[Script Info] Title: [Events] Format: Layer, Start, End, Style, Name, MarginL, MarginR, MarginV, Effect, Text Dialogue: 0,0:00:00.00,0:00:04.00,Default,,0000,0000,0000,,Sasa hivi, naona moto wa Bwana ukianguka nyumbani kwako! Dialogue: 0,0:00:04.00,0:00:07.00,Default,,0000,0000,0000,,Moto wa Bwana ukianguka juu ya moyo wako! Dialogue: 0,0:00:07.00,0:00:16.00,Default,,0000,0000,0000,,Moto wa Bwana ukianguka sasa hivi - ukiteketeza maumivu hayo, ukiteketeza mateso hayo, ukiteketeza utumwa huo! Dialogue: 0,0:00:16.00,0:00:17.00,Default,,0000,0000,0000,,Kukamata moto! Dialogue: 0,0:00:19.00,0:00:30.00,Default,,0000,0000,0000,,Mungu anabisha mlangoni mwa \Nmoyo wako sasa hivi. Dialogue: 0,0:00:30.00,0:00:33.00,Default,,0000,0000,0000,,Lakini hatajilazimisha kuingia. Dialogue: 0,0:00:33.00,0:00:39.00,Default,,0000,0000,0000,,Hapana. Hatajilazimisha \Nndani ya moyo wako. Dialogue: 0,0:00:39.00,0:00:45.00,Default,,0000,0000,0000,,Lazima umruhusu aingie sasa hivi. Dialogue: 0,0:00:45.00,0:00:52.00,Default,,0000,0000,0000,,Na tunapokaribia kuomba, nataka uzingatie jambo muhimu sana. Dialogue: 0,0:00:52.00,0:01:06.00,Default,,0000,0000,0000,,Wengi wetu tunaojiunga na ibada hii leo tunamwomba Mungu atukomboe, Dialogue: 0,0:01:06.00,0:01:17.00,Default,,0000,0000,0000,,lakini bado tunajilisha kitu kile kile ambacho kinachochea utumwa wetu. Dialogue: 0,0:01:17.00,0:01:21.00,Default,,0000,0000,0000,,Tunamwomba Mungu atuponye siku ya leo Dialogue: 0,0:01:21.00,0:01:30.00,Default,,0000,0000,0000,,lakini tunashikilia kitu kile kile ambacho kinazuia muujiza wetu. Dialogue: 0,0:01:30.00,0:01:35.00,Default,,0000,0000,0000,,Tunamwomba Mungu uhuru, \NUhuru wa Kiungu leo, Dialogue: 0,0:01:35.00,0:01:47.00,Default,,0000,0000,0000,,bado wengi wetu tunashikilia kitu kile kile ambacho kinatuweka mateka. Dialogue: 0,0:01:47.00,0:01:50.00,Default,,0000,0000,0000,,Kitu gani hicho? Dialogue: 0,0:01:50.00,0:02:01.00,Default,,0000,0000,0000,,Kutosamehe, uchungu, \Nmaudhi katika mioyo yetu. Dialogue: 0,0:02:01.00,0:02:11.00,Default,,0000,0000,0000,,Tunagaagaa katika sumu ya uchungu, lakini tunashangaa kwa nini bado tu wagonjwa kiroho. Dialogue: 0,0:02:11.00,0:02:15.00,Default,,0000,0000,0000,,Watu wa Mungu, imetosha! Dialogue: 0,0:02:15.00,0:02:23.00,Default,,0000,0000,0000,,Usingojee wakati unaofaa zaidi ili kufanya moyo wako utulie na Mungu. Dialogue: 0,0:02:23.00,0:02:30.00,Default,,0000,0000,0000,,Usingojee wakati unaofaa zaidi ili kuachilia msamaha kwa mtu huyo Dialogue: 0,0:02:30.00,0:02:36.00,Default,,0000,0000,0000,,aliyekudhulumu, aliyekudhuru, aliyekushitaki kwa uwongo, aliyekusingizia. Dialogue: 0,0:02:36.00,0:02:39.00,Default,,0000,0000,0000,,Sasa ni wakati uliowekwa. Dialogue: 0,0:02:39.00,0:02:49.00,Default,,0000,0000,0000,,Hivi sasa, kwa kila moyo uliofungwa na uchungu - nasema, ufunguliwe! Dialogue: 