-
Habari, mimi ni Daktari Amanda Cohn.
-
Mimi ni Tabibu na afisa wa matibabu
-
katika kituo cha CDC chanjo na magonjwa ya kupumua
-
na kwa sasa ninahudumu kama katibu mtendaji
-
wa kamati ya ushauri kuhusu hulka za chanzo- au ACIP.
-
Ningependa kuwajuza
-
jinsi kikundi hiki chapakazi cha wataalam huendeleza mapendekezo
-
na kushauri CDC kuhusu matumizi ya chanjo katika nchi yetu.
-
ACIP imejitolea kuendeleza mapendekezo yanayoegemea ushahidi na sayansi
-
kukinga na kudhibiti magonjwa ambayo yanaweza kingwa kwa chanjo,
-
kama UVIKO-19.
-
Wanapewa motisha na azma yao ya kuokoa maisha,
-
wako huru kutokana na ushawishi wa kisiasa na wanahakikisha uwazi.
-
kwa kuandaa mikutano yao yote wazi kwa umma
-
na kuhakikisha zinapatikana mtandaoni.
-
Kamati hii inajumuisha wanachama wapiga kura kumi na watano,
-
ambao ni wataalam wa kimatibabu na afya ya kijamii toka pande zote za Marekani,
-
pia inahusisha mtu mmoja ambaye anawakilisha umma.
-
Wanahakiki taarifa kuhusu usalama na ufanisi
-
wa chanjo na matokeo ya majaribio ya maabara halafu wanapiga kura kupendekeza
-
kama chanjo hizo zinafaa kutumiwa Marekani
-
Kamati hii pia ina wanachama ambao si wapiga kura,
-
kama vile waakilishi kutoka Muungano wa Wauguzi Marekani,
-
Muungano wa Matabibu wa Marekani, Chuo cha matibabu ya watoto cha Marekani
-
na Chuo cha Matabibu cha Marekani
-
Ni muhimu kuwa na hawa watu katika kamati,
-
kwa sababu wanachangia taswira ya madaktari, wauguzi
-
na wahudumu wengine wa kiafya,
-
ambao hufuata mapendekezo ya chanjo ya CDC na kuzitekeleza.
-
Juhudi si haba imetumiwa kuendeleza, kutafiti na kuidhinisha
-
chanjo za UVIKO-19 haraka,
-
kukabiliana na janga hili linalotukumba.
-
Inaeleweka kuwa unaweza kuwa na wasiwasi
-
kuhusu usalama wa chanjo za UVIKO-19,
-
kulingana na jinsi zimeundwa haraka.
-
Licha ya kasi,
-
Chanjo za UVIKO-19 hupitia mchakato wa uhakiki kali
-
sawa na chanjo zote nyinginezo,
-
kabla ya kamati hii kupiga kura kuhusu kuzipendekeza au la.
-
Usalama wa chanjo ni wa kipaumbele,
-
na hamna tofauti na chanjo za UVIKO-19.
-
Tangia mwanzoni mwa janga hili,
-
ACIP imekutana mara si haba,
-
kuarifiwa kuhusu chanjo za UVIKO-19.
-
Baada ya kila chanjo ya UVIKO-19 kuidhinishwa
-
au matumizi yao kukubaliwa ndani ya Marekani,
-
ACIP itakutana kwa haraka kuhakiki data iliyopo
-
kutokana na utafiti mwingi ambao watengenezaji wa chanjo wamefanya,
-
kuonyesha kuwa kila chanjo inafikia ubora wa usalama na ufanisi.
-
Baada ya kujadiliana na kuchangia kwa umma,
-
Kamati itapiga kura kupendekeza chanjo au la,
-
na wakipendekeza, unafaa kuipokea.
-
Huu ndio mchakato ambao ACIP hutumia kwa chanjo zote pia.
-
Mchakato huu pia umependekeza chanjo salama na za fanaka
-
ambazo hukinga jamii zetu
-
kutokana na magonjwa ambazo hapo mbeleni yaliua halaiki kila mwaka.
-
Natumahi ya kuwa
-
halaiki ya maisha na hata zaidi yataokolewa
-
na chanjo salama za UVIKO-19.
-
Hata hivyo, hakuna jinsi moja itakayokomesha janga la UVIKO-19.
-
Kwa sasa, kinga yako bora itakuwa ni kuunganisha kupokea chanjo ya UVIKO-19,
-
itakapopendekezwa kwako,
-
na kuendelea kufunika pua na kinywa chako kwa barakoa,
-
dumisha umbali wa angalau futi sita na wengine na unawe mikono kila mara,
-
Chanjo za UVIKO-19 zitakuwa jinsi muhimu kusaidia kukomesha janga hili.
-
Kwa taarifa ya ziada, nenda kwa tovuti ya CDC.gov/coronavirus