0:00:09.280,0:00:12.960 Neema na amani iwe kwenu nyote katika jina kuu la Yesu 0:00:12.960,0:00:20.120 na karibu katika toleo jingine la 'Imani Ni Asili' hapa kwenye TV ya Moyo wa Mungu. 0:00:20.120,0:00:26.000 Leo, nataka kuzungumzia suala ambalo limejitokeza mara nyingi sana 0:00:26.000,0:00:33.960 katika mazungumzo na watu - katika nyakati za maombi, ushauri na kutia moyo. 0:00:33.960,0:00:40.280 Nimeona tu kwamba watu wengi sana leo 0:00:40.280,0:00:47.080 wanaishi maisha yao kupitia lenzi hii ya jana, 0:00:47.080,0:00:49.040 kupitia lenzi ya walivyokuwa - 0:00:49.040,0:00:56.320 mabaya yao ya zamani, makosa, maumivu na uchungu. 0:00:56.320,0:01:02.160 Na kama matokeo ya hili, wengi hujikuta wamenaswa 0:01:02.160,0:01:12.880 katika mzunguko huu mbaya wa hatia na hukumu kwa makosa waliyofanya 0:01:12.880,0:01:18.320 au vilevile mzunguko mbaya wa uchungu na chuki 0:01:18.320,0:01:23.280 juu ya mabaya waliyofanyiwa huko nyuma. 0:01:23.280,0:01:27.240 Na ni hatari sana. 0:01:27.240,0:01:35.840 Watu wa Mungu, hii si chochote ila ni njama ya hila, hila ya kawaida ya shetani 0:01:35.840,0:01:40.880 ili kukutenganisha na Mungu. 0:01:40.880,0:01:45.520 Shetani anafurahia kujadili mambo yako ya nyuma na wewe. 0:01:45.520,0:01:52.840 Anafurahi kukukumbusha juu ya kutofaulu kwako zamani, makosa ya zamani, maumivu ya zamani. 0:01:52.840,0:01:57.800 Kwa sababu hicho ndicho kitu pekee kinachokuunganisha naye. 0:01:57.800,0:02:04.720 Hiyo ndiyo habari pekee ambayo anayo kuhusu wewe - siku zako za nyuma. 0:02:04.720,0:02:11.040 Na shetani atachukua kila njia inayopatikana 0:02:11.040,0:02:19.320 kujaribu na kukuzuia usitende Neno la Mungu sasa. 0:02:19.320,0:02:24.640 Angalia, hajali ikiwa utalichambua tu Neno. 0:02:24.640,0:02:30.640 Haijalishi kama unastaajabia Neno au hata kukubali ukweli wa Neno 0:02:30.640,0:02:35.960 mradi hutendi Neno hilo. 0:02:35.960,0:02:39.480 Hataki utende neno la Mungu! 0:02:39.480,0:02:48.840 Anataka uishi maisha yako kupitia lenzi ya maisha yako ya zamani yasiyofaa, 0:02:48.840,0:02:53.040 kwa wewe kuchuja kila kitu kupitia hiyo, 0:02:53.040,0:03:00.960 ili kulemaza uwezo wako wa kutenda imani muda huu 0:03:00.960,0:03:07.200 na hivyo kuharibu maisha yako ya baadaye. 0:03:07.200,0:03:20.120 Watu wa Mungu, ni hatari kuchukua safari zisizo za lazima hadi jana. 0:03:20.120,0:03:23.840 Ni hatari sana. 0:03:23.840,0:03:30.920 Angalia, siku zako za nyuma haziamui sasa yako 0:03:30.920,0:03:36.040 na haiamui mustakabali wako. 0:03:36.040,0:03:41.440 Unaweza kujifunza kutoka kwenye maisha yako ya zamani bila kuishi katika maisha yako ya zamani. 0:03:41.440,0:03:45.440 Usiishi ndani yake; jifunze kutoka kwake. 0:03:45.440,0:03:54.680 Usiheshimu udanganyifu wa shetani kwa umakini wako - umakini wako wa thamani. 