Wanawake wana haki sawa kama wanaume. Iwapo mwanaume, mvulana wanaweza kwenda shule, mbona msichana asiende? [Malala Yousafzai] [Mwanamke shujaa wa Wasichana wa mwaka wa 2013] Nisipoenda shuleni basi nitakuwa ninatii baba na ndugu yangu, nitakuwa nikiosha nguo kila siku, na kisha nitaolewa, kisha nitakuwa nikiwashughulikia watoto, na maisha yangu yataisha. Hao watu ambao wanatuzuia kupata elimu, wanawaogopa wanawake waliosoma na wenye nguvu. Kulikuwa na mwandishi wa makala wa BBC, na alimuuliza baba yangu, "Nataka mtu kutoka Swat anayeweza kuzungumza nami, na anayeweza kuniambia kinachofanyika huko". Kwa hivyo nilianza kuandika makala kwa ajili ya BBC. Nilikuwa nazungumza naye kwenye simu kila usiku. Sote tulitaka elimu lakini watu wengi walikuwa kimya kwa sababu waliogopa kundi la Taliban - waliogopa kifo. Lakini ujasiri ulishinda hofu hiyo. Ndiyo maana nilizungumza. Sikuwa nasubiri mtu mwingine. Niliifanya mwenyewe. [Tarehe 9 Oktoba 2012] Saa 6 mchana, nafikiri, tulikuwa tu tumeketi katika basi la shule yetu, na nikamuuliza dereva wangu, "Je, unaweza kufanya mazingaumbwe?" na alikuwa tu ameficha jiwe katika mkono wake, na tulihitaji kuipata. Na sijui nilifungua tu macho yangu na nilikuwa hospitalini. Nilijua kuwa nilipigwa risasi, na jambo la kwanza nililofanya nikushukuru Mungu nilikuwa mzima. Katika nchi yangu Pakistan na kote duniani, wasichana waliinua wito wa "Mimi ni Malala." Hio ni sauti yao ya elimu, na walipaza sauti zao dhidi ya ugaidi Ni heshima kwangu kwa sababu nihitaji wasichana, wanawake na wavulana zaidi kunisaidia katika kampeni yangu ya elimu. [Mnamo 2014, Malala alishinda tuzo la Nobel Peace.] Taliban walinipiga risasi, walifikiri kuwa wasichana wengine wanaozungumzia haki zao pia wataacha. Walifikiri kuwa watasambaza hofu, ugaidi, lakini walishindwa. Naamini kuwa iwapo unaamini moyoni wako unaweza kufanya chochote. Na ninaweza kufanya chochote