Swahili subtitles

← Kama enyi watu wazima hamtaokoa dunia, tutaiokoa sisi.

Get Embed Code
38 Languages

Showing Revision 8 created 09/29/2020 by Nelson Simfukwe.

 1. Mpendwa Abuelita,
 2. Najua sijakuwepo nyumbani kwa muda.
 3. Uko nyumbani kwetu pazuri Mexico,
 4. nami niko hapa Marekani,
 5. nikipigania maisha
  yetu ya baadaye.
 6. Pengine unanyunyuzia ua waridi maji,

 7. ukitunza fyulisi
 8. na kuhakikisha kua kasa wako wameshiba.
 9. Hiyo ni mojawapo ya vitu,
  navikumbuka sana kuhusu nyumbani --
 10. kupoteza muda na maua
 11. ukinihadithia kuhusu utoto wako
 12. Unavyojua,
  tumeishi New York City tangu 2015

 13. Lakini maisha yamebadilika mno
  kwa mwaka uliopita.
 14. Hapo mwanzoni, New York
  ilikua ni sehemu ya makumbusho
 15. na hifadhi
 16. na shule na marafiki.
 17. Saaa hii ni kama mtandao
 18. unaoniunganisha na watu wengine
 19. wanaopanga kuokoa dunia.
 20. Wajua nilianzaje ?

 21. Ni baba na busara zake.
 22. Kila kitu ulimfunza,
  alienda akafunza ulimwengu.
 23. Maneno yake yote
  kuhusu uwajibikaji tulionao kama binadamu
 24. kuishi kwa usawa na asili
 25. yalipitishwa kwangu.
 26. Nimeona kutokua sawa kwenye ulimwengu wetu
 27. na kukumbuka ulichoniambia wakati mmoja:
 28. "Acha kila kitu bora kuliko ulivyokikuta."
 29. Najua ulikuwa unaongelea kuhusu vyombo,
 30. lakini, hiyo inaleta maana kwa ulimwengu pia.
 31. Sikujua cha kufanya mwanzoni.

 32. Dunia ni kubwa mno,
 33. na ina tabia nyingi mbaya.
 34. Sikujua vile msichana mwenye miaka 15
  angebadilisha chochote.
 35. lakini ilinibidi kujaribu.
 36. Ili kuweka hii falsafa katika vitendo,

 37. Nilijiunga na klabu ya mazingira shuleni.
 38. Lakini niliona wanafunzi wenza
  wakiongelea mchakato wa taka kuna matumizi tena
 39. na kutazama filamu zinazohusu bahari.
 40. Ulikua mwonekano wa kuzingatia mazingira
 41. ulioegemea
  harakati ya kutunza hali ya hewa isiyofaa,
 42. na kutupa lawama kwa mtumiaji
  katika janga la kubadiika kwa hali ya hewa
 43. na kutangaza joto inaongezeka
 44. kwa sababu tulisahau
  kurudisaha mifuko inayoweza tumika tena dukani.
 45. Ulinifunza kwamba kutunza ulimwengu

 46. inahusu uamuzi tunaochukua kwa pamoja.
 47. Nafurahia kukuambia, Abuelita,
 48. kwamba nimebadili
  wazo la kila mtu klabuni.
 49. Badala ya kuongelea mchakato wa kufanya taka kutumika tena,
 50. tumeanza kuandikia wanasiasa wetu barua,
 51. kupiga marufuku kabisa plastiki laini.
 52. Na kisha, lisilojarajiwa likatokea:

 53. tulianza kugoma shuleni.
 54. Nafahamu ushatazama kwa habari,
 55. au pengine hio si mahususi kwa saa hii.
 56. Lakini wakati huo, ilikuwa ni jambo kubwa.
 57. Hebu fikiria watoto kutoenda shule
  kisa wanataka watu waokoe dunia.
 58. (Video) Umati: Ulimwengu mwingine
  unawezekana ! Hatuzuiliki !

 59. XiyeBastide: Kwa mgomo wa
  kwanza kimataifa wa hali ya hewa,

 60. ilioandaliwa na Greta Thunberg,
 61. Nilishawishi wanafunzi 600 wenzangu
  kutembea nami.
 62. Greta Thunberg ni kijana mwanzilishi
  wa migomo

 63. Uimara wake ulinihamasisha,
 64. na kushtuka na utambuzi huu
 65. kua kijana angebadilisha maono ya umaa kwa masuala ya kijamii
 66. Harakati zikaanza.
 67. (Video) Umati: Nyamazisha !
 68. XB: Na nikawa mmoja wa waandalizi wakuu
 69. kwa New York, Amerika na ulimwengu

 70. (Video) XB: Tunahitaji nini?
  Crowd: Haki ya hali ya hewa!

 71. XB: Tunalihitaji lini ?
  Crowd: Sasa !
 72. XB: Nilianza kuongelea haki ya hali ya hewa na haki asilia

 73. na ushirika miongoni mwa vizazi tofauti.
 74. Huu ulikuwa mwazo tu, hata hivyo.

 75. Wiki iliyokuwa na shughuli nyingi katika maisha yangu
 76. nyakati zote itakuwa ni wiki ya Septemba 20,2019.
 77. Mimi na marafiki wangu tulipata watu 300,00 kugoma kwa ajiliya hali ya hewa katika jiji la New York

 78. Natamani ungekuwepo.
 79. Tuliandamana mitaani ya Wall Street kudai haki ya hali ya hewa.
 80. (Video) Umati: Hakuna tena kamwe makaa ya mawe, kamwe tena kwa mafuta, acha kaboni kwenye ardhi !

