Weka mkono wako popote unapohisi maumivu
katika mwili wako.
Weka mkono wako hapo kama mahali pa kuwasiliana kwa imani.
Popote pale ugonjwa huo ulipokita mizizi au kukaa ndani yako,
Natangaza uponyaji!
Uponywe, katika jina la Yesu!
Maandiko yanasema katika 1 Wakorintho 6:19 miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu;
sio hekalu la roho ya magonjwa, mateso au maumivu.
Hivi sasa, kiungo chochote katika mwili wako
kilichoharibiwa na roho ya ugonjwa,
Ninatangaza urejesho.
Urejeshwe!