0,0:02:49.00,0:02:53.00,Default,,0000,0000,0000,,Ufunguliwe, katika jina kuu \Nla Yesu Kristo! Dialogue: 0,0:03:07.00,0:03:13.00,Default,,0000,0000,0000,,Dawa pekee ya sumu ya dhambi ni Damu ya thamani ya Yesu Kristo. Dialogue: 0,0:03:13.00,0:03:22.00,Default,,0000,0000,0000,,Hivi sasa, kwa kila moyo ulio na sumu ya kutosamehe, maumivu ya zamani, chuki - Dialogue: 0,0:03:22.00,0:03:30.00,Default,,0000,0000,0000,,Utakaswe kwa Damu ya Yesu Kristo! Dialogue: 0,0:03:55.00,0:04:06.00,Default,,0000,0000,0000,,Kizuizi hicho moyoni mwako - \Nkivunjwe kwa uwezo wa Mungu! Dialogue: 0,0:04:17.00,0:04:21.00,Default,,0000,0000,0000,,Kizuizi chochote cha kiroho \Nkwa muujiza wako leo, Dialogue: 0,0:04:21.00,0:04:31.00,Default,,0000,0000,0000,,Ninasema kwa imani katika jina la Yesu Kristo - ondolewa! Uondolewe sasa hivi! Dialogue: 0,0:04:45.00,0:04:50.00,Default,,0000,0000,0000,,Ndiyo, watu wa Mungu! \NNaweza kuona mioyo yenu iko tayari. Dialogue: 0,0:04:50.00,0:04:54.00,Default,,0000,0000,0000,,Ninaweza kuona mioyo yenu iko tayari \Nkupokea sasa hivi. Dialogue: 0,0:04:54.00,0:05:05.00,Default,,0000,0000,0000,,Biblia inasema katika 1 Yohana 1:5 Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza. Dialogue: 0,0:05:05.00,0:05:10.00,Default,,0000,0000,0000,,Sasa hivi, kwa mamlaka \Nkatika jina la Yesu Kristo - Dialogue: 0,0:05:10.00,0:05:21.00,Default,,0000,0000,0000,,Tengwa na giza! Dialogue: 0,0:05:35.00,0:05:42.00,Default,,0000,0000,0000,,Popote zana hizo za giza zinazofanya kazi katika maisha yako - Dialogue: 0,0:05:42.00,0:05:49.00,Default,,0000,0000,0000,,leo, kuwe na mwanga! Dialogue: 0,0:05:49.00,0:05:55.00,Default,,0000,0000,0000,,Nuru nyumbani kwako! Nuru katika afya yako! Nuru katika kazi yako! Nuru katika familia yako! Dialogue: 0,0:05:55.00,0:05:59.00,Default,,0000,0000,0000,,Pokea nuru ya Mungu sasa hivi! Dialogue: 0,0:06:20.00,0:06:25.00,Default,,0000,0000,0000,,Kuwa huru kutoka katika madhihirisho yote \Nya giza! Dialogue: 0,0:06:25.00,0:06:28.00,Default,,0000,0000,0000,,Ufunguliwe kutoka katika utumwa huo! Dialogue: 0,0:06:28.00,0:06:30.00,Default,,0000,0000,0000,,Ufunguliwe kutoka katika mateso hayo! Dialogue: 0,0:06:30.00,0:06:33.00,Default,,0000,0000,0000,,Ufunguliwe kutoka katika ndoto hiyo mbaya! Dialogue: 0,0:06:33.00,0:06:35.00,Default,,0000,0000,0000,,Ufunguliwe kutoka katika uraibu huo! Dialogue: 0,0:06:35.00,0:06:39.00,Default,,0000,0000,0000,,Ufunguliwe kutoka katika laana hiyo ya kizazi! Dialogue: 0,0:06:57.00,0:07:03.00,Default,,0000,0000,0000,,Katika 1 Wafalme 18:28, kisa cha Nabii Eliya na manabii wa Baali, Dialogue: 0,0:07:03.00,0:07:09.00,Default,,0000,0000,0000,,Biblia inasema moto wa Bwana ukaanguka! Dialogue: 0,0:07:09.00,0:07:13.00,Default,,0000,0000,0000,,Sasa hivi, naona moto wa Bwana ukianguka nyumbani kwako! Dialogue: 