[Viwango vya Uandishi wa habari] Uandishi wa habari ni desturi ya kutafiti, kuthibitisha, na kuonyesha maelezo kwa umma. Lakini si uandishi wote wa habari hubuniwa kwa njia sawa. Ripoti zinaweza kuwa taarifa fupi rasmi zilizoandikwa haraka, hadi uchunguzi thabiti ambao unaweza kuchukua muda na juhudi kutayarisha. Huenda utoaji wa ripoti unaofanana na uandishi wa habari usiwe na viwango sawa vya utafiti na msimamo kama ripoti zilizotayarishwa na mashirika ya kitaalamu. Ili kuchanganya mambo zaidi, maelezo bandia na ya kupotosha mtandaoni yanaweza pia kuonekana kama uanahabari. Kwa kuwa kuna nyenzo nyingi tofauti, ni muhimu kubaini maelezo yanayoaminika na yasiyoaminika. Njia moja kuu ya kufanya hili ni kutafuta maelezo kutoka kwa mashirika yanayofanya shughuli kulingana na viwango vilivyowekwa. Mashirika ya kitaalamu ya habari huwa si sahihi nyakati zote, lakini hadithi inaweza kuaminika zaidi iwapo lmetayarishwa katika mchakato unaojumuisha kutilia mkazo usahihi. Unaweza kutathmini ubora wa ripoti inayotokana na uandishi wa habari kwa kuangalia baadhi ya viwango vinavyobainisha uandishi wa habari Usahihi. Je, shirika hilo la habari lina sifa ya utaalamu? Je, lina sera ya kurekebisha makosa? Utafiti. Watu wangapi wamehojiwa au kunukuliwa katika hadithi? Utafiti au takwimu zipi zinazounga zimejumuishwa? Chanzo. Je, watu walionukuliwa ni wataalamu au wanastahiki kuzungumzia suala hilo? Muktadha. Je, hadithi inajumuisha maelezo ya historia ili kukusaidia kuelewa vyema mawazo makuu? Haki. Je, watu na masuala yamefafanuliwa kwa kutumia lugha ya kawaida? Si uandishi wote wa utatimiza viwango sawa. Kufahamu mashirika ya kitaalamu ya habari na viwango vinavyobainisha uandishi wa habari kunaweza kutusaidia kubaini habari za kuamini. [Imeletwa kwako na CIVIX] [Kwa usaidizi wa Kanada]