Return to Video

Chimamanda Adichie: Hatari ya simulizi moja

  • 0:00 - 0:02
    Mimi ni msimuliaji wa hadithi
  • 0:02 - 0:05
    Ningependa kuwasimulia kidogo maisha yangu
  • 0:05 - 0:10
    juu ya kile ninachopenda kuita
    "hatari ya simulizi moja"
  • 0:11 - 0:14
    Nilikulia mazingira ya chuo
    kikuu magharibi mwa Nigeria
  • 0:14 - 0:17
    Mama yangu anasema nilianza kusoma
    nikiwa na miaka miwili
  • 0:17 - 0:21
    japo nadhani miaka minne ni sahihi zaidi
  • 0:22 - 0:24
    Niliwahi sana kuanza kusoma
  • 0:24 - 0:27
    Nilisoma vitabu vya watoto vya Uingereza
    na Marekani
  • 0:28 - 0:30
    Pia nilianza kuandika katika umri mdogo
  • 0:30 - 0:34
    Na nilipoanza kuandika,
    nikiwa na takriban miaka saba,
  • 0:34 - 0:36
    hadithi za penseli na michoro ya rangi
  • 0:36 - 0:40
    ambazo mama yangu alilazimika kuzisoma,
  • 0:40 - 0:43
    niliandika hadithi
    sawa na zile nilizokuwa nazisoma:
  • 0:43 - 0:48
    Wahusika wangu wote
    walikuwa wazungu na wenye macho ya bluu.
  • 0:48 - 0:50
    Walicheza katika theluji.
  • 0:50 - 0:52
    Walikula matofaa
  • 0:52 - 0:54
    (Kicheko)
  • 0:54 - 0:56
    Na walizungumza sana kuhusu hali ya hewa,
  • 0:56 - 0:58
    jinsi ilivyo vizuri kuona jua limechomoza.
  • 0:58 - 1:00
    (Kicheko)
  • 1:00 - 1:04
    Yote haya,ingawa niliishi Nigeria.
  • 1:04 - 1:05
    Nilikuwa sijawahi kwenda nje ya Nigeria.
  • 1:07 - 1:10
    Hatukuwa na theluji, tulikula maembe.
  • 1:10 - 1:12
    Na hatukuzungumza kuhusu hali ya hewa,
  • 1:12 - 1:14
    sababu hakukuwa na haja ya kufanya hivyo.
  • 1:14 - 1:17
    Wahusika wangu pia
    walikunywa sana bia ya tangawizi
  • 1:17 - 1:19
    kwa sababu wahusika
    katika vitabu vya Uingereza
  • 1:19 - 1:21
    walikunywa bia ya tangawizi.
  • 1:21 - 1:24
    Ijapokuwa
    sikuifahamu bia ya tangawizi
  • 1:24 - 1:26
    (Kicheko)
  • 1:26 - 1:27
    Na kwa miaka mingi baadaye
  • 1:27 - 1:30
    nilikuwa na shauku
    ya kuonja bia ya tangawizi.
  • 1:30 - 1:32
    Lakini hiyo ni hadithi nyingine.
  • 1:32 - 1:34
    Ambacho hii inaonyesha,nafikiri
  • 1:35 - 1:37
    Ni namna tulivyo wajinga na wanyonge
  • 1:37 - 1:39
    Tunapokabiliana na simulizi
  • 1:39 - 1:40
    hasa hasa kama watoto
  • 1:42 - 1:45
    Sababu nilisoma vitabu
    vyenye wahusika wa kigeni
  • 1:45 - 1:48
    Nilikuwa nimeaminishwa kwamba vitabu
  • 1:48 - 1:51
    kwa asili lazima
    viwe na wahusika wageni
  • 1:51 - 1:54
    Na vielezo kuhusu mambo ambayo
    binafsi siyafahamu
  • 1:56 - 1:58
    Mambo yalibadilika
    Nilipopata vitabu vya Afrika
  • 1:59 - 2:01
    havikuwepo kwa wingi
  • 2:01 - 2:04
    Na haikuwa rahisi kuvipata
    kama vya kigeni
  • 2:04 - 2:07
    Lakini sababu ya waandishi
    kama Chinua Achebe na Camara Laye
  • 2:07 - 2:11
    Nilipata badiliko la akili
    ninavyoiona fasihi
  • 2:11 - 2:13
    Niligundua kwamba watu kama mimi,
  • 2:13 - 2:15
    wasichana weusi
  • 2:15 - 2:19
    wenye nywele ngumu
  • 2:19 - 2:20
    pia wapo katika fasihi.
