WEBVTT 00:00:10.345 --> 00:00:12.885 [Viwango vya Uandishi wa habari] 00:00:13.520 --> 00:00:15.680 Uandishi wa habari ni desturi ya kutafiti, 00:00:15.680 --> 00:00:18.320 kuthibitisha, na kuonyesha maelezo kwa umma. 00:00:19.280 --> 00:00:22.066 Lakini si uandishi wote wa habari hubuniwa kwa njia sawa. 00:00:22.383 --> 00:00:25.470 Ripoti zinaweza kuwa taarifa fupi rasmi zilizoandikwa haraka, 00:00:25.840 --> 00:00:29.840 hadi uchunguzi thabiti ambao unaweza kuchukua muda na juhudi kutayarisha. 00:00:30.060 --> 00:00:32.779 Huenda utoaji wa ripoti unaofanana na uandishi wa habari 00:00:32.779 --> 00:00:35.260 usiwe na viwango sawa vya utafiti na msimamo 00:00:35.290 --> 00:00:37.912 kama ripoti zilizotayarishwa na mashirika ya kitaalamu. 00:00:38.130 --> 00:00:39.546 Ili kuchanganya mambo zaidi, 00:00:39.566 --> 00:00:43.384 maelezo bandia na ya kupotosha mtandaoni yanaweza pia kuonekana kama uanahabari. 00:00:43.760 --> 00:00:46.265 Kwa kuwa kuna nyenzo nyingi tofauti, 00:00:46.265 --> 00:00:47.600 ni muhimu kubaini 00:00:47.600 --> 00:00:50.250 maelezo yanayoaminika na yasiyoaminika. 00:00:50.870 --> 00:00:54.510 Njia moja kuu ya kufanya hili ni kutafuta maelezo kutoka kwa mashirika 00:00:54.510 --> 00:00:57.160 yanayofanya shughuli kulingana na viwango vilivyowekwa. 00:00:58.000 --> 00:01:00.990 Mashirika ya kitaalamu ya habari huwa si sahihi nyakati zote, 00:01:00.990 --> 00:01:02.960 lakini hadithi inaweza kuaminika zaidi 00:01:02.960 --> 00:01:06.400 iwapo lmetayarishwa katika mchakato unaojumuisha kutilia mkazo usahihi. 00:01:06.650 --> 00:01:09.913 Unaweza kutathmini ubora wa ripoti inayotokana na uandishi wa habari 00:01:09.973 --> 00:01:13.131 kwa kuangalia baadhi ya viwango vinavyobainisha uandishi wa habari 00:01:15.200 --> 00:01:16.300 Usahihi. 00:01:16.480 --> 00:01:19.597 Je, shirika hilo la habari lina sifa ya utaalamu? 00:01:19.967 --> 00:01:22.240 Je, lina sera ya kurekebisha makosa? 00:01:22.960 --> 00:01:23.960 Utafiti. 00:01:24.465 --> 00:01:27.155 Watu wangapi wamehojiwa au kunukuliwa katika hadithi? 00:01:27.415 --> 00:01:30.320 Utafiti au takwimu zipi zinazounga zimejumuishwa? 00:01:31.280 --> 00:01:32.330 Chanzo. 00:01:32.400 --> 00:01:36.160 Je, watu walionukuliwa ni wataalamu au wanastahiki kuzungumzia suala hilo? 00:01:38.640 --> 00:01:39.650 Muktadha. 00:01:39.650 --> 00:01:41.800 Je, hadithi inajumuisha maelezo ya historia 00:01:41.800 --> 00:01:43.970 ili kukusaidia kuelewa vyema mawazo makuu? 00:01:45.040 --> 00:01:46.106 Haki. 00:01:46.240 --> 00:01:49.330 Je, watu na masuala yamefafanuliwa kwa kutumia lugha ya kawaida? 00:01:50.400 --> 00:01:52.740 Si uandishi wote wa utatimiza viwango sawa. 00:01:53.000 --> 00:01:55.845 Kufahamu mashirika ya kitaalamu ya habari 00:01:56.015 --> 00:01:58.196 na viwango vinavyobainisha uandishi wa habari 00:01:58.196 --> 00:02:00.445 kunaweza kutusaidia kubaini habari za kuamini. 00:02:02.698 --> 00:02:05.481 [Imeletwa kwako na CIVIX] 00:02:06.403 --> 00:02:08.738 [Kwa usaidizi wa Kanada]