0:03:54.680,0:04:00.400 Kwa sababu makosa yako hayakufafanui wewe. 0:04:00.400,0:04:03.680 Zaburi 37:24 0:04:03.680,0:04:08.920 Narudia - makosa yako hayakufafanui. 0:04:08.920,0:04:13.080 Kwa kweli, yanaweza hata kukuboresha. 0:04:13.080,0:04:21.960 Namaanisha, Mungu anaweza hata kutumia makosa yako kukupeleka mahali 0:04:21.960,0:04:32.640 anapotaka uwe - kulingana na mwitikio wako. 0:04:32.640,0:04:35.320 Jambo kuu liko kwenye mwitikio wako. 0:04:35.320,0:04:37.920 Je, unaitikiaje kwenye kosa hilo? 0:04:37.920,0:04:41.480 Sasa, ngoja nikupe mfano halisi sana. 0:04:41.480,0:04:44.240 Hebu wazia uko safarini mahali fulani. 0:04:44.240,0:04:46.240 Unaenda mahali fulani; unajua unakokwenda. 0:04:46.240,0:04:51.160 Na katika safari hii, ghafla unatambua kuwa uko mahali pasipofaa. 0:04:51.160,0:04:54.160 Umechukua hatua mbaya; umekosa mwelekeo. 0:04:54.160,0:04:56.120 Unafanya nini? 0:04:56.120,0:05:03.000 Unahitaji kurejesha hatua zako na kurudi kwenye mstari. 0:05:03.000,0:05:06.880 Ikiwa unatambua kuwa umeenda katika mwelekeo mbaya, je, unasema tu, 0:05:06.880,0:05:11.120 'Oh sawa, nimechelewa mno! Acha niendelee tu katika njia hii mbaya.' 0:05:11.120,0:05:23.680 Hapana! Unarudi haraka kwenye njia sahihi, rudi kwenye mstari na uendelee na safari yako. 0:05:23.680,0:05:32.320 Watu wa Mungu, katika safari hii ya maisha, 0:05:32.320,0:05:39.320 ukichukua hatua mbaya, unajibuje? 0:05:39.320,0:05:42.480 Je, unaitikiaje? 0:05:42.480,0:05:52.920 Je, unatambua kosa lako, rudia hatua zako na kumkimbilia Mungu kwa toba? 0:05:52.920,0:05:59.680 Au unapinga kujichunguza, 0:05:59.680,0:06:03.200 galagala kwa kujihurumia 0:06:03.200,0:06:16.760 na kuanguka ndani zaidi katika mtandao huo tatanishi wa hatia, lawama na uduni? 0:06:16.760,0:06:24.040 Je, unarudi kwenye mstari au unaenda nje zaidi? 0:06:24.040,0:06:28.160 Chaguo ni lako. 0:06:28.160,0:06:39.760 Kuchagua kuishi katika maisha yako ya zamani ni kuchagua kwenda zaidi nje ya njia. 0:06:39.760,0:06:45.080 Kuanguka katika hatia na hukumu hiyo - unaenda nje zaidi. 0:06:45.080,0:06:47.880 Vivyo hivyo, ikiwa unahalalisha kosa lako 0:06:47.880,0:06:50.560 au unanyosha vidole kushoto, kulia na katikati 0:06:50.560,0:06:57.040 au kutoa visingizio, natoka nje ya njia ya mstari. 0:06:57.040,0:07:01.680 Na jambo la hatari hapa ni kwamba 0:07:01.680,0:07:09.560 kadiri unavyoongeza kukaa kwako katika makosa, 0:07:09.560,0:07:18.840 ndivyo uharibifu zaidi shetani anavyoweza kuuletea moyoni mwako. 0:07:18.840,0:07:27.200 Na shetani anapokuwa na nafasi ndani ya moyo wako. 0:07:27.200,0:07:32.640 uharibifu huo unaweza kuenea kwa urahisi kwenye nyumba yako, 0:07:32.640,0:07:38.520 ndoa, familia, mahusiano na kazi yako. 0:07:38.520,0:07:44.960 Tunasuka mtandao ulioingiliana 0:07:44.960,0:07:52.000 wakati makosa yetu, tunakataa kuondoka. 