  • 2:21 - 2:24
    Nilianza kuandika
    vitu nilivyovifahamu
  • 2:25 - 2:28
    Nilikuwa navipenda hivyo vitabu
    vya Marekani na Uingereza
  • 2:28 - 2:32
    Viliamsha fikra zangu
    Vilifunua vitu vipya.
  • 2:32 - 2:34
    Lakini matokeo yasiyokusudiwa
  • 2:34 - 2:36
    yalikuwa; sikufahamu kuwa
    watu kama mimi
  • 2:36 - 2:37
    waweza kuwepo katika fasihi.
  • 2:38 - 2:42
    hivyo ufumbuzi wa waandishi Waafrika:
  • 2:42 - 2:46
    Uliniokoa na mtazamo mmoja
    juu ya vitabu
  • 2:47 - 2:50
    Ninatoka kwenye familia
    ya kawaida
  • 2:50 - 2:52
    Baba yangu alikuwa mhadhiri
  • 2:52 - 2:54
    Mama yangu ni
    afisa wa utawala
  • 2:55 - 2:58
    Kwa hiyo kama kawaida, tulikuwa na,
  • 2:58 - 3:03
    mtumishi wa nyumbani
    anayetoka vijiji vya jirani
  • 3:03 - 3:06
    Nilipokuwa na miaka nane
    tulipata mtumishi wa kiume
  • 3:07 - 3:08
    Jina lake aliitwa Fide
  • 3:10 - 3:14
    Mama alituambia kuwa familia
    yake ni masikini sana
  • 3:15 - 3:20
    Mama alituma magimbi na mchele
    na nguo zetu za zamani kwa familia yao
  • 3:20 - 3:23
    Na niliposhindwa kumaliza chakula
    mama alisema,
  • 3:23 - 3:27
    "Maliza chakula! kuna watu
    ambao hawana chochote
  • 3:27 - 3:31
    Niliwahurumia sana
    familia ya Fide
  • 3:32 - 3:34
    Jumamosi moja tukaenda
    kijijini kwao kutembelea
  • 3:34 - 3:38
    na mama yake akatuonyesha
    kikapu kizuri
  • 3:38 - 3:41
    kilichosukwa kwa ukili uliopakwa rangi
    na kaka yake Fide
  • 3:41 - 3:43
    Nilishangaa
  • 3:43 - 3:46
    Sikudhani kuwa yeyote katika familia yake
  • 3:46 - 3:49
    angeweza kutengeneza chochote
  • 3:49 - 3:52
    yote niliyowahi kusikia kuhusu wao
    ni namna walivyo masikini
  • 3:52 - 3:56
    Kwa hiyo ilikuwa haiwezekani kwangu
    kuwaona tofauti na umasikini wao
  • 3:57 - 4:00
    umasikini wao ilikuwa
    ni simulizi moja kwangu
  • 4:01 - 4:04
    baadaye niliwaza hili
    nilipotoka Nigeria
  • 4:04 - 4:06
    Kwenda Marekani kusoma
    chuo kikuu
  • 4:06 - 4:08
    Nilikuwa na miaka 19
  • 4:08 - 4:11
    Mmarekani niliyekuwa
    naishi naye chumba kimoja alinishangaa
  • 4:12 - 4:16
    Aliuliza wapi nimefunza
    kuzungumza kiingereza vizuri
  • 4:16 - 4:18
    Alishangaa nilipomwambia kuwa Nigeria
  • 4:18 - 4:20
    wanatumia kiingereza kama lugha ya taifa
  • 4:22 - 4:26
    Aliomba kusikiliza "nyimbo za kikabila"
  • 4:26 - 4:28
    na alipigwa butwaa vile vile
  • 4:28 - 4:30
    Nilipompa kanda yangu ya Mariah Carey
  • 4:30 - 4:33
    (kicheko)
  • 4:33 - 4:37
    Alidhani kuwa sifahamu
    kutumia jiko la umeme
  • 4:38 - 4:39
    Kilichonishangaza mimi ni hiki
  • 4:39 - 4:42
    Alikuwa ananihurimia
    hata kabla ya kuniona
  • 4:43 - 4:46
    Mtazamo wake mbovu,
    kunihusu, kama Mwafrika,
  • 4:46 - 4:49
    Ulikuwa wa huruma ya kudhalilisha,
    yenye kujali
  • 4:50 - 4:53
    Alikuwa na simulizi moja
    kuhusu Afrika:
  • 4:54 - 4:56
    Simulizi ya majanga.
  • 4:56 - 4:58
    Kwenye simulizi hii moja,
  • 4:58 - 5:02
    Hakukuwa na uwezekano wa Mwafrika
    kufanana naye kwa namna yeyote,
  • 5:02 - 5:05
    Hakukuwa na uwezekano wa hisia
    ngumu zaidi ya huruma,
  • 5:05 - 5:09
    Hakukuwa na uwezekano wa ushirikiano
    kama binadamu walio sawa.
