Swahili subtitles

← Fursa zilizofichwa katika sekta isiyo rasmi

Get Embed Code
24 Languages

Showing Revision 5 created 01/08/2018 by Joachim Mangilima.

 1. Masoko ya Afrika yasiyo rasmi huwekewa kasumba kwa kuonekana
 2. vile yana kasheshe na goigoi.
 3. Ubaya wa kusikia neno "yasiyo rasmi"
 4. hutokana na jumuiya inayojiendesha ya misaada tuliyonayo,
 5. ambayo ina mitazamo hasi sana,
 6. na ilikuwa na madhara makubwa katika kuanguka kwa uchumi,
 7. kuongeza kirahisi -- au kupunguza -- asilimia 40 hadi 60 ya ukomo wa faida
 8. kwa masoko yasiyo rasmi pekee.
 9. Ikiwa moja ya jukumu la kuweka ramani ya mzunguko wa biashara zisizo rasmi,
 10. tumetengeneza machapisho kwa kina
 11. ya ripoti zote na tafiti kwenye biashara za mipakani katika ukanda wa Afrika Mashariki,
 12. tukirudi nyuma hadi miaka 20.
 13. Hii ilikuwa ni kwa ajili ya kutuandaa kwa ajili ya kazi ya kwenda kutathmini tatizo ni nini,
 14. kipi kilichokuwa kinarudisha nyuma biashara isiyo rasmi katika sekta isiyo rasmi.
 15. Tulichogundua katika miaka 20 iliyopita ni kwamba,

 16. hakuna aliyeweza kutofautisha kati ya magendo --
 17. ambayo ni sawa na upenyeshaji mali isiyo halali au iliyopigwa marufuku katika sekta isiyo rasmi --
 18. na mali halali ambayo haikuwekwa katika kumbukumbu
 19. kama nyanya, machungwa, matunda.
 20. Uhalifu huu --
 21. ambao kwa kiswahili unafahamika kama "biashara," ambao ni biashara,
 22. ukilinganisha na "magendo", ambayo upenyeshaji bidhaa usio halali --
 23. uhalifu katika sekta isiyo rasmi,
 24. kwa Kiingereza, bila kutofautisha nyanja hizi,
 25. kwa urahisi inaweza kugharimu kila uchumi wa Afrika kati ya asilimia 60 hadi 80 ukiongezea
 26. katika ukuaji wa pato la taifa kwa mwaka,
 27. kwa sababu hatujambua injini
 28. inayofanya uchumi kuendelea.
 29. Sekta isiyo rasmi inaongeza ajira mara nne katika kiasi

 30. cha uchumi ulio rasmi,
 31. au uchumi wa "kisasa", kama wengi wauitavyo.
 32. Hutoa nafasi za ajira na kuweza kujipatia kipato
 33. kwa wale wengi ambao hawana "ujuzi wa darasani" katika nyanja mbalimbali za taaluma.
 34. Lakini, je unaweza kutengeneza mashine ya kukaanga chipsi kutokana na gari bovu?
 35. Kwa hiyo, hili, mabibi na mabwana,

 36. ni jambo ambalo linatakiwa kutambuliwa kwa shauku kubwa.
 37. Ambapo mtazamo wa sasa uliopo kuhusu sekta hii ni uhalifu,
 38. hiki ni kivuli,
 39. hii si halali,
 40. hakutakiwa na madhumuni ya kuunganisha mzunguko wa uchumi usio rasmi
 41. na ule ulio rasmi au hata ule wa kiulimwengu.
 42. Nitawaeleza hadithi inayomuhusu Teresia,

 43. mfanyabiashara ambaye anapindua mitazamo yetu yote,
 44. anatufanya kuhoji kasumba zetu zote tulizokuwa nazo,
 45. ukihusisha na ripoti ya miaka 20 nyuma.
 46. Teresia anauza nguo chini ya mti katika mji unaoitwa Malaba,
 47. katika mpaka wa Uganda na Kenya.
 48. Unadhani ni rahisi sana, au sivyo?
 49. Tutakwenda ning'iniza nguo mpya kwenye matawi,
 50. tutatandika turubai, kisha kuketi chini, kusubiri wateja,
 51. na hivyo ndivyo inakuwa.
 52. Alikuwa ni mtu ambaye tuliona anarandana na yale yaliyomo katika ripoti,
 53. katika tafiti,
 54. alikuwa ni mama mjane anayefanya biashara,
 55. akilea watoto wake.
 56. Ni kipi kilibadili udhanifu wetu?

