Return to Video

Immigrant and Refugee Mental Health

  • 0:04 - 0:05
    Hujambo, Jina langu ni Suzan Song,
  • 0:05 - 0:09
    Mwelekezi wa Idara cha Taaluma ya Ugonjwa
    wa Akili kwa Watoto, Vijana na Familia
  • 0:09 - 0:11
    ya Chuo Kikuu cha George Washington,
  • 0:11 - 0:12
    na Mshauri wa Kulinda Ubinadamu
  • 0:12 - 0:15
    kwa waathiriwa wa uhamishaji
    wa lazima kote duniani na nchini.
  • 0:15 - 0:17
    Kumekuwa na ongezeko la kipekee
  • 0:17 - 0:19
    la idadi ya wakimbizi kote ulimwenguni,
  • 0:19 - 0:23
    wakiwemo wakimbizi, watafuta
    makao, wahamiaji wasio halali
  • 0:23 - 0:25
    na watoto walio pweke.
  • 0:25 - 0:28
    Kote ulimwenguni, zaidi ya watu milioni 65
  • 0:28 - 0:32
    kwa sasa ni wakimbizi kutokana
    na vita, mateso au mgogoro wa kivita.
  • 0:32 - 0:36
    Kufikia mwanzo mwa 2018, takribani
    watoto milioni 31 kote ulimwenguni
  • 0:36 - 0:38
    walifanywa wakimbizi kutokana
    na vurugu na migogoro.
  • 0:38 - 0:40
    Iwapo mitindo hii ya sasa itaendelea,
  • 0:40 - 0:43
    mtu mmoja kati ya watu mia moja
    atakuwa mkimbizi hivi karibuni.
  • 0:43 - 0:46
    Kwa bahati mbaya, wakimbizi na
    waathiriwa wengi wa uhamaji wa lazima
  • 0:46 - 0:49
    hawapokei huduma
    inayohitajika ya afya ya akili.
  • 0:49 - 0:52
    kutokana na usiri wa huduma,
    ukosefu wa kufikia huduma ya kitaalamu,
  • 0:53 - 0:54
    na shutuma dhidi ya matatizo ya akili.
  • 0:55 - 0:57
    Wakimbizi ni wale ambao
    wametoroka katika nchi zao halisi
  • 0:57 - 1:00
    kutokana na wasiwasi wa
    mateso yaliyokithiri
  • 1:00 - 1:03
    yanayolingana na mbari, dini,
    uraia, maoni ya kisiasa
  • 1:03 - 1:06
    au uanachama katika
    kikundi fulani cha jumuiya.
  • 1:06 - 1:08
    Ingawa wakimbizi huomba
    ulinzi wakiwa ughaibuni
  • 1:08 - 1:11
    na wanapewa ruhusa ya kuingia Marekani,
  • 1:11 - 1:14
    Watu wanaotafuta
    makao pia wana hofu ya mateso.
  • 1:14 - 1:17
    Lakini wanatafuta ulinzi wakiwa
    ndani ya Marekani.
  • 1:17 - 1:19
    Wakimbizi na watu wengine
    walioathiriwa na mzozo
  • 1:19 - 1:22
    waliripotiwa kuwa na
    asilimia 15 hadi 30 ya
  • 1:22 - 1:23
    PTSD na mafadhaiko,
  • 1:24 - 1:29
    ikilinganishwa na asilimia 3.5 ya PTSD
    miongoni mwa wasio wakimbizi.
  • 1:29 - 1:31
    Mambo thabiti
    yanayoashiria afya mbovu ya akili
  • 1:31 - 1:35
    ni kupitia mateso na matukio
    mengi yanayosababisha kiwewe.
  • 1:35 - 1:39
    Lakini mateso, kutenganishwa na familia,
    michakato ya kuchosha ya kupata makao,
  • 1:39 - 1:41
    kutengwa na hali ngumu
    katika nchi mpya
  • 1:41 - 1:43
    zote huongeza ubaya wa afya ya akili.
  • 1:43 - 1:47
    Mazingira baada ya kuhama,
    hasa kipindi kirefu cha kuzuiliwa,
  • 1:47 - 1:49
    hali isiyo salama ya uhamiaji,
  • 1:49 - 1:53
    ufikiaji mbovu wa huduma
    na vikwazo vya kazi na elimu
  • 1:53 - 1:55
    vinaweza kudhoofisha zaidi afya ya akili.
  • 1:55 - 1:58
    Haya hayatoi upeo kamili wa
    matatizo ya hisia
  • 1:58 - 2:00
    yanayokumbwa na watu wengi
    walioathiriwa na mgogoro
  • 2:00 - 2:03
    ikiwa ni pamoja na huzuni isioelezeka,
    kiwewe kigumu,
  • 2:03 - 2:07
    kukata tamaa, kutengwa,
    hasira, na kutoamini.
  • 2:07 - 2:10
    Watu wengi wanakumbana na hatua za kawaida
  • 2:10 - 2:12
    kwa matukio yasiyo ya kawaida kabisa.
  • 2:12 - 2:16
    Baada ya muda, wakimbizi wengi huonyesha
    dalili chache au hawaonyeshi kabisa.
  • 2:16 - 2:18
    Idadi ndogo huonyesha mtindo wa
    kupona polepole
  • 2:18 - 2:20
    na idadi ndogo ingine
    huendelea kutatizika.
  • 2:21 - 2:25
    Kwa hivyo tunahitaji kutathmini tofauti
    kati ya hali za tukio za dhiki
  • 2:25 - 2:27
    na hali dhahiri za ugonjwa
    wa akili kwa wakimbizi.
  • 2:27 - 2:30
    Tunafanya hili kwa kulenga
    athari za kuathirika na
  • 2:30 - 2:32
    hali za awali za kiwewe,
  • 2:32 - 2:34
    mambo ya kila siku ya kusababisha msongo,
  • 2:34 - 2:37
    na mifumo mikuu ya ushirikiano wa
    kijamii ambayo mtu anahusika.
  • 2:37 - 2:40
    Wataalamu wa akili wanaweza
    kuwasaidia watu hawa
  • 2:40 - 2:44
    kupitia shughuli za kliniki zinazofaa kwa
    wakimbizi na wanaotafuta makao.
  • 2:44 - 2:47
    Kwa kiwango cha sera kwa kufanya
    tathmini za makao
  • 2:47 - 2:50
    na kwa kiwango cha utetezi kwa
    kuhimiza usawa wa kufikia,
  • 2:50 - 2:54
    uwezo wa huduma kuwastahi wakimbizi
    na watu waliohamishwa kwa lazima,
  • 2:54 - 2:57
    na kwa kushirikiana na wanachama
    wa jumuiya ya nyanja mbalimbali
  • 2:57 - 3:00
    kama vile mawakili,
    walimu na watengenezaji wa sera
  • 3:00 - 3:02
    kutoa mfumo salama ambao wakimbizi
  • 3:02 - 3:05
    na walionusurika kuhamishwa
    lazima wanaweza kutegemea.
Title:
Immigrant and Refugee Mental Health
Description:

more » « less
Video Language:
English
Team:
Amplifying Voices
Project:
Mental Health
Duration:
03:13

Swahili subtitles

Incomplete

Revisions Compare revisions