WEBVTT 00:00:09.000 --> 00:00:12.000 Neema na amani iwe kwenu nyote katika jina kuu la Yesu 00:00:12.000 --> 00:00:20.000 na karibu katika toleo jingine la 'Imani Ni Asili' hapa kwenye TV ya Moyo wa Mungu. 00:00:20.000 --> 00:00:26.000 Leo, nataka kuzungumzia suala ambalo limejitokeza mara nyingi sana 00:00:26.000 --> 00:00:33.000 katika mazungumzo na watu - katika nyakati za maombi, ushauri na kutia moyo. 00:00:33.000 --> 00:00:40.000 Nimeona tu kwamba watu wengi sana leo 00:00:40.000 --> 00:00:47.000 wanaishi maisha yao kupitia lenzi hii ya jana, 00:00:47.000 --> 00:00:49.000 kupitia lenzi ya walivyokuwa - 00:00:49.000 --> 00:00:56.000 mabaya yao ya zamani, makosa, maumivu na uchungu. 00:00:56.000 --> 00:01:02.000 Na kama matokeo ya hii, wengi hujikuta wamenaswa 00:01:02.000 --> 00:01:12.000 katika mzunguko huu mbaya wa hatia na hukumu kwa makosa waliyofanya 00:01:12.000 --> 00:01:18.000 au vilevile mzunguko mbaya wa uchungu na chuki 00:01:18.000 --> 00:01:23.000 juu ya mabaya waliyofanyiwa huko nyuma. 00:01:23.000 --> 00:01:27.000 Na ni hatari sana. 00:01:27.000 --> 00:01:35.000 Watu wa Mungu, hii si chochote ila ni njama ya hila, hila ya kawaida ya shetani 00:01:35.000 --> 00:01:40.000 ili kukutenganisha na Mungu. 00:01:40.000 --> 00:01:45.000 Shetani anafurahia kujadili mambo yako ya nyuma na wewe. 00:01:45.000 --> 00:01:52.000 Anafurahi kukukumbusha juu ya kutofaulu kwako zamani, makosa ya zamani, maumivu ya zamani. 00:01:52.000 --> 00:01:57.000 Kwa sababu hicho ndicho kitu pekee kinachokuunganisha naye. 00:01:57.000 --> 00:02:04.000 Hiyo ndiyo habari pekee ambayo anayo kuhusu wewe - siku zako za nyuma. 00:02:04.000 --> 00:02:11.000 Na shetani atachukua kila njia inayopatikana 00:02:11.000 --> 00:02:19.000 kujaribu na kukuzuia usitende Neno la Mungu sasa. 00:02:19.000 --> 00:02:24.000 Angalia, hajali ikiwa utalichambua tu Neno. 00:02:24.000 --> 00:02:30.000 Haijalishi kama unastaajabia Neno au hata kukubali ukweli wa Neno 00:02:30.000 --> 00:02:35.000 mradi hutendi Neno hilo. 00:02:35.000 --> 00:02:39.000 Hataki utende neno la Mungu! 00:02:39.000 --> 00:02:48.000 Anataka uishi maisha yako kupitia lenzi ya maisha yako ya zamani yasiyofaa, 00:02:48.000 --> 00:02:53.000 kwa wewe kuchuja kila kitu kupitia hiyo, 00:02:53.000 --> 00:03:00.000 ili kulemaza uwezo wako wa kutenda imani muda huu 00:03:00.000 --> 00:03:07.000 na hivyo kuharibu maisha yako ya baadaye. 00:03:07.000 --> 00:03:20.000 Watu wa Mungu, ni hatari kuchukua safari zisizo za lazima hadi jana. 00:03:20.000 --> 00:03:23.000 Ni hatari sana. 00:03:23.000 --> 00:03:30.000 Angalia, siku zako za nyuma haziamui sasa yako 00:03:30.000 --> 00:03:36.000 na haiamui mustakabali wako. 00:03:36.000 --> 00:03:41.000 Unaweza kujifunza kutoka kwa maisha yako ya zamani bila kuishi katika maisha yako ya zamani. 00:03:41.000 --> 00:03:45.000 Usiishi ndani yake; jifunze kutoka kwake. 00:03:45.000 --> 00:03:54.000 Usiheshimu udanganyifu wa shetani kwa umakini wako - umakini wako wa thamani. 