WEBVTT 00:00:08.380 --> 00:00:09.561 Asante 00:00:16.270 --> 00:00:21.200 Palikuwa na mfalme nchini India, Maharaja na siku yake ya kuzaliwa ilitolewa amri 00:00:21.200 --> 00:00:24.200 kwamba machifu wote walete zawadi kwa mfalme. 00:00:24.400 --> 00:00:28.370 Wengine wakaleta hariri bora, wengine wakaleta panga maridadi, 00:00:28.370 --> 00:00:29.490 wengine dhahabu 00:00:29.490 --> 00:00:32.659 mwisho wa mstari alikuja akitembea mzee mdogo mwenye makunyanzi 00:00:32.659 --> 00:00:36.630 ambaye alitembea kutoka kijijini kwake kwa safari ya siku nyingi kando ya bahari. 00:00:36.630 --> 00:00:41.150 alipokuwa akisogea mwana mfalme akauliza, 'Umemletea zawadi gani Mfalme?' 00:00:41.457 --> 00:00:44.750 Na mzee yule taratibu sana akakunjua mkono wake kuonyesha 00:00:44.750 --> 00:00:49.600 kombe la baharini zuri sana, lenye makoa ya zambarau na njano,nyekundu na bluu. 00:00:50.160 --> 00:00:51.380 Na mwana Mfalme akasema, 00:00:51.460 --> 00:00:54.400 "Hiyo si zawadi kwa Mfalme! Ni zawadi gani hiyo?" 00:00:54.600 --> 00:00:57.400 Mzee yule akamwangalia taratibu na kusema 00:00:57.590 --> 00:01:00.750 "Kutembea mwendo mrefu.. ni sehemu ya zawadi" 00:01:01.060 --> 00:01:02.560 (Kicheko) 00:01:02.900 --> 00:01:05.970 Baada ya muda mfupi, Nitawapa zawadi, 00:01:05.970 --> 00:01:08.270 zawadi niaminiyo ni zawadi inayostahili kuenezwa. 00:01:08.290 --> 00:01:10.050 Ila kabla ya hayo, ngoja niwachukue 00:01:10.050 --> 00:01:11.960 kwenye mwendo wangu mrefu. 00:01:12.160 --> 00:01:13.740 Kama wengi wenu, 00:01:13.740 --> 00:01:15.320 Nilianza maisha kama mtoto mdogo. 00:01:15.320 --> 00:01:17.460 Wangapi kati yenu mlianza maisha kama mtoto ? 00:01:17.460 --> 00:01:18.510 Aliyezaliwa mchanga? 00:01:18.740 --> 00:01:20.500 Karibia nusu yenu.. Sawa 00:01:20.570 --> 00:01:21.590 (Kicheko) 00:01:21.820 --> 00:01:24.910 Na mliobakia, vipi? Mlizaliwa mkiwa watu wazima? 00:01:25.060 --> 00:01:27.640 Ama kweli, nataka kukutana na mama zenu! 00:01:27.820 --> 00:01:29.460 Ongelea yasiyowezekana! 00:01:30.560 --> 00:01:34.740 Nikiwa mtoto mdogo, siku zote nilipendezwa kufanya mambo yasiyowezekana 00:01:35.620 --> 00:01:38.880 Leo ni siku ambayo nimekuwa nikiitarajia kwa miaka mingi, 00:01:38.880 --> 00:01:41.000 kwa sababu leo ni siku ambayo nitajaribu 00:01:41.020 --> 00:01:43.620 kufanya yasiyowezekana mbele ya macho yenu 00:01:43.620 --> 00:01:45.460 Hapahapa TEDxMaastrich 00:01:45.800 --> 00:01:48.160 Nitaanza 00:01:48.760 --> 00:01:50.880 Kwa kuonyesha mwisho wake: 00:01:51.220 --> 00:01:52.640 Na nitawathibitishia kwamba 00:01:52.640 --> 00:01:54.940 yasiyowezekana siyo hayawezekani 00:01:55.300 --> 00:01:58.210 Na nitamalizia kwa kuwapa zawadi yenye kustahili kuieneza: 00:01:58.210 --> 00:02:01.350 Nitawaonyesha kwamba unaweza kufanya yasiyowezekana maishani mwako. 00:02:02.660 --> 00:02:05.420 katika kutafuta kufanya yasiyowezekana, nimegundua kuna 00:02:05.420 --> 00:02:08.230 mambo mawili yanayofanana kati ya watu duniani. 00:02:08.230 --> 00:02:09.870 Kila mtu ana hofu, 00:02:09.870 --> 00:02:11.640 na kila mtu ana ndoto. 00:02:12.900 --> 00:02:17.560 Katika kutafuta kufanya yasiyowezekana nimegundua kuna vitu vitatu 00:02:17.560 --> 00:02:20.100 ambavyo nimevifanya miaka mingi ambavyo 00:02:20.110 --> 00:02:23.290 vimenisababishia kufanya yasiyowezekana: 00:02:24.200 --> 00:02:26.900 Mchezo wa mpira wa kuchenga au "Trefball" 00:02:27.290 --> 00:02:28.360 Superman, 00:02:28.460 --> 00:02:29.460 na Mbu 00:02:29.460 --> 00:02:30.810 Hayo ni maneno yangu matatu makuu. 00:02:30.810 --> 00:02:33.500 Mmeshajua kwanini nafanya yasiyowezekana maishani mwangu 00:02:33.610 --> 00:02:36.220 Hivyo nitawachukua katika safari yangu, ya mwendo mrefu 00:02:36.320 --> 00:02:38.680 kutoka kwenye hofu hadi ndoto 00:02:38.740 --> 00:02:40.980 kutoka kwenye maneno hadi panga, 00:02:41.160 --> 00:02:42.740 Kutoka Mpira wa kuchenga 00:02:42.850 --> 00:02:44.020 hadi Superman 00:02:44.020 --> 00:02:45.340 hadi kwa Mbu 00:02:45.800 --> 00:02:47.360 Na ninatumaini kuwaonyesha 00:02:47.360 --> 00:02:49.900 unawezaje kufanya yasiyo wezekana maishani mwako 00:02:52.480 --> 00:02:54.934 Oktoba 4, mwaka 2007. 