 57. Kipi kilitushangaza?
 58. Kwanza, Teresia analipia kodi ya serikali ya soko la mkoa
 59. kila siku anayofanya biashara
 60. kutokana na kuweka biashara chini ya mti wake.
 61. Amekuwa akifanya hivi kwa miaka saba,
 62. na amekuwa akipewa risiti.
 63. Anatunza kumbumkumbu.
 64. Tunamuona asiye hafifu,
 65. masikini,
 66. mwanamke asiye na uwezo anayefanya biashara pembezoni mwa barabara -- hapana.
 67. Tunamuona mfanyabiashara ambaye anatunza kumbukumbu za mauzo kwa miaka;
 68. mtu ambaye amekuwa na mzunguko wote wa biashara za rejareja zitokazo Uganda
 69. hadi orodha ya uchukuaji;
 70. aliye na mkokoteni unaoleta bidhaa,
 71. au wakala wa mfumo wa fedha wa simu anayekuja kuchukua pesa taslimu
 72. kila mwisho wa jioni.
 73. Unaweza kisia ni kiasi gani Teresia hutumia, kwa wastani,
 74. kila mwezi katika uorodheshaji bidhaa --
 75. shehena ya nguo mpya ambazo anapata kutoka Nairobi?
 76. Dola za Kimarekani elfu moja na mia tano.
 77. Ambayo ni takribani dola za Kimarekani 20,000 zilizowekezwa kwenye katika bidhaa za biashara na huduma
 78. kila mwaka.
 79. Huyu ni Teresia,
 80. asiyeonekana,
 81. aliyefichwa katikati.
 82. Na huyu ni mtu wa ngazi ya kwanza ya wajasiriamali wadogo,

 83. biashara ndogo ndogo zinazopatikana katika masoko ya ya miji hii.
 84. Angalau katika mpaka mkubwa wa Malaba, yupo katika ngazi ya kwanza.
 85. Watu wa mbele zaidi wanathamini mlolongo huu
 86. na kwa rahisi wanafanya biashara tatu,
 87. wakiwekeza dola za Kimarekani kati ya 2500 hadi 3000 kila mwezi.
 88. Kwa hiyo tatizo lilikuja gundulika kwamba halikuwa uhalifu;
 89. huwezi kumtuhumu mtu ambaye unamtoza na kumpa risiti.
 90. Ni ukosefu wa kutambua ujuzi wa kazi zao.
 91. Mifumo ya kibenki haina njia ya kuwatambua
 92. kama wafanyabiashara ndogo ndogo.
 93. pasipo kukataa ukweli, unajua,
 94. mti wake hauna anuani.
 95. Kwa hiyo amebanwa katikati.

 96. Anaangukia katika mpasuko wa dhana zetu.
 97. Unaijua ile mikopo midogo midogo ya kusaidia wanawake wa Kiafrika ambao ni wafanyabiashara?
 98. Watampa mkopo wa dola za Kimarekani 50 au 100.
 99. Atafanyia nini kiasi hiki?
 100. Anatumia mara 10 ya kiasi hicho kila mwezi
 101. katika uorodheshaji tu.
 102. hatuongelei huduma nyingine za ziada
 103. au mzunguko wote.
 104. Hawa ni wale ambao hawastahili kuwepo katika kasumba ya sera
 105. ya walio na ujuzi mdogo au wale duni,
 106. wala si mwajiriwa, ofisa anayelipwa mshahara
 107. au mtumishi aliye na pensheni
 108. ambapo ndipo watu wa kipato cha kati walipo.
 109. Badala yake, tulichonacho hapa ni mifano ya viwanda vidogo na vya kati

 110. hizi ni mbegu zilizo na rutuba za biashara na viwanda
 111. ambazo zinafanya injini iendelee kutembea.
 112. Vinaleta chakula mezani.
 113. Hata hapa katika hotel hii, wasioonekana --
 114. wachinjaji nyama, watengeneza mikate na watengeneza mishumaa --
 115. wanatengeneza mashine ambazo zinatengeneza chipsi
 116. na wanatengeneza vitanda vyako,
 117. Hawa ni wanawake ambao hawaonekani wanaofanya biashara mipakani,
 118. pembezoni mwa barabara,
 119. hawaonekani kwa watu wanaokusanya taarifa.
 120. Na wanawekwa pamoja katika sekta kubwa isiyo rasmi
 121. ambayo haihangaiki kutofautisha watu wanaopenyesha bidhaa na wakwepa kodi
 122. na wale wanaofanya biashara za magendo,
 123. na wanawake wanaofanya bashara,
 124. na wale wanaoleta chakula mezani na kuwasomesha watoto zao hadi chuo kikuu
 125. Kwa hiyo hili ndilo ninalouliza hapa.

 126. Hayo ndiyo tunatakiwa kuanza kufanya.
 127. Je tunaweza kuanza kwa kutambua ujuzi, kazi?
 128. Tunaweza kubadili uchumi wa sekta isiyo rasmi kwa kuanza na utambuzi huu
 129. na kisha kutengeneza milango ya wao kupita
 130. na kushirikiana na sekta iliyo rasmi,
 131. na ulimwengu,
 132. na mfumo mzima.
 133. Asante, mabibi na mabwana.

 134. (Makofi)