0:00:01.560,0:00:04.135 Hii si kwata. 0:00:04.375,0:00:06.651 Jina langu ni Greta Thunberg. 0:00:06.852,0:00:10.212 Tunaishi mwanzoni mwa uangamivu [br]mkubwa 0:00:11.171,0:00:13.612 Tabianchi yetu inakongoroka. 0:00:14.022,0:00:18.217 Watoto kama mimi wanaacha masomo yao ili waandamane. 0:00:18.561,0:00:20.897 Lakini bado tunaweza kurekebisha hili. 0:00:20.897,0:00:22.963 Bado unaweza kurekebisha hili. 0:00:23.372,0:00:26.577 Ili kuendelea kuishi, tuache kuchoma nishati ya visukuku, japo hili tu halitoshi. 0:00:27.217,0:00:29.822 Masuluhisho mengi yanatajwa, lakini vipi suluhisho lililo mbele 0:00:30.112,0:00:32.692 yetu? 0:00:32.692,0:00:35.412 Nimwachie rafiki yangu George aeleze. 0:00:35.682,0:00:38.112 Ipo mashine ya ajabu inayofyonza gesi ya ukaa hewani, ina gharama ndogo na inajijenga 0:00:38.211,0:00:42.721 yenyewe. 0:00:42.721,0:00:44.418 Inaitwa ... mti. 0:00:44.418,0:00:46.466 Mti ni mfano wa suluhisho la asili la tabianchi. 0:00:46.576,0:00:47.929 Mikoko, maeneo ya maozeo, mapori, maeneo chepechepe, sakafu za bahari, mwani, vinamasi, matumbawe, vina 0:00:47.929,0:00:48.872 chukua gesi ya ukaa hewani na kuifungia. 0:00:48.952,0:00:53.692 Maumbile asili ni zana ambayo tunaweza kutumia kurekebisha tabianchi yetu iliyokongoroka 0:00:53.692,0:00:56.502 Masuluhisho haya asili kwa tabianchi yanaweza kuleta tofauti kubwa. 0:00:56.502,0:00:58.772 Poa sana, sio? 0:00:58.772,0:01:02.692 Lakini kama tu tutaacha nishati za visukuku ardhini. 0:01:03.212,0:01:07.883 Na hii ndio balaa ... hivi sasa tunazipuuzia. 0:01:08.502,0:01:12.325 Tunatumia mara elfu zaidi kwa ruzuku kwenye nishati za visukuku duniani kuliko kwenye masuluhisho 0:01:12.325,0:01:14.012 ya asili. 0:01:14.222,0:01:17.622 Masuluhisho asili ya tabianchi hupata 2% tu 0:01:19.702,0:01:21.892 ya pesa zote zitumikazo kushughulikia kukongoroka kwa tabianchi. 0:01:21.892,0:01:24.402 Hii ni pesa yako, ni kodi zako na akiba zako. 0:01:25.744,0:01:30.548 Hata balaa zaidi, hivi sasa ambapo tunaihitaji asili zaidi 0:01:30.548,0:01:32.842 tunaiharibu haraka kuliko wakati wowote. 0:01:32.842,0:01:35.377 Hadi spishi 200 zinatoweka kila siku. 0:01:35.377,0:01:39.053 Sehemu kubwa ya barafu ya Aktiki imetoweka. 0:01:39.394,0:01:41.021 Wanyamapori wetu wengi wametoweka. 0:01:41.021,0:01:43.468 Udongo wetu mwingi umetoweka. 0:01:43.773,0:01:44.958 Sasa tufanye nini? 0:01:44.958,0:01:47.211 Utafanya nini? 0:01:47.211,0:01:50.094 Ni rahisi ... tunahitaji kulinda, kurejeza na kugharamia. 0:01:50.094,0:01:54.228 Linda. 0:01:54.462,0:01:57.050 Misitu ya tropiki inafyekwa 0:01:57.050,0:01:59.029 kwa kiwango cha viwanja 30 vya mpira kwa dakika. 0:01:59.029,0:02:01.012 0:02:01.012,0:02:02.813 Pale asili inatekeleza jambo muhimu, lazima tuilinde. 0:02:02.813,0:02:04.374 Rejeza. 0:02:04.374,0:02:05.458 Sehemu kubwa ya sayari yetu imeharibiwa. 0:02:05.458,0:02:06.225 Lakini asili inaweza kujirejeza 0:02:06.225,0:02:07.429 na tunaweza kusaidia mifumo ya ikolojia kurudi tena. 0:02:07.429,0:02:08.501 0:02:08.501,0:02:09.513 Gharamia. 0:02:10.084,0:02:11.198 Tunatakiwa kuacha kugharamia vitu vinavyoharibu asili 0:02:11.198,0:02:13.325 na kulipia vitu vinavyoisaidia. 0:02:13.325,0:02:16.153 Ni rahisi tu hivyo. 0:02:16.153,0:02:18.679 Linda, rejeza, gharamia. 0:02:18.679,0:02:20.505 Hili linaweza kufanyika kila mahali. 0:02:20.505,0:02:21.878 Watu wengi tayari wameanza kutumia masuluhisho asili kwa tabianchi. 0:02:21.878,0:02:24.581 Tunatakiwa kufanya hivyo kwa kiwango kikubwa. 0:02:24.581,0:02:26.581 Unaweza kuwa sehemu ya hili. 0:02:26.581,0:02:30.042 Pigia kura wale wanaolinda asili. 0:02:31.051,0:02:31.881 Shirikisha video hii. 0:02:32.702,0:02:36.172 Ongelea kuhusu hili. 0:02:36.172,0:02:38.412 Dunia kote kuna vikundi vya kushangaza vinavyopigania asili. 0:02:39.112,0:02:40.756 Ungana navyo! 0:02:40.756,0:02:42.018 0:02:42.018,0:02:43.044 Kila kitu ni muhimu. 0:02:43.044,0:02:43.801 Ufanyacho ni muhimu.