0,0:07:13.00,0:07:16.00,Default,,0000,0000,0000,,Moto wa Bwana ukianguka juu ya moyo wako! Dialogue: 0,0:07:16.00,0:07:25.00,Default,,0000,0000,0000,,Moto wa Bwana ukianguka sasa hivi - ukiteketeza maumivu hayo, mateso hayo, utumwa huo! Dialogue: 0,0:07:25.00,0:07:27.00,Default,,0000,0000,0000,,Kamata moto! Dialogue: 0,0:07:49.00,0:07:54.00,Default,,0000,0000,0000,,Ndiyo, kamata moto wa Roho Mtakatifu na upokee uponyaji wako! Dialogue: 0,0:07:54.00,0:07:59.00,Default,,0000,0000,0000,,Kamata moto wa Roho Mtakatifu na kupokea ukombozi wako! Dialogue: 0,0:07:59.00,0:08:04.00,Default,,0000,0000,0000,,Kamata moto wa Roho Mtakatifu na upokee mafanikio yako! Dialogue: 0,0:08:04.00,0:08:09.00,Default,,0000,0000,0000,,Kamata moto wa Roho Mtakatifu na upokee uhuru wako leo! Dialogue: 0,0:08:26.00,0:08:36.00,Default,,0000,0000,0000,,Hivi sasa, dhiki hiyo, ulevi ulioingia maishani mwako kupitia roho za mababu, Dialogue: 0,0:08:36.00,0:08:41.00,Default,,0000,0000,0000,,laana za kizazi - \Nanza kuivunja sasa hivi! Dialogue: 0,0:08:41.00,0:08:43.00,Default,,0000,0000,0000,,Vunja minyororo ya mateso! Dialogue: 0,0:08:43.00,0:08:46.00,Default,,0000,0000,0000,,Vunja minyororo ya uraibu! Ivunjwe! Dialogue: 0,0:09:08.00,0:09:14.00,Default,,0000,0000,0000,,Uraibu huo wa pombe - uvunjwe, \Nkatika jina la Yesu Kristo! Dialogue: 0,0:09:14.00,0:09:20.00,Default,,0000,0000,0000,,Uraibu huo wa sigara - uvunjwe, \Nkatika jina la Yesu Kristo! Dialogue: 0,0:09:20.00,0:09:28.00,Default,,0000,0000,0000,,Uraibu huo wa ponografia na punyeto - uvunjwe sasa hivi! Dialogue: 0,0:09:46.00,0:09:49.00,Default,,0000,0000,0000,,Ndiyo, watu wa Mungu, \Nkamata moto wa Roho Mtakatifu. Dialogue: 0,0:09:49.00,0:09:57.00,Default,,0000,0000,0000,,Weka mkono wako mahali ambapo umekuwa ukipata maumivu, magonjwa, mateso. Dialogue: 0,0:09:57.00,0:10:02.00,Default,,0000,0000,0000,,Kamata moto wa Roho Mtakatifu \Nna upokee leo! Dialogue: 0,0:10:19.00,0:10:30.00,Default,,0000,0000,0000,,Ninazungumza na roho hiyo ya uchungu.\NSikiliza sauti ya Mungu. Dialogue: 0,0:10:30.00,0:10:36.00,Default,,0000,0000,0000,,Toka, kwa jina la Yesu Kristo! Dialogue: 0,0:10:36.00,0:10:42.00,Default,,0000,0000,0000,,Maumivu hayo, mateso hayo, ugonjwa huo - toka nje! Dialogue: 0,0:10:58.00,0:11:06.00,Default,,0000,0000,0000,,Chochote ambacho shetani ameweka kwenye mfumo wako na kusababisha maumivu, ugonjwa - Dialogue: 0,0:11:06.00,0:11:11.00,Default,,0000,0000,0000,,Ninasema hivi sasa, Ondoshwa nje! Dialogue: 0,0:11:11.00,0:11:15.00,Default,,0000,0000,0000,,Usafishwe kwa Damu\Nya Yesu Kristo! Dialogue: 0,0:11:15.00,0:11:17.00,Default,,0000,0000,0000,,Tapika! Tapika huo uchungu! Dialogue: 0,0:11:17.00,0:11:21.00,Default,,0000,0000,0000,,Tapika hiyo sumu! \NItapike sasa hivi! Dialogue: 0,0:11:41.00,0:11:51.00,Default,,0000,0000,0000,,Hiyo sumu ya kiroho inayochafua