WEBVTT 00:00:00.520 --> 00:00:02.096 Siku. 00:00:02.120 --> 00:00:03.496 Damu. 00:00:03.520 --> 00:00:04.720 Hedhi. 00:00:05.440 --> 00:00:07.016 Uchafu. 00:00:07.040 --> 00:00:08.656 Siri. 00:00:08.680 --> 00:00:09.880 Kuficha. 00:00:10.400 --> 00:00:11.600 Kwanini? NOTE Paragraph 00:00:12.760 --> 00:00:14.656 Utaratibu asilia kibaolojia 00:00:14.680 --> 00:00:18.496 ambao kila msichana na mwanamke anapitia kila mwezi 00:00:18.520 --> 00:00:20.696 kwa karibia nusu ya maisha yake. 00:00:20.720 --> 00:00:23.416 Jambo ambalo ni la umuhimu mkubwa sana 00:00:23.440 --> 00:00:27.640 kiasi kwamba kupona na uenezwaji wa spishi zetu unautegemea. 00:00:28.480 --> 00:00:30.320 Bado tunauchukulia kama mwiko. 00:00:31.160 --> 00:00:34.040 Tunajisikia ugumu na fedheha kuliongelea. NOTE Paragraph 00:00:35.840 --> 00:00:37.656 Nilipopata siku zangu mara ya kwanza, 00:00:37.680 --> 00:00:40.040 Niliambiwa nifanye iwe siri nisiwaambie wengine-- 00:00:40.760 --> 00:00:42.640 hata kwa baba yangu au kaka. 00:00:43.640 --> 00:00:46.256 Baadaye wakati hili somo limejitokeza vitabuni mwetu, 00:00:46.280 --> 00:00:48.616 mwalimu wetu wa baolojia aliiruka mada. NOTE Paragraph 00:00:48.640 --> 00:00:51.320 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:00:52.000 --> 00:00:53.680 Nilijifunza nini kutokana na hili? 00:00:54.360 --> 00:00:57.520 Nilijifunza kwamba ni fedheha mno kuongelea jambo hili. 00:00:58.080 --> 00:01:00.736 Nilijifunza kufedheshwa na mwili wangu. 00:01:00.760 --> 00:01:03.816 Nilijifunza kutokufahamu siku zangu 00:01:03.840 --> 00:01:05.800 ili kuweza kubaki na heshima. NOTE Paragraph 00:01:06.440 --> 00:01:08.256 Utafiti katika sehemu mbalimbali India 00:01:08.280 --> 00:01:13.016 waonyesha wasichana watatu kati ya kumi hawafahamu kuhusu hedhi 00:01:13.040 --> 00:01:14.800 wakati wa siku zao za kwanza. 00:01:15.400 --> 00:01:17.016 Na baadhi ya sehemu za Rajasthan 00:01:17.040 --> 00:01:21.880 hii namba ni kubwa kama wasichana tisa kati ya kumi kutokufahamu 00:01:22.800 --> 00:01:24.456 Unaweza kushangazwa kujua 00:01:24.480 --> 00:01:26.696 kwamba wasichana wengi nilioongea nao, 00:01:26.720 --> 00:01:30.536 waliokuwa hawajui kuhusu siku zao wakati wa hedhi zao za kwanza 00:01:30.560 --> 00:01:32.936 walifikiria kuwa wana saratani ya damu 00:01:32.960 --> 00:01:34.560 na watakufa muda sio mrefu. NOTE Paragraph 00:01:36.760 --> 00:01:39.696 Usafi wa hedhi ni kipengele muhimu cha hatari 00:01:39.720 --> 00:01:42.280 kwa maambukizi wa mfumo wa via vya uzazi. 00:01:43.040 --> 00:01:46.216 Lakini India, ni asilimia 12 tu ya wasichana na wanawake 00:01:46.240 --> 00:01:50.000 wanaweza kupata njia za usafi wa kumudu siku zao. 00:01:50.840 --> 00:01:52.336 Ukifanya mahesabu, 00:01:52.360 --> 00:01:57.456 asilimia 88 ya wasichana na wanawake hutumia njia zisizo salama kwa siku zao. NOTE Paragraph 00:01:57.480 --> 00:01:58.680 Nilikuwa mmoja wao. 00:01:59.880 --> 00:02:02.816 Nilikulia kwenye mji mdogo uitwao Garhwa, jimbo la Jharkhand, 00:02:02.840 --> 00:02:05.960 ambako hata kununua pedi ilichukuliwa kama fedheha. 00:02:06.840 --> 00:02:08.895 Sasa nilipoanza kupata siku zangu, 00:02:08.919 --> 00:02:10.680 Nilianza kutumia matambara. 