Fursa zilizofichwa katika sekta isiyo rasmi
-
0:01 - 0:05Masoko ya Afrika yasiyo rasmi huwekewa kasumba kwa kuonekana
-
0:05 - 0:07vile yana kasheshe na goigoi.
-
0:07 - 0:10Ubaya wa kusikia neno "yasiyo rasmi"
-
0:10 - 0:13hutokana na jumuiya inayojiendesha ya misaada tuliyonayo,
-
0:13 - 0:14ambayo ina mitazamo hasi sana,
-
0:14 - 0:19na ilikuwa na madhara makubwa katika kuanguka kwa uchumi,
-
0:19 - 0:24kuongeza kirahisi -- au kupunguza -- asilimia 40 hadi 60 ya ukomo wa faida
-
0:24 - 0:27kwa masoko yasiyo rasmi pekee.
-
0:27 - 0:31Ikiwa moja ya jukumu la kuweka ramani ya mzunguko wa biashara zisizo rasmi,
-
0:31 - 0:34tumetengeneza machapisho kwa kina
-
0:34 - 0:39ya ripoti zote na tafiti kwenye biashara za mipakani katika ukanda wa Afrika Mashariki,
-
0:39 - 0:41tukirudi nyuma hadi miaka 20.
-
0:41 - 0:45Hii ilikuwa ni kwa ajili ya kutuandaa kwa ajili ya kazi ya kwenda kutathmini tatizo ni nini,
-
0:45 - 0:49kipi kilichokuwa kinarudisha nyuma biashara isiyo rasmi katika sekta isiyo rasmi.
-
0:50 - 0:53Tulichogundua katika miaka 20 iliyopita ni kwamba,
-
0:54 - 0:57hakuna aliyeweza kutofautisha kati ya magendo --
-
0:57 - 1:02ambayo ni sawa na upenyeshaji mali isiyo halali au iliyopigwa marufuku katika sekta isiyo rasmi --
-
1:02 - 1:04na mali halali ambayo haikuwekwa katika kumbukumbu
-
1:04 - 1:07kama nyanya, machungwa, matunda.
-
1:08 - 1:10Uhalifu huu --
-
1:10 - 1:15ambao kwa kiswahili unafahamika kama "biashara," ambao ni biashara,
-
1:15 - 1:19ukilinganisha na "magendo", ambayo upenyeshaji bidhaa usio halali --
-
1:19 - 1:22uhalifu katika sekta isiyo rasmi,
-
1:22 - 1:26kwa Kiingereza, bila kutofautisha nyanja hizi,
-
1:26 - 1:32kwa urahisi inaweza kugharimu kila uchumi wa Afrika kati ya asilimia 60 hadi 80 ukiongezea
-
1:32 - 1:35katika ukuaji wa pato la taifa kwa mwaka,
-
1:35 - 1:38kwa sababu hatujambua injini
-
1:38 - 1:41inayofanya uchumi kuendelea.
-
1:41 - 1:44Sekta isiyo rasmi inaongeza ajira mara nne katika kiasi
-
1:44 - 1:46cha uchumi ulio rasmi,
-
1:46 - 1:49au uchumi wa "kisasa", kama wengi wauitavyo.
-
1:49 - 1:52Hutoa nafasi za ajira na kuweza kujipatia kipato
-
1:52 - 1:56kwa wale wengi ambao hawana "ujuzi wa darasani" katika nyanja mbalimbali za taaluma.
-
1:56 - 2:00Lakini, je unaweza kutengeneza mashine ya kukaanga chipsi kutokana na gari bovu?
-
2:00 - 2:04Kwa hiyo, hili, mabibi na mabwana,
-
2:04 - 2:07ni jambo ambalo linatakiwa kutambuliwa kwa shauku kubwa.
-
2:07 - 2:11Ambapo mtazamo wa sasa uliopo kuhusu sekta hii ni uhalifu,
-
2:11 - 2:13hiki ni kivuli,
-
2:13 - 2:14hii si halali,
-
2:14 - 2:19hakutakiwa na madhumuni ya kuunganisha mzunguko wa uchumi usio rasmi
-
2:19 - 2:22na ule ulio rasmi au hata ule wa kiulimwengu.
-
2:23 - 2:26Nitawaeleza hadithi inayomuhusu Teresia,
-
2:26 - 2:30mfanyabiashara ambaye anapindua mitazamo yetu yote,
-
2:30 - 2:33anatufanya kuhoji kasumba zetu zote tulizokuwa nazo,
-
2:33 - 2:36ukihusisha na ripoti ya miaka 20 nyuma.