mwili wako, ikitesa mfumo wako, kuharibu viungo vyako - Dialogue: 0,0:11:51.00,0:11:55.00,Default,,0000,0000,0000,,Nasema, fichuliwa! Dialogue: 0,0:11:55.00,0:12:00.00,Default,,0000,0000,0000,,Itapike sasa hivi! Itapike, \Nkatika jina la Yesu Kristo! Dialogue: 0,0:12:00.00,0:12:07.00,Default,,0000,0000,0000,,Tapika hiyo sumu, adha, ugonjwa! Upone! Dialogue: 0,0:12:24.00,0:12:35.00,Default,,0000,0000,0000,,Ninazungumza na mateso hayo katika uwezo wako, \Nkatika mfumo wako, katika viungo vyako. Dialogue: 0,0:12:35.00,0:12:45.00,Default,,0000,0000,0000,,Hilo shinikizo la damu, Hiyo high cholesterol, hicho kisukari - Uponywa! Dialogue: 0,0:12:45.00,0:12:48.00,Default,,0000,0000,0000,,Upone sasa hivi! Dialogue: 0,0:13:08.00,0:13:19.00,Default,,0000,0000,0000,,Ugumu huo wa kutembea, ugumu wa kula, ugumu wa kupumua - uponywe! Dialogue: 0,0:13:19.00,0:13:21.00,Default,,0000,0000,0000,,Upone sasa hivi! Dialogue: 0,0:13:40.00,0:13:49.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa mara nyingine tena, weka mkono wako, kama kitendo cha imani, mahali popote unapopata maumivu. Dialogue: 0,0:13:49.00,0:13:54.00,Default,,0000,0000,0000,,Ikiwa una picha ya mpendwa, mtu wa familia ambaye ni mgonjwa, Dialogue: 0,0:13:54.00,0:13:56.00,Default,,0000,0000,0000,,Shikilia picha hiyo kwa imani. Dialogue: 0,0:13:56.00,0:14:00.00,Default,,0000,0000,0000,,Hebu tusihi Damu ya Yesu \Njuu ya hali hiyo. Dialogue: 0,0:14:00.00,0:14:09.00,Default,,0000,0000,0000,,Kumbuka, ni sala ya Kimaandiko inayoachilia nguvu za Mungu. Dialogue: 0,0:14:09.00,0:14:18.00,Default,,0000,0000,0000,,Katika Isaya 53:5, inasema, \N“Kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” Dialogue: 0,0:14:18.00,0:14:25.00,Default,,0000,0000,0000,,Sasa hivi, anza kusihi Damu ya Yesu juu ya hali yako, Dialogue: 0,0:14:25.00,0:14:29.00,Default,,0000,0000,0000,,juu ya familia yako, juu ya afya yako, \Njuu ya kesi hiyo. Dialogue: 0,0:14:29.00,0:14:35.00,Default,,0000,0000,0000,,Omba kwa Damu ya Yesu sasa hivi. Dialogue: 0,0:14:35.00,0:14:39.00,Default,,0000,0000,0000,,Sihi Damu ya Yesu Kristo. Dialogue: 0,0:15:02.00,0:15:06.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa wale ambao wameunganishwa na familia yako, Dialogue: 0,0:15:06.00,0:15:08.00,Default,,0000,0000,0000,,Nataka mje pamoja sasa hivi. Dialogue: 0,0:15:08.00,0:15:11.00,Default,,0000,0000,0000,,Nataka nyinyi mje pamoja \Nna kuomba pamoja. Dialogue: 0,0:15:11.00,0:15:13.00,Default,,0000,0000,0000,,Tunakwenda kuziombea familia zetu. Dialogue: 0,0:15:13.00,0:15:23.00,Default,,0000,0000,0000,,Ninaamuru kila roho ya kizuizi \NIiache familia yako! Dialogue: 0,0:15:23.00,0:15:25.00,Default,,0000,0000,0000,,Iachie familia yako leo! Dialogue: 0,0:15:38.00,0:15:48.00,Default,,0000,0000,0000,,Ninaamuru kila roho ya vilio iiache familia yako sasa hivi! Dialogue: 