00:02:55.840 --> 00:02:58.120 Moyo wangu ulienda mbio, magoti yangu yalitetema 00:02:58.120 --> 00:02:59.340 nilipokuwa napanda jukwaani 00:02:59.340 --> 00:03:00.930 kwenye ukumbi wa Sanders 00:03:01.040 --> 00:03:03.240 Chuo cha Harvard kupokea 00:03:03.240 --> 00:03:06.160 Tuzo ya Ig Nobel katika Utabibu 00:03:06.160 --> 00:03:08.660 kwa kushiriki kuandika ikisiri ya utafiti wa kitabibu 00:03:08.660 --> 00:03:10.270 ulioitwa "Kumeza Upanga... 00:03:10.420 --> 00:03:11.740 ...na Athari zake" 00:03:11.870 --> 00:03:13.275 (Kicheko) 00:03:13.840 --> 00:03:17.880 Ilichapishwa kwenye jarida dogo ambalo sikuwahi kulisoma kabla, 00:03:18.460 --> 00:03:20.419 Jarida la Kitabibu la Uingereza. 00:03:21.360 --> 00:03:24.740 Na kwangu, hiyo ilikuwa ndoto isiyowezekana kuwa kweli, 00:03:24.900 --> 00:03:28.120 ilikuwa ni mshangao usiotegemewa kwa mtu kama mimi, 00:03:28.130 --> 00:03:31.459 ilikuwa ni heshima ambayo sitaweza kusahau 00:03:31.459 --> 00:03:34.539 Lakini haikuwa sehemu ya kubwa ya kukumbuka maishani mwangu. 00:03:35.540 --> 00:03:37.640 Mnamo Oktoba 4, mwaka 1967 00:03:38.020 --> 00:03:40.260 kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba 00:03:41.100 --> 00:03:43.120 aliteseka na hofu kubwa kupita kiasi. 00:03:43.460 --> 00:03:45.579 Alipojiandaa kupanda jukwaani, 00:03:45.579 --> 00:03:47.234 moyo wake ulienda mbio, 00:03:47.500 --> 00:03:49.162 magoti yake yalikuwa yakitetemeka. 00:03:49.780 --> 00:03:52.120 Alikwenda kufungua kinywa chake kuongea, 00:03:56.490 --> 00:03:58.130 maneno hayakuweza kutoka. 00:03:58.130 --> 00:04:00.040 Alisimama akitetemeka na kutoa machozi. 00:04:00.630 --> 00:04:02.360 Alipooza kwa mshtuko wa ghafla, 00:04:02.360 --> 00:04:03.760 alipatwa fadhaa kwa hofu. 00:04:03.960 --> 00:04:06.130 huyu kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba 00:04:06.130 --> 00:04:08.142 alitesekana na hofu kubwa kupita kiasi. 00:04:08.649 --> 00:04:10.330 Alikuwa na hofu ya giza, 00:04:10.520 --> 00:04:11.640 hofu ya vimo virefu, 00:04:11.640 --> 00:04:13.040 hofu ya buibui na nyoka ... 00:04:13.040 --> 00:04:15.140 Kuna yeyote anayeogopa buibui na nyoka? 00:04:15.280 --> 00:04:16.660 Naam, wachache wenu ... 00:04:16.660 --> 00:04:19.079 Alikuwa na hofu ya maji na papa ... 00:04:19.079 --> 00:04:21.939 Hofu ya madaktari na manesi na madaktari wa meno, 00:04:21.939 --> 00:04:24.680 na sindano na kutobolewa na vitu vya ncha kali. 00:04:24.680 --> 00:04:27.380 Lakini zaidi ya chochote, alikuwa na hofu ya 00:04:27.470 --> 00:04:28.470 watu 00:04:29.380 --> 00:04:31.530 Huyo kijana mwoga,mwenye aibu na mwembamba 00:04:31.540 --> 00:04:32.570 alikuwa mimi. 00:04:33.320 --> 00:04:35.997 Nilikuwa na hofu ya kushindwa na kukataliwa, 00:04:37.300 --> 00:04:39.520 kutojithamini, kujiona duni, 00:04:39.520 --> 00:04:42.840 na kitu ambacho hata hatukujua unaweza kujiandikisha kwa siku hizo: 00:04:42.840 --> 00:04:44.660 ugonjwa wa hofu ya ukaribu na watu. 00:04:44.955 --> 00:04:48.610 Kwa sababu nilikuwa na hofu, waonevu walinitania na kunipiga. 00:04:48.610 --> 00:04:52.240 Walinicheka na kuniita majina, Hawakuniruhusu kucheza nao 00:04:52.300 --> 00:04:54.260 michezo ya aina yoyote. 00:04:55.020 --> 00:04:58.056 Ah, kulikuwa na mchezo mmoja walikuwa wakiruhusu kucheza kwenye ... 00:04:58.100 --> 00:04:59.427 Mpira wa kuchenga - 00:04:59.500 --> 00:05:01.443 na sikuwa mchengaji nzuri. 00:05:01.760 --> 00:05:03.500 Waonevu waliita jina langu, 00:05:03.500 --> 00:05:05.970 na nilipoangalia niliona mipira myekundu ya kukwepa 00:05:05.970 --> 00:05:08.200 ikivurumishwa usoni wangu kwa kasi kubwa 00:05:08.210 --> 00:05:09.950 bam, bam, bam! 00:05:10.580 --> 00:05:13.220 Ninakumbuka siku nyingi nikirudi nyumbani kutoka shule, 00:05:13.300 --> 00:05:18.180 uso wangu ulikuwa mwekundu ukichonyota, masikio yangu yalikuwa mekundu yakivuma. 00:05:18.180 --> 00:05:21.140 Macho yangu yalichoma kwa machozi, 00:05:21.180 --> 00:05:23.515 na maneno yao yalichoma masikioni mwangu. 00:05:23.740 --> 00:05:25.000 Na yeyote aliyesema, 00:05:25.020 --> 00:05:28.660 "Fimbo na mawe vyaweza kunivunja mifupa, bali maneno hayatoniumiza kamwe "... 00:05:28.880 --> 00:05:30.131 Ni uongo. 00:05:30.310 --> 00:05:31.980 Maneno huweza kukata kama kisu. 00:05:31.980 --> 00:05:34.030 Maneno huweza kupenya kama upanga. 00:05:34.210 --> 00:05:36.040 Maneno huwezafanya majeraha yenye kina 00:05:36.040 --> 00:05:37.780 yasiweze kuonekana. 