Je, wewe ni mtoaji au mpokeaji?
-
0:01 - 0:03Kila mtu achukue dakika kuangalia watu humu ndani,
-
0:03 - 0:06jaribu kumtafuta mwenye wasiwasi kuliko wote
-
0:06 - 0:07(Vicheko)
-
0:07 - 0:09Sasa nionyeshe huyo mtu kwa kidole
-
0:09 - 0:10(Vicheko)
-
0:10 - 0:12Acha, natania, usinioneshe
-
0:12 - 0:13(Vicheko)
-
0:13 - 0:15Kama mwanasaikolojia,
-
0:15 - 0:17Nimetumia muda mwingi katika mahali pa kazi,
-
0:17 - 0:19na ninaiona hio paranoia kila mahali.
-
0:19 - 0:22Paranoia inasababishwa na watu nawaita "wapokeaji."
-
0:22 - 0:24Wapokeaji ni wabinafsi katika mahusiano.
-
0:24 - 0:27Wanajali sana: utawahudumiaje wao.
-
0:27 - 0:28Kinyume chao ni "watoaji"
-
0:28 - 0:31Hawa ni watu ambao katika mahusiano yao, huuliza,
-
0:31 - 0:33"Ni namna ipi naweza kukuhudumia?"
-
0:33 - 0:36Ntawapa nafasi ya kutafakari tabia zenu.
-
0:36 - 0:38Sote tumekuwa watoaji na wapokeaji katika nyakati mbalimbali.
-
0:38 - 0:41Tabia yako ni namna unavyohusiana na watu mara nyingi,
-
0:41 - 0:42bila ya kujifikiria
-
0:42 - 0:44Nina jaribio fupi la kuwasaidia
-
0:44 - 0:46kutambua kama wewe ni mtoaji au mpokeaji;
-
0:46 - 0:48na mnaweza kulifanya sasa hivi.
-
0:48 - 0:49[Tambua kama unajihusudu)
-
0:49 - 0:52[Hatua ya 1: Chukua muda kujifikiria.]
-
0:52 - 0:53(Vicheko)
-
0:53 - 0:54[Hatua ya 2: Kama umeshaifikia hatua ya pili, haujihusudu.]
-
0:56 - 0:58(Vicheko)
-
0:58 - 1:02Hilo pekee nitasema leo bila ya data za kuthibitisha.
-
1:02 - 1:05Ninaamani kama imekuchukua muda kuicheka hii katuni
-
1:05 - 1:08tuwe na shaka kwamba wewe ni mpokeaji
-
1:08 - 1:09(Vicheko)
-
1:09 - 1:11Hakika wapokeaji wote sio wabinafsi
-
1:11 - 1:14Baadhi ni watoaji waliotumika sana na kuchoka.
-
1:14 - 1:17Pia kuna wapokeaji ambao hatutaongelea leo,
-
1:17 - 1:19wale wagonjwa wa akili.
-
1:19 - 1:20(Vicheko)
-
1:20 - 1:23Nilitaka kuthibitisha uhalali wa pande hizi mbili,
-
1:23 - 1:26hivyo nikatafiti zaidi ya watu 30,000 kwenye sekta
-
1:26 - 1:28na tamaduni mbalimbali.
-
1:28 - 1:30Nikakuta kwamba wengi
wako katikati - -
1:30 - 1:32kati ya kutoa na kupokea.
-
1:32 - 1:34Hawa huchagua mtindo wa tatu "kulipiza."
-
1:34 - 1:37Walipizaji huweka
usawa kati kutoa na kupokea: -
1:37 - 1:41nipe nikupe --nitakusaidia ukinisaidia.
-
1:41 - 1:43Inaonekana kama namna salama ya kuishi.
-
1:43 - 1:46Ila, je, ni njia fanisi ya kuishi?
-
1:46 - 1:49Jibu la hakika kwa swali hilo, ni
-
1:49 - 1:50labda.
