1 00:00:10,345 --> 00:00:12,885 [Viwango vya Uandishi wa habari] 2 00:00:13,520 --> 00:00:15,680 Uandishi wa habari ni desturi ya kutafiti, 3 00:00:15,680 --> 00:00:18,320 kuthibitisha, na kuonyesha maelezo kwa umma. 4 00:00:19,280 --> 00:00:22,066 Lakini si uandishi wote wa habari hubuniwa kwa njia sawa. 5 00:00:22,383 --> 00:00:25,470 Ripoti zinaweza kuwa taarifa fupi rasmi zilizoandikwa haraka, 6 00:00:25,840 --> 00:00:29,840 hadi uchunguzi thabiti ambao unaweza kuchukua muda na juhudi kutayarisha. 7 00:00:30,060 --> 00:00:32,779 Huenda utoaji wa ripoti unaofanana na uandishi wa habari 8 00:00:32,779 --> 00:00:35,260 usiwe na viwango sawa vya utafiti na msimamo 9 00:00:35,290 --> 00:00:37,912 kama ripoti zilizotayarishwa na mashirika ya kitaalamu. 10 00:00:38,130 --> 00:00:39,546 Ili kuchanganya mambo zaidi, 11 00:00:39,566 --> 00:00:43,384 maelezo bandia na ya kupotosha mtandaoni yanaweza pia kuonekana kama uanahabari. 12 00:00:43,760 --> 00:00:46,265 Kwa kuwa kuna nyenzo nyingi tofauti, 13 00:00:46,265 --> 00:00:47,600 ni muhimu kubaini 14 00:00:47,600 --> 00:00:50,250 maelezo yanayoaminika na yasiyoaminika. 15 00:00:50,870 --> 00:00:54,510 Njia moja kuu ya kufanya hili ni kutafuta maelezo kutoka kwa mashirika 16 00:00:54,510 --> 00:00:57,160 yanayofanya shughuli kulingana na viwango vilivyowekwa. 17 00:00:58,000 --> 00:01:00,990 Mashirika ya kitaalamu ya habari huwa si sahihi nyakati zote, 18 00:01:00,990 --> 00:01:02,960 lakini hadithi inaweza kuaminika zaidi 19 00:01:02,960 --> 00:01:06,400 iwapo lmetayarishwa katika mchakato unaojumuisha kutilia mkazo usahihi. 20 00:01:06,650 --> 00:01:09,913 Unaweza kutathmini ubora wa ripoti inayotokana na uandishi wa habari 21 00:01:09,973 --> 00:01:13,131 kwa kuangalia baadhi ya viwango vinavyobainisha uandishi wa habari 22 00:01:15,200 --> 00:01:16,300 Usahihi. 23 00:01:16,480 --> 00:01:19,597 Je, shirika hilo la habari lina sifa ya utaalamu? 24 00:01:19,967 --> 00:01:22,240 Je, lina sera ya kurekebisha makosa? 25 00:01:22,960 --> 00:01:23,960 Utafiti. 26 00:01:24,465 --> 00:01:27,155 Watu wangapi wamehojiwa au kunukuliwa katika hadithi? 27 00:01:27,415 --> 00:01:30,320 Utafiti au takwimu zipi zinazounga zimejumuishwa? 28 00:01:31,280 --> 00:01:32,330 Chanzo. 29 00:01:32,400 --> 00:01:36,160 Je, watu walionukuliwa ni wataalamu au wanastahiki kuzungumzia suala hilo? 30 00:01:38,640 --> 00:01:39,650 Muktadha. 31 00:01:39,650 --> 00:01:41,800 Je, hadithi inajumuisha maelezo ya historia 32 00:01:41,800 --> 00:01:43,970 ili kukusaidia kuelewa vyema mawazo makuu? 33 00:01:45,040 --> 00:01:46,106 Haki. 34 00:01:46,240 --> 00:01:49,330 Je, watu na masuala yamefafanuliwa kwa kutumia lugha ya kawaida? 35 00:01:50,400 --> 00:01:52,740 Si uandishi wote wa utatimiza viwango sawa. 36 00:01:53,000 --> 00:01:55,845 Kufahamu mashirika ya kitaalamu ya habari 37 00:01:56,015 --> 00:01:58,196 na viwango vinavyobainisha uandishi wa habari 38 00:01:58,196 --> 00:02:00,445 kunaweza kutusaidia kubaini habari za kuamini. 39 00:02:02,698 --> 00:02:05,481 [Imeletwa kwako na CIVIX] 40 00:02:06,403 --> 00:02:08,738 [Kwa usaidizi wa Kanada]