00:05:38.150 --> 00:05:41.070 Hivyo nilikuwa na hofu. Na maneno yalikuwa adui yangu mkubwa. 00:05:41.260 --> 00:05:42.491 Bado ni adui yangu. 00:05:43.355 --> 00:05:45.300 Lakini pia nilikuwa na ndoto. 00:05:45.300 --> 00:05:47.980 Nilienda nyumbani na kutorokea kwenye futuhi za Superman 00:05:47.980 --> 00:05:49.774 na nilisoma futuhi za Superman 00:05:49.774 --> 00:05:53.440 na niliota kutaka kuwa shujaa mkubwa kama Superman. 00:05:53.480 --> 00:05:56.240 Nilitaka kupigania kweli na haki, 00:05:56.240 --> 00:05:58.680 Nilitaka kupambana dhidi ya wahalifu na mahasimu, 00:05:58.680 --> 00:06:02.895 Nilitaka kupaa duniani kote kufanya vitendo vya ujasiri kuokoa maisha. 00:06:03.400 --> 00:06:05.850 Nilikuwa pia navutiwa mno na vitu vilivyokuwa kweli. 00:06:05.860 --> 00:06:09.460 Nilisoma kitabu cha Rekodi za Dunia za Guiness na kitabu cha Ripley kiitwacho Amini au Usiamini. 00:06:09.460 --> 00:06:13.080 Yeyote kati yenu amewahi kusoma kitabu cha Rekodi za Dunia za Guinness au kitabu cha Ripley? 00:06:13.100 --> 00:06:14.390 Navipenda vitabu hivi! 00:06:14.390 --> 00:06:16.270 Niliona watu wafanyao ujasiri halisia. 00:06:16.270 --> 00:06:17.790 Nikasema, Nataka kufanya hivyo. 00:06:17.790 --> 00:06:19.330 Ikiwa waonevu hawataniruhusu 00:06:19.330 --> 00:06:21.030 kucheza katika michezo yao yoyote, 00:06:21.030 --> 00:06:23.335 Nataka kufanya maajabu, ujasiri halisi. 00:06:23.335 --> 00:06:26.659 Nataka kufanya kitu cha kusifika ambacho hao waonevu hawawezi kufanya. 00:06:26.659 --> 00:06:28.609 Nataka kupata kusudi langu na wito wangu, 00:06:28.609 --> 00:06:30.729 Nataka kujua kuwa maisha yangu yana maana, 00:06:30.729 --> 00:06:33.320 Nataka kufanya kitu cha kushangaza kubadili ulimwengu; 00:06:33.320 --> 00:06:36.960 Ninataka kuthibitisha yasiyowezekana sio hayawezekani. 00:06:38.340 --> 00:06:40.240 Kupeleka mbele miaka 10 - 00:06:40.240 --> 00:06:42.706 Ilikuwa wiki kabla ya kutimiza miaka 21. 00:06:42.819 --> 00:06:46.799 Mambo mawili yalitokea kwa siku moja ambayo yangebadilisha maisha yangu milele. 00:06:47.040 --> 00:06:49.391 Nilikuwa nikiishi Tamil Nadu, India Kusini 00:06:49.540 --> 00:06:51.020 Nilikuwa mmishonari huko, 00:06:51.020 --> 00:06:53.090 na mshauri wangu, rafiki yangu aliniuliza, 00:06:53.090 --> 00:06:54.720 "Je, una Thromu, Daniel?" 00:06:54.720 --> 00:06:57.440 Na nikasema, "Thromu? Thromu ni nini? " 00:06:57.440 --> 00:07:00.490 Alisema, "Thromu ni malengo makuu ya maisha. 00:07:00.490 --> 00:07:04.630 Ni muunganiko wa ndoto na malengo, kama ungeweza 00:07:04.630 --> 00:07:07.240 kufanya chochote unachotaka, kwenda popote unapotaka 00:07:07.240 --> 00:07:08.479 kuwa mtu yeyote unayetaka, 00:07:08.479 --> 00:07:10.356 ungekwenda wapi? Ungefanya nini? 00:07:10.356 --> 00:07:11.280 Ungekuwa nani? 00:07:11.280 --> 00:07:14.500 Nikasema, "Siwezi kufanya hivyo! Naogopa sana! Naogopa mengi mno! " 00:07:14.500 --> 00:07:17.800 Usiku huo nilichukua mkeka wangu wa mchele juu ya paa la ghorofa, 00:07:17.810 --> 00:07:19.259 nikautandika chini ya nyota, 00:07:19.259 --> 00:07:21.869 na kuangalia popo wakiwashambulia mbu. 00:07:21.869 --> 00:07:26.200 Na yote niliyofikiria ilikuwa thromu, na ndoto na malengo, 00:07:26.200 --> 00:07:28.360 na wale washujaaji wenye mipira ya kuchenga. 00:07:28.760 --> 00:07:30.730 Masaa machache baadaye niliamka. 00:07:31.220 --> 00:07:33.940 Moyo wangu ulienda mbio, magoti yangu yakitetemeka. 00:07:34.080 --> 00:07:36.020 Safari hii haikuwa na hofu. 00:07:36.420 --> 00:07:38.395 Mwili wangu wote ulitikisika. 00:07:38.500 --> 00:07:40.180 Na kwa siku tano zilizofuata 00:07:40.330 --> 00:07:44.199 Nilipoteza na kurudisha fahamu, kitandani nikipigania maisha yangu. 00:07:44.199 --> 00:07:48.239 Ubongo wangu ulikuwa unawaka na homa ya malaria yenye jotoridi la 105. 00:07:48.390 --> 00:07:51.600 Na kila fahamu ziliponirudia, nilichowaza ilikuwa kuhusu thromu. 00:07:51.600 --> 00:07:53.820 Niliwaza "Nataka kufanya nini na maisha yangu?" 00:07:53.950 --> 00:07:56.380 Hatimaye, usiku kabla sijafikisha miaka 21, 00:07:56.380 --> 00:07:58.030 katika wakati wa kuelewa, 00:07:58.030 --> 00:07:59.639 Nilikuja kutambua: 00:07:59.639 --> 00:08:02.100 Nilitambua kwamba yule mbu mdogo, 00:08:02.620 --> 00:08:05.020 Anofelesi Stefensi, 00:08:05.280 --> 00:08:06.610 yule mbu mdogo 00:08:06.610 --> 00:08:08.390 aliye na uzito chini ya mikrogramu 5 00:08:08.390 --> 00:08:09.810 chini ya punje ya chumvi, 00:08:09.810 --> 00:08:12.780 anaweza kuangusha mtu wa ratili 170, mtu wa kilo 80, 00:08:12.780 --> 00:08:14.860 Niligundua kwamba alikuwa hasimu wangu. 