-
1:50 - 1:51(Vicheko)
-
1:51 - 1:53Nimechunguza mashirika kadhaa,
-
1:53 - 1:55maelfu ya watu.
-
1:55 - 1:58Nmepima tija miongoni wahandisi.
-
1:58 - 2:01(Vicheko)
-
2:01 - 2:04Nimeangalia maksi ya wanafunzi wa udaktari
-
2:04 - 2:06na hata mapato ya watu wa mauzo
-
2:06 - 2:07(Vicheko)
-
2:07 - 2:09Cha kushtua, ni
-
2:09 - 2:12watoaji wanafanya vibaya kuliko wote, katika kila fani.
-
2:13 - 2:15Wahandisi wanaofanya vibaya kazini
-
2:15 - 2:17ndio wanaotoa fadhila kuliko wanapokea.
-
2:17 - 2:19Wako makini kufanya kazi za watu wengine,
-
2:20 - 2:23hata hawana muda au nguvu ya
kufanya kazi zao. -
2:23 - 2:26Katika udaktari, maksi za chini ni za
-
2:26 - 2:28wanafunzi wanaokubaliana na kauli kama,
-
2:28 - 2:30"Ninapenda kuwasaidia wengine,"
-
2:31 - 2:33ambacho inapendekeza umuamini zaidi daktari
-
2:33 - 2:36ambaye hana lengo la kusaidia mtu yeyote.
-
2:36 - 2:37(Vicheko)
-
2:37 - 2:40Katika mauzo, mapato ya chini yanaokeana
-
2:40 - 2:42miongoni mwa wauzaji wakarimu.
-
2:42 - 2:44Niliongea na mmoja kati ya
-
2:44 - 2:46wauzaji ambao ni watoaji.
-
2:46 - 2:48Nikamuuliza, "Kwa nini
unafanya vibaya hivyo --" -
2:48 - 2:50Sikuuliza namna hiyo, lakini -
-
2:50 - 2:51(Vicheko)
-
2:51 - 2:53"Nini gharama ya ukarimu katika mauzo?"
-
2:53 - 2:57Akasema, "Naam, ninawajali wateja wangu
-
2:57 - 2:59kwamba kamwe siwezi kuwauzia bidhaa zetu ovyo. "
-
2:59 - 3:01(Vicheko)
-
3:01 - 3:02Hivyo, kwa faida yangu,
-
3:02 - 3:03wangapi mnajitambua zaidi kama watoaji
-
3:03 - 3:05kuliko wapokeaji au wanaolipizaji?
-
3:05 - 3:06Inua mkono.
-
3:07 - 3:10OK, ingekuwa zaidi kabla kuongelea hizi takwimu.
-
3:11 - 3:14Lakini, kuna cha kushangaza
zaidi hapa, -
3:14 - 3:17kwa sababu watoaji mara nyingi
hujitoa wenyewe, -
3:17 - 3:20huyaboresha mashirika yao zaidi.
-
3:20 - 3:23Tuna ushahidi mwingi --
-
3:23 - 3:27tafiti nyingi kuhusu tabia za watoaji
-
3:27 - 3:29katika timu au shirika --
-
3:29 - 3:32na zaidi watu wanavyosaidiana, kufundisha
-
3:32 - 3:33wengine na kushauriana,
-
3:33 - 3:36ndivyo huboresha mashirika katika kila kipimo:
-
3:36 - 3:39faida, kuridhisha wateja, kuvutia
wafanyakazi - -
3:39 - 3:41hata hupunguza gharama za uendeshaji.
-
3:41 - 3:42Hivyo watoaji hutumia muda mwingi
-
3:42 - 3:44kusaidia wengine
-
3:44 - 3:46na kuboresha timu,
-
3:46 - 3:48kwa bahati mbaya, wanajikuta kwenye hasara.
-
3:48 - 3:50Nataka kuzungumzia namna ya
-
3:50 - 3:53kujenga utamaduni ambapo watoaji wanafanikiwa.