 81. XB: Mwezi huo, nilihudhuria Mkutano wa Hali ya Hewa wa Umoja wa Mataifa.
 82. Niliongea katika jopo alipokuwepo Al Gore

 83. Nikakutana na Jay Inslee na Naomi Klein
  na Bill McKibben

 84. na rais wa Umoja wa Mataifa
 85. Ilikuwa wiki la kustaajabisha kabisa maishani mwangu,
 86. kwa sababu kila mtu ninayemjua walikuja pamoja-
 87. walimu wangu, wanafunzi wenzangu wote...
 88. Hata maduka niyapendayo yalifungwa kwa ajili ya mgomo wa hali ya hewa.
 89. Kama ungeniuiza kwa nini nilifanya haya yote,
 90. jibu langu lingekuwa,
 91. "Kwanini nishindwe?"
 92. Imekua mwaka tangu nianze,
 93. na wakati mwingine huchosha.
 94. Lakini kama kuna kitu mmoja ulinifunza, ni uthabiti.

 95. Nakumbuka ulienda jiji la Mexico kila siku kwa miaka 30
 96. ili kupata pesa ya mahitaji ya familia.
 97. Na najua Abuelito amekua akitembea nje kwa miaka 20
 98. kulinda ardhi takatifu dhidi ya makampuni makubwa yanayataka kuinyakua
 99. mwaka moja si lolote
 100. kulingana na mapambano familia yetu imepitia.
 101. Na kama mapambano yetu yanaboresha dunia,
 102. yatatufanya kuwa watu bora.
 103. Kumekuwa na matatizo, Abuelita.
 104. Ulimwenguni,
 105. watu wanatarajia watoto kama sisi kufahamu kila kitu,

 106. au angalau wanatarajia tujue,
 107. Wanauliza na najibu,
 108. na kama najua jinsi ulimwengu unavyofanya kazi.
 109. Wanahitaji matumaini, nasi tunawapa.
 110. Nimepanga, kuandika, kuongelea na kusoma kuhusu hali ya hewa na sera
 111. karibu kila siku kwa mwaka moja uliopita.
 112. Na nina wasiwasi kidogo
 113. kwamba sitoweza fanya vya kutosha, Abuelita.
 114. Kwangu, kuwa na miaka 18 and kujaribu kuokoa ulimwengu
 115. inamanisha kuwa mwanaharakati wa hali ya hewa.
 116. Awali, labda ilimanisha kusoma kuwa daktari

 117. au mwanasiasa au mtafiti.
 118. Lakini siwezi ngojea kuwa mkubwa ili niwe mojawapo ya hayo.
 119. Ulimwengu unaumia,
 120. na hatuna taanasa ya wakati kamwe.
 121. Kuokoa ulimwengu kama kijana unahitaji ueledi wa maneno,
 122. kuelewa sayansi inayohusu janga la hali ya hewa
 123. kuleta mtazamo wa kipekee kwa suala ibuka
 124. na kusahau mambo mengineyo
 125. Lakini wakati mwingine, nahisi kuzingatia mambo mengine tena.
 126. Nataka kuimba na kucheza na kufanya mazoezi ya viungo vya mwili
 127. Kiukweli nahisi ikiwa sisi sote tungelinda ulimwengu
 128. kama tabia,
 129. kama tamaduni,
 130. hakuna mtu angekua mwanaharakati wa hali ya hewa wakati wote
 131. Kama biashara zimekua endelevu,
 132. kama gridi ya umeme inaendesha kwa nishati mbadala,
 133. kama mtaala wa shule unatufundisha

 134. kuwa kuzingatia ulimwengu ni moja ya utu wetu
 135. labda naweza fanya mazoezi ya sarekasi tena.
 136. Au sivyo, Abuelita ?
 137. Tunaweza fanya hili.
 138. Yote najaribu kufanya na kazi yangu
 139. ni kuwapa watu wengine mtazamo chanya wa matumaini.

 140. Lakini ni ngumu kidogo.
 141. Kuna tamaa,
 142. kuna kiburi,
 143. kuna pesa,
 144. na pia uyakinifu.
 145. Hulka ya watu hurahisisha kuongelea haya mambo,
 146. lakini napata wakati mgumu kuwafunza.
 147. Nataka wajiamini kwa kujitahidi kila wakati.
 148. Nawatakia kua na moyo na ujasiri
 149. wa kupenda ulimwengu,
 150. kamaulivyonifunza.
 151. Nimeandika barua hii kukushukuru.
 152. Shukrani kwa kunikaribisha kupenda ulimwengu
 153. tangu nizaliwe.

 154. Shukran kwa kucheka kwa kila kitu.
 155. Shukrani kwa kunifunza
 156. kua matumaini na matarajio ndizo zana za nguvu tulizo nazo
 157. kukumbana na shida yoyote.
 158. Nafanya hili kwa kuwa ulinionyesha
 159. kwamba uthabiti, upendo na ujuzi
 160. vinatosha kuleta mabadiliko.

 161. Nataka kurudi Mexico nikutembelee.
 162. Nataka kukuonyesha picha ya vitu nilivyofanya.
 163. Nataka kukuonyesha sheria ya hali ya hewa
 164. tuliyoweza kupitisha.
 165. Nataka kunusa maua
 166. na kupigania haki ya hali ya hewa pamoja nawe
 167. Te quiero mucho.(Nakupenda sana)
 168. Nakupenda
 169. Xiye.

 170. [Te quiero mucho. Xiye.]