-
Kufanya chanjo, vipimo na dawa kupatikana
-
inaweza chukua muda mrefu
-
hata kama kuna dharura ya kiafya, kama UVIKO-19.
-
Kuhakikisha upatikanaji wa haraka kwa kila mtu
-
WHO limeunda EUL (OUD)- Orodha ya matumizi ya dharura.
-
video hii inaeleza jinsi EUL (OUD) inavyotumika.
-
Kabla ya chanjo, dawa na vipimo vya uchunguzi vinaweza fikia watu,
-
lazima zitathminiwe kuhakikisha kuwa
-
ubora, usalama na ufanisi vipo hadi kiwango
-
Hii inalinda watu kutokana na uwezekano wa madhara
-
na kuhakikisha kuwa bidhaa zinafanya zinazofaa kufanya:
-
kukinga, kupima na kutibu ugonjwa.
-
Lakini nchi nyingi hazina raslimali
-
za kutekeleza hatua hii muhimu,
-
ambayo inaweza sababisha kuchelewa kwa kupatikana kwa bidhaa za kuokoa maisha
-
kwa wale wanaozihitaji mno.
-
Changamoto ni ngumu zaidi kama ugonjwa ni mpya,
-
kama vile UVIKO-19
-
Bidhaa mpya za kiafya za UVIKO-19 lazima zichunguzwe,
-
kwa kina lakini pia haraka,
-
kuhakikisha zina ufanisi na ni salama kutumia.
-
Kuharakisha mchakato huu
-
WHO imeunda Orodha ya matumizi ya dharura -EUL (OUD)
-
ambayo inatathmini kufaa kwa bidhaa za afya
-
katika msingi wa hatari ikilinganishwa na manufaa,
-
Kwa vipimo,
-
tunatathmini ubora uliopo, usalama na data ya utendakazi
-
pamoja na wataalam huru.
-
Vipimo vingi vya UVIKO-19 tayari vimekusanywa na mahitaji yetu
-
na vimeorodheshwa kwa matumizi.
-
Kwa chanjo na madawa,
-
tunatathmini data kutoka kwa majaribio ya maabara
-
na data nyinginezo za usalama, ufanisi na ubora,
-
na kualika wataalam kutoka mamlaka za kitaifa za kiafya
-
kuzihakiki pia.
-
Pindi chanjo, dawa au kipimo
-
kimeorodheshwa kwa matumizi ya dharura,
-
tunashirikiana na washirika wetu na wataalam kueleza manufaa yake
-
na kusaidia na mchakato wa kuidhinishwa katika nchi mbalimbali.
-
Lakini hatukomi hapo.
-
WHO itaendelea kufanya uchunguzi wa mara kwa mara wa ubora wa kila bidhaa.
-
Lengo:
-
kusaidia nchi mbalimbali duniani kote
-
kuwasilisha,
-
chanjo, vipimo na madawa ya ubora wa hali ya juu
-
haraka na kwa usalama uwezekanavyo