-
3:54 - 3:57Hivyo nilijiuliza kama watoaji sio
watekelezaji bora, -
3:57 - 3:58wapi ni watekelezaji bora?
-
3:59 - 4:02Nitanza na habari njema:
siyo wapokeaji. -
4:02 - 4:03Wapokeaji hupanda haraka
-
4:03 - 4:06lakini pia huanguka upesi maofisini.
-
4:06 - 4:08Na huanguka katika mikono ya walipizaji.
-
4:08 - 4:09Kama mlipizaji,
-
4:09 - 4:11unafuata sheria ya "jicho kwa jicho" - ndiyo haki.
-
4:11 - 4:13Hivyo unapokutana na mpokeaji,
-
4:13 - 4:15unalifanya jukumu lako
-
4:15 - 4:17kumuadhibu mpokeaji, kumtia adabu.
-
4:17 - 4:18(Vicheko)
-
4:18 - 4:19Na hivyo haki hutolewa.
-
4:20 - 4:22Naam, watu wengi ni walipizaji.
-
4:22 - 4:24Ina maana, kama wewe ni mpokeaji,
-
4:24 - 4:26hatimaye, balaa hukupata;
-
4:26 - 4:27Kwendako mema, hurudi mema.
-
4:27 - 4:29Hivyo hitimisho lenye mantiki ni:
-
4:29 - 4:32walipizaji ndio wafanyakazi bora.
-
4:32 - 4:33Lakini, hapana, siyo.
-
4:33 - 4:36Katika kila fani, kila shirika, nimechunguza,
-
4:36 - 4:38watoaji, tena, ndio wenye matokeo bora.
-
4:40 - 4:43Tuangalie baadhi ya takwimu nimekusanya, za mapato
-
4:43 - 4:44ya watu wa mauzo.
-
4:44 - 4:47Unachoona ni kwamba watoaji wako katika vikomo vyote.
-
4:47 - 4:50Wengi wao huleta mapato ya chini,
-
4:50 - 4:51lakini pia mapato ya juu.
-
4:51 - 4:54Mwelekeo huo ni kweli pia kwenye tija za wahandisi
-
4:54 - 4:55na maksi za wanafunzi wa udaktari.
-
4:55 - 4:58Watoaji wana uwakilishi mkubwa
chini na juu -
4:58 - 5:00katika kila kipimo cha mafanikio.
-
5:00 - 5:02Hivyo swali ni:
-
5:02 - 5:05Jinsi gani tunaweza kujenga dunia
ambapo watoaji hufanikiwa? -
5:05 - 5:08Nitazungumzi jinsi ya kufanya hivyo, sio tu katika biashara,
-
5:08 - 5:10ila katika taasisi mbalimbali
-
5:10 - 5:11na hata serikalini.
-
5:11 - 5:12Mko tiyari?
-
5:12 - 5:13(Makofi)
-
5:13 - 5:16Ningewaambia hata hivyo, ila asante kwa shauku.
-
5:16 - 5:17(Vicheko)
-
5:17 - 5:19Kitu cha kwanza muhimu
-
5:19 - 5:22ni kutambua kwamba watoaji ni watu muhimu,
-
5:22 - 5:25ila tusipoangalia, tutawakatisha tamaa.
-
5:25 - 5:27Hivyo, tunabidi kuwalinda watoaji miongoni mwetu
-
5:27 - 5:31Nimejifunza mengi kutoka kwa mwanamitandao bora wa Fortune.
-
5:33 - 5:34Ni huyo mtu, sio paka
-
5:34 - 5:36(Vicheko)
-
5:36 - 5:37Anaitwa Adamu Rifkin.
-
5:37 - 5:40Yeye ni mwekezaji mahiri.
-
5:40 - 5:42Hutumia muda mwingi akisaidia wengine.
-
5:42 - 5:45Siri yake ya mafanikio ni kutoa dakika tano za fadhila.