  • 5:09 - 5:11
    Lazima niseme kuwa
    kabla ya kwenda Marekani,
  • 5:11 - 5:13
    Sikuwa nikijitambua kwa undani
    kama Mwafrika.
  • 5:14 - 5:17
    Lakini Marekani, popote Afrika ilipotajwa,
    watu walinigeukia.
  • 5:17 - 5:20
    Bila kujali kuwa sifahamu chochote
    kuhusu nchi kama Namibia.
  • 5:21 - 5:23
    Lakini nilikuja kuupokea
    huu utambulisho mpya,
  • 5:23 - 5:26
    Na kwa namna nyingi sasa
    ninajitazama kama Mwafrika.
  • 5:26 - 5:30
    Ijapokuwa bado ninakasirishwa sana
    pale Afrika inapoelezewa kama ni nchi
  • 5:30 - 5:34
    Mfano wa karibu, ni safari yangu ya ndege
  • 5:34 - 5:35
    Kutoka Lagos hivi juzi,
  • 5:35 - 5:38
    Ambapo kulikuwa na tangazo
  • 5:38 - 5:43
    Kuhusu kazi ya kujitolea kule
    "India, Afika na nchi nyingine"
  • 5:43 - 5:44
    Kicheko
  • 5:44 - 5:48
    Baada ya kuishi Marekani kama Mwafrica
  • 5:48 - 5:51
    Nikaanza kuelewa mwitikio wa
    niliyekuwa naishi naye chumba kimoja
  • 5:52 - 5:54
    kama sikukulia Nigeria
  • 5:54 - 5:57
    Na kama kila nilichofahamu kuhusu Afrika
    kilitokana na picha maarufu
  • 5:57 - 6:02
    Mimi pia ningedhani kuwa Africa ni mahali
    penye mandhari nzuri,
  • 6:02 - 6:04
    Wanyama wa kupendeza,
  • 6:04 - 6:06
    na watu wasioeleweka,
  • 6:06 - 6:10
    wapiganao vita visivyo na maana,
    wanaokufa na umasikini na UKIMWI
  • 6:10 - 6:12
    wasioweza kujisemea
  • 6:12 - 6:16
    wanaosubiri kusaidiwa na
    mtu mweupe, mgeni mwenye ukarimu
  • 6:17 - 6:19
    Ningewaona waafrika
    kwa namna ile ambayo mimi,
  • 6:19 - 6:22
    nilipokuwa mtoto,
    niliiona familia ya Fide
  • 6:23 - 6:27
    Hii simulizi moja kuhusu Afrika
    nadhani inatokana na fasihi za magharibi
  • 6:27 - 6:32
    Sasa, huu ni msemo kutoka katika uandishi
    wa mfanyabiashara wa London aitwaye John Lok,
  • 6:32 - 6:35
    aliyesafiri kwa maji kuelekea
    Afrika magharibi mwaka 1561
  • 6:35 - 6:39
    na aliweka hazina ya kuvutia
    kutokana na safari yake.
  • 6:40 - 6:44
    Baada ya kuwaita Waafrika weusi kama
    " hayawani wasio na nyumba,"
  • 6:44 - 6:48
    aliandika,"Pia kuna watu wasio na vichwa,
  • 6:48 - 6:52
    midomo na macho yao
    yapo katika vifua vyao."
  • 6:53 - 6:55
    Sasa, nilicheka kila
    nikisoma haya maneno.
  • 6:55 - 6:58
    Na lazima mtu
    atakubaliana na fikira za John Lok.
  • 6:59 - 7:01
    Lakini kipi ni muhimu
    kuhusu uandishi wake
  • 7:01 - 7:03
    ni kwamba inawakilisha mwanzo
  • 7:03 - 7:06
    wa utamaduni wa kuelezea hadithi
    za Afrika kwa Magharibi:
  • 7:06 - 7:09
    Utamaduni wa kusini mwa jangwa la Sahara
    kama sehemu isiyofaa,
  • 7:09 - 7:12
    yenye utofauti, yenye kiza,
  • 7:12 - 7:17
    ya watu ambao, kutokana na maneno ya
    mshairi bora aitwaye Rudyard Kipling,
  • 7:17 - 7:19
    ni "nusu shetani, nusu watoto."