0:07:52.000,0:07:54.880 Sisemi kwamba hutafanya makosa. 0:07:54.880,0:07:58.000 Kila mtu hufanya makosa katika safari hii. 0:07:58.000,0:08:00.480 Kila mtu hukosa alama. 0:08:00.480,0:08:05.280 Ninamaanisha, angalia tu Biblia, mwongozo wetu, Neno la Mungu - 0:08:05.280,0:08:10.440 wahusika wengi wakuu wa Biblia tunaowasoma. 0:08:10.440,0:08:14.200 Nuhu alipambana na pombe. 0:08:14.200,0:08:16.320 Yakobo alitumia udanganyifu. 0:08:16.320,0:08:19.600 Lutu alipambana na uchu. 0:08:19.600,0:08:25.080 Vipi kuhusu Musa ambaye alipambana na hasira. 0:08:25.080,0:08:31.080 Petro mara nyingi aliingiwa na woga, Tomaso na mashaka. 0:08:31.080,0:08:36.560 Vipi kuhusu Mfalme Daudi, Sulemani, Samsoni - wote walishindwa na tamaa. 0:08:36.560,0:08:44.000 Hakuna mkamilifu katika ulimwengu huu (Warumi 3:10, 23) 0:08:44.000,0:08:51.840 Sisi sote hujikwaa kwa njia nyingi (Yakobo 3:2) 0:08:51.840,0:08:58.600 Katika ulimwengu huu mwovu, kutakuwa na mzozo huo daima, 0:08:58.600,0:09:04.320 ile vita ndani ya moyo wa mwanadamu kati ya mwili na roho. 0:09:04.320,0:09:11.640 Wazo lililo moyoni mwako ni vita utakayokabiliana nayo hadi siku ya mwisho, 0:09:11.640,0:09:15.880 mpaka Yesu atakapokuja - ndivyo vita utakavyokabiliana nayo. 0:09:15.880,0:09:22.320 Kwa hiyo, faraja yangu kwenu leo, watu wa Mungu, ni hii: 0:09:22.320,0:09:30.280 Mara tu unapogundua kuwa umechukua hatua mbaya, 0:09:30.280,0:09:36.040 rudi haraka kwenye mstari. 0:09:36.040,0:09:45.680 Usiongeze muda wa kukaa kwako katika makosa kwa kujitetea kwenye hilo. 0:09:45.680,0:09:54.480 Angalia, kama mtoto wa Mungu, unaweza kujua unapochukua hatua mbaya. 0:09:54.480,0:10:02.920 Vipi? Roho wa Mungu atachochea dhamiri yako kutubu. 0:10:02.920,0:10:07.880 Warumi 9:1, 2 Wakorintho 7:10 0:10:07.880,0:10:14.040 Roho Mtakatifu ataisukuma dhamiri yako kutubu. 0:10:14.040,0:10:25.280 Swali ni - roho yako ni sikivu kiasi gani? 0:10:25.280,0:10:32.760 una haraka kiasi gani kujitetea? 0:10:32.760,0:10:42.960 Kasi ambayo unatambua kosa lako ni sawia 0:10:42.960,0:10:52.680 na kiwango ambacho Neno la Mungu linatawala moyo wako. 0:10:52.680,0:11:03.960 Na kuwa mwangalifu zaidi kwa msukumo wa Roho wa Mungu katika roho yako, 0:11:03.960,0:11:09.960 inakupasa kutumia muda mwingi zaidi miguuni pake, 0:11:09.960,0:11:13.320 muda mwingi mbele zake, 0:11:13.320,0:11:16.160 muda zaidi katika Neno Lake. 0:11:16.160,0:11:22.240 Lazima aongezeke; lazima upungue (Yohana 3:30). 0:11:22.240,0:11:26.400 Kwa sababu yote yanamhusu Yesu; haikuhusu wewe. 0:11:26.400,0:11:31.960 Sio juu ya kustahili kwako kwa sababu hakuna mtu anayestahili. 0:11:31.960,0:11:39.160 Sio juu ya udhaifu wako kwa sababu kila mtu ana udhaifu. 