00:08:14.860 --> 00:08:17.150 Kisha nikagundua, hapana, hapana, sio mbu, 00:08:17.150 --> 00:08:19.480 Ni vimelea vidogo ndani ya mbu, 00:08:19.480 --> 00:08:23.160 Plasmodium Falciparum, ambao huua zaidi ya watu milioni kwa mwaka 00:08:23.509 --> 00:08:25.999 Kisha nikagundua Hapana, hapana, tena ni ndogo zaidi, 00:08:25.999 --> 00:08:28.550 lakini kwangu, ilionekana kubwa zaidi. 00:08:28.550 --> 00:08:29.640 Niligundua, 00:08:29.640 --> 00:08:31.270 hofu ilikuwa hasimu yangu, 00:08:31.270 --> 00:08:32.140 vimelea yangu, 00:08:32.140 --> 00:08:34.990 vilivyonitia ulemavu na kunipooza mimi maisha yangu yote. 00:08:35.200 --> 00:08:38.080 Unajua, kuna tofauti kati ya hatari na hofu. 00:08:38.109 --> 00:08:39.699 Hatari ni halisi. 00:08:39.990 --> 00:08:42.010 Hofu ni hiari. 00:08:42.080 --> 00:08:44.309 Na nikagundua kuwa nina hiari: 00:08:44.309 --> 00:08:48.180 Aidha niishi kwa hofu, na kufa katika kushindwa usiku ule, 00:08:49.070 --> 00:08:52.080 au ningeweza kuua hofu yangu, na ningeweza 00:08:52.080 --> 00:08:56.060 kufikia ndoto zangu, Ningeweza kuthubutu kuishi maisha. 00:08:56.680 --> 00:08:59.560 Na unajua, kuna kitu kuhusu kuwa kwenye kitanda cha mauti 00:08:59.560 --> 00:09:04.080 na kukabiliwa na kifo ambacho haswa kinakufanya utake kweli kuishi maisha. 00:09:04.180 --> 00:09:07.140 Nikagundua kuwa kila mtu hufa, si kila mtu huishi. 00:09:08.040 --> 00:09:09.890 Ni katika kufa ndio sisi tunaishi. 00:09:09.890 --> 00:09:11.580 Unajua, wakati unapojifunza kufa, 00:09:11.580 --> 00:09:13.070 unajifunza kweli kuishi. 00:09:13.070 --> 00:09:15.140 Kwa hiyo nikaamua nitaenda kubadilisha 00:09:15.140 --> 00:09:16.420 hadithi yangu usiku huo. 00:09:16.915 --> 00:09:18.230 Sikutaka kufa. 00:09:18.230 --> 00:09:20.010 Hivyo nikafanya sala ndogo, nikasema, 00:09:20.010 --> 00:09:22.230 "Mungu, ukiniruhusu niishi nifikishe miaka 21, 00:09:22.230 --> 00:09:24.544 Sitaruhusu hofu itawale maisha yangu tena. 00:09:24.670 --> 00:09:26.520 Nitaziweka hofu zangu kifoni, 00:09:26.520 --> 00:09:29.530 Nitaenda kuzifikia ndoto zangu, 00:09:29.530 --> 00:09:31.270 Ninataka kubadilisha mtazamo wangu, 00:09:31.270 --> 00:09:33.540 Nataka kufanya kitu cha ajabu na maisha yangu, 00:09:33.540 --> 00:09:35.550 Nataka kupata kusudi langu na wito wangu, 00:09:35.550 --> 00:09:38.632 Ninataka kujua kuwa yasiyowezekana si hayawezekani. " 00:09:38.780 --> 00:09:42.820 Sitawaambia kama nilinusurika usiku ule; Nitawaacha mfikirie. 00:09:42.850 --> 00:09:43.978 (Kicheko) 00:09:43.978 --> 00:09:47.100 Lakini usiku huo niliandika orodha ya Thromu zangu 10 za kwanza: 00:09:47.100 --> 00:09:50.210 Niliamua nilitaka kutembelea mabara makubwa 00:09:50.210 --> 00:09:51.820 kutembelea Maajabu 7 ya Dunia 00:09:51.820 --> 00:09:53.410 kujifunza lugha nyingi, 00:09:53.410 --> 00:09:54.940 kuishi kwenye kisiwa kitupu, 00:09:54.940 --> 00:09:56.480 kuishi kwenye meli baharini, 00:09:56.480 --> 00:09:58.650 kuishi na kabila la Wahindi katika Amazon, 00:09:58.650 --> 00:10:01.210 kupanda hadi juu ya mlima mrefu kuliko yote Sweden, 00:10:01.210 --> 00:10:03.180 Nilitaka kuona mawio Mlima Everest, 00:10:03.190 --> 00:10:05.390 kufanya kazi na biashara ya muziki Nashville, 00:10:05.400 --> 00:10:07.060 Nilitaka kufanya kazi ya sarakasi, 00:10:07.080 --> 00:10:09.120 na nilitaka kuruka nje ya ndege. 00:10:09.120 --> 00:10:12.380 Zaidi ya miaka ishirini iliyofuata, Nilitimiza thromu hizo kwa wingi. 00:10:12.410 --> 00:10:14.650 Kila wakati niliondoa thromu kwenye orodha yangu, 00:10:14.650 --> 00:10:18.190 Niliongeza 5 au 10 zaidi kwenye orodha na orodha yangu iliendelea kukua. 