  • 7:20 - 7:23
    Hivyo, nilianza kuelewa kwamba mwanafunzi
    Mmarekani ninayeshirikiana nae chumba
  • 7:23 - 7:25
    lazima katika maisha yake
  • 7:25 - 7:29
    atakuwa ameona na kusikia
    namna mbalimbali za hii hadithi moja,
  • 7:29 - 7:31
    kama ilivyo kwa profesa,
  • 7:31 - 7:35
    ambaye aliwahi niambia kuwa
    riwaya yangu haikuwa "na uhalisia wa Kiafrika,"
  • 7:36 - 7:38
    Sasa, nilikubaliana na kuchanganua
  • 7:38 - 7:41
    kwamba kulikuwa na baadhi ya vitu
    ambavyo si sawa katika riwaya hii,
  • 7:41 - 7:44
    na kuwa nilifeli katika maeneo mbalimbali,
  • 7:44 - 7:46
    lakini sikufiria kwamba ilifeli
  • 7:46 - 7:49
    katika kutekeleza
    uhalisia wake wa Kiafrika.
  • 7:49 - 7:53
    Kiukweli, sikufahamu
    uhalisia wa Kiafrika ni upi.
  • 7:54 - 7:58
    Profesa alinielezza kwamba wahusika kwenye riwaya
    walikuwa wanafanana mno kama yeye,
  • 7:58 - 8:00
    msomi aliye katika maisha ya kati.
  • 8:00 - 8:03
    Wahusika wangu waliendesha magari.
  • 8:03 - 8:05
    Hawakuwa wanashinda na njaa.
  • 8:05 - 8:08
    Kwa hiyo hawakuwa Waafrika halisi.
  • 8:09 - 8:12
    Lakini niongeze haraka-haraka
    kwamba najisikia hatia
  • 8:12 - 8:14
    katika swali la la hadithi iliyo moja.
  • 8:15 - 8:18
    Miaka michache iliyopita,
    nilitembelea Mexico nikitokea Marekani.
  • 8:19 - 8:22
    Hali ya kisiasa nchini Marekani
    wakati huo ilikuwa tete,
  • 8:22 - 8:25
    kulikuwa na majadiliano yanayoendelea
    kuhusu uhamiaji.
  • 8:25 - 8:27
    Na, mara kwa mara hutokea Marekani,
  • 8:27 - 8:30
    neno uhamiaji likaja kuwa
    linahusishwa na watu wenye asili ya Mexico.
  • 8:31 - 8:33
    Kulikuwa na hadithi ndefu
    kuhusu Wamexico
  • 8:33 - 8:36
    kama watu wanaonyonya mfumo wa afya,
  • 8:36 - 8:38
    wanajipenyeza kwenye mipaka,
  • 8:38 - 8:40
    wanakamatwa kwenye mipaka,
    vitu kama hivyo.
  • 8:42 - 8:46
    Nakumbuka siku ya kwanza nilipokuwa natembea
    eneo liitwalo Guadalajara,
  • 8:46 - 8:48
    nikiwaangalia watu wakielekea makazini,
  • 8:48 - 8:50
    wakitengeneza tortilla maeneo ya sokoni,
  • 8:50 - 8:52
    wakivuta sigara, wakicheka.
  • 8:53 - 8:56
    Nakumbuka kwa mara ya kwanza
    nilipatwa na mshangao kidogo.
  • 8:56 - 8:59
    Kisha, nikagubikwa na aibu.
  • 8:59 - 9:04
    Nikatambua ya kwamba nimezama sana katika habari zinazoelezea watu wa Mexico
  • 9:04 - 9:06
    ambao wamekuwa jambo katika akili yangu,
  • 9:06 - 9:08
    wahamiaji duni,
  • 9:09 - 9:11
    nilidanganyika katika hadithi moja
    ya watu wa Mexico
  • 9:11 - 9:14
    na sikuweza kujisikia aibu zaidi.
  • 9:14 - 9:17
    Kwa hiyo hiyo ndiyo
    namna ya kutengeneza hadithi moja.
  • 9:17 - 9:19
    kuwaeleza watu kama jambo moja,
  • 9:19 - 9:21
    kama jambo moja tu,
  • 9:21 - 9:23
    tena na tena,
  • 9:23 - 9:25
    na hivyo ndivyo watakavyokuwa.
  • 9:26 - 9:28
    Haiwezekani kuongelea kuhusu hadithi moja
  • 9:28 - 9:30
    bila kuongelea kuhusu uwezo ya mamlaka.
  • 9:31 - 9:33
    Kuna neno, neno la lugha ya Igbo,
  • 9:33 - 9:37
    ambalo huwa naliwaza kila nikifikiria
    mfumo wa mamlaka wa dunia,
  • 9:37 - 9:38
    na hili "nkali".
  • 9:38 - 9:43
    Ni nomino ambayo inatafsiriwa kama
    "kuwa juu zaidi ya mwigine."
