Je unafikiri vitu tunavyojenga leo
vitahesabika kama maajabu miaka ijayo?
Tafakari kuhusu Stonehenge,
Mapiramidi,
Machu Picchu na Kisiwa cha Easter
Vyote hivi ni tofauti sana
na vile tunavyofanya leo,
na yale mawe makubwa,
yakiwa yamepangwa katika hali ya kiutata
hali ngumu kuelewa
na mabaki yake yote ya ujenzi
yakifutwa,
ikiyaacha katika hali ya kutojulikana
Inaonekana kama vile watu hawakuweza
kujenga vitu hivi,
kwa sababu watu hawakujenga.
Vilitengenezwa kwa uangalifu na
jamii ya majitu
yajulikanayo kama Cyclops.
(Vicheko)
Na nimekuwa nashirikiana na
majitu haya
ili kujifunza siri zao
za kuhamisha mawe hayo makubwa.
na ni kwamba,
Cyclops hawana nguvu kivile,
Ni wajanja sana katika
kufanya vitu kufanya kazi kwa niaba yao.
Video, ambazo mnaziona nyuma yangu
za vitu vinavyobadilika vikubwa,kama mawe
ni matokeo ya ushirikiano huu.
SAWA, inawezekana Cyclops
vikawa ni viumbe vya kufikirika
lakini maajabu haya bado ni halisi.
Watu waliyajenga.
Lakini pia waliunda dhana
kuhusu hayo
na kuhusu maajabu, kuna kiunganishi
kinene
kati ya dhana fikirishi na uhalisia.
Chukulia mfano wa Kisiwa cha Easter.
Pale wavumbuzi wa Kidachi
walipokifikia kwa mara ya kwanza kisiwa hiki,
Waliwauliza watu wa Rapa Nui
Vile mababu zao walivyoweza kuhamisha
sanamu hizi kubwa
Na watu wa Rapa Nui wakasema,
"Mababu zetu hawakuhamisha sanamu hizo,
kwa sababu zilitembea zenyewe."
Kwa karne kadhaa, hili lilikataliwa,
lakini ni kweli kabisa.
Sanamu, zijulikanazo kama moai,
zilihamishwa zikiwa zimesimama,
zikishikiliwa pande moja hadi nyingine.
SAWA?
Pamoja na uzuri wa moai kwa wageni leo,
unahitaji kuwaza kuwa pale wakati ule,
na moai makubwa yakitembea
katika kisiwa.
Kwa sababu kumbukumbu halisi sio
vitu vyenyewe,
Ilikuwa ni utamaduni
wa kulifanya jiwe liwe hai.
Kwa hiyo kama msanifu majengo,
nimekuwa nakimbizana na ndoto hiyo.
Tunawezaje kuhamisha dhana yetu ya ujenzi
ili kutoa nafasi ya dhana hii fikirishi
Kwa hiyo kile nimekuwa nafanya
ni kujipa changamoto mwenyewe
kwa kufanya maonyesho kadhaa
ya zamani lakini
yaliyo na jukumu la wazi kabisa
ya kuhamisha na kusimamisha
vitu vikubwa vizito,
kama vile jiwe hili kubwa
lililosanifiwa kutembea ardhini
na kusimama wima
au jiwe hili kubwa lenye uzito
wa 4,000 linaloibuka likiwa hai
ili kucheza stejini
na nilichojifunza ni kuwa kwa
kuwaza kuhusu usanifu majengo
si kama bidhaa ya mwisho bali kama onyesho
kutoka wazo mpaka kukamilika,
tunajikuta tunagundua njia bora sana
za kujenga hivi leo.
Unajua, sehemu kubwa ya mazungumzo
kuhusu zsiku zetu za baadaye
yanaangazia zaidi teknolojia,
ufanisi na uharaka.
Lakini kama nimejifunza chochote kuhusu Cyclops,
ni kuwa maajabu yanaweza
kuwa ya kijanja, mazuri sana
na endelevu --
kutokana na uwingi na kutoeleweka kwake.
na pamoja na kuwa wanahitaji kujua
jinsi maajabu haya yalivyojengwa,
Nimekuwa nikiwauliza Cyclops
jinsi ya kuunda sintofahamu hii
ambayo inawalazimisha watu
kuuuliza swala lenyewe hasa.
Kwa sababu katika zama
ambazo tunasanifu majengo
kudumu kwa miaka 30, labda 60,
ningependa nijifunze
jinsi ya kutengeneza kitu
ambacho kinaweza kuburudisha milele.
Asante
(Makofi)