00:10:18.800 --> 00:10:23.280 Kwa miaka saba iliyofuata, niliishi kwenye kisiwa kidogo katika Bahamas 00:10:23.320 --> 00:10:25.360 kwa karibu miaka saba 00:10:25.370 --> 00:10:27.274 katika kibanda cha makuti, 00:10:29.480 --> 00:10:33.820 nikiwinda papa na taa wa kula, nikiwa mtu pekee kwenye kisiwa, 00:10:33.820 --> 00:10:36.249 nikiwa nimevaa msuli, 00:10:36.680 --> 00:10:39.160 na nikajifunza kuogelea na papa. 00:10:39.160 --> 00:10:40.980 Na kutoka huko, nikahamia Mexico, 00:10:40.980 --> 00:10:45.000 na kisha nikasafiri kwa bonde la Mto Amazon nchini Ecuador, 00:10:45.241 --> 00:10:48.100 Pujo Pongo Ecuador, niliishi na kabila moja huko, 00:10:48.100 --> 00:10:52.180 na kidogo kidogo nilianza kuongeza kujiamini kwa thromu zangu tu. 00:10:52.180 --> 00:10:55.100 Nilihamia biashara ya muziki Nashville, kisha Sweden, 00:10:55.110 --> 00:10:57.870 nikahamia Stockholm, kufanyakazi katika biashara ya muziki, 00:10:57.870 --> 00:11:01.920 ambapo nilipanda kilele cha Ml. Kebnekaise juu ya mzunguko wa Arctic. 00:11:03.300 --> 00:11:04.750 Nilijifunza udamisi, 00:11:04.750 --> 00:11:05.860 na viinimacho, 00:11:05.860 --> 00:11:07.480 na kutembea kama ngongoti, 00:11:07.480 --> 00:11:10.440 kuendesha baiskeli kwa tairi moja, kula moto, kula kioo. 00:11:10.450 --> 00:11:13.620 Mwaka 1997 nilisikia kuna wameza panga wasiozidi kumi na mbili 00:11:13.620 --> 00:11:15.410 na nikasema, "Inabidi kufanya hivyo!" 00:11:15.420 --> 00:11:18.290 Nilikutana na mmeza panga, na nikamwomba vidokezo. 00:11:18.290 --> 00:11:20.190 Akasema, "Naam, nitakupa vidokezo 2: 00:11:20.190 --> 00:11:21.926 Namba 1: Ni hatari sana, 00:11:21.926 --> 00:11:23.948 Watu wamekufa wakifanya hivi. 00:11:23.948 --> 00:11:24.953 Namba 2: 00:11:24.953 --> 00:11:26.206 Usijaribu! " 00:11:26.206 --> 00:11:27.520 (Kicheko) 00:11:27.540 --> 00:11:29.540 Basi nikaiongeza kwenye orodha ya thromu. 00:11:30.440 --> 00:11:33.320 Na nikafanya mazoezi mara 10 hadi 12 kwa siku, kila siku 00:11:33.660 --> 00:11:35.160 kwa miaka minne. 00:11:35.209 --> 00:11:36.709 Sasa nilipigia hesabu hizo... 00:11:36.709 --> 00:11:40.020 4 x 365 [x 12] 00:11:40.020 --> 00:11:42.660 Ilikuwa karibu 13,000 majaribio yasiyofanikiwa 00:11:42.660 --> 00:11:45.420 kabla sijatia panga langu wa kwanza chini koo mwaka 2001. 00:11:46.002 --> 00:11:47.630 Wakati huo nikaweka thromu 00:11:47.630 --> 00:11:50.940 kuwa mtaalamu wa ulimwengu kwa kumeza panga. 00:11:50.970 --> 00:11:53.820 Basi nilitafuta kila kitabu, gazeti, makala ya gazeti, 00:11:53.820 --> 00:11:57.670 kila ripoti ya kitabibu, Nilijifunza fiziolojia, anatomia, 00:11:57.676 --> 00:11:59.719 Niliongea na madaktari na manesi, 00:11:59.719 --> 00:12:01.760 niliwakutanisha wameza panga wote pamoja 00:12:01.760 --> 00:12:04.250 kwenye Shirikisho la Wameza Panga Kimataifa, 00:12:04.250 --> 00:12:06.450 nikafanya ikisiri miaka 2 ya utafiti kitabibu 00:12:06.450 --> 00:12:08.580 kuhusu Umezaji wa Panga na athari zake 00:12:08.580 --> 00:12:10.980 iliyochapishwa katika Jarida la Kitabibu Uingereza. 00:12:10.980 --> 00:12:11.840 (Kicheko) 00:12:11.840 --> 00:12:12.940 Asanteni. 00:12:12.960 --> 00:12:17.748 (Makofi) 00:12:18.200 --> 00:12:21.570 Na nilijifunza mambo ya kuvutia sana kuhusu umezaji wa panga. 00:12:21.571 --> 00:12:25.260 Vitu vingine ambavyo haujawahi kufikiria kabla, hutasahau baada ya usiku huu. 00:12:25.260 --> 00:12:28.550 Wakati utakapoenda nyumbani, na unakata steki yako na kisu chako 00:12:28.550 --> 00:12:31.759 au panga, au "bestek" zako, utafikiri juu ya hili ... 00:12:34.257 --> 00:12:36.589 Nilijifunza kwamba umezaji panga ulianzia India - 00:12:36.589 --> 00:12:39.889 mahali nilipona kwa mara ya kwanza nikiwa kijana wa miaka 20 - 00:12:39.889 --> 00:12:42.290 karibu miaka 4000 ya kale, karibu 2000 BC. 00:12:42.290 --> 00:12:45.580 Zaidi ya miaka 150 iliyopita, wameza panga walitumika 00:12:45.590 --> 00:12:47.400 katika medani za sayansi na kitabibu 00:12:47.480 --> 00:12:51.160 ili kusaidia kuunda endoskopia imara mwaka 1868 00:12:51.160 --> 00:12:53.820 wakiwa na Dk. Adolf Kussmaul wa Freiburg, Ujerumani 00:12:53.880 --> 00:12:56.639 Mnamo 1906, elektrokadiogramu huko Wales, 00:12:56.639 --> 00:13:00.240 kujifunza matatizo ya kumeza, na mmeng'enyo wa chakula, 00:13:00.240 --> 00:13:01.860 aina ya bronkoskopia, . 00:13:01.860 --> 00:13:03.840 Lakini zaidi ya miaka 150 iliyopita, 00:13:03.840 --> 00:13:07.860 tunajua mamia ya madhara na vifo kadhaa ... 00:13:07.880 --> 00:13:14.560 Hii ni endoskopia imara iliyoanzishwa na Dk. Adolph Kussmaul. 00:13:14.740 --> 00:13:18.679 Lakini tuligundua kuwa kulikuwa na Vifo 29 zaidi ya miaka 150 iliyopita. 