Hapa, tuna tuna umbo la pande nne, au pembenne, ambapo pande mbili ni sambamba. Na kwa hiyo hii ni trapeza. Na tunachotaka kufanya ni, kupitia vipimo tulivyopewa, tutafute eneo la trapeza. Kwa hebu tufikiri. Tutapata nini kama tukizidisha hichi kitako kirefu 6 mara urefu 3? Kwa hiyo utapata nini ukizidisha 6 mara 3? Tutapata eneo la mstatili ambalo ni hatua 6 upana na kimo ni hatua 3. Kwa hiyo hiyo itatupa eneo la umbo ambalo litaonekana kama-- hebu nichore kwa rangi ya pinki. Eneo la umbo ambalo linaonekana kama hivi litakuwa 6 mara 3. Kwa hiyo litatupa eneo lote pale. Sasa, trapeza ni ndogo kuliko hiyo lakini hebu tufanye kwa majaribio. Sasa nini kitatokea tukichukua 2 mara 3? Tutakuwa tunatafuta eneo la mstatili ambalo lina upana wa 2 na urefu wa 3. Kwa hiyo unaweza kuchukulia kwamba huo ni huu mstatili hapa. Huu mstatili hapa. Kwa hiyo huo ni mstatili wa 2 mara 3. Sasa inaonekana kama eneo la trapeza linatakiwa liwe kati ya namba hizi mbili. Labda inaweza kuwa nusu yake kwa sababu ukiangalia eneo tofauti kati ya mistatili miwili -- na ngoja nitumie rangi. Kwa hiyo hii ni tofauti ya eneo upande wa kushoto. Na hii ni tofauti ya eneo upande wa kulia. Na tukiweka msisitizo kwenye trapeza, kama tukianzia kwenye huu mstatili mdogo wa njano, inachukua nusu ya eneo, nusu ya tofauti kati ya mstatili mdogo na mkubwa upande wa kushoto. Tunapata nusu ya eneo upande wa kushoto. Na tunapata nusu ya tofauti kati ya mstatili mdogo na mkubwa upande wa kulia. Kwa hiyo inaleta maana kwamba eneo la trapeza, hili eneo lote hapa, inatakiwa iwe wastani. Inatakiwa iwe nusu kati ya maeneo ya mstatili mdogo na mstatili mkubwa. Kwa hiyo hebu tuchukue wastani wa hizo namba mbili. Itakwenda kuwa 6 mara 3 jumlisha 2 mara 3, yote hiyo juu ya 2. Kwa hiyo ukifikiria kuhusu eneo la trapeza, unaangalia vitako viwili, kitako kirefu na kitako kifupi. Zidisha kila ya hicho mara urefu, na halafu unaweza kuchukua wastani wake. Au unaweza kuifikiria kama hii ni kitu kile kile kama 6 jumlisha 2. Na ninatoa nje 3 hapa. 6 jumlisha 2 mara 3, na halafu yote hiyo juu ya 2, ambayo ni kitu kile kile kama-- na ninaiandika katika njia tofauti. Hizi ni njia tofauti za kuifikiria -- 6 jumlisha 2 juu ya 2, na halau hiyo juu ya 3. Kwa hiyo unaweza kuiona kama wastani wa pembetatu ndogo na kubwa Kwa hiyo zidisha kila ya hichi kitako mara urefu na halfu chukua wastani. Unaweza kuiona kama-- ngoja tujumlishe urefu wa vitako viwili, zidisha kwa kimo, na halafu gawanya kwa 2 Au unaweza kusema, hebu tuchukue wastani wa urefu vitako viwili na zidisha kwa 3, N ahiyo inakupa njia nyingine ya kuvutia ya kufikiria kuhusu hili. Ukichukua wastani wa` urefu wa mistari hii miwili, 6 jumlisha 2 juu ya 2 ni 4. Kwa hiyo huo utakuwa ni upana ambao unaonekana kitu kama hiki. Upana wa 4 utaonekana kitu kama hiki. Upana wa 4 uanonekana kitu kama hicho, na unazidisha hicho kwa kimo. Huo utakuwa mstatili kama huu ambao ni nusu kati ya maeneo ya mstatili mdogo na mkubwa. Kwa hiyo hizi zote ni sawa sawa. Sasa hebu tukokotoe. Kwa hiyo tunaweza kufanya lolote kati ya haya. 6 mara 3 ni 18. Hii ni 18 jumlisha 6, juu ya 2. Hiyo ni 24/2, au 12. Ungeweza pia kufanya kwa njia hii. 6 jumlisha 2 ni 8, mara 3 ni 24, gawanya kwa 2 ni 12. 6 jumlisha 2 gawanya kwa 2 ni 4 mara 3 ni 12. Kwa njia yoyote, eneo la trapeza ni hatua za mara 12.