00:02:12.560 --> 00:02:15.216 Baada ya kila matumizi niliyafua na kuyatumia tena. 00:02:15.240 --> 00:02:16.496 Lakini kuyahifadhi, 00:02:16.520 --> 00:02:19.136 Niliyaficha na kuyaweka sehemu yenye giza na unyevu 00:02:19.160 --> 00:02:21.760 ilikwamba mtu asijue kuwa niko kwenye hedhi. 00:02:22.520 --> 00:02:25.136 Kwa kuyarudia kufua matambara yalikuja kuwa magumu, 00:02:25.160 --> 00:02:28.160 na mara nyingi nilipata upele na maambukizi kwa kuyatumia. NOTE Paragraph 00:02:28.880 --> 00:02:33.160 Niliyavaa kwa muda wa miaka mitano hadi nilipohama ule mji. 00:02:35.640 --> 00:02:37.976 Suala lingine ambalo siku zilileta maishani mwangu 00:02:38.000 --> 00:02:40.296 lile la kuwekewa mipaka kijamii 00:02:40.320 --> 00:02:44.656 iliyowekwa kwa wasichana wetu na wanawake wakiwa kwenye siku zao. 00:02:44.680 --> 00:02:46.976 Nafikiri wote lazma mtakuwa mnajua, 00:02:47.000 --> 00:02:49.960 lakini bado nitaelezea kwa wale wachache wasiojua. NOTE Paragraph 00:02:50.720 --> 00:02:53.200 Sikuruhusiwa kula au kugusa vitu vichachu. 00:02:53.840 --> 00:02:58.696 Sikuruhusiwa kukaa kwenye sofa au kitandani mwa ndugu wa familia. 00:02:58.720 --> 00:03:01.176 Nilitakiwa kufua mashuka kila baada ya siku zangu, 00:03:01.200 --> 00:03:03.136 hata kama hazikuchafuka kwa madoa. 00:03:03.160 --> 00:03:04.976 Nilichukuliwa kama najisi 00:03:05.000 --> 00:03:09.800 na kukatazwa kuabudu au kugusa kitu chochote chenye umuhimu kidini. 00:03:10.880 --> 00:03:13.096 Ulikutana na matangazo nje ya misikiti 00:03:13.120 --> 00:03:15.560 kukataza wasichana na wanawake walio kwenye hedhi. NOTE Paragraph 00:03:17.080 --> 00:03:18.456 Chakuchekesha, 00:03:18.480 --> 00:03:21.296 wakati wote ni wanawake watu wazima 00:03:21.320 --> 00:03:25.760 ndio walioweka vizuizi hivyo kwa wasichana wadogo katika familia. 00:03:26.360 --> 00:03:30.536 hata hivyo, wamekua wakikubali vizuizi hivyo kama desturi. 00:03:30.560 --> 00:03:33.576 Na katika kukosekana kwa kuingiliwa, 00:03:33.600 --> 00:03:35.616 ni imani potofu na kutoeleweka 00:03:35.640 --> 00:03:38.240 kunakoenezwa kizazi hata kizazi. NOTE Paragraph 00:03:39.240 --> 00:03:41.096 Kwa miaka nilyofanyia kazi taaluma hii, 00:03:41.120 --> 00:03:42.616 Nimeshakutana na hadithi 00:03:42.640 --> 00:03:46.256 ambapo wasichana walitakiwa kula na kuosha vyombo vyao kwa kutengwa. 00:03:46.280 --> 00:03:48.616 Hawakuruhusiwa kuoga wakati wa siku zao, 00:03:48.640 --> 00:03:52.720 na katika nyumba nyingine walitengwa hata na ndugu wengine wa familia. 00:03:53.720 --> 00:03:57.256 Kiasi cha asilimia 85 za wasichana na wanawake India 00:03:57.280 --> 00:04:02.600 walifuata moja au zaidi ya masharti ya mila kwenye siku zao kila mwezi. 00:04:03.320 --> 00:04:04.856 Unafikiria hii inafanya nini 00:04:04.880 --> 00:04:07.840 katika kujithamini na kujiamini kwa msichana mdogo? 00:04:08.720 --> 00:04:11.456 Kiwewe cha kisaikolojia ambacho hili huumiza, 00:04:11.480 --> 00:04:14.056 kuathiri haiba yake, 00:04:14.080 --> 00:04:15.816 utendaji wake kimasomo 00:04:15.840 --> 00:04:20.480 na kila kipengele cha ukuaji katika miaka ya awali ya uumbaji wake? NOTE Paragraph 00:04:21.760 --> 00:04:25.800 Nilifuata kwa bidii masharti haya yote ya kimila kwa miaka 13, 00:04:26.400 --> 00:04:28.776 hadi mjadala na mshirika mwenzangu, Tuhin, 00:04:28.800 --> 00:04:31.360 ulipobadilisha mtazamo wangu kuhusu hedhi milele. 