Hii kura ya Britain kuuacha Umoja wa Uropa italeta madhara makuu tusioweza kutabiri. Kwengine twaweza, ila kwingi hatuwezi. Lakini kwa sasa ni vigumu kuona nchi hizi nyingi tofauti zikiwa na historia tofauti sana, zikiwemo historia za uadui kwa wenzio, ni vigumu sana kuziona zikiweza kuungana pamoja. Asili ya Umoja wa Uropa ni, bila shaka, Vita vya pili vya Ulimwengu- hili janga lisilo la kawaida- kizazi cha watu wa Uropa, waliosema, "Hatutafanya hivi tena!" Kulikuwa na kuelewana eti, ungalitaka kuweka amani, inabidi uwe na aina ya mfumo wa kiuchumi ambao husababishi chuki ama kusababisha ubinafsi. Watu wengi hawataelewa ama kujua eti dini ilikuwa hasa chembe muhimu sana katika uanzishwaji wa jamii ya Uvhumi Uropa. Bado kuna kipengele cha kidini kwa wingi wa mjadala katika Umoja wa Uropa. Katika mwanzo wa 2000, aliyekuwa Rais wa Tume ya Uropa, Romano Prodi, alinakiri kitabu. Kiliandikwa kwa Ki-Italia, lakini tafsiri ya mada ina maana, "Wazo la Uropa". Na akasema, "Nini chaweza shika hizi nchi nyingi tofauti? Haitoshi kwa wasomi kupendekeza muungano wa kisiasa. Lazima pawe na jambo la kitamaduni." Na akasema, "Lile jambo moja wa-Uropa wote hufanana, jambo moja la kutufunganisha pamoja ni uaminifu kwa Kanisa." Lakini alikuwa muItalia. Alimaanishaje? Alimaanisha, Kanisa la Kirumi Katoliki. Hio ndio hadithi ya watu wanaojaribu kufanya Uropa iwe chumba-umeme na bado kushindwa, tena na tena. Muwaze Napoleon: yote yalionekana timilifu, ila, mwongo tu, na ikashindwa. Muwaze Hitler: ikashindwa. Kama mwanaUropa, nilikua nikiuliza: "Uropa huingianaje na unabii wa Biblia?" Danieli sura 2: mfalme anaota ndoto - Nebuchardnezzar anaota - na kwa hiyo ndoto, anaona mchongo kubawa, mchongo wa kucutia. Vyuma tofauti vinatumika kuashiria falme tofauti. anatagulia kama kichwa, kichwa cha dhahabu Babylon, Medo-Persia, himaya ya Kiyunani na mwisho, nguvu ya himaya ya Kirumi, lakini kuna jambo lingine. Kuna vidole vya miguu, na miguu, iliyoundwa na mchanganyiko wa udongo na chuma. Na Danieli, kwa namna, asema, "Havitashikamana. Vingine vina nguvu, vingine ni dhaifu." Na hio inaonekana ndiyo hadithi ya Uropa. Haswa unapotizama matukio hivi karibuni- matukio Uyunani, Spain, Italia, Cyprus - ambapo msingi wa nchi za EU, nchi za kaskazini za EU, zinaonekana zikionea, jinsi ya kuingilia mwaswala ya watu, vilevile inabidi tuseme, aina zote za chuki za kikablia na kitaifa zilizoonekana kama ziliaga katika mabaki ya Vita vya pili vya Ulimwengu, na havijaonekana kwa miak 70, vinarejea kifulani kwa fujo na kimiujiza. Hivo, ukiwaza matatizo yote yaliyomo kwa Umoja wa Uropa, kwa moja ya zile tatu uchumi kuu, inayochangia zaidi kwa ulinzi wa kawaida na sera geni, kuondoka - hii italeta utupu pale katikati. Unabii sio tu jambo la kuvutia tusomalo, wajua, kwa vitabu historia, ama madarasa ya Biblia. Twawezapata mielekeo yetu, mwelekeo muu, picha kuu kutoka unabii. Maandiko yanatwambia hapatakuwa Uropa moja nyingine, Itakuwa dhaifu and yenye nguvu. Na tunaona hilo. Lakini hadithi haikomei pale. Danieli sura 2 haikomi na ule mchongo na miguu ulochanganyika chuma na udongo. Kuna mwamba: ni ndogo mwanzo, lakini lili jiwe linauvunja mchongo wote. Hilo jiwe ndogo linalokuwa jiwe kubwa, ni Yesu Kristo. Ufalme mpya. Ufalme wa Mungu.