0,0:16:01.00,0:16:12.00,Default,,0000,0000,0000,,Ninaamuru kila roho inayosumbua ustawi wa familia yako iondoke sasa hivi! Dialogue: 0,0:16:12.00,0:16:14.00,Default,,0000,0000,0000,,Ondoka, kwa jina la Yesu Kristo! Dialogue: 0,0:16:30.00,0:16:39.00,Default,,0000,0000,0000,,Roho yoyote ya mpasuko ambayo inajaribu kugawanya familia yako - Dialogue: 0,0:16:39.00,0:16:46.00,Default,,0000,0000,0000,,Namwambia huyo roho wa ajabu, ondoka! \NOndolewa sasa hivi! Dialogue: 0,0:17:01.00,0:17:11.00,Default,,0000,0000,0000,,Kila nguvu ya kiroho inayofanya kazi dhidi ya umoja wenu, umoja, amani kama familia - Dialogue: 0,0:17:11.00,0:17:16.00,Default,,0000,0000,0000,,Ondolewa! Ondolewe sasa hivi! Dialogue: 0,0:17:35.00,0:17:43.00,Default,,0000,0000,0000,,Katika familia yako, kamata moto wa \NRoho Mtakatifu na acha furaha itawale! Dialogue: 0,0:17:43.00,0:17:47.00,Default,,0000,0000,0000,,Kamata moto wa Roho Mtakatifu na \Namani itawale! Dialogue: 0,0:17:47.00,0:17:53.00,Default,,0000,0000,0000,,Kamata moto wa Roho Mtakatifu na \Nuache umoja utawale! Dialogue: 0,0:17:53.00,0:17:57.00,Default,,0000,0000,0000,,Pokea kwa imani katika jina la \NYesu Kristo! Dialogue: 0,0:18:19.00,0:18:27.00,Default,,0000,0000,0000,,Kila roho itendayo kazi \Nkinyume cha uthabiti wenu, Dialogue: 0,0:18:27.00,0:18:34.00,Default,,0000,0000,0000,,ambayo inasababisha kutofautiana katika kutembea kwako kiroho na Bwana - Dialogue: 0,0:18:34.00,0:18:43.00,Default,,0000,0000,0000,,Namwambia huyo roho wa ajabu, toka nje!\NToka, katika jina la Yesu Kristo! Dialogue: 0,0:19:03.00,0:19:12.00,Default,,0000,0000,0000,,Najua kuna wengi wetu ambao tumekuwa tukipata msongo wa mawazo usio wa kawaida Dialogue: 0,0:19:12.00,0:19:25.00,Default,,0000,0000,0000,,katika maeneo yetu ya kazi, kazi, familia, ndoa na fedha. Dialogue: 0,0:19:25.00,0:19:35.00,Default,,0000,0000,0000,,Hivi sasa, kwa kila moyo uliounganishwa kwa wakati huu ambao unasumbuliwa na mafadhaiko yasiyo ya kawaida - Dialogue: 0,0:19:35.00,0:19:39.00,Default,,0000,0000,0000,,Ninasema, pokea nguvu za Kimungu! Dialogue: 0,0:19:39.00,0:19:42.00,Default,,0000,0000,0000,,Pokea nguvu isiyo ya kawaida! Dialogue: 0,0:19:42.00,0:19:45.00,Default,,0000,0000,0000,,Pokea nguvu za kushinda! Dialogue: 0,0:19:45.00,0:19:50.00,Default,,0000,0000,0000,,Pokea nguvu za kushinda, \Nkatika jina la Yesu Kristo. Dialogue: 0,0:20:08.00,0:20:19.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa ule moyo uliolemewa na mitego na mahangaiko ya maisha haya - fanywa upya leo! Dialogue: 0,0:20:19.00,0:20:23.00,Default,,0000,0000,0000,,Uwe huru, katika jina la Yesu Kristo! Dialogue: 0,0:20:44.00,0:20:53.00,Default,,0000,0000,0000,,Ukombolewe na roho hiyo ya ulegevu. Dialogue: 0,0:20:53.00,0:20:57.00,Default,,0000,0000,0000,,Ufanywe upya! Dialogue: 0,0:20:57.00,0:21:03.00,Default,,0000,0000,0000,,Katika