00:03:54.000 --> 00:04:00.000 Kwa sababu makosa yako hayakufafanui wewe. 00:04:00.000 --> 00:04:03.000 Zaburi 37:24 00:04:03.000 --> 00:04:08.000 Narudia - makosa yako hayakufafanui. 00:04:08.000 --> 00:04:13.000 Kwa kweli, yanaweza hata kukuboresha. 00:04:13.000 --> 00:04:21.000 Namaanisha, Mungu anaweza hata kutumia makosa yako kukupeleka mahali 00:04:21.000 --> 00:04:32.000 anapotaka uwe - kulingana na mwitikio wako. 00:04:32.000 --> 00:04:35.000 Jambo kuu liko kwenye mwitikio wako. 00:04:35.000 --> 00:04:37.000 Je, uaikiaje kwenye kosa hilo? 00:04:37.000 --> 00:04:41.000 Sasa, ngoja nikupe mfano mzuri sana. 00:04:41.000 --> 00:04:44.000 Hebu wazia uko safarini mahali fulani. 00:04:44.000 --> 00:04:46.000 Unaenda mahali fulani; unajua unakokwenda. 00:04:46.000 --> 00:04:51.000 Na katika safari hii, ghafla unatambua kuwa uko mahali pasipofaa. 00:04:51.000 --> 00:04:54.000 Umechukua hatua mbaya; umekosa mwelekeo. 00:04:54.000 --> 00:04:56.000 Unafanya nini? 00:04:56.000 --> 00:05:03.000 Unahitaji kurejea hatua zako na kurudi kwenye mstari. 00:05:03.000 --> 00:05:06.000 Ikiwa unatambua kuwa umeenda katika mwelekeo mbaya, je, unasema tu, 00:05:06.000 --> 00:05:11.000 'Oh sawa, nimechelewa mno! Acha niendelee tu katika njia hii mbaya.' 00:05:11.000 --> 00:05:23.000 Hapana! Unarudi haraka kwenye njia sahihi, rudi kwenye mstari na uendelee na safari yako. 00:05:23.000 --> 00:05:32.000 Watu wa Mungu, katika safari hii ya maisha, 00:05:32.000 --> 00:05:39.000 ukichukua hatua mbaya, unajibuje? 00:05:39.000 --> 00:05:42.000 Je, unaitikiaje? 00:05:42.000 --> 00:05:52.000 Je, unatambua kosa lako, rudia hatua zako na kumkimbilia Mungu kwa toba? 00:05:52.000 --> 00:05:59.000 Au unakataa kujichunguza, 00:05:59.000 --> 00:06:03.000 galagala kwa kujihurumia 00:06:03.000 --> 00:06:16.000 na kuanguka ndani zaidi katika mtandao huo tatanishi wa hatia, lawama na uduni? 00:06:16.000 --> 00:06:24.000 Je, unarudi kwenye mstari au unaenda nje zaidi? 00:06:24.000 --> 00:06:28.000 Chaguo ni lako. 00:06:28.000 --> 00:06:39.000 Kuchagua kuishi katika maisha yako ya zamani ni kuchagua kwenda zaidi nje ya njia. 00:06:39.000 --> 00:06:45.000 Kuanguka katika hatia na hukumu hiyo - unaenda nje zaidi. 00:06:45.000 --> 00:06:47.000 Vivyo hivyo, ikiwa unahalalisha kosa lako 00:06:47.000 --> 00:06:50.000 au unanyosha vidole kushoto, kulia na katikati 00:06:50.000 --> 00:06:57.000 au kutoa visingizio, natoka nje ya njia. 00:06:57.000 --> 00:07:01.000 Na jambo la hatari hapa ni kwamba 00:07:01.000 --> 00:07:09.000 kadiri unavyoongeza kukaa kwako katika makosa, 00:07:09.000 --> 00:07:18.000 ndivyo uharibifu zaidi shetani anavyoweza kuuletea moyoni mwako. 00:07:18.000 --> 00:07:27.000 Na shetani anapokuwa na nafasi ndani ya moyo wako. 00:07:27.000 --> 00:07:32.000 uharibifu huo unaweza kuenea kwa urahisi kwenye nyumba yako, 00:07:32.000 --> 00:07:38.000 ndoa, familia, mahusiano na kazi yako. 00:07:38.000 --> 00:07:44.000 Tunasuka mtandao uliochanganyikiwa 00:07:44.000 --> 00:07:52.000 wakati makosa yetu, tunakataa kuondoka. 