00:13:18.679 --> 00:13:22.462 pamoja na mmezaji panga huko London aliyetoboa moyo wake kwa panga 00:13:23.142 --> 00:13:25.340 Tulijifunza pia kuwa kuna kesi tatu hadi nane za 00:13:25.340 --> 00:13:27.780 madhara mkubwa ya umezaji panga kila mwaka. 00:13:27.780 --> 00:13:29.880 Najua kwa sababu mimi hupata simu. 00:13:29.880 --> 00:13:31.150 Nilikuwa na wawili, 00:13:31.150 --> 00:13:34.320 mmoja kutoka Sweden, na kutoka Orlando wiki chache zilizopita, 00:13:34.320 --> 00:13:37.019 wamezaji panga waliopo hospitalini kutokana na madhara. 00:13:37.019 --> 00:13:38.769 Kwa hiyo ni hatari sana. 00:13:38.769 --> 00:13:41.629 Jambo jingine nililojifunza ni kuwa kumeza panga huchukua 00:13:41.629 --> 00:13:44.320 miaka 2 hadi miaka 10 kujifunza jinsi ya kumeza panga 00:13:44.320 --> 00:13:45.610 kwa watu wengi. 00:13:45.610 --> 00:13:48.020 Lakini ugunduzi unaovutia sana Nilijifunza ilikuwa 00:13:48.020 --> 00:13:51.360 jinsi wameza panga wanavyojifunza kufanya yasiyowezekana. 00:13:51.460 --> 00:13:53.460 Nami nitawapa siri ndogo: 00:13:53.520 --> 00:13:57.580 Usizingatie kwenye asilimia 99.9 kuwa haiwezekani. 00:13:57.580 --> 00:14:02.030 Unazingatia hiyo 1% ambayo inawezekana, na fikiria jinsi ya kufanya iwezeikane 00:14:02.817 --> 00:14:06.140 Sasa napenda kukupeleka kwenye safari ndani ya akili ya mmeza panga. 00:14:06.140 --> 00:14:09.479 Ili kumeza panga, inahitaji akili itafakari jambo, 00:14:09.479 --> 00:14:12.270 uzingativu wa hali ya juu, kuonyesha ufasaha ili 00:14:12.270 --> 00:14:15.670 kutenganisha viungo vya ndani vya mwili na kushinda vitendo hiari mwilini 00:14:15.710 --> 00:14:20.370 kupitia njia ya ubongo iliyoimarishwa, kupitia marido ya kumbukumbu ya misuli 00:14:20.450 --> 00:14:23.720 kwa mazoezi ya makusudi zaidi ya mara 10,000. 00:14:24.020 --> 00:14:28.090 Sasa ngoja niwasafirishe kidogo ndani ya mwili wa mmeza panga 00:14:28.310 --> 00:14:30.130 Ili kumeza panga, 00:14:30.130 --> 00:14:32.250 Lazima niteleze panga juu ya ulimi wangu, 00:14:32.250 --> 00:14:34.780 nizuie kutaka kutapika kwenye shingo ya umio, 00:14:34.780 --> 00:14:37.740 zungusha mgeuko wa nyuzi 90 chini ya gegedu ya ulimi, 00:14:38.240 --> 00:14:41.040 pitia kwenye msuli juu ya kilinda umio, 00:14:41.060 --> 00:14:42.600 zuia vitendohiari vya tumbo, 00:14:42.600 --> 00:14:44.380 telezea makali kwenye shimo la kifua 00:14:44.380 --> 00:14:45.960 kati ya mapafu. 00:14:46.080 --> 00:14:48.349 Katika hatua hii, 00:14:48.399 --> 00:14:50.389 Lazma kweli nisukume moyo wangu pembeni. 00:14:50.389 --> 00:14:51.720 Ikiwa utaangalia kwa makini, 00:14:51.720 --> 00:14:53.860 unawezaona moyo ukidunda kwa panga langu 00:14:53.860 --> 00:14:55.859 kwa sababu linaegemea moyo 00:14:55.859 --> 00:14:58.809 ikitenganishwa na karibu thumuni ya inchi ya tishu ya umio. 00:14:58.809 --> 00:15:00.580 Hicho sio kitu unaweza kudanganya. 00:15:00.580 --> 00:15:02.710 Kisha hutelezesha kupita mfupa wa kifua, 00:15:02.710 --> 00:15:05.540 kupita kilinda umio, chini ndani ya tumbo, 00:15:05.540 --> 00:15:09.020 zuia vitendohiari ndani ya tumbo njia yote hadi kwenye mbuti. 00:15:09.020 --> 00:15:09.750 Rahisi sana. 00:15:09.750 --> 00:15:10.930 (Kicheko) 00:15:10.930 --> 00:15:12.880 Kama ningetakiwa kwenda zaidi ya hapo, 00:15:12.880 --> 00:15:17.720 hadi kufikia mirija yangu ya mayai. mirija ya mayai! (Kidachi) 00:15:17.720 --> 00:15:20.980 Wanaume, mnaweza kuwauliza wake zenu kuhusu hiyo baadaye ... 00:15:22.160 --> 00:15:23.900 Watu huniuliza, wanasema, 00:15:23.900 --> 00:15:26.740 "lazima kuchukua ujasiri mwingi ili kuhatarisha maisha yako, 00:15:26.740 --> 00:15:28.800 kusogeza moyo wako, na kumeza panga ... " 00:15:28.800 --> 00:15:30.500 Hapana. Kinachofanya ujasiri halisi 00:15:30.500 --> 00:15:33.020 ni kwa yule kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba 00:15:33.080 --> 00:15:35.620 kwa kuhatarisha kushindwa na kukataliwa, 00:15:35.620 --> 00:15:37.040 kufungua moyo wake, 00:15:37.040 --> 00:15:38.240 na kumeza kiburi chake 00:15:38.240 --> 00:15:41.060 na kusimama hapa mbele ya kundi la watu asiowafahamu kabisa 00:15:41.060 --> 00:15:43.670 na kukuambia hadithi yake kuhusu hofu na ndoto zake, 00:15:43.680 --> 00:15:47.580 kwa hatarisha kumwaga habari zake, vyote kihalisia na kitamathali. 00:15:48.280 --> 00:15:49.450 Unaona - asante. 