00:04:32.280 --> 00:04:37.736 Mwaka 2009, mimi na Tuhin tulikuwa tunasoma stashada katika ubunifu. 00:04:37.760 --> 00:04:39.416 Tukapendana 00:04:39.440 --> 00:04:41.880 na nilikuwa huru kujadiliana naye kuhusu siku zangu. 00:04:42.640 --> 00:04:44.560 Tuhin alijua kidogo kuhusu siku. NOTE Paragraph 00:04:45.520 --> 00:04:47.800 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:04:51.800 --> 00:04:55.416 Alishangazwa kujua kwamba wasichana hupata maumivu makali 00:04:55.440 --> 00:04:56.856 na hutokwa damu kila mwezi. NOTE Paragraph 00:04:56.880 --> 00:04:58.976 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:04:59.000 --> 00:05:00.496 Ndio. 00:05:00.520 --> 00:05:02.296 Alishtushwa kabisa kujua 00:05:02.320 --> 00:05:07.496 kuhusu vizuizi vinavyowekwa kwa wasichana na wanawake walio kwenye hedhi 00:05:07.520 --> 00:05:10.096 na familia pamoja na jamii zao wenyewe. 00:05:10.120 --> 00:05:12.176 Ili kuweza kunisaidia na maumivu yangu, 00:05:12.200 --> 00:05:16.000 alikwenda kwenye mtandao wa intaneti kujifunza kuhusu hedhi. 00:05:16.600 --> 00:05:18.336 Aliponielezea alichojifunza, 00:05:18.360 --> 00:05:21.360 Niligundua ufahamu mdogo nilionao kuhusu hedhi, 00:05:21.960 --> 00:05:25.080 na vitu vingi nilivyoamini vilikuja kuwa ni imani potofu, NOTE Paragraph 00:05:26.360 --> 00:05:27.896 Ndipo nilipojiuliza: 00:05:27.920 --> 00:05:30.256 kama sisi, tumesoma vizuri hivi, 00:05:30.280 --> 00:05:32.376 tumefundishwa vibaya kuhusu hedhi, 00:05:32.400 --> 00:05:36.400 kutakuwa na mamilioni ya wasichana huko nje waliofundishwa vibaya, pia. 00:05:37.760 --> 00:05:38.976 Kusoma-- 00:05:39.000 --> 00:05:40.776 kuelewa tatizo vizuri, 00:05:40.800 --> 00:05:45.416 Nilifanya utafiti wa mwaka mmoja kujifunza ukosefu wa ufahamu kuhusu hedhi 00:05:45.440 --> 00:05:47.040 na chanzo chake nyuma yake. NOTE Paragraph 00:05:47.960 --> 00:05:49.696 Wakati kiujumla inaaminika 00:05:49.720 --> 00:05:55.696 kwamba kutokufahamu hedhi na kuelewa vibaya ni tatizo la vijijini, 00:05:55.720 --> 00:05:56.936 katika utafiti wangu, 00:05:56.960 --> 00:05:59.936 Niligundua kwamba ni tatizo la mijini pia. 00:05:59.960 --> 00:06:04.320 Na lipo kwa daraja la walioelimika mijini, pia. 00:06:05.280 --> 00:06:07.776 Wakati naongea na wazazi wengi pamoja na waalimu, 00:06:07.800 --> 00:06:13.096 Niligundua kuwa wengi wao walitaka kuelimisha wasichana kuhusu siku zao 00:06:13.120 --> 00:06:15.760 kabla hawajaanza kupata mzunguko wao wa hedhi. 00:06:16.840 --> 00:06:18.056 Na-- 00:06:18.080 --> 00:06:21.616 lakini wenyewe walikosa njia stahiki. 