-
5:45 - 5:48Adamu alisema, "Huhitaji kuwa Mama Teresa or Gandhi
-
5:48 - 5:49kuwa mtoaji.
-
5:49 - 5:52Unabidi utafute njia ndogondogo tu
-
5:52 - 5:53za kushika maisha ya watu."
-
5:53 - 5:55Kama kuwatambulisha watu wawili
-
5:55 - 5:58wanaoweza kufaidika kwa kujuana.
-
5:58 - 6:01Inaweza kuwa kutoa maarifa yako
au kutoa maoni. -
6:01 - 6:03Au hata kusema kitu kama,
-
6:04 - 6:05"Unajua,
-
6:05 - 6:07nitajaribu kumtambua mtu
-
6:07 - 6:10ambaye kazi yake hakujatambuliwa. "
-
6:10 - 6:13Hizo dakika tano za fadhila ni muhimu
-
6:13 - 6:14kusaidia watoaji kujiwekea mipaka
-
6:14 - 6:16na kujihami.
-
6:16 - 6:17Jambo la pili la msingi
-
6:17 - 6:20katika kujenga utamaduni ambapo watoaji wanafanikiwa,
-
6:20 - 6:23ni kuhamasisha utamaduni wa kutafuta msaada;
-
6:23 - 6:24ambapo watu huuliza na huomba kusaidiwa.
-
6:25 - 6:27Hii inaweza kuwaogopesha baadhi yenu.
-
6:27 - 6:30[katika mahusiano yako, ni lazima uwe mtoaji daima?]
-
6:30 - 6:31(Vicheko)
-
6:31 - 6:33Utakachogundua katika watoaji waliofanikiwa
-
6:33 - 6:36ni wanatambua kwamba ni sawa
kuwa mpokeaji pia. -
6:37 - 6:40Kama unamiliki shirika,
tunaweza kukurahisishia. -
6:40 - 6:42Tunaweza kurahishia watu kuomba msaada.
-
6:42 - 6:44Mimi na wenzangu tulifanya utafiti katika mahospitali.
-
6:44 - 6:47Tuligundua wauguzi katika baadhi za wadi
-
6:47 - 6:50waliomba kusaidiwa, kuliko wadi nyingine.
-
6:50 - 6:53Kilichozitofautisha wadi ambazo
-
6:53 - 6:54kuomba msaada ilikuwa kawaida, ni kulikuwa
-
6:54 - 6:56na muuguzi mmoja ambaye kazi yake
-
6:57 - 6:59ni kuwasaidia wengine katika kitengo.
-
6:59 - 7:00Msaada ulipohitajika, wauguzi walisema,
-
7:00 - 7:04"Sio aibu kuomba msaada -
-
7:04 - 7:05bali tabia inayohamasishwa."
-
7:06 - 7:09Kutafuta msaada ni muhimu
katika kuwalinda, -
7:09 - 7:11pia kwa ajili ya ustawi wa watoaji.
-
7:11 - 7:13Na kuhamisisha tabia za watoaji,
-
7:13 - 7:15kwa sababu takwimu zinaonyesha kwamba
-
7:15 - 7:18asilimia 75 hadi 90 ya utoaji
-
7:18 - 7:20huanzia na ombi.
-
7:20 - 7:21Lakini watu wengi hawaulizi.
-
7:21 - 7:23Wanahofia kuonekana hawajui,
-
7:24 - 7:26hawajui wageukia wapi, wanaogopa kuwasumbua wenzao.
-
7:26 - 7:29Ikiwa kamwe hakuna anayeomba msaada,
-
7:29 - 7:31utakuwa na watoaji wengi waliokatishwa tamaa,
-
7:31 - 7:33ambao wangependa kuchangia kwa kusaidia,
-
7:33 - 7:35laiti wangejua nani anahitaji msaada na kwa namna gani.