-
2:38 - 2:43Teresia anauza nguo chini ya mti katika mji unaoitwa Malaba,
-
2:43 - 2:45katika mpaka wa Uganda na Kenya.
-
2:46 - 2:48Unadhani ni rahisi sana, au sivyo?
-
2:49 - 2:51Tutakwenda ning'iniza nguo mpya kwenye matawi,
-
2:51 - 2:54tutatandika turubai, kisha kuketi chini, kusubiri wateja,
-
2:54 - 2:56na hivyo ndivyo inakuwa.
-
2:56 - 2:59Alikuwa ni mtu ambaye tuliona anarandana na yale yaliyomo katika ripoti,
-
2:59 - 3:00katika tafiti,
-
3:01 - 3:04alikuwa ni mama mjane anayefanya biashara,
-
3:04 - 3:06akilea watoto wake.
-
3:07 - 3:10Ni kipi kilibadili udhanifu wetu?
-
3:10 - 3:11Kipi kilitushangaza?
-
3:11 - 3:15Kwanza, Teresia analipia kodi ya serikali ya soko la mkoa
-
3:15 - 3:17kila siku anayofanya biashara
-
3:17 - 3:20kutokana na kuweka biashara chini ya mti wake.
-
3:20 - 3:22Amekuwa akifanya hivi kwa miaka saba,
-
3:22 - 3:24na amekuwa akipewa risiti.
-
3:25 - 3:26Anatunza kumbumkumbu.
-
3:26 - 3:29Tunamuona asiye hafifu,
-
3:29 - 3:31masikini,
-
3:31 - 3:36mwanamke asiye na uwezo anayefanya biashara pembezoni mwa barabara -- hapana.
-
3:36 - 3:41Tunamuona mfanyabiashara ambaye anatunza kumbukumbu za mauzo kwa miaka;
-
3:41 - 3:47mtu ambaye amekuwa na mzunguko wote wa biashara za rejareja zitokazo Uganda
-
3:47 - 3:49hadi orodha ya uchukuaji;
-
3:49 - 3:53aliye na mkokoteni unaoleta bidhaa,
-
3:53 - 3:56au wakala wa mfumo wa fedha wa simu anayekuja kuchukua pesa taslimu
-
3:56 - 3:58kila mwisho wa jioni.
-
3:58 - 4:02Unaweza kisia ni kiasi gani Teresia hutumia, kwa wastani,
-
4:02 - 4:05kila mwezi katika uorodheshaji bidhaa --
-
4:05 - 4:07shehena ya nguo mpya ambazo anapata kutoka Nairobi?
-
4:08 - 4:10Dola za Kimarekani elfu moja na mia tano.
-
4:11 - 4:16Ambayo ni takribani dola za Kimarekani 20,000 zilizowekezwa kwenye katika bidhaa za biashara na huduma
-
4:16 - 4:18kila mwaka.
-
4:18 - 4:19Huyu ni Teresia,
-
4:19 - 4:20asiyeonekana,
-
4:20 - 4:22aliyefichwa katikati.
-
4:22 - 4:27Na huyu ni mtu wa ngazi ya kwanza ya wajasiriamali wadogo,
-
4:27 - 4:31biashara ndogo ndogo zinazopatikana katika masoko ya ya miji hii.
-
4:31 - 4:36Angalau katika mpaka mkubwa wa Malaba, yupo katika ngazi ya kwanza.
-
4:37 - 4:39Watu wa mbele zaidi wanathamini mlolongo huu
-
4:39 - 4:42na kwa rahisi wanafanya biashara tatu,
-
4:42 - 4:47wakiwekeza dola za Kimarekani kati ya 2500 hadi 3000 kila mwezi.
-
4:48 - 4:52Kwa hiyo tatizo lilikuja gundulika kwamba halikuwa uhalifu;
-
4:52 - 4:56huwezi kumtuhumu mtu ambaye unamtoza na kumpa risiti.
-
4:57 - 5:02Ni ukosefu wa kutambua ujuzi wa kazi zao.
-
5:03 - 5:07Mifumo ya kibenki haina njia ya kuwatambua
-
5:07 - 5:09kama wafanyabiashara ndogo ndogo.
-
5:09 - 5:11pasipo kukataa ukweli, unajua,
-
5:11 - 5:13mti wake hauna anuani.
-
5:14 - 5:16Kwa hiyo amebanwa katikati.
-
5:16 - 5:19Anaangukia katika mpasuko wa dhana zetu.