  • 9:44 - 9:46
    Kama ulivyo ulimwengu wa
    kiuchumi na kisiasa,
  • 9:47 - 9:51
    hadithi pia huelezwa kwa kanuni ya nkali:
  • 9:51 - 9:53
    Zinaelezwaje, nani anaelezea,
  • 9:53 - 9:56
    wakati gani zilielezwa,
    hadithi ngapi zinaelezwa,
  • 9:56 - 9:58
    haya yote yanategemea sana
    nguvu ya mamlaka.
  • 10:00 - 10:03
    Mamlaka ni uwezo sio tu wa kueleza
    hadithi ya kuhusu mtu mwingine,
  • 10:03 - 10:07
    lakini kuifanya iwe hadithi mahususi
    kuhusu mtu huyo.
  • 10:07 - 10:09
    Mshairi wa Kipalestina
    Mourid Barghouti aliandika
  • 10:09 - 10:12
    kwamba kama unataka kuwaondoa watu,
  • 10:12 - 10:15
    njia rahisi ya kufanya hivyo
    ni kuelezea hadithi yao
  • 10:15 - 10:17
    na kuanza na, "pili."
  • 10:18 - 10:22
    Anza hadithi na mishale
    ya waliokuwa wakazi halisi wa Amerika,
  • 10:22 - 10:25
    na sio baada ya kufika kwa Waingereza,
  • 10:25 - 10:28
    na utakuwa na hadithi tofauti nyingine kabisa.
  • 10:28 - 10:32
    Anza na hadithi kuhusu
    kuanguka kwa dola za Kiafrika,
  • 10:32 - 10:36
    na sio dola za Kiafrika
    zilizotokana na ukoloni,
  • 10:36 - 10:39
    na utakuwa na hadithi tofauti kabisa.
  • 10:40 - 10:42
    Hivi karibun nilitoa hotuba katika chuo
  • 10:42 - 10:46
    ambapo mwanafunzi aliniambia
    kwamba ilikuwa ni aibu
  • 10:46 - 10:49
    kwamba wanaume wa Kinigeria
    walikuwa wanyanyasaji
  • 10:49 - 10:51
    kama alivyo muhusika
    ambaye ni baba katika riwaya yangu.
  • 10:52 - 10:56
    Nikamwambia nimesoma riwaya
    iitwayo "Mwendawazimu wa Kiamerika" --
  • 10:56 - 10:58
    (Kicheko)
  • 10:58 - 11:00
    -- na kwamba ilikuwa aibu
  • 11:00 - 11:03
    kwamba vijana wadogo wa Kiamerika
    walikuwa wauaji waliokubuhu.
  • 11:03 - 11:07
    (Kicheko)
  • 11:07 - 11:13
    (Makofi)
  • 11:13 - 11:16
    Sasa, kiukweli nilisema hili
    kutokana na kukerwa.
  • 11:16 - 11:18
    (Kicheko)
  • 11:18 - 11:20
    Lakini isingeweza kutokea kwangu kuwaza
  • 11:20 - 11:24
    kwamba kwa sababu nimesoma riwaya
    ambayo muhusika ni muuaji wa kufululiza
  • 11:24 - 11:28
    kwamba kwa kiasi fulani
    wanawakilisha Wamarekani wote.
  • 11:28 - 11:31
    Hii si kwamba mimi
    ni mtu bora kuliko yule mwanafunzi,
  • 11:31 - 11:34
    lakini kwa sababu ya utamaduni
    na nguvu ya uchumi wa Marekani,
  • 11:34 - 11:36
    Nilikuwa nina hadithi nyingi za Marekani.
  • 11:36 - 11:40
    Nilisoma Tyler na Updike
    na Steinbeck na Gaitskill.
  • 11:40 - 11:43
    Sikuwa na hadithi moja ya Marekani.
  • 11:44 - 11:45
    Nilipojifunza, miaka kadhaa iliyopita,
  • 11:45 - 11:50
    kwamba waandishi wanategemewa kuwa na maisha ya utotoni ambayo siyo ya furaha
  • 11:50 - 11:52
    ili kuja kufanikiwa baadaye,
  • 11:52 - 11:56
    Nilianza kuwaza ni namna gani naweza buni
    vitu vibaya ambavyo wazazi wangu walinifanyia.
  • 11:56 - 11:58
    (Kicheko)
  • 11:58 - 12:02
    Lakini ukweli ni kwamba nilikuwa na maisha ya utoto ambayo yalikuwa ya furaha sana,
  • 12:02 - 12:05
    yaliyojaa vicheko na upendo,
    katika familia iliyo na ukaribu sana.
  • 12:05 - 12:08
    Lakini pia nilikuwa na mababu
    waliofia kwenye kambi za wakimbizi.