00:07:52.000 --> 00:07:54.000 Sisemi kwamba hutafanya makosa. 00:07:54.000 --> 00:07:58.000 Kila mtu hufanya makosa katika safari hii. 00:07:58.000 --> 00:08:00.000 Kila mtu hukosa alama. 00:08:00.000 --> 00:08:05.000 Ninamaanisha, angalia tu Biblia, mwongozo wetu, Neno la Mungu - 00:08:05.000 --> 00:08:10.000 wahusika wengi wakuu wa Biblia tunaowasoma. 00:08:10.000 --> 00:08:14.000 Nuhu alipambana na pombe. 00:08:14.000 --> 00:08:16.000 Yakobo alitumia udanganyifu. 00:08:16.000 --> 00:08:19.000 Lutu alipambana na uchu. 00:08:19.000 --> 00:08:25.000 Vipi kuhusu Musa ambaye alipambana na hasira. 00:08:25.000 --> 00:08:31.000 Petro mara nyingi aliingiwa na woga, Tomaso na mashaka. 00:08:31.000 --> 00:08:36.000 Vipi kuhusu Mfalme Daudi, Sulemani, Samsoni - wote walishindwa na tamaa. 00:08:36.000 --> 00:08:44.000 Hakuna mkamilifu katika ulimwengu huu (Warumi 3:10, 23) 00:08:44.000 --> 00:08:51.000 Sisi sote hujikwaa kwa njia nyingi (Yakobo 3:2) 00:08:51.000 --> 00:08:58.000 Katika ulimwengu huu mwovu, kutakuwa na mzozo huo daima, 00:08:58.000 --> 00:09:04.000 ile vita ndani ya moyo wa mwanadamu kati ya mwili na roho. 00:09:04.000 --> 00:09:11.000 Wazo lililo moyoni mwako ni vita utakayokabiliana nayo hadi siku ya mwisho, 00:09:11.000 --> 00:09:15.000 mpaka Yesu atakapokuja - ndivyo vita utakavyokabiliana nayo. 00:09:15.000 --> 00:09:22.000 Kwa hiyo, faraja yangu kwenu leo, watu wa Mungu, ni hii: 00:09:22.000 --> 00:09:30.000 Mara tu unapogundua kuwa umechukua hatua mbaya, 00:09:30.000 --> 00:09:36.000 hrudi haraka kwenye mstari. 00:09:36.000 --> 00:09:45.000 Usiongeze muda wa kukaa kwako katika makosa kwa kujitetea kwenye hilo. 00:09:45.000 --> 00:09:54.000 Angalia, kama mtoto wa Mungu, unaweza kujua unapochukua hatua mbaya. 00:09:54.000 --> 00:10:02.000 Vipi? Roho wa Mungu atachochea dhamiri yako kutubu. 00:10:02.000 --> 00:10:07.000 Warumi 9:1, 2 Wakorintho 7:10 00:10:07.000 --> 00:10:14.000 Roho Mtakatifu ataisukuma dhamiri yako kutubu. 00:10:14.000 --> 00:10:25.000 Swali ni - roho yako ni sikivu kiasi gani? 00:10:25.000 --> 00:10:32.000 una haraka kiasi gani kujitetea? 00:10:32.000 --> 00:10:42.000 Kasi ambayo unatambua kosa lako ni sawia 00:10:42.000 --> 00:10:52.000 na kiwango ambacho Neno la Mungu linatawala moyo wako. 00:10:52.000 --> 00:11:03.000 Na kuwa mwangalifu zaidi kwa msukumo wa Roho wa Mungu katika roho yako, 00:11:03.000 --> 00:11:09.000 inakupasa kutumia muda mwingi zaidi miguuni pake, 00:11:09.000 --> 00:11:13.000 muda mwingi mbele zake, 00:11:13.000 --> 00:11:16.000 muda zaidi katika Neno Lake. 00:11:16.000 --> 00:11:22.000 Lazima aongezeke; lazima upungue (Yohana 3:30). 00:11:22.000 --> 00:11:26.000 Kwa sababu yote yanamhusu Yesu; haikuhusu wewe. 00:11:26.000 --> 00:11:31.000 Sio juu ya kustahili kwako kwa sababu hakuna mtu anayestahili. 00:11:31.000 --> 00:11:39.000 Sio juu ya udhaifu wako kwa sababu kila mtu ana udhaifu. 