-
7:35 - 7:37Lakini jambo muhimu zaidi kama
-
7:37 - 7:40unataka kujenga utamaduni
ambapo watoaji wanafanikiwa, -
7:40 - 7:43ni kuwa mwangalifu kuhusu nani
unaweka kwenye timu yako. -
7:43 - 7:46Kama unataka utamaduni
wa ukarimu na uzalishaji, -
7:46 - 7:48unapaswa kuajiri watoaji.
-
7:48 - 7:51Lakini nilishangaa kugundua kwamba hiyo haikuwa sahihi --
-
7:52 - 7:54mapungufu ya mpokeaji
-
7:54 - 7:57ni mara mbili au mara tatu
zaidi kuliko manufaa ya mtoaji. -
7:58 - 7:59Ifiikirie hivi:
-
7:59 - 8:00tunda moja baya linaweza kuharibu kikapu chote,
-
8:00 - 8:03lakini yai moja nzuri haliwezi kuboresha dazeni nzima.
-
8:04 - 8:05Sijui hii ina maana gani--
-
8:06 - 8:07(Vicheko)
-
8:07 - 8:08Lakini natumaini mnaelewa.
-
8:08 - 8:11Yani-- weka hata mpokeaji mmoja kwenye timu,
-
8:11 - 8:14na utaona kwamba watoaji
wataacha kusaidia. -
8:15 - 8:18Watasema, "Nimezungukwa
na rundo la nyoka na papa. -
8:18 - 8:19Kwa nini mimi nichangie? "
-
8:19 - 8:21Wakati, ukiweka mtoaji mmoja kwenye timu,
-
8:21 - 8:23huwezi kupata mlipuko wa ukarimu.
-
8:23 - 8:25Mara nyingi zaidi, watu hufikiri,
-
8:25 - 8:27"Afadhali! Huyo anaweza kufanya kazi yetu yote."
-
8:27 - 8:30Hivyo, ufanisi katika kuajiri na kujenga timu
-
8:30 - 8:32haihusishi kuleta pamoja watoaji tu;
-
8:32 - 8:34ila pia kuwatoa wapokeaji nje ya shirika.
-
8:35 - 8:36Ukifanikiwa,
-
8:36 - 8:38utabakiza watoaji na walipizaji.
-
8:38 - 8:40Watoaji watakuwa wakarimu
-
8:40 - 8:42kwa sababu hawana wasiwasi
kuhusu kupokea fadhila. -
8:42 - 8:45Na uzuri wa walipizaji ni kwamba wanafuata musuada uliopo.
-
8:45 - 8:48Hivyo ni jinsi gani utamtambua mpokeaji, mapema?
-
8:49 - 8:52Sio rahisi kumtambua mpokeaji
-
8:52 - 8:53hasa kufuata tu hisia zetu za mwanzo.
-
8:54 - 8:56Kuna tabia ambayo hutupotosha .
-
8:56 - 8:57Inaitwa wito upendezi,
-
8:57 - 8:58kati ya vipimo vikuu vya hulka
-
8:58 - 9:00miongoni mwa tamaduni mbalimbali.
-
9:00 - 9:03Watu wapendezi ni wakarimu, wema, wanyenyekevu.
-
9:03 - 9:05Utawakuta wengi wao Kanada --
-
9:05 - 9:07(Vicheko)
-
9:07 - 9:10Ambapo kulikuwa na shindano la kitaifa
-
9:10 - 9:13la kutafuta kauli mbiu mpya ya Kanada
kwa kujaza tashbihi, -
9:13 - 9:15"Mkanada kama ..."
-
9:15 - 9:17Nilidhani kauli mbiu itakayoshinda ingekuwa,
-
9:17 - 9:20"Mkanada kama maple syrup,"
au, "... Hoki ya barafuni ." -
9:20 - 9:23Lakini, hapana. Kura zilichagua kauli mbiu mpya kuwa -
-
9:23 - 9:24na siwatanii --
-
9:24 - 9:26"Mkanada kama iwezekanavyo,
katika mazingira haya. " -
9:26 - 9:29(Vicheko)
-
9:30 - 9:32Sasa kwa wale ambao ni wapendezi,
-
9:32 - 9:34au labda ni wakanada kidogo
-
9:34 - 9:35mtaielewa upesi.