  • 12:09 - 12:13
    Binamu yangu Polle alifariki
    sababu hakupata matibabu yanayostahili.
  • 12:13 - 12:16
    Mmoja wa rafiki zangu,Okoloma,
    alifariki kwenye ajali ya ndege
  • 12:16 - 12:19
    kwa sababu gari zetu za zimamoto
    hazikuwa na maji.
  • 12:19 - 12:22
    Nimekulia katika serikali ya kijeshi
    ambayo ni kandamizi
  • 12:22 - 12:24
    ambayo haikujali elimu,
  • 12:24 - 12:27
    kwa muda mwingine,
    wazazi walikuwa hawalipwi mishahara.
  • 12:27 - 12:31
    Hivyo, kama mtoto, nilianza kuona jamu hakuna mezani wakati wa kupata kifungua kinywa,
  • 12:31 - 12:33
    kisha siagi nayo ikakosekana,
  • 12:34 - 12:36
    kisha mkate ukawa ghali sana,
  • 12:36 - 12:38
    kisha maziwa yakapungua.
  • 12:39 - 12:43
    Na katika yote, hali ya hofu ya kisiasa
  • 12:43 - 12:44
    ikaingilia maisha yetu,
  • 12:46 - 12:48
    Na hadithi zote hizi zimenitengeneza mimi wa leo.
  • 12:48 - 12:52
    Lakini kusisitiza katika hizi hadithi hasi
  • 12:52 - 12:55
    ni kuongeza uzoefu wangu
  • 12:55 - 12:59
    na kuachana na hadithi nyinginezo nyingi ambazo zimenitengeneza mimi.
  • 12:59 - 13:02
    Hadithi moja hutengeneza tabaka,
  • 13:02 - 13:07
    na tatizo la tabaka
    si kwamba hazina kweli,
  • 13:07 - 13:09
    lakini hazijakamilika.
  • 13:09 - 13:12
    Hufanya hadithi moja kuwa hadithi pekee.
  • 13:13 - 13:16
    Hakika, Afrika ni bara
    ambalo limejaa majanga:
  • 13:16 - 13:19
    Kuna majanga yaliyo makubwa,
    kama ubakaji wa kutisha nchini Congo
  • 13:19 - 13:21
    na wa kudidimiza,
  • 13:21 - 13:25
    kama ukweli kwamba watu 5000 wanaomba
    nafasi moja ya kazi nchini Nigeria.
  • 13:26 - 13:30
    Lakini kuna hadithi nyingine
    ambazo hazihusiani na majanga,
  • 13:30 - 13:33
    na ni muhimu sana, ni namna kuziongelea.
  • 13:33 - 13:35
    Wakati wote nimekuwa nikihisi haiwezekani
  • 13:35 - 13:38
    kujiunga kwa utaratibu na sehemu au mtu
  • 13:38 - 13:42
    bila kuhusiana na hadithi zote
    za mahala pale au mtu huyo.
  • 13:42 - 13:46
    Madhara ya hadithi moja ni kwamba:
  • 13:46 - 13:48
    Hunyang'anya watu wa heshima.
  • 13:48 - 13:52
    Hufanya utambuzi wetu
    wa usawa wa kibinadamu kuwa mgumu.
  • 13:52 - 13:56
    Husisitiza ni jinsi gani tulivyo tofauti
    kuliko vile tulivyo sawa.
  • 13:57 - 13:59
    Inakuwaje wakati
    kabla ya safari yangu ya Mexico,
  • 14:00 - 14:03
    Ningefatilia majadiliano ya uhamiaji
    kutoka pande zote,
  • 14:03 - 14:05
    upande wa Marekani na wa Mexico?
  • 14:05 - 14:09
    Ingekuwaje kama mama yangu angeniambia
    familia ya Fide ilikuwa masikini
  • 14:09 - 14:11
    na ya wachapakazi?
  • 14:11 - 14:13
    Inakuwaje kama tungekuwa
    na mtandao wa televisheni wa Kiafrika
  • 14:13 - 14:17
    ambao unarusha vipindi
    vya hadithi za Afrika duniani kote?
  • 14:17 - 14:21
    Kitu ambacho muandishi wa Kinigeria Chinua Achebe
    anaita "usawa wa hadithi."
  • 14:21 - 14:25
    Inakuweaje kama mwanafunzi niliyeishi naye chumba kimoja angefahamu kuhusu mchapishaji wangu wa Kinigeria,
  • 14:25 - 14:27
    Muhtar Bakare,
  • 14:27 - 14:29
    mtu wa kipekee ambaye
    aliacha kazi ya benki
  • 14:29 - 14:32
    na kufuata ndoto zake
    na kuanzisha nyumba ya uchapishaji
  • 14:32 - 14:36
    Sasa, hekima iliyozoeleka ilikuwa kwamba
    Wanigeria huwa hawasomi fasihi.
