WEBVTT 00:00:00.940 --> 00:00:04.940 Nchini India, wasichana milioni tatu hawaendi shule. 00:00:04.940 --> 00:00:08.260 Hiyo ni msichana mmoja kati ya watatu wenye umri wa miaka 10 hadi 14. 00:00:08.260 --> 00:00:11.770 Lakini 'Educate Girls' inabadilisha hali hiyo. 00:00:15.885 --> 00:00:18.755 Mtazamo uliokithiri ni 00:00:18.755 --> 00:00:22.825 kwamba mbuzi yangu ni mali na msichana wangu ni dhima. 00:00:22.825 --> 00:00:25.975 Na inahusu tu kubadilisha mtazamo. 00:00:29.635 --> 00:00:31.775 Jina langu ni Bhagwanti. 00:00:33.607 --> 00:00:36.637 Kabla niende shule, lazima nifanye kazi ya nyumbani: 00:00:36.637 --> 00:00:40.267 kupika vyakula, kuosha, kupeleka mbuzi malishoni. 00:00:40.267 --> 00:00:42.655 Wakati mwingine nasafisha nyumba pia. 00:00:44.408 --> 00:00:47.568 Kwanza, katika kila kijiji tunakoingia 00:00:47.568 --> 00:00:49.978 tunapata mtu aliyejitolea wa jamii. 00:00:49.978 --> 00:00:53.238 Watu wetu waliojitolea ni wachanga, wamesoma na wana shauku. 00:00:53.238 --> 00:00:56.288 Wenyewe wangependa kuona mabadiliko. 00:00:57.848 --> 00:01:01.848 Wanakweda lango hadi lango, na wanapata kila msichana ambaye haendi shuleni. 00:01:04.705 --> 00:01:07.255 Kisha, wanaketi na jamii 00:01:07.295 --> 00:01:09.655 na wanabuni mipango ya usajili kulingana na jamii 00:01:09.655 --> 00:01:12.145 ya kurudisha wasichana hawa shuleni. 00:01:12.145 --> 00:01:15.095 Wanaojitolea au 'Balikas' hufanya kazi na shule za vijiji... 00:01:15.095 --> 00:01:17.715 ili kuhakikisha ziko salama na zina vyoo vya wasichana. 00:01:17.735 --> 00:01:20.967 Pia wanasaidia kuwafunza wasichana. 00:01:24.257 --> 00:01:27.174 Kwa hivyo, kisha wanaojitolea "Team Balika' huingia 00:01:27.174 --> 00:01:28.824 katika darasa la shule ya serikali 00:01:28.824 --> 00:01:31.724 na wanatoa mafunzo ya Hindi, Kiigereza na Hesabu 00:01:31.724 --> 00:01:34.454 ili kuhakikisha kuwa watoto wote - wavulana na wasichana, 00:01:34.474 --> 00:01:37.684 wanapata matokeo yanayohitajika ya elimu. 00:01:40.032 --> 00:01:44.411 Inahusu kila msichana kuja shuleni. 00:01:44.601 --> 00:01:49.387 Inahusu kila msichana kuchangia katika dunia inayobadilika. 00:01:49.593 --> 00:01:53.803 Inahusu kila msichana kuchangia mabadiliko katika famili, 00:01:53.974 --> 00:01:57.974 na inahusu kila msichana kuchangia katika mabadiliko 00:01:57.974 --> 00:01:59.847 katika jamii pana. 00:01:59.847 --> 00:02:03.497 Tunazungumzia afya bora, mapato bora. 00:02:03.497 --> 00:02:08.210 Tunazungumzia elimu bora, kwa hivyo ni kwa kila mtoto. 00:02:10.658 --> 00:02:14.518 Kuna takribani asilimia 50, 60 ya wasichana huko Rajasthan ambao wameolewa 00:02:14.518 --> 00:02:15.768 chini ya umri wa miaka 18. 00:02:15.768 --> 00:02:19.318 Kote nchini, asilimia hiyo ya watoto kuolewa iko juu sana. 00:02:20.535 --> 00:02:23.666 Watoto wengi pia, takribani asilimia 10 hadi 15 00:02:23.666 --> 00:02:26.006 wameolewa chini ya umri wa miaka 10. 00:02:26.052 --> 00:02:28.312 Niliozwa na wazazi wangu nikiwa na miaka 14. 00:02:28.332 --> 00:02:31.992 Nilikuwa mwanafunzi katika darasa la 8. Wazazi wa mvulana walikuwa wamekubali 00:02:32.012 --> 00:02:35.202 kuendeleza masomo yangu lakini baada tu ya matokeo yangu kutoka 00:02:35.232 --> 00:02:38.564 hawakutimiza ahadi yao. 00:02:39.442 --> 00:02:42.472 Neelam ni mojawapo ya Balikas 10,000 katika Educated Girls. 00:02:42.472 --> 00:02:46.472 Wamewasaidia watoto milioni mbili. 00:02:48.280 --> 00:02:52.360 Ningependa kuwa mwalimu baada ya masomo na niwafundishe wasichana wengine 00:02:52.360 --> 00:02:56.280 kwa sababu ukipata elimu una ujasiri, 00:02:56.280 --> 00:02:59.735 unaweza kujitegemea, kupata kazi 00:02:59.735 --> 00:03:02.755 na kusaidia familia yako kifedha. 00:03:03.738 --> 00:03:07.738 Kila mwaka wa ziada wa shule unaweza kuzidisha mapato ya mwanamke kwa hadi 20%. 00:03:07.738 --> 00:03:10.808 Katika miaka 10 iliyopita, najivunia kusema tumewapata 00:03:10.808 --> 00:03:14.448 na kuwarudisha shuleni wasichana 150,000 walioondoka shule 00:03:14.448 --> 00:03:18.598 ambao sasa wameunganishwa na wanahudhuria shule na kupata mafunzo.