00:15:49.450 --> 00:15:53.720 (Makofi) 00:15:53.850 --> 00:15:56.250 Unaona, jambo la kustaajabisha sana ni 00:15:56.250 --> 00:15:58.650 Nimetaka kufanya mambo ya kusifika maishani mwangu 00:15:58.650 --> 00:15:59.780 na sasa nimesifika. 00:15:59.780 --> 00:16:02.880 Lakini jambo la kusifika haswa sio kwamba ninaweza kumeza 00:16:02.880 --> 00:16:05.170 panga 21 kwa mara moja, 00:16:07.640 --> 00:16:10.500 au futi 20 chini ya maji kwenye tanki la papa 88 na taa 00:16:10.500 --> 00:16:12.307 kwa kitabu cha Amini au Usiamini, 00:16:13.840 --> 00:16:17.600 au kuchowa hadi kuwa mwekundu nyuzi 1500 kwa Watu jasiri wa Stan Lee 00:16:17.610 --> 00:16:19.470 kama "Mtu wa Chuma" 00:16:19.520 --> 00:16:21.574 na yule jamaa alikuwa moto! 00:16:22.460 --> 00:16:24.920 Au kuvuta gari kwa upanga kwa Ripley, 00:16:24.930 --> 00:16:26.290 au Guinness, 00:16:26.290 --> 00:16:28.760 au kufikia fainali za shindano la vipaji Marekani, 00:16:28.820 --> 00:16:31.540 au kushinda 2007 tuzo ya Ig Nobel katika Utabibu. 00:16:31.550 --> 00:16:33.900 La, hilo sio jambo la kusifika sana. 00:16:33.900 --> 00:16:36.350 Hivyo ndio watu wanafikiria. La, la, la. Sio hivyo. 00:16:36.350 --> 00:16:37.800 Jambo la kusifika sana 00:16:37.800 --> 00:16:40.660 ni Mungu angemchukua kijana, mwoga, mwenye aibu mwembamba 00:16:40.660 --> 00:16:42.200 aliyehofia vimo virefu, 00:16:42.200 --> 00:16:43.890 aliyehofia ya maji na papa, 00:16:43.890 --> 00:16:46.370 na madaktari na manesi na sindano na vyenye ncha kali 00:16:46.370 --> 00:16:47.640 na kuzungumza na watu 00:16:47.640 --> 00:16:49.800 na sasa ananifanya nipae duniani kote 00:16:49.800 --> 00:16:51.320 katika kina cha futi 30,000 00:16:51.320 --> 00:16:53.900 kumeza vitu vya ncha chini ya maji ya tanki ya papa, 00:16:53.900 --> 00:16:57.430 na kuzungumza na madaktari na wauguzi na hadhira kama ninyi duniani 00:16:57.430 --> 00:16:59.580 Hilo ni jambo la kustaajabu sana kwangu. 00:16:59.580 --> 00:17:01.450 Nimetaka kufanya mambo yasiyowezekana - 00:17:01.450 --> 00:17:02.380 Asante. 00:17:02.380 --> 00:17:03.760 (Makofi) 00:17:03.760 --> 00:17:05.220 Asante. 00:17:05.660 --> 00:17:09.040 (Makofi) 00:17:09.700 --> 00:17:12.569 Sikuzote nilitaka kufanya yasiyowezekana, na sasa nimeweza. 00:17:12.569 --> 00:17:15.858 Nilitaka kufanya kitu cha kusifika maishani na kubadilisha ulimwengu, 00:17:15.858 --> 00:17:16.899 na sasa nimeweza. 00:17:16.899 --> 00:17:19.819 Siku zote nilitaka kupaa duniani kote kufanya vitendo vigumu 00:17:19.819 --> 00:17:21.379 na kuokoa maisha, sasa nimeweza. 00:17:21.379 --> 00:17:22.720 Na unajua nini? 00:17:22.720 --> 00:17:25.569 Bado kuna sehemu ndogo ya ndoto kubwa ya yule mtoto mdogo 00:17:25.569 --> 00:17:27.291 ndani kabisa. 00:17:30.320 --> 00:17:36.197 (Kicheko) (Makofi) 00:17:37.000 --> 00:17:40.240 Na unajua, sikuzote nilitaka kupata kusudi langu na wito wangu, 00:17:40.270 --> 00:17:41.530 na sasa nimepata. 00:17:41.540 --> 00:17:42.920 Lakini nadhani nini? 00:17:42.920 --> 00:17:46.230 Si kwa panga, sio unavyofikiria, si kwa nguvu zangu. 00:17:46.230 --> 00:17:48.510 Ni kwa udhaifu wangu, maneno yangu. 00:17:48.510 --> 00:17:51.090 Kusudi langu na wito ni kubadili ulimwengu 00:17:51.090 --> 00:17:52.390 kwa kukata kupitia hofu, 00:17:52.390 --> 00:17:54.910 upanga mmoja kwa wakati, neno moja kwa wakati, 00:17:55.070 --> 00:17:57.450 kisu moja kwa wakati, maisha kwa wakati, 00:17:57.540 --> 00:17:59.700 kuhamasisha watu kuwa mashujaa 00:17:59.700 --> 00:18:01.860 na kufanya yasiyowezekana maishani mwao. 00:18:02.060 --> 00:18:04.680 Kusudi langu ni kusaidia wengine kupata yao. 00:18:04.680 --> 00:18:05.680 La kwako ni lipi? 00:18:05.680 --> 00:18:06.960 Nini kusudi lako? 00:18:06.960 --> 00:18:08.960 Uliwekwa kufanya nini hapa? 00:18:09.260 --> 00:18:11.590 Naamini sisi wote tumeitwa kuwa mashujaa. 00:18:12.160 --> 00:18:14.260 Nguvu yako kubwa ni nini? 00:18:14.560 --> 00:18:17.990 Kati ya idadi ya watu duniani ya watu zaidi ya bilioni 7, 00:18:17.990 --> 00:18:20.250 kuna wameza upanga wachache sana 00:18:20.250 --> 00:18:21.661 waliobakia duniani kote leo, 00:18:21.661 --> 00:18:22.940 lakini kuna wewe mmoja. 00:18:22.940 --> 00:18:24.070 Wewe ni wa pekee. 00:18:24.070 --> 00:18:25.540 Hadithi yako ni nini? 00:18:25.540 --> 00:18:27.760 Nini kinakufanya uwe tofauti? 00:18:27.760 --> 00:18:29.180 Simulia hadithi yako, 00:18:29.180 --> 00:18:31.721 hata kama sauti yako ni nyembamba na inatetemeka. 