509 --> 00:00:31.740 wanawaogopa wanawake waliosoma na wenye nguvu. 00:00:34.220 --> 00:00:36.340 Kulikuwa na mwandishi wa makala wa BBC, 00:00:36.520 --> 00:00:38.060 na alimuuliza baba yangu, 00:00:38.060 --> 00:00:40.689 "Nataka mtu kutoka Swat anayeweza kuzungumza nami, 00:00:40.689 --> 00:00:42.790 na anayeweza kuniambia kinachofanyika huko". 00:00:43.060 --> 00:00:45.550 Kwa hivyo nilianza kuandika makala kwa ajili ya BBC. 00:00:45.590 --> 00:00:48.260 Nilikuwa nazungumza naye kwenye simu kila usiku. 00:00:48.880 --> 00:00:52.840 Sote tulitaka elimu lakini watu wengi walikuwa kimya 00:00:52.840 --> 00:00:56.192 kwa sababu waliogopa kundi la Taliban - waliogopa kifo. 00:00:58.080 --> 00:01:00.691 Lakini ujasiri ulishinda hofu hiyo. 00:01:02.101 --> 00:01:03.686 Ndiyo maana nilizungumza. 00:01:03.816 --> 00:01:05.483 Sikuwa nasubiri mtu mwingine. 00:01:05.983 --> 00:01:07.290 Niliifanya mwenyewe. 00:01:07.810 --> 00:01:09.690 [Tarehe 9 Oktoba 2012] 00:01:10.060 --> 00:01:11.805 Saa 6 mchana, nafikiri, 00:01:11.825 --> 00:01:14.080 tulikuwa tu tumeketi katika basi la shule yetu, 00:01:14.080 --> 00:01:17.400 na nikamuuliza dereva wangu, "Je, unaweza kufanya mazingaumbwe?" 00:01:17.400 --> 00:01:19.590 na alikuwa tu ameficha jiwe katika mkono wake, 00:01:19.590 --> 00:01:21.230 na tulihitaji kuipata. 00:01:21.580 --> 00:01:24.699 Na sijui nilifungua tu macho yangu na nilikuwa hospitalini. 00:01:28.021 --> 00:01:29.750 Nilijua kuwa nilipigwa risasi, 00:01:29.750 --> 00:01:33.867 na jambo la kwanza nililofanya nikushukuru Mungu nilikuwa mzima. 00:01:36.537 --> 00:01:39.190 Katika nchi yangu Pakistan na kote duniani, 00:01:39.960 --> 00:01:42.920 wasichana waliinua wito wa "Mimi ni Malala." 00:01:43.806 --> 00:01:45.757 Hio ni sauti yao ya elimu, 00:01:46.337 --> 00:01:49.590 na walipaza sauti zao dhidi ya ugaidi 00:01:50.330 --> 00:01:51.778 Ni heshima kwangu 00:01:51.778 --> 00:01:57.300 kwa sababu nihitaji wasichana, wanawake na wavulana zaidi 00:01:57.990 --> 00:02:00.710 kunisaidia katika kampeni yangu ya elimu. 00:02:02.609 --> 00:02:05.439 [Mnamo 2014, Malala alishinda tuzo la Nobel Peace.] 00:02:06.149 --> 00:02:08.600 Taliban walinipiga risasi, walifikiri 00:02:09.698 --> 00:02:13.570 kuwa wasichana wengine wanaozungumzia haki zao pia wataacha. 00:02:15.050 --> 00:02:18.910 Walifikiri kuwa watasambaza hofu, ugaidi, 00:02:19.810 --> 00:02:20.850 lakini walishindwa. 00:02:22.300 --> 00:02:25.730 Naamini kuwa iwapo unaamini moyoni wako 00:02:25.730 --> 00:02:27.170 unaweza kufanya chochote. 00:02:27.170 --> 00:02:29.729 Na ninaweza kufanya chochote