00:06:21.640 --> 00:06:22.896 Na kwavile ni mwiko, 00:06:22.920 --> 00:06:25.960 wanajisikia kusita na fedheha kuongelea jambo hilo. NOTE Paragraph 00:06:26.840 --> 00:06:31.456 Wasichana siku hizi hupata siku zao wakiwa darasa la sita na la saba, 00:06:31.480 --> 00:06:33.096 lakini mtaala wetu wa elimu 00:06:33.120 --> 00:06:36.920 hufundisha wasichana kuhusu siku zao darasa la nane na la tisa tu. 00:06:37.800 --> 00:06:39.360 na kwa vile ni mwiko, 00:06:40.000 --> 00:06:43.440 waalimu bado wanairuka mada. NOTE Paragraph 00:06:44.840 --> 00:06:49.096 Hivyo shule haziwafundishi wasichana kuhusu siku zao, 00:06:49.120 --> 00:06:51.256 wazazi hawazungumzii jambo hilo. 00:06:51.280 --> 00:06:52.680 Wasichana wanaenda wapi? 00:06:53.680 --> 00:06:56.520 Miongo miwili iliyopita na sasa-- 00:06:57.120 --> 00:06:58.400 hakuna kilichobadilika. 00:07:00.120 --> 00:07:02.940 Nilimshirikisha Tuhin matokeo yangu na tulijiuliza 00:07:02.960 --> 00:07:04.576 Itakuwaje tukianzisha kitu 00:07:04.600 --> 00:07:09.176 ambacho kitasaidia wasichana kuelewa kuhusu hedhi wao wenyewe -- 00:07:09.200 --> 00:07:13.416 Kitu ambacho kitawasaidia wazazi na waalimu 00:07:13.440 --> 00:07:16.360 kuongelea kuhusu siku za hedhi kwa raha kwa wasichana wadogo? NOTE Paragraph 00:07:17.840 --> 00:07:19.456 Wakati wa utafiti wangu, 00:07:19.480 --> 00:07:21.456 Nilikuwa nakusanya hadithi nyingi. 00:07:21.480 --> 00:07:26.160 Hizi ni hadithi za mambo waliyopitia wasichana kipindi cha siku zao. 00:07:26.800 --> 00:07:30.056 Hadithi hizi zitawafanya wasichana wawe wadadisi na kuvutiwa 00:07:30.080 --> 00:07:34.016 katika kuongea kuhusu hedhi ndani ya watu wao wa karibu. 00:07:34.040 --> 00:07:35.496 Hicho ndio tulichotaka. 00:07:35.520 --> 00:07:38.856 Tulitaka kitu ambacho kingewafanya wasichana wawe wadadisi 00:07:38.880 --> 00:07:41.056 na kuwasukuma kujifunza. 00:07:41.080 --> 00:07:44.240 Tulitaka kutumia hadithi hizi kufundisha wasichana kuhusu siku zao. NOTE Paragraph 00:07:45.360 --> 00:07:48.456 Hivyo tukaamua kutengeneza kitabu cha vikatuni 00:07:48.480 --> 00:07:51.736 ambapo wahusika wa katuni wataigiza hadithi hizi 00:07:51.760 --> 00:07:55.640 na kuwaelimisha wasichana kuhusu hedhi kwa njia ya kufurahisha na kuwashirikisha. 00:07:56.360 --> 00:07:59.376 Kuwasilisha wasichana katika hatua zao tofauti za kubalehe, 00:07:59.400 --> 00:08:01.040 tunao wahusika watatu. 00:08:01.560 --> 00:08:04.736 Pinki, ambaye hajapata siku zake bado, 00:08:04.760 --> 00:08:08.256 Jiya anayepata siku zake wakati wa simulizi za kitabu 00:08:08.280 --> 00:08:11.536 na Mira ambaye tayari amekuwa akipata siku zake. 00:08:11.560 --> 00:08:13.976 Kuna mhusika wa nne, Priya Didi. 00:08:14.000 --> 00:08:17.536 Kupitia yeye, wasichana wanakuja kujua kuhusu vipengele kadhaa vya ukuaji 00:08:17.560 --> 00:08:19.360 na kusimamia usafi wa hedhi. NOTE Paragraph 00:08:20.455 --> 00:08:22.398 Utengenezaji kitabu, ulitumia umakini 00:08:22.423 --> 00:08:26.376 hakuna katika vielelezo ambavyo vilikuwa na pingamizi lolote 00:08:26.400 --> 00:08:28.360 na hiyo ni nyeti kitamaduni. 00:08:29.200 --> 00:08:33.056 Wakati wa majaribio ya sampuli ya awali tuligundua wasichana wakilipenda kitabu. 00:08:33.080 --> 00:08:34.456 Walikuwa na hamu ya kukisoma 00:08:34.480 --> 00:08:37.240 na kujua zaidi na zaidi kuhusu siku zao wao wenyewe. 