-
9:35 - 9:37Ninawezaje kusema kuwa mimi ni aina moja pekee
-
9:37 - 9:40wakati daima ninajibadilisha kuridhisha wengine?
-
9:40 - 9:42Watu nongwa hujaribu mara chache zaidi.
-
9:42 - 9:45Hawa, wana mashaka, ni wakasoaji, ni changamoto
-
9:45 - 9:48na ndio wenye kwenda kusoma sheria.
-
9:48 - 9:49(Vicheko)
-
9:49 - 9:52Hiyo sio utani; ni kweli kama kanuni.
-
9:52 - 9:53(Vicheko)
-
9:53 - 9:56daima nildhani watu wapendezi ni watoaji
-
9:56 - 9:58na watu nongwa ni wapokeaji.
-
9:58 - 9:59Nilipofanya utafiti,
-
9:59 - 10:02nilistaajabu kukuta hakuna uhusiano katika sifa hizo,
-
10:02 - 10:05kwa sababu tabia ya upendezi au nongwa
-
10:05 - 10:06ni gamba la nje tu:
-
10:06 - 10:08Je, watu wanajisikiaje baada ya kuzungumza na wewe?
-
10:08 - 10:11Wakati kutoa na kupokea inategemea nia yako:
-
10:11 - 10:14Je, maadili yako ni yapi?
Je, nia yako kwa wengine ni ipi? -
10:14 - 10:16Kama unataka kusoma watu kwa usahihi,
-
10:16 - 10:20utataka kuwepo katika chumba wakati kila mshauri anasubiri,
-
10:20 - 10:21kupata picha halisi.
-
10:21 - 10:24(Vicheko)
-
10:25 - 10:28Ni rahisi kuwatambua watoaji wapendezi:
-
10:28 - 10:30wao husema ndiyo kwa kila kitu.
-
10:32 - 10:35Wapokeaji nongwa wanatambulika kirahisi pia,
-
10:35 - 10:39ingawa unaweza kuwaita
kwa jina tofauti kidogo. -
10:39 - 10:40(Vicheko)
-
10:42 - 10:44Tunasahau makundi mengine mbili.
-
10:44 - 10:47Kuna watoaji nongwa
katika mashirika. -
10:47 - 10:50Hawa wanaonekana wagumu kwa nje
-
10:50 - 10:52lakini hujali sana maslahi ya wengine.
-
10:53 - 10:54Au kama mhandisi anavyoiweka,
-
10:54 - 10:56"Ah, watoaji nongwa ni -
-
10:56 - 10:58kama mtu mwenye kiolesura kibaya cha mtumiaji
-
10:58 - 11:00lakini mfumo mzuri."
-
11:00 - 11:01(Vicheko)
-
11:01 - 11:03Kama inawasaidia.
-
11:03 - 11:04(Vicheko)
-
11:04 - 11:08Watoaji nongwa hawathaminiwi katika mashirika yetu,
-
11:08 - 11:11kwa sababu huotoa changamoto
-
11:11 - 11:13ambazo watu hawataki kusikia
hata kama tunahizitaji. -
11:13 - 11:16Tunahitaji kuwathamini zaidi
watu hawa -
11:16 - 11:17badala ya kuwapuuza,
-
11:18 - 11:19na kusema, "Eh, wanakera,
-
11:19 - 11:21lazima awe mpokeaji nongwa."
-
11:22 - 11:25Kundi jingine hatari tunasahau ni-
-
11:25 - 11:27mpokeaji mpendezi, pia anajulikana kama muigizaji.
-
11:28 - 11:31Huyu ni mtu mwema akiwa mbele yako,
-
11:31 - 11:33na ukigeuka hukuchoma.