00:11:39.000 --> 00:11:45.000 Yote ni juu ya utayari wako - 00:11:45.000 --> 00:11:49.000 utayari wako wa kukiri kosa lako, 00:11:49.000 --> 00:11:53.000 kuweka kiburi chako kando, 00:11:53.000 --> 00:11:59.000 rudia hatua zako, rudi kwenye mstari na Mungu 00:11:59.000 --> 00:12:03.000 na endelea na safari yako ya imani. 00:12:03.000 --> 00:12:10.000 Kwa sababu si lazima uwe mkamilifu ili uwe mtoto wa Mungu; 00:12:10.000 --> 00:12:14.000 unatakiwa tu upatikane. 00:12:14.000 --> 00:12:18.000 Watu wa Mungu, nitawaacha leo na neno la Maandiko 00:12:18.000 --> 00:12:22.000 kutoka kwa Mtume Paulo katika Warumi 8:1. 00:12:22.000 --> 00:12:35.000 Akasema, Sasa basi, hakuna hukumu ya adhabu 00:12:35.000 --> 00:12:39.000 kwa wale walio katika Kristo Yesu." 00:12:39.000 --> 00:12:44.000 Sasa, Maandiko haya hayatupi msingi wa kuhurumia dhambi, 00:12:44.000 --> 00:12:50.000 kuhalalisha makosa au kuchukua neema kirahisi. Hapana! 00:12:50.000 --> 00:13:00.000 Lakini inasisitiza tu kwamba hatupaswi kuruhusu hatia ya makosa yetu 00:13:00.000 --> 00:13:10.000 kutunyang'anya amani ya pekee inayopatikana katika msamaha wa Kristo. 00:13:10.000 --> 00:13:15.000 Badala ya kosa lako kukutoa mbele za Mungu, 00:13:15.000 --> 00:13:23.000 inapaswa kuwa sababu ya wewe kumkaribia Yeye zaidi. 00:13:23.000 --> 00:13:27.000 Kwa sababu katika maneno ya Nabii TB Joshua: 00:13:27.000 --> 00:13:38.000 "Unaweza kujua wewe ni mtoto wa Mungu wakati makosa yako yanapochochea maisha yako ya kiroho." 00:13:38.000 --> 00:13:40.000 Asante, Yesu Kristo. 00:13:40.000 --> 00:13:44.000 Sasa hivi, watu wa Mungu, ni wakati wa maombi. 00:13:51.000 --> 00:13:59.000 Hivi sasa, kwa kila moyo uliochafuliwa na hatia - 00:13:59.000 --> 00:14:05.000 takaswa, katika jina kuu la Yesu Kristo! 00:14:05.000 --> 00:14:10.000 kwa kila roho inayosumbuliwa na hukumu, 00:14:10.000 --> 00:14:18.000 takaswa kwa Damu ya thamani ya Yesu Kristo! 00:14:18.000 --> 00:14:26.000 Damu ya Yesu Kristo inapokusafisha, umetakaswa kwelikweli! 00:14:26.000 --> 00:14:29.000 Jitakase sasa hivi! 00:14:29.000 --> 00:14:38.000 Katika roho yako, katika nafsi yako, katika mwili wako - takaswa! 00:14:38.000 --> 00:14:48.000 Kila roho ya dhiki, utumwa, udhaifu, ndoto mbaya - 00:14:48.000 --> 00:14:53.000 uoshwe kwa Damu ya Yesu Kristo! 00:14:53.000 --> 00:15:03.000 Uoshwe sasa hivi, katika jina kuu la Yesu Kristo! 00:15:03.000 --> 00:15:07.000 Pokea ujasiri! 00:15:07.000 --> 00:15:10.000 Pokea nguvu! 00:15:10.000 --> 00:15:20.000 Pokea usadikisho wa kushikilia msimamo wako katika Kristo! 00:15:20.000 --> 00:15:27.000 Ee Bwana, rekebisha kila moyo mkaidi na utashi. 00:15:27.000 --> 00:15:30.000 Ongoza hatua zinazoenda kombo. 00:15:30.000 --> 00:15:35.000 Osha madoa ya hatia. 00:15:35.000 --> 00:15:41.000 Tusaidie kuona kupitia macho yako. 00:15:41.000 --> 00:15:48.000 Tuvute kwa uhusiano wa karibu na Wewe 00:15:48.000 --> 00:15:56.000 na utujalie ufahamu mkubwa zaidi wa moyo Wako. 00:15:56.000 --> 00:16:06.000 Katika jina kuu la Yesu Kristo! Amina! 00:16:06.000 --> 00:16:08.000 Asante, Yesu Kristo.