-
5:19 - 5:22Unaijua ile mikopo midogo midogo ya kusaidia wanawake wa Kiafrika ambao ni wafanyabiashara?
-
5:23 - 5:25Watampa mkopo wa dola za Kimarekani 50 au 100.
-
5:26 - 5:27Atafanyia nini kiasi hiki?
-
5:27 - 5:29Anatumia mara 10 ya kiasi hicho kila mwezi
-
5:29 - 5:31katika uorodheshaji tu.
-
5:31 - 5:33hatuongelei huduma nyingine za ziada
-
5:33 - 5:35au mzunguko wote.
-
5:36 - 5:39Hawa ni wale ambao hawastahili kuwepo katika kasumba ya sera
-
5:39 - 5:42ya walio na ujuzi mdogo au wale duni,
-
5:42 - 5:45wala si mwajiriwa, ofisa anayelipwa mshahara
-
5:45 - 5:47au mtumishi aliye na pensheni
-
5:47 - 5:50ambapo ndipo watu wa kipato cha kati walipo.
-
5:50 - 5:55Badala yake, tulichonacho hapa ni mifano ya viwanda vidogo na vya kati
-
5:55 - 5:58hizi ni mbegu zilizo na rutuba za biashara na viwanda
-
5:58 - 6:00ambazo zinafanya injini iendelee kutembea.
-
6:00 - 6:02Vinaleta chakula mezani.
-
6:02 - 6:05Hata hapa katika hotel hii, wasioonekana --
-
6:05 - 6:09wachinjaji nyama, watengeneza mikate na watengeneza mishumaa --
-
6:09 - 6:11wanatengeneza mashine ambazo zinatengeneza chipsi
-
6:11 - 6:12na wanatengeneza vitanda vyako,
-
6:12 - 6:16Hawa ni wanawake ambao hawaonekani wanaofanya biashara mipakani,
-
6:17 - 6:19pembezoni mwa barabara,
-
6:19 - 6:22hawaonekani kwa watu wanaokusanya taarifa.
-
6:23 - 6:26Na wanawekwa pamoja katika sekta kubwa isiyo rasmi
-
6:26 - 6:31ambayo haihangaiki kutofautisha watu wanaopenyesha bidhaa na wakwepa kodi
-
6:31 - 6:34na wale wanaofanya biashara za magendo,
-
6:34 - 6:36na wanawake wanaofanya bashara,
-
6:36 - 6:40na wale wanaoleta chakula mezani na kuwasomesha watoto zao hadi chuo kikuu
-
6:40 - 6:44Kwa hiyo hili ndilo ninalouliza hapa.
-
6:44 - 6:46Hayo ndiyo tunatakiwa kuanza kufanya.
-
6:47 - 6:51Je tunaweza kuanza kwa kutambua ujuzi, kazi?
-
6:52 - 6:56Tunaweza kubadili uchumi wa sekta isiyo rasmi kwa kuanza na utambuzi huu
-
6:56 - 7:01na kisha kutengeneza milango ya wao kupita
-
7:01 - 7:03na kushirikiana na sekta iliyo rasmi,
-
7:03 - 7:04na ulimwengu,
-
7:04 - 7:06na mfumo mzima.
-
7:06 - 7:08Asante, mabibi na mabwana.
-
7:08 - 7:11(Makofi)
- Title:
- Fursa zilizofichwa katika sekta isiyo rasmi
- Speaker:
- Niti Bhan
- Description:
-
Niti Bhan anatafiti mikakati ya kibiashara kwa soko lisilo rasmi la Afrika: maduka madogo, wabunifu walio na ujuzi na wafanya kazi ambao ni injini isiyoonekana ambayo inafanya uchumi wa bara kusonga mbele. Inashawishi kuwaza kwamba wafanya kazi hawa ni wakwepa kodi, wahalifu -- lakini anaelezea suala hili kwamba kipande hiki ambacho kinakuza uchumi ni halali kinafaa kuwekeza. Kama tutafanya, anasema, tutatengeneza maelfu ya ajira. "Hizi ni mbegu zenye rutuba za biashara na viwanda," Bhan anasema. "Je, tunaweza kuanza kwa kutambua ujuzi huu na kazi?"
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 07:26
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for The hidden opportunity of informal markets | ||
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for The hidden opportunity of informal markets | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for The hidden opportunity of informal markets | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for The hidden opportunity of informal markets | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for The hidden opportunity of informal markets | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for The hidden opportunity of informal markets | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for The hidden opportunity of informal markets |