-
11:33 - 11:34(Vicheko)
-
11:35 - 11:38Napenda kuwakamata
hawa watu katika usahili -
11:38 - 11:39kwa kuuliza swali,
-
11:39 - 11:41"Je, unaweza kunipa majina ya watu wanne
-
11:41 - 11:43ambao umewasaidia kimsingi kazini?"
-
11:44 - 11:46Wapokeaji watakupa hayo majina manne,
-
11:46 - 11:49na wote watakuwa na mafinikio zaidi kuliko wao,
-
11:49 - 11:50kwa sababu wapokeaji ni wastadi katika kunyenyekea
-
11:50 - 11:53wakuu wao na kudharau walio chini.
-
11:53 - 11:56Watoaji wanajua zaidi majina ya watu chini ya uongozi wao,
-
11:56 - 11:58ambao hawana mamlaka mingi,
-
11:58 - 11:59ambao hawana mchango muhimu kwao.
-
12:00 - 12:03Hakika, tunafahamu kuwa tunajifunza mengi kuhusu tabia ya mtu
-
12:03 - 12:05kwa kumuangalia anavyohusiana na mhudumu
-
12:06 - 12:07au dereva wa Uber.
-
12:07 - 12:09Hivyo tukifanya yote vizuri,
-
12:09 - 12:11kama tutatoa wapokeaji katika mashirika,
-
12:11 - 12:13kama tutaweza kuwahakikishia usalama wanaoomba msaada,
-
12:13 - 12:15kama tutaweza kuwalinda watoaji wasichoke
-
12:15 - 12:18na kuwawezesha kutimiza malengo yao
-
12:18 - 12:20na pia kusaidia watu wengine,
-
12:20 - 12:21tunaweza kubadilisha mtizamo wa watu
-
12:21 - 12:23wanavyotizama mafanikio.
-
12:23 - 12:26Badala ya kuona ni mashindano,
-
12:26 - 12:30watu watatambua mafanikio kama mchango kijumuiya zaidi.
-
12:31 - 12:33Naamini kuwa njia kuu ya kufanikiwa
-
12:33 - 12:35ni kuwasaidia watu wengine wafanikiwe.
-
12:35 - 12:37Na kama tunaweza kusambaza imani hio,
-
12:37 - 12:39tunaweza kweli kuigeuza paranoia.
-
12:39 - 12:41Kuna jina kwa ajili hiyo
-
12:41 - 12:42inaitwa "pronoia."
-
12:43 - 12:45Pronoia ni imani kwamba
-
12:45 - 12:47wengine wanapanga mema kwa ajili yako.
-
12:47 - 12:49(Vicheko)
-
12:51 - 12:53Kwamba wanakuzunguka
-
12:53 - 12:56na kuimba sifa zako.
-
12:58 - 13:01Uzuri wa utamaduni wa watoaji
ni kwamba hio sio njozi, -
13:01 - 13:03huo ndio uhalisia.
-
13:04 - 13:06Ningependa kuishi kwenye dunia ambayo watoaji wanafanikiwa.
-
13:06 - 13:09Natumaini nyote mtanisaidia kujenga ulimwengu huo.
-
13:09 - 13:09Asanteni.
-
13:10 - 13:10(Makofi)
- Title:
- Je, wewe ni mtoaji au mpokeaji?
- Speaker:
- Adam Grant
- Description:
-
Katika kila mahali pa kazi, kuna aina tatu za msingi za watu: watoaji, wapokeaji na walipizaji. Mwanasaikoloji Adam Grant anazifafanua hizi nafsi tatu na anatoa mikakati ya kukuza utamaduni wa ukarimu na jinsi ya kuwaepuka wafanyakazi wabinafsi kuchukua zaidi kuliko sehemu yao.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 13:28
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for Are you a giver or a taker? | ||
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for Are you a giver or a taker? | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Are you a giver or a taker? | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Are you a giver or a taker? | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Are you a giver or a taker? | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Are you a giver or a taker? | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Are you a giver or a taker? | ||
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Are you a giver or a taker? |