00:08:38.039 --> 00:08:41.056 Wazazi na waalimu walikuwa hawaoni shida kuongea kuhusu siku 00:08:41.080 --> 00:08:42.775 kwa wasichana wadogo kutumia kitabu 00:08:42.799 --> 00:08:45.776 na wakati mwingine hata wavulana walivutiwa kukisoma. NOTE Paragraph 00:08:45.800 --> 00:08:47.936 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:08:47.960 --> 00:08:49.720 (Makofi) NOTE Paragraph 00:08:51.840 --> 00:08:55.656 Kitabu cha vikatu kilisaidia katika kujenga mazingira 00:08:55.680 --> 00:08:58.120 ambapo itasimamisha hedhi kuwa mwiko. 00:08:58.720 --> 00:09:02.776 Wengi wa waliojitolea walichukua hii sampuli ya awali kuelimisha wasichana 00:09:02.800 --> 00:09:06.736 na kufanya warsha za kuelimisha hedhi katika majimbo matano tofauti India. 00:09:06.760 --> 00:09:10.136 na mmoja wa waliojitolea alitumia sampuli hii kuelimisha watawa vijana 00:09:10.160 --> 00:09:12.376 na aliipeleka kwenye nyumba ya utawa Ladakh. NOTE Paragraph 00:09:12.400 --> 00:09:15.736 Tulitengeneza toleo la mwisho la kitabu, tukakiita "Menstrupedia Comic" 00:09:15.760 --> 00:09:18.520 na kukizindua Septemba mwaka jana. 00:09:19.120 --> 00:09:20.496 Na mpaka sasa, 00:09:20.520 --> 00:09:24.856 zaidi ya wasichana 4,000 wameelimika kwa kutumia kitabu India na -- NOTE Paragraph 00:09:24.880 --> 00:09:27.536 (Makofi) NOTE Paragraph 00:09:27.560 --> 00:09:28.776 Asanteni. NOTE Paragraph 00:09:28.800 --> 00:09:31.120 (Makofi) NOTE Paragraph 00:09:34.240 --> 00:09:36.040 na nchi nyingine 10. 00:09:37.160 --> 00:09:40.176 Mara kwa mara tunakitafsiri kitabu katika lugha tofauti 00:09:40.200 --> 00:09:42.936 Na kushirikiana na mashirika ya ndani nchi 00:09:42.960 --> 00:09:45.616 na kufanya hiki kitabu kipatikane katika nchi tofauti. NOTE Paragraph 00:09:45.640 --> 00:09:48.576 Mashule 15 katika sehemu tofauti India 00:09:48.600 --> 00:09:52.016 yamekifanya kitabu hiki kuwa sehemu ya mtaala wa shule zao 00:09:52.040 --> 00:09:53.816 kufundisha wasichana kuhusu hedhi. NOTE Paragraph 00:09:53.840 --> 00:09:56.240 (Makofi) NOTE Paragraph 00:10:00.440 --> 00:10:05.776 Nafurahishwa kuona jinsi wanaojitolea, 00:10:05.800 --> 00:10:09.936 watu binafsi, wazazi waalimu, wakuu wa mashule 00:10:09.960 --> 00:10:11.456 wamekutana pamoja 00:10:11.480 --> 00:10:15.736 na kufanya msukumo huu wa ufahamishaji wa hedhi kwa jamii zao, 00:10:15.760 --> 00:10:19.456 wamehakikisha wasichana wanajifunza kuhusu siku zao katika umri sahihi 00:10:19.480 --> 00:10:21.640 na kusaidia katika kuvunja mwiko huu NOTE Paragraph 00:10:23.040 --> 00:10:27.336 Ninaota maisha ya mbele ambapo hedhi sio laana, 00:10:27.360 --> 00:10:28.896 sio ugonjwa, 00:10:28.920 --> 00:10:31.360 ila ni mabadiliko katika maisha ya msichana. 00:10:32.120 --> 00:10:33.336 Na ninge -- NOTE Paragraph 00:10:33.360 --> 00:10:35.480 (Makofi) NOTE Paragraph 00:10:37.960 --> 00:10:39.336 Na ningependa kumalizia hii 00:10:39.360 --> 00:10:43.256 kwa ombi dogo kwa wazazi wote hapa. NOTE Paragraph 00:10:43.280 --> 00:10:44.480 Wapendwa wazazi, 00:10:45.240 --> 00:10:47.456 kama mtakuwa mnafedheheshwa na hedhi 00:10:47.480 --> 00:10:49.696 na mabinti zenu watafedheheshwa, pia. 00:10:49.720 --> 00:10:52.176 Hivyo tafadhali muwe na mtazamo chanya katika siku. NOTE Paragraph 00:10:52.200 --> 00:10:53.416 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:10:53.440 --> 00:10:54.656 Asanteni. NOTE Paragraph 00:10:54.680 --> 00:10:57.403 (Makofi)