roho yako, ndani ya nafsi yako, katika mwili wako - \Nufanywe upya leo! Dialogue: 0,0:21:19.00,0:21:23.00,Default,,0000,0000,0000,,Ufanywe upya ili uendelee kukazana! Dialogue: 0,0:21:23.00,0:21:25.00,Default,,0000,0000,0000,,Fanywa upya ili uendelee! Dialogue: 0,0:21:25.00,0:21:28.00,Default,,0000,0000,0000,,Fanywa upya ili uendelee kukua! Dialogue: 0,0:21:28.00,0:21:32.00,Default,,0000,0000,0000,,Ufanywe upya ili uendelee kung’aa kwa furaha ya Bwana! Dialogue: 0,0:21:32.00,0:21:34.00,Default,,0000,0000,0000,,Ifanywe upya sasa hivi! Dialogue: 0,0:21:50.00,0:21:59.00,Default,,0000,0000,0000,,Sasa hivi, mwombe Mungu Mwenyezi \Nakusaidie kutenganisha Dialogue: 0,0:21:59.00,0:22:05.00,Default,,0000,0000,0000,,kutoka kwa chochote kinachojaribu kukutenganisha Naye. Dialogue: 0,0:22:05.00,0:22:06.00,Default,,0000,0000,0000,,Muulize sasa hivi. Dialogue: 0,0:22:28.00,0:22:33.00,Default,,0000,0000,0000,,Najua kuna wengi wetu tunapambana \Nna udhaifu. Dialogue: 0,0:22:33.00,0:22:39.00,Default,,0000,0000,0000,,Inaweza kuwa udhaifu wa kimwili, kihisia, kiakili au kiroho. Dialogue: 0,0:22:39.00,0:22:44.00,Default,,0000,0000,0000,,Haijalishi udhaifu huo ni upi, \Nahadi ya Mungu ni hiyo Dialogue: 0,0:22:44.00,0:22:50.00,Default,,0000,0000,0000,,Atadhihirisha nguvu zake \Nkatika udhaifu huo. Dialogue: 0,0:22:50.00,0:22:51.00,Default,,0000,0000,0000,,Muulize sasa hivi. Dialogue: 0,0:22:51.00,0:22:55.00,Default,,0000,0000,0000,,Mwombe Mungu aonyeshe nguvu zake \Nkatika udhaifu wako. Dialogue: 0,0:22:55.00,0:23:00.00,Default,,0000,0000,0000,,Mwambie adhihirishe nguvu zake katika udhaifu wako sasa hivi. Dialogue: 0,0:23:27.00,0:23:31.00,Default,,0000,0000,0000,,Kumbuka, ulikuwa ni udhaifu wa Daudi Dialogue: 0,0:23:31.00,0:23:39.00,Default,,0000,0000,0000,,ambao kwa hakika ulionyesha nguvu za Mungu katika kukutana kwake na Goliathi. Dialogue: 0,0:23:39.00,0:23:44.00,Default,,0000,0000,0000,,Mwambie Mungu sasa hivi adhihirishe nguvu zake katika udhaifu wako, Dialogue: 0,0:23:44.00,0:23:48.00,Default,,0000,0000,0000,,ili utukufu wake uonekane katika maisha yako. Dialogue: 0,0:23:48.00,0:23:50.00,Default,,0000,0000,0000,,Muulize sasa hivi. Dialogue: 0,0:24:22.00,0:24:27.00,Default,,0000,0000,0000,,Katika jina kuu la Yesu Kristo tunaomba. Dialogue: 0,0:24:33.00,0:24:43.00,Default,,0000,0000,0000,,Watu wa Mungu najua mmepatwa moto wa Roho Mtakatifu leo. Dialogue: 0,0:24:43.00,0:24:49.00,Default,,0000,0000,0000,,Na nini kinatokea wakati roho yako inapounganishwa na Roho Wake? Dialogue: 0,0:24:49.00,0:24:51.00,Default,,0000,0000,0000,,Uponyaji hufanyika. Dialogue: 0,0:24:51.00,0:24:52.00,Default,,0000,0000,0000,,Ukombozi unafanyika. Dialogue: 0,0:24:52.00,0:24:55.00,Default,,0000,0000,0000,,Uhuru unafanyika. Dialogue: 0,0:24:55.00,0:24:56.00,Default,,0000,0000,0000,,Mafanikio hufanyika. Dialogue: 