  • 14:36 - 14:37
    Yeye alikataa.
  • 14:37 - 14:40
    Alihisi kwamba watu
    ambao wanaweza kusoma, wangesoma,
  • 14:40 - 14:44
    kama ungefanya kazi ya fasihi iwe katika bei nafuu na kupatikana kiurahisi.
  • 14:45 - 14:47
    Muda mfupi baada ya kuchapisha
    riwaya yangu ya kwanza,
  • 14:47 - 14:50
    Nilikwenda kwenye kituo cha televisheni
    kilichopo Lagos kwa ajili ya mahojiano,
  • 14:50 - 14:53
    na mwanamke ambaye anafanya kazi pale kama karani alinifata na kusema,
  • 14:53 - 14:56
    "Nimependa sana riwaya yako.
    Sijapenda mwishoni mwake.
  • 14:56 - 14:59
    Sasa, ni lazima uandike muendelezo
    na hiki ndicho kitatokea ..."
  • 14:59 - 15:02
    (Kicheko)
  • 15:02 - 15:05
    Na alipoendelea kunielezea
    kipi cha kuandika kwenye muendelezo.
  • 15:06 - 15:08
    Si kwamba nilivutiwa tu,
    lakini pia nilisisimka.
  • 15:08 - 15:11
    Huyu ni mwanamke, mmoja wa watu wengi
    wa kawaida waliopo Nigeria,
  • 15:11 - 15:13
    ambao hawakutakiwa kuwa wasomaji.
  • 15:14 - 15:16
    Si kwamba alisoma tu kitabu,
  • 15:16 - 15:17
    lakini pia alikimiliki
  • 15:17 - 15:20
    na aliona ana haki kuaniambia
    kitu cha kuandika katika muendelezo.
  • 15:22 - 15:25
    Sasa, ingekuwaje kama mwanafunzi niishiye nae chumba kimoja angejua kuhusu rafiki yangu Funmi Lyanda,
  • 15:25 - 15:28
    mwanamke jasiri ambaye anaongoza
    kipindi cha televisheni Lagos,
  • 15:28 - 15:31
    na anadhamiria kuelezea hadithi
    ambazo tunapendelea kuzisahau?
  • 15:32 - 15:35
    Inakuwaje kama mwenzangu
    angetambua kuhusu upasuaji wa moyo
  • 15:35 - 15:38
    ambao ulifanyika wiki iliyopita
    jijini Lagos?
  • 15:38 - 15:42
    Inakuwaje angefahamu
    kuhusu muziki wa kisasa kwa Kinigeria,
  • 15:42 - 15:45
    watu wenye vipaji wanaoimba
    katika lugha za Kiingereza na pijini,
  • 15:45 - 15:47
    na Kiigbo na Kiyoruba na Kiijo,
  • 15:47 - 15:51
    wakichanganya ushawishi
    kutoka kwa Jay Z hadi kwa Fela
  • 15:51 - 15:53
    kwenda kwa Bob Marley na babu zao.
  • 15:54 - 15:56
    Inakuwaje kama angejua
    kuhusu wakili mwanamke
  • 15:56 - 16:00
    ambaye hivi karibuni alienda mahakamani nchini Nigeria kuipa changamoto sheria isiyo na maana
  • 16:00 - 16:03
    ambayo inawataka wanawake
    kupewa ruhusa na waume zao
  • 16:03 - 16:06
    kabla ya kutengeneza hati mpya ya kusafiria?
  • 16:06 - 16:09
    Inakuwaje kama angefahamu kuhusu Nollywood,
  • 16:09 - 16:13
    iliyojawa na watu wabunifu wanaotengeneza filamu ingawaje kuna changamoto nyingi za kiufundi,
  • 16:13 - 16:15
    filamu ambazo ni maarufu sana
  • 16:15 - 16:20
    ambazo ni mfano mzuri unaoonyesha Wanigeria wanatumia kile wanachotengeneza?
  • 16:20 - 16:23
    Inakuwaje kama angefahamu
    kuhusu msusi wangu bora kabisa,
  • 16:23 - 16:27
    ambaye ameanza biashara yake mwenyewe
    akiuza nywele za kuongezea?
  • 16:27 - 16:31
    Au kuhusu mamilioni ya Wanigeria wengine ambao huanza biashara na muda mwingine kuanguka,
  • 16:31 - 16:34
    lakini huendelea kukuza azma yao?
