WEBVTT 00:00:01.560 --> 00:00:04.135 Hii si kwata. 00:00:04.375 --> 00:00:06.651 Jina langu ni Greta Thunberg. 00:00:06.852 --> 00:00:10.212 Tunaishi mwanzoni mwa uangamivu mkubwa 00:00:11.171 --> 00:00:13.612 Tabianchi yetu inakongoroka. 00:00:14.022 --> 00:00:18.217 Watoto kama mimi wanaacha masomo yao ili waandamane. 00:00:18.561 --> 00:00:20.897 Lakini bado tunaweza kurekebisha hili. 00:00:20.897 --> 00:00:22.963 Bado unaweza kurekebisha hili. 00:00:23.372 --> 00:00:26.577 Ili kuendelea kuishi, tuache kuchoma nishati ya visukuku, japo hili tu halitoshi. 00:00:27.217 --> 00:00:29.822 Masuluhisho mengi yanatajwa, lakini vipi suluhisho lililo mbele 00:00:30.112 --> 00:00:32.692 yetu? 00:00:32.692 --> 00:00:35.412 Nimwachie rafiki yangu George aeleze. 00:00:35.682 --> 00:00:38.112 Ipo mashine ya ajabu inayofyonza gesi ya ukaa hewani, ina gharama ndogo na inajijenga 00:00:38.211 --> 00:00:42.721 yenyewe. 00:00:42.721 --> 00:00:44.418 Inaitwa ... mti. 00:00:44.418 --> 00:00:46.466 Mti ni mfano wa suluhisho la asili la tabianchi. 00:00:46.576 --> 00:00:47.929 Mikoko, maeneo ya maozeo, mapori, maeneo chepechepe, sakafu za bahari, mwani, vinamasi, matumbawe, vina 00:00:47.929 --> 00:00:48.872 chukua gesi ya ukaa hewani na kuifungia. 00:00:48.952 --> 00:00:53.692 Maumbile asili ni zana ambayo tunaweza kutumia kurekebisha tabianchi yetu iliyokongoroka 00:00:53.692 --> 00:00:56.502 Masuluhisho haya asili kwa tabianchi yanaweza kuleta tofauti kubwa. 00:00:56.502 --> 00:00:58.772 Poa sana, sio? 00:00:58.772 --> 00:01:02.692 Lakini kama tu tutaacha nishati za visukuku ardhini. 00:01:03.212 --> 00:01:07.883 Na hii ndio balaa ... hivi sasa tunazipuuzia. 00:01:08.502 --> 00:01:12.325 Tunatumia mara elfu zaidi kwa ruzuku kwenye nishati za visukuku duniani kuliko kwenye masuluhisho 00:01:12.325 --> 00:01:14.012 ya asili. 00:01:14.222 --> 00:01:17.622 Masuluhisho asili ya tabianchi hupata 2% tu 00:01:19.702 --> 00:01:21.892 ya pesa zote zitumikazo kushughulikia kukongoroka kwa tabianchi. 00:01:21.892 --> 00:01:24.402 Hii ni pesa yako, ni kodi zako na akiba zako. 00:01:25.744 --> 00:01:30.548 Hata balaa zaidi, hivi sasa ambapo tunaihitaji asili zaidi 00:01:30.548 --> 00:01:32.842 tunaiharibu haraka kuliko wakati wowote. 00:01:32.842 --> 00:01:35.377 Hadi spishi 200 zinatoweka kila siku. 00:01:35.377 --> 00:01:39.053 Sehemu kubwa ya barafu ya Aktiki imetoweka. 00:01:39.394 --> 00:01:41.021 Wanyamapori wetu wengi wametoweka. 00:01:41.021 --> 00:01:43.468 Udongo wetu mwingi umetoweka. 00:01:43.773 --> 00:01:44.958 Sasa tufanye nini? 00:01:44.958 --> 00:01:47.211 Utafanya nini? 00:01:47.211 --> 00:01:50.094 Ni rahisi ... tunahitaji kulinda, kurejeza na kugharamia. 00:01:50.094 --> 00:01:54.228 Linda. 00:01:54.462 --> 00:01:57.050 Misitu ya tropiki inafyekwa 00:01:57.050 --> 00:01:59.029 kwa kiwango cha viwanja 30 vya mpira kwa dakika. 00:01:59.029 --> 00:02:01.012 00:02:01.012 --> 00:02:02.813 Pale asili inatekeleza jambo muhimu, lazima tuilinde. 00:02:02.813 --> 00:02:04.374 Rejeza. 00:02:04.374 --> 00:02:05.458 Sehemu kubwa ya sayari yetu imeharibiwa. 00:02:05.458 --> 00:02:06.225 Lakini asili inaweza kujirejeza 00:02:06.225 --> 00:02:07.429 na tunaweza kusaidia mifumo ya ikolojia kurudi tena. 00:02:07.429 --> 00:02:08.501 00:02:08.501 --> 00:02:09.513 Gharamia. 00:02:10.084 --> 00:02:11.198 Tunatakiwa kuacha kugharamia vitu vinavyoharibu asili 00:02:11.198 --> 00:02:13.325 na kulipia vitu vinavyoisaidia. 00:02:13.325 --> 00:02:16.153 Ni rahisi tu hivyo. 00:02:16.153 --> 00:02:18.679 Linda, rejeza, gharamia. 00:02:18.679 --> 00:02:20.505 Hili linaweza kufanyika kila mahali. 00:02:20.505 --> 00:02:21.878 Watu wengi tayari wameanza kutumia masuluhisho asili kwa tabianchi. 00:02:21.878 --> 00:02:24.581 Tunatakiwa kufanya hivyo kwa kiwango kikubwa. 00:02:24.581 --> 00:02:26.581 Unaweza kuwa sehemu ya hili. 00:02:26.581 --> 00:02:30.042 Pigia kura wale wanaolinda asili. 00:02:31.051 --> 00:02:31.881 Shirikisha video hii. 00:02:32.702 --> 00:02:36.172 Ongelea kuhusu hili. 00:02:36.172 --> 00:02:38.412 Dunia kote kuna vikundi vya kushangaza vinavyopigania asili. 00:02:39.112 --> 00:02:40.756 Ungana navyo! 00:02:40.756 --> 00:02:42.018 00:02:42.018 --> 00:02:43.044 Kila kitu ni muhimu. 00:02:43.044 --> 00:02:43.801 Ufanyacho ni muhimu.