0,0:24:56.00,0:25:00.00,Default,,0000,0000,0000,,Umeipokea katika Roho leo! Dialogue: 0,0:25:00.00,0:25:11.00,Default,,0000,0000,0000,,Biblia inasema kwamba Mungu ametuita kutoka gizani na kutuingiza katika nuru yake ya ajabu! Dialogue: 0,0:25:11.00,0:25:18.00,Default,,0000,0000,0000,,Leo, Mungu amekuita utoke katika magonjwa na uwe na afya njema. Dialogue: 0,0:25:18.00,0:25:22.00,Default,,0000,0000,0000,,Amewaita kutoka katika utumwa \Nna kuingia katika uhuru. Dialogue: 0,0:25:22.00,0:25:26.00,Default,,0000,0000,0000,,Amekuita kutoja kwenye hofu na imani. Dialogue: 0,0:25:26.00,0:25:30.00,Default,,0000,0000,0000,,Amekuita kwa uhuru wako leo. Dialogue: 0,0:25:30.00,0:25:33.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hivyo sasa hivi, anza kufurahi! Dialogue: 0,0:25:33.00,0:25:41.00,Default,,0000,0000,0000,,Furahia uhuru wako, ukombozi, uponyaji, mafanikio! Dialogue: 0,0:25:41.00,0:25:48.00,Default,,0000,0000,0000,,Hata kama bado haujaona udhihirisho huo kwa macho au kimwili, unaweza kufurahi! Dialogue: 0,0:25:48.00,0:25:51.00,Default,,0000,0000,0000,,Unaweza kufurahi kama kitendo cha imani. Dialogue: 0,0:25:51.00,0:25:55.00,Default,,0000,0000,0000,,Furahia sasa hivi! Dialogue: 0,0:25:55.00,0:26:03.00,Default,,0000,0000,0000,,Na mnapofurahia watu wa Mungu ngoja niwakumbushe jambo la maana sana. Dialogue: 0,0:26:03.00,0:26:19.00,Default,,0000,0000,0000,,Pale Mungu anapoingilia kati, huwezi kutenganisha suluhisho na wokovu. Dialogue: 0,0:26:19.00,0:26:27.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa maneno mengine, chochote unachopokea kutoka kwa Yesu Kristo - Dialogue: 0,0:26:27.00,0:26:33.00,Default,,0000,0000,0000,,ni juu ya jukwaa la wokovu\Nwa nafsi yako. Dialogue: 0,0:26:33.00,0:26:39.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hivyo, lazima uangalie zaidi ya muujiza uliopokea leo. Dialogue: 0,0:26:39.00,0:26:46.00,Default,,0000,0000,0000,,tukio ulilokumbana nalo leo, \Nmguso uliohisi leo - angalia zaidi ya hapo. Dialogue: 0,0:26:46.00,0:26:53.00,Default,,0000,0000,0000,,Je, utaendeleaje na safari ya imani? Dialogue: 0,0:26:53.00,0:27:10.00,Default,,0000,0000,0000,,Yesu Kristo alisema kwamba lazima tukeshe na kuomba (Mathayo 26:40-41). Dialogue: 0,0:27:10.00,0:27:21.00,Default,,0000,0000,0000,,Jihadhari na ushawishi wowote katika ulimwengu huu ambao unajaribu kukudanganya Dialogue: 0,0:27:21.00,0:27:32.00,Default,,0000,0000,0000,,kupunguza kiwango cha Neno la Mungu na kuifanya dhambi kuwa ya kawaida. Jihadharini. Dialogue: 0,0:27:32.00,0:27:38.00,Default,,0000,0000,0000,,Weka moyo wako upatane na kweli ya Neno la Mungu. Dialogue: 0,0:27:38.00,0:27:44.00,Default,,0000,0000,0000,,Fanya maisha yako yaendane na nuru yake Dialogue: 0,0:27:44.00,0:27:51.00,Default,,0000,0000,0000,,na nuru hiyo iangaze ndani yako na kupitia kwako, katika jina la Yesu.