-
Polio ni ugonjwa unaosababisha kupooza ya kudumu.
-
Hatuwezi kuiponya lakini tunaweza kuizuia.
-
Taratibu mbili zinasaidia kuzuia polio.
-
Chanjo mbili salama na fanisi
-
Mojawapo ya chanjo hizi hupeanwa na matone mawili tu
-
ndani ya kinywa cha mtoto,
-
hii huitwa chanjo ya polio ya kinywani.
-
nyingine hupeanwa kama shindano,
-
hii huitwa chanjo ya virusi vya polio visivyoamilishwa.
-
Zote zinafunza miili ya watoto kupambana na virusi vya Polio.
-
Lakini vinafanya hivi kwa njia mbalimbali.
-
Chanjo ya polio ya kinywani hujenga ulinzi ndani ya matumbo ya mtoto
-
Chanjo hii hailindi tu mtoto anayeipokea,
-
bali pia na wale walio karibu na mtoto aliyechanjwa
-
Dozi kadhaa ya chanjo ya polio ya kinywani inafaa kupewa kila mtoto
-
katika eneo ambayo polio ni tishio.
-
Chanjo ya shindano inajenga kinga damuni badala ya mfereji wa chakula.
-
Inasaidia kuongeza kinga na kufanya nchi ziwe bila polio.
-
Lakini haikomeshi kusambaa kwa polio kati ya watoto,
-
kwa hivyo si muhimu sana katika maeneo ambayo polio bado inasambaa.
-
Tunahitaji chanjo ya kinywani kukomesha virusi popote ipatikanapo.
-
Pindi polio inapokomeshwa kila pahali,
-
chanjo ya virusi vya polio visiyoamilishwa vitatumiwa pekee yao
-
kuhakikisha umma imekingwa.
-
Chanjo hizi zote zimeidhinishwa kuwa salama na fanisi
-
na Shirika la Afya Ulimwenguni.
-
Kuhakikisha utendakazi bora, zinaafaa kupewa watoto wote
-
bila kujali wanapoishi.
-
Kwa sababu ya hizi chanjo
-
visa vya polio vimepungua kwa asilimia 99 kote duniani.
-
Tuchanje kila mtoto!
-
Tuangamimize polio damia!