  • 16:35 - 16:37
    Muda wote nikiwa nyumbani hukutana
  • 16:37 - 16:40
    na vyanzo vya kila wakati vya kukwaza
    kwa Wanigeria wengi:
  • 16:40 - 16:43
    miundombinu yetu mibovu,
    serikali iliyoanguka,
  • 16:43 - 16:46
    lakini pia kwa ustahimilivu mkubwa
  • 16:46 - 16:49
    wa watu ambao hufanikiwa,
    bila ya kutegemea serikali,
  • 16:49 - 16:50
    bila yenyewe kabisa.
  • 16:51 - 16:54
    Huwa natoa mafunzo ya uandishi
    kila kipindi cha joto jijini Lagos,
  • 16:54 - 16:57
    na huwa inanishangaza
    kwa namna gani watu wengi hujiunga,
  • 16:57 - 17:00
    namna ambavyo watu wengi wana shauku ya kuandika,
  • 17:00 - 17:01
    ili kueleza hadithi.
  • 17:02 - 17:05
    Mimi na mchapishaji wa kitabu changu
    tumeanzisha taasisi isiyo ya kibiashara
  • 17:05 - 17:07
    inayofahamika kama Farafina Trust,
  • 17:07 - 17:10
    na tuna ndoto kubwa ya kujenga maktaba
  • 17:10 - 17:12
    na kukarabati maktaba ambazo tayari zipo
  • 17:12 - 17:15
    na kutoa vitabu kwa shule za majimboni
  • 17:15 - 17:17
    ambazo hazina vitabu katika maktaba zao,
  • 17:17 - 17:20
    na kuandaa mafunzo mengi mno,
  • 17:20 - 17:21
    katika kuandika na kusoma,
  • 17:21 - 17:24
    kwa watu wote ambao wana shauku
    ya kuelezea hadithi zetu nyingi.
  • 17:24 - 17:26
    Hadithi zina maana.
  • 17:26 - 17:28
    Hadithi nyingi zina maana.
  • 17:28 - 17:32
    Haidithi zimekuwa
    zikitumika kupokonya na kukejeli,
  • 17:32 - 17:36
    lakini hadithi zinaweza tumika
    kuhamasisha na kuleta ubinadamu.
  • 17:37 - 17:39
    Hadithi zinaweza kuvunja heshima ya watu,
  • 17:39 - 17:43
    lakini hadithi zinaweza
    kurudisha heshima iliyopotea.
  • 17:44 - 17:46
    Mwandishi wa Kimarekani
    Alice Walker aliandika
  • 17:46 - 17:50
    kuhusu ndugu zake wanaotokea Kusini
    ambao walihamia Kaskazini.
  • 17:50 - 17:52
    Aliwaonyesha kitabu kuhusu
  • 17:52 - 17:54
    maisha ya Kusini ambayo wameyaacha nyuma.
  • 17:56 - 17:59
    "Walikaa, na wakakisoma kitabu,
  • 17:59 - 18:05
    nisikilize mimi soma kitabu,
    na raha ya dunia utaipata tena."
  • 18:06 - 18:08
    Ningependelea kumalizia na hili wazo:
  • 18:08 - 18:11
    Kwamba pale tunapokataa hadithi moja,
  • 18:11 - 18:14
    tunapogundua kwamba hakuna hadithi moja
  • 18:14 - 18:16
    kuhusu sehemu yoyote,
  • 18:16 - 18:18
    huwa tunarejesha Furaha.
  • 18:19 - 18:20
    Asante.
  • 18:20 - 18:23
    (Makofi)
Title:
Chimamanda Adichie: Hatari ya simulizi moja
Speaker:
Chimamanda Ngozi Adichie
Description:

Maisha yetu, tamaduni zetu, vimeumbwa na hadithi nyingi zinazoingiliana. Mwandishi wa riwaya Chimamanda Adichie anatoa simulizi ya jinsi alivyogundua sauti yake halisi kiutamaduni -- na anatahadharisha kwamba kama tukisikia hadithi moja juu ya mtu mwingine ama nchi nyingine, tupo hatarini kuelewa visivyo.

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDTalks
Duration:
18:29
Nelson Simfukwe approved Swahili subtitles for The danger of a single story
Nelson Simfukwe accepted Swahili subtitles for The danger of a single story
Miriam Loivotoki Elisha edited Swahili subtitles for The danger of a single story
Miriam Loivotoki Elisha edited Swahili subtitles for The danger of a single story
Miriam Loivotoki Elisha edited Swahili subtitles for The danger of a single story
Miriam Loivotoki Elisha edited Swahili subtitles for The danger of a single story
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for The danger of a single story
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for The danger of a single story
Show all

Swahili subtitles

Revisions