Saida Aden Said: Bado nina taswira hii
mbaya katika kumbukumbu zangu.
ningeweza ona watu wakianguka chini,
milio ya risasi.
Niliogopa sana.
Kwa kweli, nililia sana.
Mtu aliyewajua baba na mama yangu
akanishika mkono, akisema,
"Twenda! Twende! Twende!"
Nikawa nasema," Mamangu yuwapi?
Mama yangu? Mama yangu?"
Noria Dambrine Dusabireme:
Usiku tungesikia milio ya risasi,
tulisikia bunduki,
Uchaguzi ulitakiwa kufanyika.
Vijana walienda barabarani,
walikuwa na migomo.
Na vijana wengi walifariki
SAS: Tulipanda gari.
Lilikuwa limejaa sana
Watu walikimbia kunusuru maisha yao,
Hivi ndivyo nilivyochipuruka Somalia.
Mama yangu alinimisi sana.
Hakuna yeyote aliyemweleza nilikokwenda.
NDD:Ukweli ni kwamba,
hatukusoma,
Hatukuweza kwenda sokoni,
tulibaki nyumbani tu
ikanifanya nijue kuwa ningepata
nafasi ya kuchagua kitu kizuri,
ningeweza kukichagua na kuwa na
maisha bora mbeleni.
(Muziki)
Ignazio Matteini: Duniani,
idadi wa watu walio uhamishoni
imekuwa ikiongezeka
Sasa takriban watu Millioni 60
wako uhamishoni duniani
Na kwa bahati mbaya, haipungui.
Chrystina Russell:Nafikiri jamii
ya misaada kibinadamu
inaanza kugundua kutokana na
utafiti na uhakika
tunaongelea tatizo la kudumu zaidi
Baylie Damtie Yeshita: Wanafunzi hawa,
wanahitaji elimu ya juu,
shahada wanayoweza kuitumia.
Ikiwa wanafunzi wanaishi Rwanda sasa,
Ikiwa watahama,
bado wataendelea na masomo yao.
Bado, shahada yao itakuwa na maana,
kokote wako
CR: Mradi wetu wa kijasiri
ulikuwa ni kwa ajili ya kupima
Vuguvugu la Elimu Ulimwenguni la Chuo cha
New Hampshire ya Kusini
uwezo wa kukuza
shahada za kwanza na
mifumo ya kupata ajira
kufikia wahamiaji na wale ambao
wasingeweza kufikia elimu ya juu
SAS: Kama mhamiaji,
ni changamani
kujiendeleza kielimu
na kitaaluma.
Jina langu ni Saida Aden Said,
Na ninatokea Somalia,
Nilikuwa na miaka tisa,
nilipokuja Kakuma,
na nikaanza shule nikiwa na miaka 17
Kwa sasa nafanya shahada yangu ya kwanza
na SNHU.
NDD: My name is Noria Dambrine Dusabireme.
Ninasomea shahada ya kwanza ya sanaa
katika mawasiliano
nikijikita katika masuala ya biashara.
CR:Tunahudumia wanafunzi kutoka
nchi tano tofauti:
Lebanon, Kenya, Malawi,
Rwanda na Afrika ya Kusini.
Tunafurahia wahitimu wa kiwango cha AA
800 na zaidi ya 400 wa shahada ya kwanza
na karibu wanafunzi 1000
walioandikisha kwa sasa.
la ajabu, tunaangazia maisha ya
wakimbizi kama yalivyo.
Hakuna ubaguzi kitabaka
Hakuna mihadhara.
Hakuna tarehe za mwisho
Hakuna mitihani ya mwisho.
shahada hili linapima uwezo
na haujafungwa na muda.
Unachagua muda wa kuanza mradi wako.
Unachagua utakavyoikabili
NDD:Unapofungua jukwaa,
ndipo unapoweza kuona malengo.
Kwenye kila lengo, tunaweza kupata miradi.
Unapofungua mradi,
unakutana na uweza
ambao unatakiwa kumudu,
uelekeo
na muhtasari wa mradi,
CR: Kiungo muhimu cha SNHU
ni kujumuisha usomaji kwa kuangalia
uwezo
pamoja na usomaji wa pamoja na washirika
ili kuwa na msaada pande zote
Hii ni pamoja na ufundishaji kitaaluma.
Inamaanisha msaada saikolojia-jamii,
msaada wa kimatibabu,
na pia ni ule msaada wa mlango
wa nyuma wa ajira
ndiyo inasababisha
hitimu kwa asilimia 95,
na asilimia 88 kuajiriwa,
NDD: mimi mzoezi wa
vitendo ya kuratibu mitandao ya kijamii.
Inahusiana na shahada ya
mawasiliano ninayoifanya.
Nimejifunza mambo mengi
katika mradi huu na dunia halisi.
CR: Mazoezi ya vitendo yanayoongozwa
ni nafasi
kwa wanafunzi kufanyia mazoezi ujuzi wao
kwa sisi kutengeneza daraja katika
mazoezi kwa vitendo
na upatikanaji wa nafasi za kazi baadae.
(Muziki)
Hii ni modeli ambayo inazuia
kuweka muda
na sera za chuo kikuu
na utaratibu kipao mbele
na badala yake unamweka mwanafunzi
kileleni
IM: Modeli ya SNHU ni njia kubwa ya
kutikisa mti.
Kubwa
ni mtikisiko mkubwa kwenye njia ya
asili ya elimu ya juu hapa
BDY:inaweza badilisha maisha
ya wanafunzi
kutoka katika hali ya mashaka na
ukimbizi
NDD: nikipata shahada
naweza rudi na kufanya
kazi popote nitakapo
Ninaweza kufanya shahada ya pili
kwa ujasiri katika Kiingereza,
kitu nisingewazia
hapo awali
Na nina ujasiri na ujuzi unaohitajika
kwenda na kupambana katika
mazingira ya kazi
bila kujali kuwa nitaweza.
SAS: Nilitaka kufanya kazi na jamii.
Nataka kuanzisha shirika isiyo ya faida
Tunahimiza elimu ya wanawake.
Ninataka kuwa mtu ambaye
ni kama balozi
na kuwashawishi kusoma
na kuwaambia hawajachelewa.
Ni ndoto