Mambo ambayo yanaweza kusababisha migongano,kutokuelewana na matatizo katika mahusiano ya kibinadamu, huwa hayakosekani, Lakini kadiri unavyotegemea mwitiko wako kwenye matendo ya mtu mwingine, kamwe hautapatia. Namaanisha nini? 'Hey, alinikasirisha. Ndiyo maana nina hasira.' 'Aliniambia hivi. Ndiyo maana nilimfokea tena.' Kadiri unavyoegemeza mwitikio wako kwenye kitendo cha mtu huyo, umekosea kwa sababu unafanya kazi chini ya kiwango kilichoundwa na mwanadamu, si kiwango cha Mungu. Mtu anaweza kukuchokoza. Angalia, simtetei mtu kama huyo. Ni vibaya kumkasirisha mtu. Lakini majibu yangu ya hasira sio jukumu la mtu huyo, ni langu. Jibu langu la hasira linaonyesha mahali ambapo moyo wangu hauko vizuri na Mungu, si kile ambacho mtu huyo amekifanya ili kunikasirisha.