00:18:31.900 --> 00:18:33.340 Je, thromu zako ni nini? 00:18:33.340 --> 00:18:35.850 kama ungefanya chochote, kuwa yeyote, kwenda popote - 00:18:35.850 --> 00:18:37.430 Ungefanya nini? Ungekwenda wapi? 00:18:37.430 --> 00:18:38.480 Ungefanya nini? 00:18:38.480 --> 00:18:40.340 Unataka kufanya nini na maisha yako? 00:18:40.340 --> 00:18:41.760 Nini ndoto zako kubwa? 00:18:41.760 --> 00:18:44.450 Nini ndoto zako kubwa ulipokuwa mdogo? Fikiria tena 00:18:44.450 --> 00:18:46.240 Nina uhakika hii haikuwa hivyo, si ndiyo? 00:18:46.483 --> 00:18:47.880 Nini zilikuwa ndoto zako kuu 00:18:47.880 --> 00:18:50.450 ulizofikiri zilikuwa ajabu sana na zisizoeleweka? 00:18:50.450 --> 00:18:54.040 Hakika hii inafanya ndoto zako zisionekane za ajabu tena, sivyo? 00:18:55.370 --> 00:18:57.050 Upanga wako ni nini? 00:18:57.050 --> 00:18:58.650 Kila mmoja wenu ana upanga, 00:18:58.650 --> 00:19:00.600 upanga wa pande mbili wa hofu na ndoto. 00:19:00.600 --> 00:19:03.520 Meza upanga wako, chochote utachokuwa. 00:19:03.890 --> 00:19:05.870 Fuata ndoto zako, mabibi na mabwana, 00:19:05.870 --> 00:19:08.900 Hujachelewa sana kuwa chochote unataka kuwa. 00:19:09.720 --> 00:19:12.920 Kwa wale waonevu na mipira ya kukwepa, wale watoto waliodhani 00:19:12.920 --> 00:19:14.916 kuwa sitaweza kufanya yasiyowezekana, 00:19:15.060 --> 00:19:17.645 Nina kitu kimoja tu cha kuwaambia: 00:19:17.645 --> 00:19:18.841 Asanteni. 00:19:18.940 --> 00:19:22.220 Kwa sababu kama si kwa wahalifu, tusingekuwa kuwa na mashujaa. 00:19:23.020 --> 00:19:27.237 Nipo hapa kuthibitisha yasiyowezekana si hayawezekani. 00:19:28.300 --> 00:19:32.310 Hii ni hatari sana, Inaweza kuniua. 00:19:32.340 --> 00:19:33.720 Natumaini mtafurahia. 00:19:33.720 --> 00:19:35.260 (Kicheko) 00:19:36.350 --> 00:19:38.700 Nitahitaji msaada wenu kwenye hili. 00:19:46.731 --> 00:19:48.405 Hadhira:Mbili, tatu. 00:19:48.405 --> 00:19:52.100 Dan Meyer:La, la, la. Nahitaji msaada wenu kwenye kuhesabu, nyote, sawa? 00:19:52.100 --> 00:19:53.210 (Vicheko) 00:19:53.210 --> 00:19:55.840 Kama unajua maneno? Sawa? Hesabu na mimi. Tayari? 00:19:55.870 --> 00:19:56.964 Moja. 00:19:56.964 --> 00:19:58.150 Mbili. 00:19:58.170 --> 00:19:58.980 Tatu. 00:19:58.980 --> 00:20:00.920 La, hiyo ni 2, lakini mmeelewa 00:20:06.760 --> 00:20:07.780 Hadhira: Moja. 00:20:07.840 --> 00:20:08.750 Mbili. 00:20:08.800 --> 00:20:10.010 Tatu. 00:20:11.260 --> 00:20:13.280 (Vuta pumzi) 00:20:14.360 --> 00:20:15.940 (Makofi) 00:20:16.251 --> 00:20:17.450 DM: Ndiyo! 00:20:17.450 --> 00:20:23.100 (Makofi) (Kushangilia) 00:20:23.100 --> 00:20:24.820 Asanteni sana. 00:20:25.450 --> 00:20:28.800 Asante, asante, asante. Asante kutoka kina cha moyo wangu 00:20:28.800 --> 00:20:31.290 Kweli, asante kutoka chini ya tumbo langu. 00:20:31.880 --> 00:20:35.020 Niliwaambia nimekuja hapa kufanya yasiyowezekana, na sasa nimeweza. 00:20:35.030 --> 00:20:37.730 Ila hii haikuwa isiyowezekana. Ninafanya hivi kila siku. 00:20:37.800 --> 00:20:42.800 Kitu kisichowezekana ilikuwa yule mwoga, mwenye aibu mwembamba kukabili hofu zake 00:20:42.840 --> 00:20:44.600 kusimama hapa kwenye jukwaa la [TEDx], 00:20:44.600 --> 00:20:47.100 na kubadilisha dunia, neno moja kwa wakati, 00:20:47.100 --> 00:20:49.080 upanga kwa wakati, maisha kwa wakati. 00:20:49.080 --> 00:20:52.060 kama nimekufanya ufikiri kwa njia mpya, kama nimekufanya uamini 00:20:52.060 --> 00:20:54.460 yasiyowekana si hayawezekani, 00:20:54.460 --> 00:20:57.960 ikiwa nimekufanya uelewe kuwa waweza fanya yasiyowezekana maishani mwako, 00:20:58.120 --> 00:21:01.020 basi kazi yangu imekwisha, na yako ndiyo kwanza imeanza. 00:21:01.020 --> 00:21:04.100 Usiache kuwa na ndoto. Usiache kuamini. 00:21:04.820 --> 00:21:06.350 Asanteni kwa kuniamini 00:21:06.350 --> 00:21:08.250 na asanteni kuwa sehemu ya ndoto yangu. 00:21:08.250 --> 00:21:09.550 Hii ni zawadi kwenu: 00:21:09.550 --> 00:21:11.486 Yasiyowezekana si ... 00:21:11.486 --> 00:21:12.920 Hadhira: Hayawezekani. 00:21:12.920 --> 00:21:14.920 Mwendo mrefu ni sehemu ya zawadi. 00:21:15.100 --> 00:21:19.560 (Makofi) 00:21:19.560 --> 00:21:21.020 Asanteni. 00:21:21.060 --> 00:21:25.360 (Makofi) 00:21:25.580 --> 00:21:27.560 (Kushangilia) 00:21:27.750 --> 00:21:30.570 Mwenyeji: Asante, Dan Meyer, wow!