[Viwango vya Uandishi wa habari]
Uandishi wa habari ni desturi ya kutafiti,
kuthibitisha, na kuonyesha
maelezo kwa umma.
Lakini si uandishi wote wa habari
hubuniwa kwa njia sawa.
Ripoti zinaweza kuwa taarifa fupi rasmi
zilizoandikwa haraka,
hadi uchunguzi thabiti ambao unaweza
kuchukua muda na juhudi kutayarisha.
Huenda utoaji wa ripoti unaofanana na
uandishi wa habari
usiwe na viwango sawa vya
utafiti na msimamo
kama ripoti zilizotayarishwa na
mashirika ya kitaalamu.
Ili kuchanganya mambo zaidi,
maelezo bandia na ya kupotosha mtandaoni
yanaweza pia kuonekana kama uanahabari.
Kwa kuwa kuna nyenzo nyingi tofauti,
ni muhimu kubaini
maelezo yanayoaminika na yasiyoaminika.
Njia moja kuu ya kufanya hili ni kutafuta
maelezo kutoka kwa mashirika
yanayofanya shughuli kulingana na
viwango vilivyowekwa.
Mashirika ya kitaalamu ya habari
huwa si sahihi nyakati zote,
lakini hadithi inaweza kuaminika zaidi
iwapo lmetayarishwa katika mchakato
unaojumuisha kutilia mkazo usahihi.
Unaweza kutathmini ubora wa ripoti
inayotokana na uandishi wa habari
kwa kuangalia baadhi ya viwango
vinavyobainisha uandishi wa habari
Usahihi.
Je, shirika hilo la habari
lina sifa ya utaalamu?
Je, lina sera ya kurekebisha makosa?
Utafiti.
Watu wangapi wamehojiwa
au kunukuliwa katika hadithi?
Utafiti au takwimu zipi zinazounga
zimejumuishwa?
Chanzo.
Je, watu walionukuliwa ni wataalamu au
wanastahiki kuzungumzia suala hilo?
Muktadha.
Je, hadithi inajumuisha
maelezo ya historia
ili kukusaidia kuelewa vyema mawazo makuu?
Haki.
Je, watu na masuala yamefafanuliwa
kwa kutumia lugha ya kawaida?
Si uandishi wote wa utatimiza
viwango sawa.
Kufahamu mashirika ya kitaalamu ya habari
na viwango vinavyobainisha
uandishi wa habari
kunaweza kutusaidia kubaini
habari za kuamini.
[Imeletwa kwako na CIVIX]
[Kwa usaidizi wa Kanada]