0:11:39.160,0:11:45.200 Yote ni juu ya utayari wako - 0:11:45.200,0:11:49.280 utayari wako wa kukiri kosa lako, 0:11:49.280,0:11:53.160 kuweka kiburi chako kando, 0:11:53.160,0:11:59.040 rudia hatua zako, rudi kwenye mstari na Mungu 0:11:59.040,0:12:03.440 na endelea na safari yako ya imani. 0:12:03.440,0:12:10.520 Kwa sababu si lazima uwe mkamilifu ili uwe mtoto wa Mungu; 0:12:10.520,0:12:14.760 unatakiwa tu uwepo. 0:12:14.760,0:12:18.720 Watu wa Mungu, nitawaacha leo na neno la Maandiko 0:12:18.720,0:12:22.960 kutoka kwa Mtume Paulo katika Warumi 8:1. 0:12:22.960,0:12:35.480 Akasema, Sasa basi, hakuna hukumu ya adhabu 0:12:35.480,0:12:39.000 kwa wale walio katika Kristo Yesu." 0:12:39.000,0:12:44.760 Sasa, Maandiko haya hayatupi msingi wa kuhurumia dhambi, 0:12:44.760,0:12:50.360 kuhalalisha makosa au kuchukua neema kirahisi. Hapana! 0:12:50.360,0:13:00.960 Lakini inasisitiza tu kwamba hatupaswi kuruhusu hatia ya makosa yetu 0:13:00.960,0:13:10.480 kutunyang'anya amani ya pekee inayopatikana katika msamaha wa Kristo. 0:13:10.480,0:13:15.680 Badala ya kosa lako kukutoa mbele za Mungu, 0:13:15.680,0:13:23.800 inapaswa kuwa sababu ya wewe kumkaribia Yeye zaidi. 0:13:23.800,0:13:27.520 Kwa sababu katika maneno ya Nabii T.B. Joshua: 0:13:27.520,0:13:38.640 "Unaweza kujua wewe ni mtoto wa Mungu wakati makosa yako yanapochochea maisha yako ya kiroho." 0:13:38.640,0:13:40.560 Asante, Yesu Kristo. 0:13:40.560,0:13:44.720 Sasa hivi, watu wa Mungu, ni wakati wa maombi. 0:13:51.160,0:13:59.760 Hivi sasa, kwa kila moyo uliochafuliwa na hatia - 0:13:59.760,0:14:05.600 takaswa, katika jina kuu la Yesu Kristo! 0:14:05.600,0:14:10.880 kwa kila roho inayosumbuliwa na hukumu, 0:14:10.880,0:14:18.960 takaswa kwa Damu ya thamani ya Yesu Kristo! 0:14:18.960,0:14:26.680 Damu ya Yesu Kristo inapokusafisha, umetakaswa kwelikweli! 0:14:26.680,0:14:29.120 Takaswa sasa hivi! 0:14:29.120,0:14:38.000 Katika roho yako, katika nafsi yako, katika mwili wako - takaswa! 0:14:38.000,0:14:48.640 Kila roho ya dhiki, utumwa, udhaifu, ndoto mbaya - 0:14:48.640,0:14:53.160 uoshwe kwa Damu ya Yesu Kristo! 0:14:53.160,0:15:03.640 Uoshwe sasa hivi, katika jina kuu la Yesu Kristo! 0:15:03.640,0:15:07.160 Pokea ujasiri! 0:15:07.160,0:15:10.080 Pokea nguvu! 0:15:10.080,0:15:20.160 Pokea usadikisho wa kushikilia msimamo wako katika Kristo! 0:15:20.160,0:15:27.040 Ee Bwana, rekebisha kila moyo mkaidi na utashi. 0:15:27.040,0:15:30.680 Ongoza hatua zinazoenda kombo. 0:15:30.680,0:15:35.520 Osha madoa ya hatia. 0:15:35.520,0:15:41.320 Tusaidie kuona kupitia macho yako. 0:15:41.320,0:15:48.720 Tuvute kwenye uhusiano wa karibu na Wewe 0:15:48.720,0:15:56.560 na utujalie ufahamu mkubwa zaidi wa moyo Wako. 0:15:56.560,0:16:06.000 Katika jina kuu la Yesu Kristo! Amina! 0:16:06.000,0:16:08.280 Asante, Yesu Kristo.